Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mohamed Said hakika wenye kasoro ya msimamo wa akili tu ndio utakao wabeba,

Yaani unauaminisha umma kuwa Mwalimu Nyerere aliihujumu EAMWS?

Halafu hapo husemi wazi kuwa aliyekuwa mfadhiri mkuu wa EAMWS ambae ni Agakhan yupo hadi hii leo anaendesha shughuli zake salama,

Hivi mwenye akili anakushangaa tu kwa huo uzushi unaouzusha ndugu Mohaned unalengo gani?

Kama kweli Nyerere alihujumu mradi huo kwa lengo lolote lile bila shaka angeihujumu ama kuwafukuza kabisa Aghakhan nchini.


Mohamed unawatesa vijana na kuwapandikiza chuki zako zisizo namsingi wowote mwisho wa siku taifa liingie machafukoni kwa ujuha wa mtu mmoja.
 

Mohamed kuweka vitu vingi si hoja, jambo la maana ni kuweka ukweli tu,

TANU haianzii Barma kama unavyotaka iwe, bali inaanzia na Nyerere kama historia inavyoaminika.

Kusema ilianzia Butiama hiyo nikejeri ya kukosa adabu tu, uaelewa fika kuwa chimbuko la TANU ni matokeo ya uchaguzi wa 1953 pale Anautogulo Mnazi mmoja uliomleta Mwalimu Nyerere.

Ideology yake ya TAWA ya makerere ndio iliyopalilia kuzaliwa kwa TANU.

Mohame Said ni kweli wewe wayajua mengi juu ya historia ya uhuru wetu, tatizo moja ni kuwa una agenda yako katika ngano zako.

Unafanya kila liwezalo kuyumbisha historia na kuweka uyatakayo hata kama hayasimami ipasavyo.

Sisi tumesimama na kukwambia wazi acha uzushi, uchochezi na ulanguzi wa fikra,
 

Sasa hapa ndio ninatannabahi chanzo cha gogoro na hizi tuhuma za uchochezi. Yericko and Co. wanashikilia kama TANU imeanza na Nyerere..ilihali Mohammed Saidi anadai kama TANU imeanzia mbaali zaidi ya hapo. Nadhani Mohammed Saidi watu wameshamsoma sana. Maana kitabu chake chenye understanding hii kipo kwenye public siku nyingi.

Ushauri uliotolewa kabla ndio mujarrab. Ni vyema wana jopo la msimamo wa kuwa TANU imeanzia kwa Mwl Nyerere wakaja na kazi ya kitafiti nao wakaeleza the other side of the story na Ndugu Yericko ambaye ni family member wa Mwl akatutolea shajara ambazo kutoka kwa kwenye library ya mwalimu kuwa yeye ndie alikuwa kila kitu.
 


Yericko anatia shaka kama kweli ni mwanafamilia wa ukoo ule..
Hata hotuba za mzee wake na baadhi ya matukio yake anakosa??
Hii inaingia vipi akilin??
 

UJUMBE kaupata,sasa hivi kakaa kitako-humu JF,fire will be met by fire-nothing else, ukija na longolongo au ngonjera,everything including the kitchen sink will be thrown at you
 
Yericko anatia shaka kama kweli ni mwanafamilia wa ukoo ule..
Hata hotuba za mzee wake na baadhi ya matukio yake anakosa??
Hii inaingia vipi akilin??
Ndugu yangu,

Ninajua mengi sana juu ya historia ya harakati za uhuru wa nchi hii,

Hayo niliyokupeni yenye kulihusisha kanisa ni dozi ndogo tu,

Sijui unataka nini ambacho kwako kitakuwa na mafaa ambacho waamini fika kuwa mimi sina?

