Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


The Big Show,

Halafu EAMWS inataka kujenga Chuo Kikuu wanahujumu na kwa
kumsingizia Sheikh Hassan bin Amir kuwa ati alikuwa na mipango
ya kupindua serikali ya Nyerere.

Watu wasiopenda shule wanajenga Chuo Kikuu?

Hii JF Allah aidumishe sie tungepata wapi uwanja wa kucheza kidari
kama hapa...

Wapi tungepewa nafasi ya kueleza historia ya Waswahili wa Gerezani
walivyopambana na Gavana Twinning...

Idumu JF!
Hongera Yericko Nyerere!
 


Naam,,
Kwa kweli JF izidi kudumu,na nina mpango wa kutenga vijisenti vyangu ili nizidi kuichangia changia hii Forum idumu daima na daima..
Naskia Naskia Yericko ana fikiria kurusha taulo kati kati ya uringo ili kunusuru uhai wa fikra zake..
Atulie tuli umpe darsa hapa..
Thanks JF kwa kuwa na watu adimu sampuli yako..
 
Last edited by a moderator:

Nadhani utakuwa unamaanisha Barnes and Noble.
 
Wewe ni mwanahistoria mzuri katika kuboresha historia yetu na kwa faida ya wanajamvi tupashe habari za harakati za kisiasa za Mwl Nyerere, pale Chuo Kikuu cha Makelele.

ID yako mpya haijifichi, kiswahili huwa kinakupa tabu kuandika, akuna, aeleweki, usubutu na hii makelele hahahahaha!!!!!!!!!
 
At any rate,that does not tell us why,a century ago,the Germans built schools along the coast and the vast majority of their eager students were MUSLIMS.
WHY SHOULD OUR INDEPENDENT GOVERMENTS FAIL WHERE THE COLONIAL ADMINSTRATION SUCCEEDED???
Ah sisi ni wapenda kahawa na kashata tuuh..
@THE BIG SHOW,hizo shule along the coast unafikiri walikuwa wanasoma akina nani? labda kama mjerumani alikuwa anatumia kiboko-at all cost mjerumani na shule zake asingeweza kucheza na indoctrination ya madras
 

Jumamosi R Mengi kakupeni 100 million,ili muboreshe elimu,sasa mnatakiwa mzitumie hizi pesa for ELIMU,na sio anything else alaafu mnakuja kulalamika humu.
 
Mengi abarikiwe sana..
Vip nikuongeze ya tano?

kabla ujanipa ya tano,naomba hujibu hii

"THE BIG SHOW,hizo shule along the coast unafikiri walikuwa wanasoma akina nani? labda kama mjerumani alikuwa anatumia kiboko-at all cost mjerumani na shule zake asingeweza kucheza na indoctrination ya madras"
 
Mohamed,AMNUT walikuwa na majaribio mawili ya kumuondoa Nyerere katika uongozi kwa sababu ya dini yake. Hili umeliandika mwenyewe.
Hivi ilikuwaje Nyerere amsakame sheikh Amir na kumuacha mlezi Agakhan?

EAMWS ilianzishwa na Wapakistan. Tunao mfano wa Sheikh Malik aliyetuletea hii tabu ya ubaguzi tunayoendelea nayo leo. Tunaye Sheikh Rukara wa World Muslim League ambaye alikuwa mfanyakazi kutoka Burundi lakini akijihusisha sana na shughuli za kisiasa nchini hasa misikitini. Leo ni Rukara yule yule aliyekuwa na passport ya Tanzania ni senator wa Burundi.

Mifano hiyo miwili inatosha kukupa picha Sheikh Amir aliyewahi kuendesha jaribio la kumuondoa Nyerere madarakani alikuwa mtu wa namna gani. Nadhani hadi hapo neno ''kumsingizia'' limeshapoteza thamani yake.
 
Ndio maana Nyerere,hakutaka kuandika kitabu,ameenda na mengi peponi-ufisadi umeanza kabla nchi haijapata uhuru

Ha ha ha!!

Mkuu nasikia Rafiki yangu Ritz kala Ban,dah!,pole yake ila asijali mwambie Spike Lee yupo hapa kuchukua nafasi yake.

