Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ngoma inogilee,sindimba imepamba moto..
Mwanakiijiji amehamia kwenye makabila sasa..
Kweli mfa maji haachi kutapa tapa,enhe sasa atueleze takwimu hizo uwiano wake ukoje?
Wapi kapata takwimu hizo,au ndio histohisia zake?

The Big Show,

Salaam.

Mwanakijiji hajajibu hoja zangu kwa kina kama dasturi yake lakini tuendelee na mnakasha. Unaona jamaa sasa wametufunza wenyewe ukosefu wa adabu na leo tumekua mastadi ati wanalalama? Waswahili wanena; ukangia mji wa vipofu fumba lako jicho,nasi inatulazim.

Ati jamaa sasa pamoja na sifa zoo
te zile chafu pita kiasi imeongezwa kuwa Sheikh Mohammed Said ana wafuasi ambao ni sisi na wale woote kila wanaomkubali hoja zake. Tunaambiwa tuna chuki,wadini na hatuna uzalendo!ahaha!!

Kwa sasa hapa hakuna tena darsa wala Ilm naona zogo limetawala mno,na fouls ni nyingi lakini jamaa tunajua wao hapa ni uwanja wao wa nyumbani.

Jamaa wametoa adress na biography zao saana,tumejaribu kuwajuza inakua tabu ileile? Lakini nahisi pana tafauti pia ya matumizi ya lugha.

Ile habari ya kutaka kutia fitna baina ya Waislamu kwa maeneo na mila tafauti,imetumika saana hapa jamvini. Nashukuru ilipewa jawabu murua na Kadogoo. Jamaa sasa wanatumia hila za character deformation ili wapate sympathy za baadhi ya watazamaji!ahaha!!

Salaam Sheikh Mohammed Said mpe saana ahsanta kwa ile Historia ya Zanzibar,alotia hapa kiduchu leo.

Ritz;ile habari ilikua ni wewe!?...nafikiri umenifahamu!? Nijulishe tafadhali.

Cc; Ritz,Kadogoo,Boko Haram,Ami
 
gombesugu kwa mipasho na story ndeefu. Wakati mwingine hata huelewi hoja anayotaka kuijenga.

Nakusamehe,kwanza nahisi hiki Kiswahili si lugha yako ya awali na pili yaelekea hufuatilii huu mtiririko unavyokwenda. Hayo ilikua tu ni majibu machache kwa yale yalotajwa na baadhi ya jamaa zako.

Wenye ujumbe wao nina hakika wamefahamu,na wewe tuendelee na mnakasha. Au unatafuta sababu ya kuniadhiri zaidi!?
 


Na hujalazimishwa kuamini,,
Kipi kinachokufanya ukeshe hapa kama umeamua kuipuuza si uipuuzee?
Bila shaka moyoni mwako unakiri uhalisia huu..
 



Naam,sisi tushazoea kejeli zao,
Na ni wao wameamua kutuchagulia upande wa kuegemea,na upande wenyewe ni huu wa Moh Said,mimi naona wametupendelea sana kutuchagulia upande huu,yani kama ni football team na mpira wenyewe ndio historia basi Moh Said namfananisha na Barcelona,anaichambua historia kama anacheza mpira wa Samba wa kibrazili au hangaisha ----- ya wakatalunya spain,huchoki kumsoma kama vile usivochoka kuitizama Barcelona ikicheza,Bur'dani sana..
 
Platozoon,
Asante kwa hili. Barubaru ana tabia ya kutumia uwongo kujenga hoja zake. Nyirabu alimaliza BA Makerere mwaka 1963 akiwa na honours katika uchumi. Miaka miwili baadaye alienda kusoma Cambrigde University, Mass. alipopata M.A. katika uchumi akawekwa Dev plan chini ya waziri Bomani. Niambie ni nani katika miaka hiyo ya 62-66 aliyekuwa na M.A. ambaye hakupata cheo katika serikali ya Tanzania. Nyirabu hakubebwa hata kidogo, hata kwa ukabila. Warioba ni Mwikizu. Lakini kwa watu kama Barubaru that does not make a difference. Mwambie aendeleze uongo wake kule Zanzinet. Hapa tutamuumbua tu.
 

Acha uwongo wako hapa. Angalia jibu nililolitoa kwenye thread ya Platozoon. Kuteuliwa kwa Warioba na Nyirabu kulifuata merits na wala si ukabila.
 
Ndugu yangu naona jinsi gani nilivyo zimwi katika ndoto zako. Hakuna unachoandika bila kuhakikisha unatumbukiza Nguruvi3.
Mimi ahdi tyangu ni moja, kutomuonea mtu au kumuonea haya. Natumbukiza kisu hadi kigonge mfupa sheikh, ushanfahamu.

Hivi nikikuambia familia yangu ni ya Mndolwa hiyo inasaidia nini katika mnakasha. Tanga nyumbani kwetu. Tena waijua mjni, mimi kuanzia Magoroto, kicheba, mtindiro, mjasani, pongwe, Lusanga, magunga, Mnyuzi, Tengeni tena hapo daah hata usiseme, bonde Muheza nyumbani usinitoe machozi kijana wee! Unaijua barabara ya 10!

