Sheikh Mohammed Said,
Salaam sana.
Hapa pana mambo mengi mno yenye kuleta rabsha kiduchu na vichekesho vingi. Nafikiri unakumbuka ile bayana yangu ya awali kwako,sababu nilichelea kuingia mambo kama haya ya udini,kutaja majina na kuwaadhiri jamaa zetu toka family mbalimbali tunazozistahi na mikanganyiko mingi saana,na matokeo yake tupo nje kabisa na hii mada/shutuma dhiki yako.
Imekua kama mtego wa panya sasa,anangia alokuwamo na asokuwamo!ahaha!!
Nimecheka pasi kiasi na yale majibu ulotoa kuhusu hiyo habari ya mmanyema mkristo. Nafikiri Sheikh Mohammed labda kitambo hujenda tembea pale Ujiji kuona "mabadiliko". Mimi binafsi pia pana pahala kwingi nahitaji nikatupie jicho Insha Alaah penye uhai na maajaliwa.
Hii habari ya makabila, ama kwa hakika imenichekesha kiduchu hasa ulipotaja Wangazija Wakristo. Unajua pale Comoro siku hizi pana wale "Wangazija pori" ambao huenda pale "kununua baraza" na kujinasibu Ungazija pasi kiasi. Ukizungumza na Bwana Ahmed Rajab atakuchekesha zaidi juu ya habari hizi.
Nafikiri hata ndugu zetu wa kiZaramo zamani nao walikua na dasturi na ustaarabu kama huo wa kukaribisha "wabweshu" na kuita "udugu wa khiyari". Tena walikua wakifanza na sherehe kubwa mno siku ya kutimiza huo "udugu". Napenda saana tamaduni na mapenzi yalokuwapo zamani baina yetu.
Sijui lini utapata fursa tuwekee na habari za mapinduzi ya Zanzibar,hasa wale wamakonde wa Kipumbwi,Ushongo na Sakura walotumiwa kuua ndugu zetu na kumuweka madarakani yule Mnyasa alokuja Unguja mtoto wa mgongoni(yaleyale ya Musharaf kuja Pakistani mtoto wa mgongoni halafu kuwafanzia watu hadaa). Ndugu na jamaa zetu wengi walitolewa roho na yule dhalim.
Uncle yangu Commando Amour Dougheish,ndo alokua akamkamate yule Mnyasa toka pale Ikulu na kumpeleka pale Idara ya habari - Rahaleo, halafu atangaze kuwa nchi isharejeshwa na imo mikononi kwa wananchi wenyewe. Wallahi,lile jambo mpaka leo najuta halikufanikiwa.
Basi Insha Allah tuendelee na mnakasha.
Ahsanta.
Kiongozi, tukubaliane kimsingi tu kuwa makabila na dini zetu hazina tija ktk mustakabali mwema wa Taifa na jamii zetu. Taifa na makabila yetu yana mchanganyiko wa ajabu sana, kusimamia hoja dhaifu kama "hakika hakuna Mmanyema, Mgoma, Mtongwe au Mkayamba Mkristo au Muislamu" ni hoja duni sana ambayo wajinga wengi huzisimamia na kutofautiana kiasi cha kuuana hata kama wametoka familia moja.
Hoja kama hiyo inapoibushwa na mtu mwenye elimu na umri wa Sheikh Said, ambaye ametengeneza wafuasi wengi ambao miongoni mwao hawana uwezo wa kuhoji lolote linaloibuliwa naye, wenye hekima lazima tuhoji, tujiulize lengo lake ni nini na kutoa majibu mwafaka hata kwa hoja yake dhaifu ili kuwapa ufahamu hata wale wajinga.