Ni kweli naweza kabisa nisiwe na vyote au nisiijue historia yote, lakini niliyokupa yatosha kufungua medula zako
 
Jamani nilikuwa likizo kidogo, naona mnakasha bado unaendelea. Mohamed, si sahihi kusema kuwa waislamu walileta uhuru wa Tanganyika. Waislamu walianzisha harakati za kupigania uhuru katika eneo la pwani, hasa jiji la Dar-es- Salaam, hilo ni sahihi. Wakamwamini Julius Nyerere kuongoza harakati hizo, hilo pia ni sahihi. Lakini mizizi ya harakati ilienea nchi nzima hata katika maeneo ambayo waislamu si wengi. Lakini wewe unataka kutuaminisha kuwa ni waislamu pekee ndio waliopigania uhuru wa nchi hii, na kumalizia kwa kibwagizo kuwa baadaye wakabaguliwa. Nitarudi tena baadaye, ngoja ni "catch up" kidogo. Rafiki yangu Ritz yuko wapi?
 

nadhani hajasema kama ni wadini yake pekee. La hasha. Anachosisitiza ni kuwa kuna orodha kubwa ya wazee wake imesahaulwa na historia ya kivukoni.
Hivyo na yeye akaamua kuwataja kwenye kitabu chake.
 
nadhani hajasema kama ni wadini yake pekee. La hasha. Anachosisitiza ni kuwa kuna orodha kubwa ya wazee wake imesahaulwa na historia ya kivukoni.
Hivyo na yeye akaamua kuwataja kwenye kitabu chake.

Kuwataja ni jambo zuri. Ambapo hatukubaliani naye ni pale anapo insinuate kuwa Nyerere aliwabagua waislamu baada yao kumfadhili. Yaliyotokea baada ya uhuru, kukamatwa kwa mashehe, kufukuzwa kwa baadhi yao, kulifanyika kwa minajili ya kulinda the state. Lakini hapo hapo si mashehe peke yao waliokamatwa. Kuna wakristo wengi tu waliowekwa detention enzi hizo kwa hiyo unapozungumzia mashehe usisahau hao wakristo waliowekwa kizuizini vile vile. Nyerere was a nationalist. He was not anti-islam.
 
Mohamed, tukiweka hoja kama za WML hutaki kujibu. Tukichangia tunachoelewa unasema ''sisi na nyie''.

Kuuliza swali si kuwa mtu hajui Mzee Said!!! Mtu anayeuliza swali anjaua na ndio maana siku zote tunaanza na maswali halafu unakwama! Ukikwama unasema kaandikieni vitabu! Ebo! Yaani uniambie kuwa Tanzania ni mwanachama wa commonwealth kwasababu ya mfumo kristo nikikuambia hapana unasema niandike kitabu!

Kwamba Nigeria ina waislam wengi nikkikuambia hapana unataka niandike kitabu.
Kwamba Warioba alitoka machungani na kuingia uwaziri mkuu , nikisema hapana unataka niandike kitabu.

Kule mkwajuni wanakokaa wakiachama na kupiga makofi si hapa.
Mohamed wa leo si yule anayejulikana miaka 15.
Sasa hivi kabla hajatupa namba au nukuu lazima aidurusu!
 
Nguruvi,
Nimekuwekea hapo nyuma tu jinsi Abdu na Nyerere walivyosigana
kuhusu historia ya TANU.

Au imekupita?

Abdu anaanza na baba yake Nyerere anaukataa mwanzo huo wa
harakati.

Lakini mzee Said na wewe unawapotosha watu; historia ya TANU ukitaka kurudi nyuma kweli haikuanza na babake Abdule - Kleist Sykes. Hili nimelisoma kwenye kitabu cha Illife - Modern "Tanzanians"
 