Hebu tuendelee na mnakasha maana tutasema mengine na wengine kupatwa na fadhaa kama si soni.
 
Jasusi,baada ya jitihada za kumdhalilisha Nyerere kwa nyumba za kula, kuomba vitoweo, kuvaa suruali kugonga mwamba sasa zinatafutwa hoja za kuokota tu.

Namshangaa sana Barubaru, huyu kasoma na Dau na Warioba eti halafu anaamini kuwa Warioba alibebwa kutoka machungani akiwa na kata mbuga kuja kuwa waziri mkuu.

Maana hakuwa na credential wala hakujulikana kasema Maalim Mohamed, basi tunabaki kubuni na kubabaika babaika tu kuwa Nyerere kamzoa wakati akiwa na Ng'ombe wake! Sijui kama nitakuwa nimekosea maana hakujulikana na alikuwa hana credential kabisa.
Unless awepo wa kutueleza upya Warioba alikuwaje waziri mkuu akiwa hajulikani na hana credentials!
 
gombesugu kwa mipasho na story ndeefu. Wakati mwingine hata huelewi hoja anayotaka kuijenga.

Wanaukumbi,

Naomba tujikumbushe baadhi ya mambo huenda tukajenga fikra zetu upya na kwa utulivu:

Tanganyika Kama Nchi Chini ya Udhamini waUmoja wa Mataifa


Mwanzowa Siasa Katika Tanganyika: 1950- 1954

Tanganyika African Association: 1950-1954

Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA: 1951- 1954
Baadaya Vita Vya Pili Vya Dunia Uingereza ilikabidhiwa Tanganyika chini ya kifungu76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingerezailitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii yaTanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo.

Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe yakikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwawengi na wenye nchi. Wakati Wazungu na Wahindi walikuwa na jumuia zao kuendeleza maslahi ya watu wao katika Tanganyika, Waafrika walikuwa hawana uwakilishi wowote.

Wazungu walikuwa na European Association na Wahindi walikuwakilishwa naIndian Association. Vyote viwili vilishugulika na watu wao wenyewe. LakiniWaafrika hawakuwa na chama kama hicho kuwatetea. Katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika waliwakilishwa na mmishionari Mzungu jina lake Father Gibbons, aliyekuwa akifanya kazi Misheni ya Minaki maili kadhaa nje ya Dar es Salaam, Mzungu huyu hakuwa na uhusiano wowote na Waafrika aliokuwa akiwawakilisha na akikaa Minaki Misheni nje ya Dar es Salaam.

Kwa ajili hii Waafrika walipohisi hawawakilishwi na hawana chama kama kile cha Wazungu na Waasia kutafuta haki zao, walikutana na kuamua kuunda chama chao wenyewe. Gavana wa Donald Cameron ambae alitawala Tanganyika kuanzia mwaka wa 1925 hadi 1929 ndiye aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria la kwanza katika mfumo wa "IndirectRule."

Gavana Cameron hakupinga kuanzishwa kwa African Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929 ila aliiasa kuwa chama kisijiingize kabisa katikasiasa. Vipi sasa Waafrika wataikomboa nchi yao ikiwa hawaruhusiwa kufanya siasa?

Waafrika vijana waliotoka vitani na vijina wasomi waliomaliza elimu yaMakerere College Uganda hawakukubaliana na msimamo huu wa kujiweka mbali na siasa. Mwaka 1950 vijana hawa walifanya mabadiliko makubwa katika Tanganyika African Association (TAA) kama ilivyokuwa ikijulikana baada ya kubadilisha jina mwaka 1948

Katika uchaguzi uliofanyika Dar es Salaam Dr Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes walichaguliwa rais na katibu. Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wakushughulikia hali ya siasa.

Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi.
Jambo la kwanza lililofanywa na uongozi huu mpya mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyokuwana wajumbe hawa wafuatao: Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa Mufti wa Tanganyikana Zanzibar; Dr Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwaLiwali wa Mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando.

Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kwa kipindi cha miaka ishirini namoja African Association ilifanya kazi chini ya katiba isiyokuwa ya siasa. Kwa mara ya kwanza mwaka 1950, TAA chini ya uongozi mpya, ilijipa hadhi ya chama cha siasa, siyo kwa kubadilisha katiba yake lakini kwa kuunda kamati ya siasa ndani ya chama.

Kamati hii ilikuwa na watu wenye kuwakilisha maslahi na uwezo tofauti, wakiwa halikadhalika wanatokana na uzoefu na hali tofauti. SheikhHassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye Mufti wa Tanganyika na aliwakilishaWaislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali.

Nyuma ya Sheikh Hassan bin Amir walikuwa masheikh, makhalifa wa tarikambalimabali na Waislam wote kwa ujumla. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo waDar es Salaam na vitongoji vyake.

JohnRupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wachama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza, na aliyejulikana kwa misimamomikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere. Alikuwapo Abdulwahid Sykes, mfadhiliwa chama ambae baba yake ndiye alikuwa katibu muasisi wa African Association.