Mkuu huu mnakasha umekuwa na vitisho vingi mara...nitakupuuza... Nitakuweka kwenye list ya nini sijui....sasa labda wajadiliane wenyewe tuh kwasababu ndo "intellectual wannabe" alichoomba kutoka kwa mwalimu wafungue uzi mpya wapeane "Darsa"...

Hata hivyo Mashairi yamepungua humu ndani na yale majina ya "wazee wetu"yaliyokuwa yameanza kujaza page humu
 
Last edited by a moderator:
Hapa nina tatizo kabla sijachangia mchango wako. Hivi katika marais tuliowahi na tulio nao nani anaweza kuwa credited kwa kuongelea matatizo yanayodaiwa kuhusu waislam. Naomba msaada kidogo.

*****Big show naomba hoja ilitujadili hoja zako nzito tukiwa na ufahamu mzuri***
 
Jumamosi R Mengi kakupeni 100 million,ili muboreshe elimu,sasa mnatakiwa mzitumie hizi pesa for ELIMU,na sio anything else alaafu mnakuja kulalamika humu.

Mkuu Mengi kawapa Hela BAKWATA au Waislam?! because as long as I can remember BAKWATA ni kigango cha Kanisa.kwahiyo nadhani hicho chuo hakiwahusu na Mfumo kristo bado upo pale pale.
 
Wanajamvi, nimeweka majadiliano yangu na Mohamed hapa ili kupata taswira halisi ya kile kilichojadiliwa hadi kufikia neno Makerere. Naona spinning zimekuwa nyingi na hili linafanyika makusudi.

Hata hivyo bandiko hili linahitaji mtu mwenye kusoma na kuelewa kubaini kuwa majibu yapo ndani.
Kwa anayesoma kama hadithi bandiko hili halitamsadia kwani lipo katika kiwango tofauti.

Kuna swali muhimu sana nimeuliza na hakuna aliyejitokeza kulijibu.
Endapo hakuna jibu la swali langu basi nasimama kusema hoja yangu imejijibu na inasimama bila ushabiki.
Swali ni hili:
Hivi tunapoongelea harakati huwa tunamaanisha kitu gani? Na hapa naongeza, wakati wa mkoloni harakati zilijulikana kwa kitu gani
 
Nadhani utakuwa unamaanisha Barnes and Noble.

Khasa ndiyo hiyo Barnes and Noble.
Ahsante Nyambala.

Nawaheshimu watu wale kama ninavyowastahi HMV.
Santuri yeyote watakuletea mradi uwaeleze karekodi nani.
 


Nguruvi,
Hizo zimepitwa na muda.

Lete mpya.
 
Nguruvi,Hizo zimepitwa na muda.Lete mpya.
Ni hoja! ambayo hujaweza kuijibu kwahiyo utatumbukiza kejeli, dharau, maneno kama nimekusoma, sina ujuzi n.k.

Kama hilo la AMNUT limepitwa na wakati, hoja yangu imejibu vizuri kuwa neno ''kusingiziwa'' huna uhakika nalo.
Hata hivyo kwa vile limepitwa na wakati, sasa tujadili hili tulilo nalo.

Mohamed, Nini World Muslim League ilikuwa inanfanya nchini?
Je, hilo ni shirika la waislam
Nini ushiriki wako katika harakati na sheikh Rukara mkiwa na WML huku tukijua alikuwa ana harakati za kisiasa za nchi kwake na ndani ya nchi yetu!

Hili halijapitwa na wakati
 

Nguruvi,
Nimekuwekea hapo nyuma tu jinsi Abdu na Nyerere walivyosigana
kuhusu historia ya TANU.

Au imekupita?

Abdu anaanza na baba yake Nyerere anaukataa mwanzo huo wa
harakati.

Miaka zaidi ya 60 imepita toka Abdu aikatae historia ya uongo leo
sisi tuko hapa JF tunabishana lakini hamjapata ujasiri wa kusema
historia ya TANU ianze Butiama.

Nimekuwekeeni vitu vingi sana.
Nyie mmebakia na maswali kama tuko Mkwajuni kwa Hakimu Kiruka.
 

