Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mkuu, Nguruvi3,

Bila uwepo wako hapa jamvini ingekuwa hatali kubwa.
Kwa kwali mchango wako hauna mfanoe. labda mtu akusome kwa kutanguliza dini yake tofauti na hivyo huna mpinzani.
 

Barubaru nadhani nimefurahi na mchango wako. Nauliza kitu kimoja. Watu wawili wamefanya jambo pengine lilelile au limetofautiana. Katika kueleza, wewe unamwita mmoja wao "Abdallah kafanya kadha......". Unahamia yule wa pili unamwita "Mission educated Nguruvi kafanya kadhaa....." maana yako nini? Huhitaji kusoma UDSM kujibu swali hili. Wewe toa analysis yako.
 
mada hii inaweza kuendela jadiliwa hata miaka 5, ila kweli ipo pale pale ya wkamba historia ya uhuru ilichakachuliwa kwa kipindi kirefu na watu hakujua ukweli halisi, pia jingine hakuna mtu anayeweza kupinga kitabu hiki.
 
Reactions: Ami
mada hii inaweza kuendela jadiliwa hata miaka 5, ila kweli ipo pale pale ya wkamba historia ya uhuru ilichakachuliwa kwa kipindi kirefu na watu hakujua ukweli halisi, pia jingine hakuna mtu anayeweza kupinga kitabu hiki.


ME SIMO..
Watakuja hapa muda si mrefu kukuweka katika list yetu ya walamba buti za moh said..
Hawana dogo wala kubwa hao,pia wapo waandika vitabu vya mapenz nao wanataka waonekane kuwa ni waandishi wenye weledi kama Moh Said n,k,Wapo pia wafia dini wanaopigana Crusade War wamejaa humu,we subiri uone cha moto..
Sisi wenzako tushazoea sasa..
 

Jasusi;

Ni Mkristo yupi aliyekamatwa na kutupwa jela halafu akasafirishwa nje ya nchi? Ni jumuiya ipi ya Kikristo iliyofutwa kipindi hicho? Kumbuka Nyerere alitangaza vita na Vigogo wa EAMWA akina Tewa Saidi Tewa na Bibi Titi Mohamed kwa msimamo wao wa kuilinda na kuienzi jumuiya hiyo hata kama Mwalimu hakuwa radhi! sasa wataje hao Viongozi wa Kikristo waliokamatwa na kuswekwa jela kwa sababu za kutaka kumpindua Mwalimu au kwa sababu zingine!
 

Kadogoo
,


..acha ubishi ndugu yangu, Waislamu wa Machame, Usangi, Kagera, wanazingatia elimu kuliko wenzao walioko Pwani na Kusini.

Si kweli unayosema kwani hakuna utafiti uliofanya kuthibitisha dai lako!
Jee; vipi Waislamu wa Kondoa, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Musoma, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Iringa, Morogoro, Singida, Manyara, na Zanzibar wao vipi mazingatio yao ya elimu kulinganisha na wenzao wa Pwani na Kusini?
 
Ningependa sana nijue idadi ya washiriki wa huu mjadala ambao kweli wamekisoma hicho kitabu cha historia ya TANU kinachoitwa cha Kivukoni. Inaonekana wengi hawachangii kulingana na yaliyoandikwa humo na badala yake wanachangia kulingana na simulizi/madai ya Mohamed Said. Naomba nitoe kwa ufupi sana nukuu chache za yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho kama inavyopatikana kwenye website rasmi ya CCM.
Ndugu wanajamvi, naomba wote ambao wangependa kujua ukweli wafanye angalau jitihada za kukitafuta kitabu hicho...wakisome halafu walinganishe na dai la Mohamed Said la wazee wake wa Gerezani kutotajwa/kusahauliwa. Mimi, pamoja na kutoipenda CCM, nasifu kitabu hicho kwa kuwakumbuka wazee wetu wote kama Watanganyika bila ubaguzi wowote kama anaouleta mdini Mohamed Said.

Mohamed Said aliwahi hata kudai kuwa Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, hakuweza kumtaja na hata kumkumbuka Marehemu Abdulwahid Sykes. Ajabu ni kwamba hata pale alipoletewa maandishi ya hotuba hiyo, aliendelea kupinga akidai sauti/video na kwamba hiyo hotuba iliyoletwa hapa ilichakachuliwa!

Huyo ndiye Mohamed Said! Jamani tafuteni hicho kitabu mjisomee wenyewe kama humo ndani ukoo wa Sykes hautajwi! Anayeamua kuamini maneno ya Mohamed Said kuhusu hilo rukhsa lakini abaki akijua kuwa mwisho wa uongo ni pale ukweli unapojitokeza. Wengine wetu tumejitahidi sana kuliweka hilo wazi na kama wapo bado hawakubali, wana lao!
 