Baadaya kuunda kamati hii, Abdulwahid akiwa kama katibu alianza kuyaandikia matawiya TAA nchi nzima kuyahuisha. Jambo kubwa lililokabili TAA ilikuwa ni hadhi yaTanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa. TAA alimuingiza katika ile kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba ili iwezekukabiliana na serikali ya kikoloni.

Seaton alitakiwa kuishauri TAA jinsi yakuliendea shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru Tanganyika ijitawale yenyewekwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhanini wa Umoja wa Mataifa. Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilituma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika mwaka wa 1948 kuja kukagua hali ya siasa ya Waafrikakama wanaweza kukabidhiwa madaraka ya kuendesha nchi yao.

Lakini hakuna jambololote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo. Lakini ilikuwa wazi kuwakuanzia mwaka 1950 Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dr Kyaruzina Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa ilikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito na ilikuwa imejiwekea lengo.
Uongozi wa chama cha TAA ulipata changamoto yake ya kwanza kupitia Constitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba) iliyoundwa na Gavana Edward Francis Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru.

Gavana wa wakati ule Edward Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamiina ''Native Authorities'' watoe mapendekezo vipi Tanganyika itawaliwe.

Kamati yasiasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wotewa kamati ya siasa. Sheikh Hassan binAmir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.

TAA Ilitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrikayalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria. Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli hoja na kwa takwimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Memorandum ya TAA kwa Constitutional DevelopmentCommittee ambayo Pratt iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu. TAA ilipendekez akuwa ndani ya Baraza la Kutunga Sheria Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka kumi na mbili na baada ya hapo wajumbe wachaguliwe kwa kupigiwa kura.
Gavana Twining iliyapuuza mapendekezo ya kamati ya TAA. Serikali iliendelea na mipango yake ya muda mrefu ya kuwaimarisha Wazungu na Waasia waliokuwa wachache na kuwasukuma kando Waafrika kinyume kabisa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zilizokuwa chini ya udhamini.

Waafrika wengi walionelea kuwa mapendekezo ya TAAndiyo yangekuwa msingi wa katiba ya baadaye ya Tanganyika kama jamii ya watu wa rangi zote. Hata hivyo moyo wa mapendekezo yale ya TAA haukufa.

Mapendekezo yale yaliletwa tena katika mkutano wa kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai, 1954. Mapendekezo hayo ndiyo baadaye yalitiwa katika hotuba ya Julius Nyerere aliyoisoma mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, mwezi waMachi, 1955.

Baada ya mapendekezo ya TAA kukataliwa, uongozi wa TAA Makao Makuu ulielekeza nguvu zake zote katika kuimarisha matawi katika majimbo na kutafutamawasiliano zaidi na Umoja wa Mataifa la kutaka kutambulikana.
Juhudi hizi zilizaa matunda kwa sababu Umoja wa Mataifa ulianza kuiletea TAA taarifa na majarida kuhusu mambo mengi ya kamati zake tofauti. Kufuatia mwamko huu wa chama, serikali ilishtuka na ikaanza kuingia hofu, ikaamua kumpa uhamisho Dr Kyaruzi, rais wa TAA, kutoka Dar es Salaam kwenda Hospitali ya Gereza laKingolwira karibu na Morogoro.

Serikali ya kikoloni iliamini kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza kasi ya TAA katika uwanja wa siasa. Serikali ilidhani kwa kumtoa Dr Kyaruzi Dar es Salaam, jambo hilo lingedhoofisha uongozi wa TAA pale makao makuu. Lakini Dr Kyaruzi hakuzuiliwa na huo uhamisho.

Kila mwisho wa juma alisafiri kuja Dar es Salaam kushauriana na Abdulwahid. Serikali ilipotambua kuwa uhamisho huo haukuathiri chochote katika mchango wa Dr Kyaruzi kwenye uongozi wa TAA, alihamishwa tena kutoka Kingolwira hadi Nzega mbali kabisa na Dar es Salaam.

Katika mkutanio mkuu wa TAA wa mwaka 1951 katibu wa TAA Abdulwahid aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu. Abdulwahid aliwataarifu wanachama kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu na wanachama walijulishwa kuwepo katikachama mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA.
Wanachama walijulishwa mchango wake katika kutayarisha mapendekezo ya katiba yaliyowasilishwakwa Gavana Twining. Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria.

Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki. Vilevile aliwaeleza kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya India. Abdulwahid alieleza kwa ufupi juu ya kuundwa kwa African Parents Association kwa msaada wa Dr Raymond na European Parents Association.
Katika safari yake ya Nairobi Abdulwahid alikutana kwa siri na Jomo Kenyatta nauongozi wa juu wa KAU lakini hili halikuweza kuwekwa bayana.

Mwaka wa 1950 utaingia katika historia ya Tanganyika kama wakati wasomi wa Makerere,waliingia TAA kwa wingi sana. Wote walikuwa vijana na walitaka kufanya mambomengi kwa haraka na kutimiza kila kitu mara moja. Migongano katika mawazo na mbinu za siasa hayakuwa mambo mageni.

