Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
- #13,161
Swahiba wamgu Mohamed Said na wafuasi wako mtiifu,
Huku mkiendelea kutafakari jinsi tulivyoyanyambua maandishi ya kitabu hicho cha kichochezi cha Mohamed,
Hebu burudikeni na ngano hiii kutoka
"Vita dhidi ya Ugaidi"
Kuyumba kwa uchumi wa Marekani, vita ndefu ya Iraq isiyokwisha, kuendelea kuandamwa na jinamizi la ugaidi, ukosefu wa ajira, vita kali ya kiuchumi kati yake na China inayoonyesha dhahiri kuwa vijana wa Mao Tse-tung wanapata ushindi. Hayo yanakuwa nikiashirio thabiti cha kutabiri anguko la dola mufilisi. Taifa hilo lililo ishika dunia pabaya na dunia ikaacha kumsujudu Mungu na kuisujudi Marekani tena kwakutembelea magoti kabisa.
Amerika imeshindwa kusoma alama za nyakati, kwani kwanza, dunia ilianza kushuhudia kunako karne ya 15 uwezo wa kidunia ukishamiri mitaa ya Ulaya, Kitendo hicho kilizaa dunia tunayoifahamu hivi sasa ya sayansi na teknolojia, biashara, ubepari, na mapinduzi ya viwanda na kilimo. Hapo ndipo mataifa ya Magharibi yalipotawala mlengo wa siasa. Hayo yalitosha kabisa kuipa jeuri Ulaya.
Pili ni mwishoni mwa karne ya 19 ambapo bila kutarajia Ulaya ilizima kama mshumaa!, wale wababe na mashujaa wa kuiendesha dunia kama Adolf Hitler,(Ujerumani) Francisco Franco,(Hispania) Benito Mussolini (Italia) nk, Hawakufua dafu mbele ya alama za nyakati na kilichotokea ni uwezo wa kidunia kuhamia Amerika. Kutokana na viwanda, kilimo na masoko makubwa Amerika ikajiimarisha vya kutosha, mpaka ikaanzisha kupindisha nadharia na muundo wa vyombo vingi vya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Benki ya dunia, Kituo cha biashara cha kimataifa, Shirika la afya dunia nk na kuviundia mfumo hodhi kwa mwavuli wa sheria ya haki miliki. Mfumo huu na sheria hii ndivyo vilivyo izima Ulaya,
Karne ya 15 mfumo na sheria hii vingekuwepo Ulaya ingalikuwa bado inameno tena makali. Tafakari mfumo huo na sheria hiyo ingekuwepo enzi hizo, leo Mlima Kilimanjaro, Ziwa Victori, Ziwa Tanganyika na vivutio vingi vilivyopo barani Afrika ambavyo inanenwa kuwa viligunduliwa na wazungu kutoka Ulaya japo Wachaga,Wasukuma na Wahaa waliishi katika maeneo yaliyo bainishwa hapo, tusitumie rasilimali hizo bila kibali cha walio gundua.
Na karne ya 21 kinachotokea ni badiliko kuu la tatu kiulimwengu. Dunia inashuhudia mtikisiko mkubwa wa kiuwezo ambapo inabashiriwa kuwa baada ya miongo mitatu tu vitabu vya historia juu ya Marekani vitafunikwa na kufunuliwa vya ukanda mwingine ambapo njozi zinaelekeza Mashariki ya Mbali. Wamarekani wanaona dunia mpya inazaliwa, ila wasiwasi wao ni mfumo wa uzaliwaji unaopangiliwa na mataifa ya nje na watu wa nje kabisa.
Matukio yaliyotokea ndani ya miaka nane kati ya mwaka 2000-2008 yanatanabaisha kuporomoka kwa dola hiyo mfano: Jengo refu kuliko yote duniani lipo Taipei (Taiwan), Kiwanda cha kutengeneza ndege kubwa kiko Ulaya, Binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani alipatikana mwaka 2007 Kilimanjaro (Tanzania), Katika orodha ya matajiri zaidi duniani Marekani ilibakiwa na wawili kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2007, Kamari inachezwa zaidi Macao China kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006,
Takwimu hizi zinaweza kuonekana kama za kipuuzi! Lakini, hicho ni kiashiria tosha, kwani miaka 15 nyuma Marekani ilikuwa kinara wa kila kitu duniani. Wakati dunia inaenda kwa kasi ya ajabu katika mageuzi mbalimbali wamarekani wamepigwa butwaa na kuacha Mashariki ya mbali wakienda sambamba na mageuzi hayo. Haiyumukiniki kama Marekani itakuwa akilini mwa mwanadamu baada ya miongo mitatu hivi, labda kwa bara la Afrika lisilojitambua kuwa nitajiri, lililopandikizwa mfumo musonge na sera mufilisi baada ya kukubali kufuata torati za mashirika mumiani ya kimataifa
Hayo ndiyo yaliyo iimarisha Marekani na kuwa taifa lenye nguvu duniani tangu karne ya 19 mpaka karne ya 21 ambapo dalili zinaonyesha safari ya kupokezana kijiti cha ubabe wa dunia inaenda sehemu nyingine. Baada ya uwezo wa kidunia kuonyesha dalili za kushamimiri na kuhamia kabisa pale Maashariki ya Mbali, kwa kufuata mtiririko wa alama za nyakati taswira ya dhahiri inaturudisha Afrika. Afrika panatabiriwa kuja kuwa mahali pa tamko kuu la kidunia katika nyanja zote baada ya miongo mitano.
Na Yericko Nyerere
Huku mkiendelea kutafakari jinsi tulivyoyanyambua maandishi ya kitabu hicho cha kichochezi cha Mohamed,
Hebu burudikeni na ngano hiii kutoka
"Vita dhidi ya Ugaidi"
DOLA YA AMERIKA YAWEZA KUANGUKA