Kadogoo kama hata hilo unauliza basi hili jukwaa linakuzidi kimo na hivyo nakuomba ubaki msomaji/mtazamaji tu, hakuna atakayekudharau! Wewe bila shaka ni mmojawapo kati ya wale walioathirika kweli kweli na porojo za Mohamed Said!
 
Last edited by a moderator:

WICKAMA;

Shule za Mudio na Kirinjiko zinapokea wanafunzi toka kila pembe ya nchi yetu na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Burundi na sio kwa ajili ya Wamachame tu au Wapare! tena hayo makabila wanafunzi wao ni wachache sana kuliko wengine kwasababu ada za shule hizo hazibagui kama huyu ni Mmachame au Mpare bali inategemea na mfuko wa Mzazi jinsi ulivyo!

Kwa taarifa yako Shule hizi zinafanya bidii na juhudi zote hizo kwasababu haziko chini ya Bakwata ambayo pia inamiliki shule ktk maeneo hayohayo unayosifia! mfano: Shule ya Kolila Secondary iliyoko Kwasadala Masama, Alnahdwa na Bakwata Secondary School izilizoko Moshi na Shule zingine za Bakwata huko Upare!
Sasa jiulize kwanini Shule za Bakwata huko Uchagani na Upareni zinatia aibu lakini zilizochini ya Jumuiya zingine zinaongoza? kwa mtazamo wako Wachaga na Wapare wanaosoma ktk Shule za Mudio na Kirinjiko wanaakili au mwamko zaidi kuliko wenzao wanaosoma ktk Shule za Bakwata?
 
Kadogoo kama hata hilo unauliza basi hili jukwaa linakuzidi kimo na hivyo nakuomba ubaki msomaji/mtazamaji tu, hakuna atakayekudharau! Wewe bila shaka ni mmojawapo kati ya wale walioathirika kweli kweli na porojo za Mohamed Said!


Kipi kilichokusibu siku hizi za karibuni??
Umechuja sana na umekua dhaifu kama nyumba ya BUIBUI..
Mwenzako Gwlihenzi wa mkokoteni yuko wapi??
Naona mnaanza kupotea mmoja baada ya mwingine..
Poleni Sana..
 

Huyo ndiyo Kadogoo, kazi kwelikweli. Waiteni hawa wengine wasio na mashule yao toka huko ulikotaja waje pale Mudio/Kirinjiko Islamic wajifunze nyie mmewezaje. Haiwezekani nyie mchangikishane mpaka mlio Dar, mfyatue tofali, mtafute waalimu na kujenga mashule halafu wengine wajilie raha huku wakivuta uradi na kumlaani Mkapa. Swala na kazi Kadogooo, Hata ungekuwa Freemason lazima uhenyee maendeleo yako.
 
Kadogoo kama hata hilo unauliza basi hili jukwaa linakuzidi kimo na hivyo nakuomba ubaki msomaji/mtazamaji tu, hakuna atakayekudharau! Wewe bila shaka ni mmojawapo kati ya wale walioathirika kweli kweli na porojo za Mohamed Said!

MAG3;

Kama mmeshindwa kujibu hoja heri kunyamaza wala sio aibu!
 

WICKAMA;

Shule za Mudio na Kirinjiko zinapokea wanafunzi toka kila pembe ya nchi yetu na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Burundi na sio kwa ajili ya Wamachame tu au Wapare! tena hayo makabila wanafunzi wao ni wachache sana kuliko wengine kwasababu ada za shule hizo hazibagui kama huyu ni Mmachame au Mpare bali inategemea na mfuko wa Mzazi jinsi ulivyo!

Kwa taarifa yako Shule hizi zinafanya bidii na juhudi zote hizo kwasababu haziko chini ya Bakwata ambayo pia inamiliki shule ktk maeneo hayohayo unayosifia! mfano: Shule ya Kibohehe Secondary iliyoko Kwasadala Masama, Alnahdwa na Bakwata Secondary School izilizoko Moshi na Shule zingine za Bakwata huko Upare!
Sasa jiulize kwanini Shule za Bakwata huko Uchagani na Upareni zinatia aibu lakini zilizochini ya Jumuiya zingine zinaongoza? kwa mtazamo wako Wachaga na Wapare wanaosoma ktk Shule za Mudio na Kirinjiko wanaakili au mwamko zaidi kuliko wenzao wanaosoma ktk Shule za Bakwata?
 