Lakini migongano hii ndiyo hasa ilikuwakichocheo cha kuendesha utawala mzuri katika chama. Taarifa ya katibu ilieleza mafanikio na matatizo ya TAA. Ofisi ya TAA haikuwa na umeme na aliwaelezawanachama mipango ya kuingiza umeme, kufungua maktaba ndogo na kuanzisha masomo ya usiku kwa watu wazima.
Hatimaye taarifa ilizungumzia juu ya ukomunisti na uhusiano kati ya watu wa rangi mbalimbali. Taarifa ilitahadharisha dhidi ya taathira za ukomunisti katika siasa za Tanganyika na ilihimiza ushirikiano baina ya wanachama wa TAA na watu wa mataifa mengine.

Wakati huo baadhi ya viongozi wa TAA walikuwa wakifahamikakwa misimamo mikali. Miongoni mwao alikuwa Stephen Mhando na Hamza Mwapachu.Wakati huo Mwapachu alikuwa akiandika katika ''The Sentinel,'' jarida la Fabian Society lililokuwa likichapishwa London.

Hawa Fabian walikuwa wana mrengo wa kushoto katika Labour Party ya Uingereza. Wakati ule kulikuwa na machifu wengi katika Baraza la Kutunga Sheria na katika hao aliyekuwa mashuhuri sana wote alikuwa Chifu Kidaha Makwaia wa Shinyanga.

Chifu Kidaha ndiyo kwanza alikuwa amerudi kutoka Uingereza masomoni. Mara tu aliporudi alitoa hotuba kali katika Baraza la Kutunga Sheria, akiiasa serikaliya kikoloni ibadilishe msimamo wake wa kuwapiga marufuku wafanyakazi Waafrikas erikalini kushiriki katika siasa.

Machifu wengi wakati huo walikuwa na hofujuu ya TAA na uongozi wake uliokuwa ukiibuka kwa kasi. Waliiona TAA kama tishio kwa mamlaka yao.Serikali ya kikoloni katika utawala wake wa ''indirect rule'' ilikuwa inawatambua machifu na sio African Association kama wakilishi wa maslahi ya Waafrika.

Ilikuwakatika kipindi cha uongozi wa Abdulwahid ndipo alipomwendea Chifu KidahaMakwaia na kumuomba achukue uongozi wa chama kama rais. Abdulwahid alimwambia Chifu Kidaha kuwa endapo atachukua uongozi wa TAA, kwa kuchukua kwake uongoziwa Waafrika, angekua amefungua dimba la mageuzi Tanganyika kwa sababu machifu wengine wangemfuata.

Kidaha alikuwa chifu aliyependwa mno na serikali ya kikoloni, kwa ajili hiyo hakuweza kwa wakati ule kuona busara ya kukubali ombi hilo. Pamoja na kauli aliyotoa kuhusu watumishi Waafrika serikalini waruhusiwe kushiriki katika siasa, kauli ambayo huenda ndiyo iliyofanya uongozi wa TAA kumuomba achukuwe uongozi, Chifu Kidaha aliuamini uchifu na ushirikiano wakaribu na serikali ya Kiingereza kwa kupitia "indirect rule."

Chifu Kidaha hakuwa tayari kuweka rehani nafsi yake na na maslahi ya watu wake kwa kukiunga mkono chama kilichokuwa kinapinga ukoloni. Hii ndiyo ilikuwa hali ya siasakatika Tanganyika wakati viongozi wa TAA walipokuwa wanajitayarisha kuunda TANU chama kilichokuja kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.
 

Its true what Americans do is not fair, abuse of power. Wanajifanya ndo polisi wa dunia, wana impose sunctions on countries ambapo mwisho wake inawa affect watu wakawaida na kulazimisha nchi zisishirikiane na nchi nyingine, just because they said so.

But then this is purely politics and protecting its interests.

Kwenye hili la bad and terrorist, hakuna kitu kama hiko.

Hakuna good terrorist hata siku moja, no matter what interest ana serve. Hata akiwa katumwa na Pope, i will still rebuke the act and Pope.

Terrorist is a terrorist, Period. The mayhem atakayo cause can never be good, akiua watu, there will be vilio in some families, there will children taken from their parents, parents from their children... Ni vilio na simanzi.
This act can never be good or holy hata siku moja. Not in the right mind.

Al qaida, Al shabab, Boko haram wao wenyewe wakishafanya ugadi wanasema and claim the act in the name of uislamu. And that how people will look at them.

But we all know Uislamu has nothing to do with their act, Uislamu does not condone killing of innocent people, uislamu utawakana siku za mwisho na watashangaa.
 

gombesugu,

Kwa kweli nikisoma bayana zako humu jamvini walaahi najisikia murua raha mstarehe.

Hawa ndugu zetu wanasema tusitumie neno "sisi" au "nyie" wanasema siyo uzalando wakati huo huo hao wanaotoa kauli hizo ndiyo wanaotuita sisi wafuasi wa Mohamed Said na wale wote wanaopingana na fikra za Nyerere.

Kwa maana hivyo hawa wote ambao ni Wakirsto ni wafuasi wa Nyerere. Sisi watu wa madarasa akili zetu na fikra zetu zinafanana kama machinas..ha haa haa.