Gombesugu, umejitahidi sana kujificha katika pazia. Tulikwambia kuwa ni suala la muda true color zitajitokeza na sasa zimejitokeza. Bandiko lako hili hukuwa na sababu ya kutumia neno mtu au watu. Hili umemlenga Nguruvi3.
Mimi nipo na Mohamed siku nyingi na moja kati ya mambo hayanisumbui ni kudharauliwa, kutukanwa au kudhalilishwa.
Mambo hayo hayanisumbui kwasababu kama kuna mtu mmoja ananielewa si tatiziki na 10 wasionielewa
gombesugu;6133278]Salaam. Nakufahamu ndugu yangu na Insha Allah Mola taajalia kila mmoja wetu miongoni mwetu anusurike na chuki na shari walonayo baadhi ya jamaa humu dhidi yetu.
Hili ni kosa lile lile la kila mara. ''baadhi yetu akina nani? Hivi akitokea kaka yako hakubaliana na Mohamed huyo ni ''baadhi yetu'' au inakuwaje.
Nadhani kama umesoma vizuri kuhusu Mohamed, dhima ya andiko lake ni chuki, farki, tashtiti n.k. Kama unachukia chuki basi Mohamed hafai kuwa ''baadhi yetu''. Kwanini ndugu yangu usisimame katika ukweli? Hapa tuna uelewa tofauti na ni vema tukasadiana. Endapo kuna kitu kimefanyika kisayansi, methodically basi tunakuomba sana utusaidie. Na hapa nitakuuliza kitu kimoja. Je, upo tayari nikuwekee habari ya Mohamed utuelezee kisayansi ili utusaidie kitaalauma na ki-uwanazuoni kuonyesha chuki na dhalili anazofanyiwa?
Kama utakuwa tayari nifahamishe. Si kweli, labda kama unamuongelea Mohamed. Mohamed anajulikana jamvini kwa kauli za ''sina ujuzi'', nimekusoma, tuendelee na darsa, hilo tuliache kwanza, inasemekana, andika kitabu, nimekwenda ulaya, nimekula na wazungu n.k. katika kukimbia hoja.
Mfano, mumekomalia Makerere, nimeweka mnakasha niliokuwa nao na Mohamed,si hoja imekwisha!
Nimewauliza kwani harakati ni kitu gani hakuna aliyeeleza, hoja ikaisha. Nafahamu unachukia sana hoja za Mohamed kubomolewa lakini spade iitwe spade na siyo big spoon.Ukweli ni sehemu ya dini na imani kwa waumini.

Wala usiseme jamaa sema Nguruvi3. Nimeweka hoja hiyo kwasababu imesemwa kuwa waislam hata walisoma wananyijmwa nafasi. Nikasema basi kama yupo Zoologist ajitokeze maana kuna shirika '(siyo mimi linahitaji mtu)Katika kufanya spinning zile zile za Ritz nawe umeniwekea maneno. Hilo sijali kwasababu kumbu kumbu zipo.
Narudia kama kuna Zoologist ajitokeze, kama hakuna shirika hilo hilo linatafuta local epidemiologist hasa mwenye background ya vetenary. Kama hakuna basi hapo ndipo mahali pa kuanzia kwanza kujiuliza kwanini? Nimesema waislam specifi kwasababu ndio wenye malalamiko ya kupea nafasi za menial job hata kama ni qualified kama alivyosema Mohamed. Nimeongeza Epidemiology na zaidi kama yupo mtu wa Eng-Agric aliye na utaalamu katika combine harvester naye pia ajitokeze na qualification zake tusaidiane.
I know for fact that, that kind of narrow minded bigotry views aren't representation of many among myrespectifulChristians,Atheists,Scientologists,Animists friends I know
And respectful Muslims to add on.
Hapo juu umelalamika sana kuhusu matusi, kwa bahati mbaya na hili nakusamehe umerudia kile kile usichokitaka.

Gombesugu, Uislam ni dini ya mwenyezi mungu. Uislam hauna miliki au hati miliki isipokuwa kwa muumini. Baru baru aliwahi kusema si kila mwislam ni muumini lakini kila muumini ni mwislam. Uislam unasimama katika amani, haki na ukweli.

Uislam si ushabiki na Uislam umesisitiza katika kutafuta maarifa. Maarifa yaweza kupatikana hadi China. Maarifa si ushabiki, ni utambuzi na ufahamu. Kila anayekwenda kinyume na mafunzo ya Allah anamhalifisha Mwenyezi Mungu.

Uislam hauzui kusema au kukubali ukweli. Na hakika hiyo ni moja ya hidaya ya mwenyezi mungu kwa waja wake.
Hakika yule anayesimama katika ukweli basi atakuwa ameiona nuru na atakuwa miongoni mwa waja wema.

Mohamed Said akisema, yule mwenye elimu ana bahri, hivyo usichoke kujifunza na wala usijizuie kujifunza.
Kujifunza kunahitaji ustahamilivu hekima na busara. Hasira, jwazba na unyonge ni silaha mbaya unapokuwa katika kujifunza. Jifunze kila kilichopo katika mazingira yako, kiwe ndani ya msikiti, kanisa, sinagogi au Jamatini.

Basi tumuombe mwenyezi akunusuru na hasira na matusi, ili sote tuwe waja wake.
Mimi nimekusamehe kwasababu hakika hakuna mtimilifu miongoni mwetu wanadamu.