Mag3; Mohammed SAid anatumia ignorance ya baadhi ya watu kuwalisha uongo. Habari za wazee wake zimeandikwa kwa kirefu kama sehemu ya historia yetu kama taifa. Nilisema huko nyuma kuwa nilikuwa nimeagiza baadhi ya vitabu ambavyo Bw. Said amevitumia sana kupotosha historia; tayari ninavyo viwili ambavyo vimefika katika ya karibu 14 ambavyo nimeagiza toka maktaba mbalimbali hapa.

Historia ya TANU ilianza na Kleist Sykes?

Kitabu cha Modern Tanganyika cha John Iliffe kinatudokeza hivi (Iliffe yeye alikuwa mhariri tu; maandishi hapa chini ni ya Daisy Sykes mjukuu wa Kleist):

While Kleist was settling down in family life and in his new job during the 1920s, he was alo beginning to become involved in mattrs of social and political concern. When the famous Ghanian educater Dr. Aggrey visited Dar es Salaam in 1924 Kleist was among those who welcome him and exchanged views with him. It is said that Aggrey gave a copy of one of his books to Kleist.... It is likely that Aggrey first interested Kleist in politics, for a few years laer Kleist was one of the small group of men who formed the Tanganyika African Association (pg 101)

Anaendelea

It is said that Rawson Watts, who used to work at the Secretariat, was the originator of the idea of an Association. When this idea became known amongst his friends in Dar es Salaam - meaning the people mentioned above - the idea seemed agreeable. So they met at Cecil Matola's house to discuss it. (pg 102)

Sasa ukikubaliana na historia ya Iliffe ambayo ndio msingi wa simulizi la Mohammed Said utaona kuwa

a. Kleist Sykes alichochewa kuingia katika siasa na Dr. Aggrey (Mghana, na I suppose Mkristu -kama suala la dini ni la msingi).

b. Wazo la kuanzisha Association halikutoka kwa Kleist Sykes bali kwa Rawson Watts. Kama kweli Watts ndiye mwanzilishi wazo la kuanzisha Association Kleist Sykes anapewa credit ya nini? Daisy (Mjukuu wa Kleist na mtoto wa Abdul) anamuona kama mmoja tu wa waanzilishi.

c. Mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola siyo kwa Sykes. Na inaonekana Cecil Matola alikuwa na nafasi ya pekee kiasi cha kuwa ni Rais wa kwanza (japo wengine wanasema Rawson Watts ndiye alikuwa Rais wa kwanza wa TAA)

Kwa hiyo hoja kuwa historia ya TANU ni lazima uende nyuma hadi Kleist haina msingi wowote; kwani ukiishia kwa Kleist tu bado hujafika mwisho ni lazima ufike kwa Watts na kwa Dr. Aggrey. Bahati mbaya waanzishili hawa wa mawazo ya kuunda TAA ni Wakristu na Mohammed Said hakutaka kuwapa Credit due to them.
 

There you are at last!!!!! Mimi sina tatizo na taasisi. Bakwata sio dhehebu. Wenye uchungu na maendeleo yao na waunde hata taasisi ya kuwasimamia kile wanachotaka!!!!! Issue hapa ni kuwa nyie waislamu wa Machame mmethubutu. Mmeonyesha dira. mmeonyesha kumbe inawezekana,na sasa hata vijana wasio waislamu wanakuja Mudio. Tunalopinga ni mtu kudanganya waumini wa kiislamu kama wa Ujiji, Pangani, Horohoro au Musoma mjini mpaka maskini wakaamini wao ni mfumo umewanyima fursa ya kuwa na Mudio Islamic kama yenu. By the way watu kama wanataka kuendesha biashara zao nje ya taasisi kama bakwata tatizo liko wapi? Wakiristo wangapi wana mashule yakaitwa St. Fulani na wala hayana uhusiano na Makanisa au madhehebu yao. Bakwata is not a big deal. In fact huenda Bakwata pia ni victim wa "do-nothing" syndrome. Kesho Bakwata ikifa AMINI bado waislamu wataunda tena taasisi ya kuwaleta pamoja kwa namna yoyote ile. Kadogoo hakuna mtu asiyetaka quality. Ndio maana wanatoka Uganda kuleta watoto hapo Mudio. Hata wanaopanda majukwaani kumlaani Mkapa/Nyerere lazima wanapeleka watoto kwenye mashule mazuri, asikudanganye mtu. Mtu akikwambia watoto wa kiislamu hawana akili mpeleke polisi, kakutukana. Dini haina uhusiano na akili. wayahudi, Wachina, wahindi, wajapani wengi kabisa sio waislamu wala wakiristo. At some point baadhi yenu mtoke humu JF mwende kuongoza bakwata, kuilaani tuu na kuwaita vibaraka endlessly sio tiba. Huenda nyie mkaiboresha.
 