Kuna jamaa mmoja humu yeye alienda mbali zaidi akasema kuwataja hao wazee wa kariakoo humu jamvini kwake ni matusi makubwa huyu huyu ndiye anatoa darsa kwa Waislam, ha ha haaa.

Kuna mwingine yeye bingwa wa tambo na majingambo anawaita wazee wetu "mwanameka" yeye anaita kukata kisu na mfupa, ha haa ha.

Karibu sana mie napata uji wa shurba na mkate wa ufuta.
 
Last edited by a moderator:
Unanikumbusha mambo ya Rostam Aziz/Lowasa na Urais wa Jakaya wetu. Kwa hiyo Abdu wako alikuwa "KingMaker", akisaidia kwa hali na mali ili Mwalimu awe Rais wa TANU na baadae Tanganyika! Kishindo wala hakipo labda kwa ambao hawakumfahamu Mwalimu. Akili kubwa sana ya Mwalimu isingeweza kuongozwa na akili ndogo ya standard 10 ya Abdu!
 

Nilipo Blue.

Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.

Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.

Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.

maa salaam
 
Yericko,
Sivijui visa hivyo.

Ningependa kuvisikia.

Kabla sijakupa visa hivyo, hebu chukua hii kwa faida ya vizazi vyako Shehe wangu,



UCHUMI WA DUNIA CHINI YA FIKRA ZA KIGAIDI Suala la ugaidi kwa kiasi fulani, limeonekana kujitenga na dhana ya uchumi duniani hususani katika bara la Afrika. Amerika na baadhi ya nchi pale Ulaya ndizo zilizo athirika kiuchumi. Marekani walilazimika kuwekeza katika ulinzi huku wakiacha sekta muhimu ambazo ni uti wa mgongo wa taifa hilo zikidorora kama vile elimu, afya, ajira, viwanda, kilimo na miswaada mingi yenye mwelekeo wa mageuzi kiuchumi. Hali kadharika Uingereza na mataifa mengine washirika.


Kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kulileta mageuzi makubwa katika uchumi wa Tanzania. Tanzania inajivunia kuwa ni moja kati ya nchi za mfano wa maendeleo barani Afrika tangu ikumbatie sera za soko na uchumi huria kutokana na kupigwa mwereka kwa Azimio la Arusha la 1967 na Azimio la Zanzibar la 1992. Takwimu zinaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa kasi nzuri kwa kipindi kifupi. Kwa mfano mwaka 1996 uchumi ulikuwa kwa asilimia 4.2, mwaka 1999 asilimia 4.7, mwaka 2001 asilimia 5.7, mwaka 2002 asilimia 6.2 nakufuatia hali mbaya yahewa mwaka 2003 kasi ya ukuaji wa uchumi ilipungua na kukua kwa asilimia 5.6, mwaka 2004 ulipanda tena asilimia 6.3.

Kwaupande mwingine mfumuko wa bei umeshuka kwa kasi sana. Ulishuka kutoka zaidi yaasilimia 16 desemba 1997 na kufika asilimia 6.0 Novemba 2000 na kushuka zaidi hadi kwenye asilimia 4.5 kwa wastani hadi 2005. Hii tena ni dalili njema kabisa kwakuwa hakuna atakayependa kuwekeza katika uchumi ambao mfumuko wa bei unakimbilia asilimia 100. Lakini dalili hii nzuri yakukua kwa uchumi inakwenda sambamba na kukua kwa tabaka la matajiri na masikini.

Ongezeko hilo limekuwa kwa kupindukia, Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 20% ya matajiri mwaka2001 ilitumia kiasi cha 44% ya matumizi yote ya kaya, ikilinganishwa na 43% ya mwaka 1991. Kukua kwa uchumi kunakoambatana na ongezeko la pengo la walionacho na wasio nacho kunaonyeshwa na kipimo kiitwacho GINI ambacho kwa Tanzania kilionyesha kuongezeka toka 0.34 mwaka 2001 hadi 0.345 mwaka 2005. Kadiri tarakimu hii inavyokua ndivyo pengo linavyozidi kukua.

Mfano: jamii ambayo mgawanyo wa pato unauwiano mzuri sana tarakimu hii hupungua nakuwa ndogo, na kwa jamii au nchi yenye mgawanyo mbovu tarakimu huwa kubwa sana. Matharani, tarakimu hii ikiwa 0 nikwamba wote mnagawana pato sawa, naikiwa 1 inawezekana mtu mmoja anakuwa na pato kubwa. Ninadra! Haijapata kutokea na haitotoke tarakimu hii iwe 0 au 1 kutokana na mageuzi ya kiuchumi huku ufisadi ukishika kasi katika dola nyingi duniani hususani Tz. Mfano, nchi za China na Norway ambapo kuna uwiano mzuri wa mgawanyo wa pato bado hawawezi kuwa na 0 au 1. Takwimu zinazotumika kujua pato la nchi kwa Tanzania, zinakinzana na ukweli wa pato la kaya.