Masalaam, msalimie Ahli na nduguzo.
 
Nanyumba liyotoa Cameron nayo si ilisemwa imejengwa na Sykes!
Hii Nyumba umeitaja sana.Sasa jibu limetolewa
Nafyonza Ilm kisha naenda zangu tarudi tena.

Nguruvi !
:A S 114: :A S 114: :A S 114:
 
Mnakasha umejaa vitishoo!!
Mara....list this...list that...nitakupuuza...nitaku-nini sijui aaah!!

Hii ni ishara ya kuishiwa hoja.
 
, Uislam ni dini ya mwenyezi mungu. Uislam hauna miliki au hati miliki isipokuwa kwa muumini. Baru baru aliwahi kusema si kila mwislam ni muumini lakini kila muumini ni mwislam. Uislam unasimama katika amani, haki na ukweli.

Uislam si ushabiki na Uislam umesisitiza katika kutafuta maarifa. Maarifa yaweza kupatikana hadi China. Maarifa si ushabiki, ni utambuzi na ufahamu. Kila anayekwenda kinyume na mafunzo ya Allah anamhalifisha Mwenyezi Mungu.

Uislam hauzui kusema au kukubali ukweli. Na hakika hiyo ni moja ya hidaya ya mwenyezi mungu kwa waja wake.
Hakika yule anayesimama katika ukweli basi atakuwa ameiona nuru na atakuwa miongoni mwa waja wema.

Mohamed Said akisema, yule mwenye elimu ana bahri, hivyo usichoke kujifunza na wala usijizuie kujifunza.
Kujifunza kunahitaji ustahamilivu hekima na busara. Hasira, jwazba na unyonge ni silaha mbaya unapokuwa katika kujifunza. Jifunze kila kilichopo katika mazingira yako, kiwe ndani ya msikiti, kanisa, sinagogi au Jamatini.

Basi tumuombe mwenyezi akunusuru na hasira na matusi, ili sote tuwe waja wake.
Mimi nimekusamehe kwasababu hakika hakuna mtimilifu miongoni mwetu wanadamu.

Masalaam, msalimie Ahli na nduguzo.[/QUOTE]

Nguruvi kwahaya maneno nimekubali uko vizuri :yo::yo::yo: na wewe naomba ukubali mzee MS yuko vizuri hata kama umeona kuna makosa kwenye historia yake yeye ni binadamu kwasababu kitabu chake si msahafu ninacho kushauri huu mnakasha tuendenao kwa ustaarabu bila madharau kwasababu ziko pande mbili hapa lakini kunaupande ambao unadharau upande mwingine eti kwasababu wanasoma madrasa hilo sio jambo lilotuleta kwenye huu mnakasha kwahiyo respect ni kitu muhimu sana sawa mkubwa
 

Nguruvi3,

Nguruvi napenda kupingana na wewe hapo nilipo bold. Kwani huo ni mtazamo hasi kwa jamii. Kumbuka kuwa UDSM si kuwa ni pekee na maarufu sana duniyani kulinganisha na nyingine kama hivyo kwa historia ya nchi yenu Tanzania ambayo UDSM ipo inapokataa kukipitia kitabu cha kitaaluma kinachozungumzia historia ya nchi yenu huo utakuwa uvivu na unafiki wa watafiti wenu katika chuo hicho katika kutaka kutoa historia ya kweli.

Kwa mtazamo wangu kinachofanyika kwenye mnakasha huu kilitakiwa kifanywe na UDSM kudadisi na kukisoma kitabu hichi ikiwemo kumwalika mwandishi afike na kutoa muhadhara ili wapate kuumuuliza masuala mbalimbali katika historia hiyo aliyoandika na kama wataona kuna mapungufu kidogo basi wakifanyie masahihisho na kama kimepotoka kabisa basi wakiandike kingine kupingana na hicho.

Huo ndio sisis tunaita usomi wa kuelimika na sio usomi wa ulafi wa fedha. Au hata hili la kuandika historia sahihi ya nchi enu mnahitaji wafadhwili waje wawasaidie.