Nguruvi,
Unaikumbuka ile list yangu?
 
gombesugu, niliwahi kuandika hivi;
Kama nilivyosema mwanzo kuhusu post yako ya kwanza kabisa, mimi Mag3 niliipokea kwa moyo usio na doa and my greatest expectation was for you to be for real!
I really had great expectation...how wrong I was! Kumbe wewe ama ni mongoni wa wale wale aliowalenga Mohamed Said...the easily manipulated and duped au ni part and parcel katika lile "gang of goboes" , hebu soma hii simulizi/hadithi kwa umakini halafu, uitafakari halafu ujiulize maswali kadhaa;
Mohamed Said anaendelea kwa kueleza jinsi baada ya kurudi walikuta Tanganyika African Association (TAA) imezorota na mwaka 1950 wakafanya mapinduzi yaliyofanikiwa kwa nguvu ya ngumi badala ya nguvu ya hoja. Katika uchaguzi uliofuatia mapinduzi hayo Dr. Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa Raisi na Abdulwahid Sykes Katibu.

Wakoloni kwa hila za kufifisha nguvu za TAA wakawapa uhamisho wa nguvu waliokuwa viongozi wasomi na vinara wa TAA, Vedasto Kyaruzi na Hamza Mwapachu kwa kilichotafsiriwa kama kifungo cha kisiasa.
Mohamed Said said:
Abdulwahid occupied his former office at the TANU headquarters; the one which he had occupied in the 1950s when he was TAA President...

President? mpaka wakati huo jina TANU halitajwi popote na pia haielezwi jinsi Abdulwahid alivyoukwaa Uraisi wa TAA na je Ukatibu alimkabidhi nani. Ukweli ni kuwa alikaimu tu hizo nafasi mbili hadi uchaguzi ulipokuja kufanyika baadaye...
gombesugu chaguzi zinazoelezwa na zilizofanyika wakati huo ni hizi;

  • Mwaka 1953 Mwalimu Nyerere alipochaguliwa kuwa Raisi wa TAA katibu wake akiwa Abdulwahid Sykes...hata hivyo haieleweki kwa nini uchaguzi huu ilibidi ufanyike kama TAA tayari ilikuwa na Raisi.
  • Mwaka 1954, Mwalimu Nyerere kwa mara nyingine alichaguliwa kuwa Raisi wa kwanza muasisi wa chama kipya cha siasa TANU makamu akiwa John Rupia na Katibu Abdulwahid Sykes.
Mohamed Said said:
Hizi ndizo fikra za Kiwanuka, ambaye aliaminiwa na CCM kusimamia utafiti na uandishi wa historia mahsusi ya TANU. Kilichomkera ni kusema kuwa Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kudai uhuru wa Tanganyika.
Kwa makusudi Mohamed Said hawezi hata kuitaja dini ya huyo Kiwanuka, kutaja dini kutafifisha madai yake kwani Muislaam yeyote analazimika kutetea hoja zake hata kama hazina ukweli. Mimi ni Mkristo ingawa si Mkatoliki lakini najua kuwa miongoni mwetu tunaompinga na kukatalia kabisa madai yake wapo Waislaam tena safi kabisa. Katika kuwabagua Watanzania kwa misingi ya dini, hawezi kuamini kabisa uwezekano huo wa kuwepo Waislaam who see him for what he is na katu hawamuungi mkono.
Huyu ndiye Mohamed Said ambaye kila kitu hukiangalia kwa mtazamo wa dini...je, hayo mawazo hayo ya kichochezi aliyatoa wapi? Soma hapa;
Pro. Malik, mpakistani aliyepanda mbegu ya chuki mioyoni mwa vijana wa Kiislaam mojawapo akiwa Mohamed Said!...kwa mbali nakumbuka nchi ya Jamhuri ya Kiislaam ya Pakistan ilivyozaliwa mwaka 1947 baada ya nchi ya India kumeguka vipande viwili. Pamoja na kuwa nchi ya Kiislaam, mwaka 1971 Pakistan yenyewe ilibidi nayo imeguka na kuzaliwa nchi ya Kiislaam ya Bangladesh. Dhambi ya kubaguana haina mwisho...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…