Mfumo unaotumika kujua wastani wa pato la kila mmoja hupatikana baada ya kujumlisha pato la nchi na kuligawa kwa idadi ya watu wa nchi hiyo.Inamaana kwamba kila mwananchi anahesabika kuwa ni mmiliki wa.kilichozalishwa katika uchumi kwa mwaka huo. Dalili hii ya kukua kwa uchumi na pengo la masikini na matajiri kuongezeka, linaendelea kuumiza vichwa vya wanauchumi wengi duniani kwani tatizo hili si kwa Tanzania tu bali nchi zote zinazo endelea kukua.

Nukuu za wanauchumi maarufu dunia zinazoonyesha kutimilika:

John Maynard Keynes
wa Uingereza ananena yakuwa, "Yamukini pengo la masikini na matajiri likawa dhahiri kadiri nchi zinavyo endelea kukua".

Brentano Lujo
aliyezaliwa Aschaffenburg, Bavaria (Ujerumani ya sasa) "Inafurahisha na kusikitisha kwani kuna uwezekano wa kuongezeka maradufukwa umasikini kwa nchi zinazo endelea:.

Simon Kuzinets
mwanauchumi wa Marekani aliyezaliwa Kharkiv nchini Ukraine: "Mgawanyo wa pato hautakuwa sawia na huenda usawa ukaongezeka kupungua baadae kadiri pato lanchi linavyo zidi kukua".

Joseph A. Schumpeter
mchumi wa Kimarekani aliyezaliwa Triesch, Moravia (Jamuhuri ya Czech kwa sasa) "Katikati ya mwanga mwanana wa machipuko ya kiuchumi panaibuka zuio la tathimini, tatizo hili litastawi katika mataifa yanayoendelea".

Kwa Tanzania kinacholeta kanganyiko huu wa kutopungua umasikini wakati ambapo uchumi unakua ni kwamba ukuaji wa uchumi haujagusa sekta kiongozi ya kilimo. Sekta hii inayoimbwa kila siku kuwa ndio uti wa mgongo wa taifa letu. Licha ya sekta ya kilimo kuchangia kiasi cha asilimia 45 ya pato la taifa, asilimia 85 ya mauzo ya nje na kuajili asilimia 80 ya watanzania wote, ukuaji wa sekta hii umezorota kwa kipindi cha miaka ya karibuni.

Mfano sekta hii ilikua kwa asilimia 5.5 mwaka 2001, mwaka 2002 asilimia 5.0, mwaka 2003 asilimia 4.0, mwaka 2004 asilimia 3.8, mwaka 2005 asilimia 3.7 na mwaka 2006 asilimia 3.5. Hii inaonyesha kwamba vipato vya asilimia 80 ya waajiliwa wa sekta hii vimekuwa duni kwa miaka hiyo, hivyo kutia shaka kama umasikini unaweza kupungua miongoni mwa watu hao. Sekta iliyokua kwa kasi ni ya madini ambayo inaonyesha kwamba imekua toka asilimia 13.5 mwaka 2001 hadi asilimia 15.0 mwaka 2002 na asilimia 17.0 mwaka 2003. Sekta hii ni mpya na imekuwa ikipata wawekezaji wengi kwa haraka sana.

Tatizo kubwa la sekta kama ya madini hasa katika nchi za Afrika ambazo husafirisha madini ghafi ni kwamba haizalishi ajira zinazoweza kupunguza umasikini kwa kasi sambamba na ukuaji wa uchumi. Hii inatokana na ukweli kwamba madini ghafi husafirishwa nje ya nchi na kukatwa katika maumbo mbalimbali tayari kwa uuzaji. Hivyo sekta hii haina uhusiano wa karibu na sekta ya viwanda katika nchi zinazo zalisha na kusafirisha madini ghafi.

Pili ajira inayozalishwa ni ndogo kutokana na matumizi ya mashine katika uzalishaji wa madini hayo. Hali ya ardhi yetu si mbaya na njia pekee itakayo harakisha kupungua kwa umasikini wetu pamoja na kuongeza thamani ya madini ni kuwekeza katika kilimo. Fedha zinazopatika katika madini ziwekezwe katika kilimo ilikuwasaidia asilimia 80 ya watanzani walioajiliwa katika sekta hii. Hii ni changamoto kubwa kwa Tanzania kufikia malengo ya milenia ya kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umuasikini wa kupindukia ifikapo mwaka 2015. Ili malengo ya timie inatakiwa uchumi ukue kwa wastani wa asilimia 3.8 hadi 4.5 kwa mwaka, mpaka ifikapo 2015 Nimuhimu kutilia mkazo elimu itakayo wawezesha watu kujiajiri wenyewe,kwani hii ni njia rahisi ambayo inaweza kumkwamua mtu katika umasikini.

Bilashaka nchi nyingi za Asia ya Mashariki ambazo tunapenda kuiga namna zilivyoweza kukua kiuchumi kwa kasi ya ajabu ni kwamba ziliweza kuua ndege wengi kwa jiwe moja, ukuaji wa pato la kila mwananchi kwa wastani ulikua kwa kasi ya kutisha, wastani wa umri wa kuishi uliongezeka, kuongeza kasi ya elimu na upunguzaji wa umasikini kwa kasi. Waliweza kufanya hayo bila kufuata TORATI walizopewa na mabwana wa IMF na Benki ya Dunia. Walitilia mkazo elimu ya ufundi, utafiti na uwekezaji katika teknolojia sahihi. Ukuaji wa uchumi ambao hauwezi kubadili maisha ya watu masikini hautakuwa na mafaa yoyote. Utakuwa ni ukuaji wa uchumi kitakwimu zaidi kuliko kuleta maisha bora ya watu.

