Gombesugu, umejitahidi sana kujificha katika pazia. Tulikwambia kuwa ni suala la muda true color zitajitokeza na sasa zimejitokeza. Bandiko lako hili hukuwa na sababu ya kutumia neno mtu au watu. Hili umemlenga Nguruvi3.
Mimi nipo na Mohamed siku nyingi na moja kati ya mambo hayanisumbui ni kudharauliwa, kutukanwa au kudhalilishwa.
Mambo hayo hayanisumbui kwasababu kama kuna mtu mmoja ananielewa si tatiziki na 10 wasionielewa
gombesugu;6133278]Salaam. Nakufahamu ndugu yangu na Insha Allah Mola taajalia kila mmoja wetu miongoni mwetu anusurike na chuki na shari walonayo baadhi ya jamaa humu dhidi yetu.
Hili ni kosa lile lile la kila mara. ''baadhi yetu akina nani? Hivi akitokea kaka yako hakubaliana na Mohamed huyo ni ''baadhi yetu'' au inakuwaje.
Nadhani kama umesoma vizuri kuhusu Mohamed, dhima ya andiko lake ni chuki, farki, tashtiti n.k. Kama unachukia chuki basi Mohamed hafai kuwa ''baadhi yetu''. Kwanini ndugu yangu usisimame katika ukweli?
Sheikh Mohammed Said amekua kama vile "punching bag" lao,kila mwenye fedhuli na tashtit basi humtupia yeye. Ati hana facts,hatumii mantiki,methodology na wala hana ushahidi wa kisayansi na mengineyo kadhaa. Ama kwa hakika inadhihiri wao ndo dhalili wa hoja na wasokua na ustaarabu wala uungwana wa majadiliano ya kitaaluma au ki-Wanazuoni.
Hapa tuna uelewa tofauti na ni vema tukasadiana. Endapo kuna kitu kimefanyika kisayansi, methodically basi tunakuomba sana utusaidie. Na hapa nitakuuliza kitu kimoja. Je, upo tayari nikuwekee habari ya Mohamed utuelezee kisayansi ili utusaidie kitaalauma na ki-uwanazuoni kuonyesha chuki na dhalili anazofanyiwa?
Kama utakuwa tayari nifahamishe.
Infact,these are the same people quite often when asked question/s or clarification,would deploy every tactics at their disposal to avoid or even worse,their answer would create more intriguing questions. And still,they never tired of displaying much pretentiousness
Si kweli, labda kama unamuongelea Mohamed. Mohamed anajulikana jamvini kwa kauli za ''sina ujuzi'', nimekusoma, tuendelee na darsa, hilo tuliache kwanza, inasemekana, andika kitabu, nimekwenda ulaya, nimekula na wazungu n.k. katika kukimbia hoja.
Mfano, mumekomalia Makerere, nimeweka mnakasha niliokuwa nao na Mohamed,si hoja imekwisha!
Nimewauliza kwani harakati ni kitu gani hakuna aliyeeleza, hoja ikaisha. Nafahamu unachukia sana hoja za Mohamed kubomolewa lakini spade iitwe spade na siyo big spoon.Ukweli ni sehemu ya dini na imani kwa waumini.
Naona kuna jamaa humu very open and very energetically,amefikia kibri cha ku-challenge na kutoa offer ya mshahara in US$ nyingi! Ati kuthibitisha kuwa waIslam hapo Tanzania hawajasoma ni watu duni na hatuna viwango vizuri vya elimu, ati tumtafutie au kumuonyesha muIslam yeyote hapo Tanzania ambae ni Zoologist (Mtaalamu wa kuchungulia tupu za wanyama!). Na kama tunae "huyo jamaa" ati aliahidi kumtafutia ajira/kibarua kwa haraka saana!?
Wala usiseme jamaa sema Nguruvi3. Nimeweka hoja hiyo kwasababu imesemwa kuwa waislam hata walisoma wananyijmwa nafasi. Nikasema basi kama yupo Zoologist ajitokeze maana kuna shirika '(siyo mimi linahitaji mtu)Katika kufanya spinning zile zile za Ritz nawe umeniwekea maneno. Hilo sijali kwasababu kumbu kumbu zipo.
Narudia kama kuna Zoologist ajitokeze, kama hakuna shirika hilo hilo linatafuta local epidemiologist hasa mwenye background ya vetenary. Kama hakuna basi hapo ndipo mahali pa kuanzia kwanza kujiuliza kwanini? Nimesema waislam specifi kwasababu ndio wenye malalamiko ya kupea nafasi za menial job hata kama ni qualified kama alivyosema Mohamed.
Lakini nastaajabu alikua too selective kwenye kuonyesha huo "udhaifu wa elimu kwa waIslam". Mbona hakuuliza kama wapo waIslam hapo Tanzania ambao ni ma-Nuclear Scientists au taaluma nyingine anazohisi yeye kuwa mahiri zaidi!?Lakini jamaa wa aina hizi ndo mahodari wa kujinasibisha na usomi,wanataaluma na ati wanajadili hoja kwa matinki na ustaarabu.
Nimeongeza Epidemiology na zaidi kama yupo mtu wa Eng-Agric aliye na utaalamu katika combine harvester naye pia ajitokeze na qualification zake tusaidiane.
I know for fact that, that kind of narrow minded bigotry views aren't representation of many among myrespectifulChristians,Atheists,Scientologists,Animists friends I know
And respectful Muslims to add on.
Hapo juu umelalamika sana kuhusu matusi, kwa bahati mbaya na hili nakusamehe umerudia kile kile usichokitaka.
Gombesugu, Uislam ni dini ya mwenyezi mungu. Uislam hauna miliki au hati miliki isipokuwa kwa muumini. Baru baru aliwahi kusema si kila mwislam ni muumini lakini kila muumini ni mwislam. Uislam unasimama katika amani, haki na ukweli.
Uislam si ushabiki na Uislam umesisitiza katika kutafuta maarifa. Maarifa yaweza kupatikana hadi China. Maarifa si ushabiki, ni utambuzi na ufahamu. Kila anayekwenda kinyume na mafunzo ya Allah anamhalifisha Mwenyezi Mungu.
Uislam hauzui kusema au kukubali ukweli. Na hakika hiyo ni moja ya hidaya ya mwenyezi mungu kwa waja wake.
Hakika yule anayesimama katika ukweli basi atakuwa ameiona nuru na atakuwa miongoni mwa waja wema.
Mohamed Said akisema, yule mwenye elimu ana bahri, hivyo usichoke kujifunza na wala usijizuie kujifunza.
Kujifunza kunahitaji ustahamilivu hekima na busara. Hasira, jwazba na unyonge ni silaha mbaya unapokuwa katika kujifunza. Jifunze kila kilichopo katika mazingira yako, kiwe ndani ya msikiti, kanisa, sinagogi au Jamatini.
Basi tumuombe mwenyezi akunusuru na hasira na matusi, ili sote tuwe waja wake.
Mimi nimekusamehe kwasababu hakika hakuna mtimilifu miongoni mwetu wanadamu.
Masalaam, msalimie Ahli na nduguzo.