Historia mnayoitumia ni ile ya kijitabu kilichitungwa na Chuo cha kivukoni ambayo hakuna hata University moja dunini wanayoweza kuitumia na kubakia kusomwa hapo UDSM ambayo inaonyesha kuwa kuna siri ndanimwe yya kutaka kuficha ukweli.

Kitabu cha MS kimepitiwa na kinazidi pitiwa na taasisi na vyuo vikuu vingi na hata kutumiwa kama reference katika vyuo mbalimbali ambavyo MS ametubainishia humu kwa ushahidi thabiti.

Je unaweza nieleza kijitabu cha Historia ya uhuru wa tanganyika inapitiwa na University gani nyingine nje ya UDSM? Je kwanini?

Nafikiri sasa ni wakti wa kusema ukweli na kuacha tarbia ya kuficha ukweli na kueneza propaganda katika mambo ya historia kwani siku zote historia huwa inajirudia.

Funguka kiakili usikumbwe na ushabiki wa kuficha ukweli kwa kumpendelea mtu kwa faida yako.
 

Umenifurahisha sana Mkuu, kuwa kwangu nje ya mnakasha kwa siku chache, mengi yamenipita.
Sheikh Said anajua wazi kuwa pasi kuyatumia hayo maneno ya "NYIE" na "SISI" hawezi kupata uungaji mkono.
Siku zote, mwanasisa duni (labda Mzee Said si mwanasiasa ingawa anatumia dini kisiasa) hutumia hoja za kidini kupata manufaa ya muda mfupi kisiasa, lakini yenye madhira ya muda mrefu kwa Taifa na watu wake.
 

Umenifurahisha sana Mkuu, kuwa kwangu nje ya mnakasha kwa siku chache, mengi yamenipita.
Sheikh Said anajua wazi kuwa pasi kuyatumia hayo maneno ya "NYIE" na "SISI" hawezi kupata uungaji mkono.
Siku zote, mwanasisa duni (labda Mzee Said si mwanasiasa ingawa anatumia dini kisiasa) hutumia hoja za kidini kupata manufaa ya muda mfupi kisiasa, lakini yenye madhira ya muda mrefu kwa Taifa na watu wake. -,
 
Mzee Said, hizo kambi mbili ni zipi? Na una hakika gani kuwa wanaokubali hoja zako wote ni kambi "SISI" na wasiokubali hoja zako ni kambu "NYIE"?

Kwa hizo "fitna" zako sio ajabu kuwa mihadhara kuhusu vitabu vyako unafanyiaga Misikitini ambako kambi ya "NYIE' hawawezi kuingia na kuuliza ili kukupa changamoto, na kwenye redio (bila shaka ni ile iliyofungiwa) ambayo hadhira ni ile ambayo haina Waandishi wenye kuzingatia weledi wa Tasnia ya habaru.
 



Kwani wewe hujui ya kwamba wa kwanza kuanza kujenga pande mbili katika mnakasha huu ni nyinyi??
Mmesahau kuwa ni nyinyi ndio wa kwanza kumwambia Moh Said anaoga na watoto wadogo,ya kwamba hawa ni walamba buti wa Moh Sadi,na kwamba hawa ni wafuasi wa Moh Said kisa tuh wameonekana kukubaliana na Moh Said katika mnakasha huu??
Sasa kipi kinachhokushangaza Moh Said akisema nyie na sie??,hopless blocks..

THE FIFTH ESCAPE ROUTE..

The fith escape route;

inasemaa,,inasema..

The fifth escape route is to frighten people away fom discussing the Muslims question by making it a political taboo.
To raise it is to threaten our country's peace and security..!,,yes,to threaten peace & security together with country's prosperity,,,"afanalekii !!"
Th
is strategy is of little value because Muslims have never been known to be peace - and -order fanatics,who regard human life so precious and peace so valuable,as to be brought at the price of servitude.
To them peace and order do not constitute an ultimate value,to be held dear irrespective of what they preserve.In any case,trying to scare away a debt collector,is not a reliable way of attaining peace,even of mind.
Wanywa kahawa tuna msemo unaosema ya kwamba "DAWA YA JINO NI KUNG'OA",,'DAWA YA DENI NI KULIPA",,

"A bad tooth has to be removed and replaced,but a debt has to be paid"

Waanzilishi wa "sisi na nyie" ni nyinyi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…