Hayo ndiyo tumekuwa tukishuhudia zaidi katika nchi nyingi za kiafrika na Latini Amerika ambapo takwimu huonyesha kuwa uchumi unapanda kwa kasi nzuri, lakini ukweli ni kwamba ukiingia kwenye nyumba ya mtu wa kawaida kunawaka moto. Ukuaji wanamna hiyo wa uchumi hunufaisha kundi dogo la jamii na kujikita katika ukuaji wa vitu vichache ambavyo huwa nafaida ndogo kwa jamii kubwa. Mf: sekta ya madini ikikua kwa faida kubwa ya mwekezaji, haitakuwa na maana kama watanzania hawafaidi matunda yake. Badala yake tunapewa viini macho vya wawekezaji kwa kujengewa shule na zahanati ambazo maranyingi huwa na lengo la kuwaduwaza wanavijiji na wanaotembelea migodi hiyo.

Kinachotakiwa ni maendelo ya kweli yatakayoletwa na ukuaji wa sekta hii kwa maana ya kodi za kutosha na gawio linaloonekana. Tusizugwe na wanayoipa jina la misaada ya milioni 200 kwa kupoteza mabilioni ya fedha zetu za madini na ajira ambazo kwakukata madini hapa nchini tungezipata. Kwaujumla ukuaji wa uchumi haujapunguza makali ya maisha ya watanzania walio wengi Tangu nchi yetu ifuzu kujiunga na kikundi cha nchi tegemezi zinazotembeza bakuli kila kukicha mwaka 1997 baada ya kuifurahisha Benki ya Dunia (WB) na Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) juu yauzingatiaji wa TORATI ya mashirika hayo mumiani, zaidi ya watanzania 50% ni masikini wa kutupwa wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (Poverty line) kwa matumizi chini ya Tsh 260 kwa siku, asilimia36% ni masikini sana, Wakati watanzania asilimia 14% ni matajiri wa kupindukia wanaoishi maisha ya anasa, wakimiliki mahekalu, magari ya kifahari na ya gharama kubwa na watoto wao kusoma shule za sifa ya kimataifa.

Hawa ndio wanaodhibiti uchumi na siasa ya nchi hii kwa gharama ya watanzania asilimia 86 walio nje ya kundi hili.


"VITA DHIDI YA UGAID
"

Na: Yericko Nyerere
 
Wanajamvi leo tumeingia page # 649,Mzee wetu Mohamed Said anaelekea kukubali makosa ya kitabu chake namwona hatu lugha anayoitumia si ile ya mwanzo ana weka tahadhari kubwa kabla hajachangia hoja si kama kule mwanzo.

Napenda kuwapongeza Mag3 Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Jasusi platozoom WildCard Wickama .......Kazi mliyoifanya si haba Mzee wetu Moh kajivunza mambo mengi hakujua Nyerere alishaingia Dar kabla ya mwaka 1950.Hakuwa anajua Nyerere alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 huko Tabora.Hakupenda wasomaji wake wafahamu Rais wa kwanza wa AA alikuwa Cecil Matola angetokea Gerezani angeandika page 10 kumwelezea uhodari wake,usomi wake ......Mzee wetu kwa maksudi alitaka kutudanganya kwamba Abdul Sykes ndiye aliyemtambulisha Nyerere katika siasa za Dar hakujua Nyerere alionana na Dossa Aziz mwaka 1945 bila shaka Abdul Sykes wakati huo hakuwa na ushawishi wowote na kama alikuwa nao basi ulikuwa hauvuki Gerezani.

Nasema tena nawashukuru sana kazi mliyoifanya ni kubwa na mnastahili nishani ya uraia wema uliotukuka.Uchambuzi na hoja mbali mbali hakika ni funzo kubwa kwa anayetaka kujifunza.
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi leo tumeingia page # 649,Mzee wetu Mohamed Said anaelekea kukubali makosa ya kitabu chake namwona hatu lugha anayoitumia si ile ya mwanzo ana weka tahadhari kubwa kabla hajachangia hoja si kama kule mwanzo.

Napenda kuwapongeza Mag3 Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Jasusi platozoom WildCard Wickama .......Kazi mliyoifanya si haba Mzee wetu Moh kajivunza mambo mengi hakujua Nyerere alishaingia Dar kabla ya mwaka 1950.Hakuwa anajua Nyerere alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 huko Tabora.Hakupenda wasomaji wake wafahamu Rais wa kwanza wa AA alikuwa Cecil Matola angetokea Gerezani angeandika page 10 kumwelezea uhodari wake,usomi wake ......Mzee wetu kwa maksudi alitaka kutudanganya kwamba Abdul Sykes ndiye aliyemtambulisha Nyerere katika siasa za Dar hakujua Nyerere alionana na Dossa Aziz mwaka 1945 bila shaka Abdul Sykes wakati huo hakuwa na ushawishi wowote na kama alikuwa nao basi ulikuwa hauvuki Gerezani.