Maskini Wa Fikra,Pole sana..
Kwahiyo unajiona umeandika au umefanya uchambuzi wa maana??
Kikubwa kinachojionesha hapo ni mwendelezo wako wa kufia dini huku unajificha nyuma ya kivuli chako..
Nilienda Mliman City Jana na kufanikiwa kununua kile kitabu cha ngano zako za mapenzi,umejitahidi sana...
Nadhani uwanja ule na kukipigania chama chetu cha chadema unakufaa sana..
Huku kwa kwa kweli unazid tuh kujidhalilisha,sisi hatutachoka kuipandisha (......) juu ili kuilinda heshima yako..
 

Mwanakijiji,this is Good. Kumbe Kleist alikuwa na interaction nzuri na "mission-educated" Aggrey!!!! I can feel BIG SHOW on the screen looking for spelling mistakes!!!!!! hahahahahahah....
 
Mzee Mwanakijiji hata mimi kitabu cha John Iliffe ninacho na kila wakati Mohamed Said anapohubiri uongo wake kuwa muasisi wa AA ni Kleist Sykes, nabaki mdomo wazi! Lakini la kushangaza zaidi ni ule ujasiri wake wa kujaribu kutetea huo uongo humu JF...sijui anawachukuliaje wasomaji wa JF! Of course wapo kina Kadogoo watakaomfuata wakipiga makofi hata kama anawaelekeza shimoni, hilo sikatai, wapo, ila upofu wa kidini umewatanda kiasi hawawezi hata kufungua macho watazame wanakoelekea...this is really sad!

Mohamed Said lives and thrives by taking advantage of the disadvantaged, yes the disadvantaged, and they will gobble whatever he hands out to them. The guy has been doing this for, well, over 15 years and the only reason he always got away with it, is because his listeners, the always gullible and trusting, never took him to task. Each year he grew bolder and bolder in his assertions until one unlucky day, he got the nerve to venture into the JF atmosphere, the Great Thinkers den...am sure now he is getting his fair share!

Anaposema wapo wazee wake walisahauliwa sijui ni nani hao alitaka majina yao yaingizwe ndani ya hicho kitabu; Hicho kitabu kingekuwa na kurasa ngapi? Kama yeye aliwataka wazee wote wa mitaa ya Gerezani, Kipata, Udowe, Idrissa, Mkunguni watajwe, ni Mtanganyika yupi ingekuwa sawa akiachwa; wa Tarime? wa Kibosho? wa Kilwa? wa Tandahimba? wa Tunduru? wa Kibondo? wa Kaliwa? wa Ntuzu? wa Malampaka?, wa Ngara? wa Uyole? wa Nansio? wa Arumeru? wa Kongwa? wa Ludewa? wa Misenyi? wa Kiteto? wa Misungwi? wa....nachoka!
 
Kadogoo, Wickama,

..nadhani mwamko wa elimu ktk maeneo hayo ndiyo uliopelekea bakwata na taasisi nyingine nyingi kujenga shule huko.

..labda nikuulize; Bakwata mkoa wa pwani wana shule ngapi za sekondari, na wamezifungua lini? Kwa uelewa wangu mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa yenye shule kongwe za sekondari za Bakwata.

..kuna jamaa yangu alinitonya kwamba, Kilimanjaro kulikuwa na shule ya misheni wakati wa mkoloni. Baada ya uhuru wazazi wakawa wanataka shule ya sekondari. What they did, ni kuikabidhi shule hiyo kwa Bakwata ambao walianzisha shule ya sekondari !! sasa tell me if that can happen ktk maeneo ya pwani.

..Shule za Bakwata zilizoko Kilimanjaro zinatia aibu kwasababu taasisi hiyo haina FUNDS za kutosha, pamoja UTAALAMU wa kuendesha shule hizo. Mimi nadhani wakiwezeshwa wanaweza kuwa wanatoa products nzuri tu.

NB:

..Nimeangalia matokeo ya Kirinjiko nimekuta wamefanya vizuri kuliko baadhi ya shule za misheni.

..Kwa kweli wanastahili pongezi kwa kuonyesha mfano kwamba INAWEZEKANA!!

..Sasa tunataka Feza na Kirinjiko zisambae kila pembe ya Tanzania.

cc: gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…