Nasema tena nawashukuru sana kazi mliyoifanya ni kubwa na mnastahili nishani ya uraia wema uliotukuka.Uchambuzi na hoja mbali mbali hakika ni funzo kubwa kwa anayetaka kujifunza.
 
Last edited by a moderator:

Nanren,

Moja ya tatizo nililolibaini huko Tanzania ni watu kujigeuza mbuni yaani kuficha kichwa chini yya majani wakti mwili wote upo nje akidhani kuwa haonekani.

Nimebainisha hapo Juu kuwa Kuna mazuri ya JKN na mabaya pia. Hakuna anayepinga kuwa JKN ni
mmoja wa waasisi wa Tanu, Rais wa tanganyika na Tanzania pia. Sasa unapotolewa ushahidi kuthibitisha yeye ni mmoja wa waasisi na sio kinara katika uasisi tena kwa kupewa ushahidi madh'buti unakataa sijui unataka nini. Ikumbukwe kuwa Nyerere hakuwa na uenyeji Dar na hata tunapoambiwa nyumba alipofikia baada ya kuacha ualimu pugu alipewa kwa ufadhwili tu wa watu mnabisha.

nafikiri Nanren inabidi mfunguke hata kwa ushahidi wa mazingira tu. Nyerere hakuwa na pesa wala uenyeji wa Dar jiulizeni alikuwa anaishije ishije dar? hapo utaona kulikuwa na watu waliojitolea kumfadhwili. sasa anapotokea mtu kuachambua hao wafadhwili ambao wamesahaulika katika historia usipinge bali ingzeni katika historia yenu na sio kuficha kichwa mkidhani kuwa hamuonekani. Namshukuru Al Akhiy Mohamed Said kutujuza mengi ambayo tulikuwa hatuyajui pamoja na kuisoma historia ya nchi hiyo lakin hatufahamishwi na kufundishwa.

Binafsi nimekulia na kusomea Bara toka skuli ya msingi darasa la nne mpaka UDSM hivyo nimeona mengi na nimejifunza mengi sana na hata kuona huo ubaguzi sio tu nikiwa skuli lakin pia hata nilipokuwa kazini. nafikiri nimebainisha aibu walizokuwa nazo waislam waliosoma au kupata madaraka kuogopa kwenda kuswali nyakati za swala. Nimeyaona hayo nilipokuwa Serikalini na mwote nilimotembelea nikiwa kama afsa mwandamizi wa Serikali.

Lakin la udugu mimi nina jamaa wengi na marafiki wengi sana wakristo na hata mpaka sasa nalea watoto watano wa Driver wangu almarhum Julius Rweikiza (nilipokuwa RDD Mwanza) toka wakiwa darasa la kwanza wengine wadogo kabisa mpaka leo nimeshawaoza wote kabisa na harisi ya mwisho ilikuwa mwaka jana mwishoni ambapo nilikuja na familia yangu wote kwenda Bukoba. sasa sina chuki nao . Na siku zote nasikitika kusikia hilo ambalo mwanzo lilikuwa kama siri sasa ndio lipo hadhwarani.

Ushauri wangu kama ningekuwa kiongozi au Mtz ningeshauri mumeke tume ya makubaliano na maridhiano kuhusu hili la udini kwani hili mlipandikiziwa na wakoloni. Kumbuka kuwa Mkoloni alitumia divide and Rule katika kuwatawala. Katika Uganda na Kenya alitumia ukabila na katika Tanganyika alitumia UDINi kwa Tanganyika ilikuwa na makabila mengi sana ukilinganisha na kenya na Uganda.

msipozinduka na kulitazama kwa nia njema hilo litawaumbua kwani nao waislam wameshaelevuka na kujua haki zao ambazo zimekuwa zikiminywa na Serikali yenu kupitia Bakwata.

Nafikiri nitakuwa nimekujibu lakin kama utahitaji ziada basi Bismillah


 

Ngongo,
Naona vibaya kuja na maneno ambayo kwa wengine yanachoma.
Kwa ajili hii nitasema kitu kimoja tu.

Kama ni kutaka kusema kuwa Nyerere alisimama kwa miguu yake
mwenyewe alipofika Dar es Salaam na hakuwa muhitaji hii si kweli.

Hayo ya umaarufu kabla ya kutoka UNO Machi 1955 wala sitatia neno.

Ila jiulize kipi kilichofanya Tanzania ya leo impe Abdu na Ally Sykes medali
baada ya miaka 50 ya uhuru?

Kipi kikubwa walichofanya?
 

Ukweli unatabia moja kuu,

nayo ni KUJITENGA na UONGO.


Hatukuwa na maana ya kumdharirisha ama kumdhihaki ndugu yetu Mohamed Said, bali lengo kuu ilikuwa ni kuzuia upotoshwaji na uchochezi usio wa lazima katika jamii yetu MOJA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…