Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kiongozi, tukubaliane kimsingi tu kuwa makabila na dini zetu hazina tija ktk mustakabali mwema wa Taifa na jamii zetu. Taifa na makabila yetu yana mchanganyiko wa ajabu sana, kusimamia hoja dhaifu kama "hakika hakuna Mmanyema, Mgoma, Mtongwe au Mkayamba Mkristo au Muislamu" ni hoja duni sana ambayo wajinga wengi huzisimamia na kutofautiana kiasi cha kuuana hata kama wametoka familia moja.
Hoja kama hiyo inapoibushwa na mtu mwenye elimu na umri wa Sheikh Said, ambaye ametengeneza wafuasi wengi ambao miongoni mwao hawana uwezo wa kuhoji lolote linaloibuliwa naye, wenye hekima lazima tuhoji, tujiulize lengo lake ni nini na kutoa majibu mwafaka hata kwa hoja yake dhaifu ili kuwapa ufahamu hata wale wajinga.
 


Inawezekana mwenzako anadhani MAJI MAJI WAR n etc zilikuwa ni vita vya kikabila,
Aje atupe darsa hilo,hata sisi tunasubiria kwa ham pia...
 
Ndugu yangu yaani nilipatwa na mshutuko kusoma kuwa balozi wa Marekani aliwahi kuhutubia bunge. Afadhali umelileta.

Mohamed Said, Balozi wa marekani alihutubia Bunge lini?

Pole sana ndugu ya Nguruvi3 kwa kupata mshutuko tumshukuru Allah akufanyie wepesi usije kupata maradwi mengine kama kiarusi na sukari haya yote yanaletwa na mshutuko.

Nakushauri siku ingine ukipata mshutuko basi kunywa vijiko vitatu vya asali mbichi.

Balozi Royall alihutubia bunge la Tanzania tarehe 15 May 2003.
 

Ni dasturi ya siku nyingi Makabila kudharauriana.
Mfano, Waha, Wahangaza, Warundi na Wanyarwanda, mtu asiye wa kabila lao huitwa Mnyamahanga, Wachaga huwaita Chasaka, Wagogo huwaita Wakonongo nk...

Lkn kwenye Imani ni tofauti sana, mtu huamua kuamini anachoamini, leo anaamua kumwamini ng"ombe kama mungu wake, kesho akaamini Jua au Mwezi kama mungu wake.

Kwa hoja za Sheikh Said na utavyoshangaa kukuta Wangazija Wakristo ambao utawaita Wangazija Pori nashindwa kukuelewa hao Wairaq na Wairan Wakristo.
 
Balozi wa Marekani hajawahi kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano; niko tayari kusahihishwa. Lini Balozi Royall alihutubia Bunge la Tanzania? ili tupitie hansard.

Mzee Mwanakijiji,

Unabisha tu kubisha sababu kasema Mohamed Said au unabisha ili unataka kufahamu.

Sasa nakata kisu kwenye mfupa usipende kuonga swiming pool na watoto wadogo chukua hii.

Balozi Royall alihutubia bunge la Tanzania tarehe 15 may 2003 na mada yake ilikuwa "Blood Money and Financing Terrorism."

Cc.. gombesugu, Kadogoo, Ami, Barubaru,
 
Last edited by a moderator:

Ritz,
Hivi hawa jamaa wanajua kuwa mimi nilipata mwaliko nikatoe mada Chuo Kikuu Cha Ibadan.
Hivi hawa jamaa hawajiulizi vipi nimealikwa mie...

Hivi hawa jamaa wanadhani mimi nitafunga safari na nisimame kwenye kilinge kisha niseme
maneno ya kutunga?

Laiti wangelikuwa si wachovu wa kufikiri hawakuwa hata na haja ya kuleta swali lile la Balozi
wa Marekani hapa jamvini.

Utafiti mdogo tu wangelipata jibu.
Naogopa kuwapa sifa yao kamili isijeonekana natumia lugha zisizopendeza.

Sishangai hadi leo wanashindwa kuandika hata kitabu kidogo cha historia
au pitio la kitabu changu kunipinga.

Wao wamekuwa kama Hakimu Nasoro Kiruka.
Maswali,mswali, maswali...
 

Wimana,
Unanipeka mbali sana.

Mwanamme wa Kimanyema akioa mke si Mmanyema basi ndugu zake
watamwangalia huyo mama kama ana tambo yaani ana kile kimo cha
binti wa Kimanyema.

Akiwa ana mwili mdogo watanong'onezana kusema, ''Kinyangarakata.''
Yaani, ''Ah si lolote.''

Udhaifu wetu wa kibinadamu.
 

Mohamed Said,

Wewe endelea kutoa darsa jikite zaidi kwa wasomaji wa huu munakasha kuweka bayana historia yetu ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo,

..wewe una kengeza la UDINI.

..kama sheria ya Ugaidi inawahusu Waislamu, kama unavyodai, kwanini basi Lwakatare na Ludovick wanashtakiwa kwa sheria hiyo wakati wao ni Wakristo??

..umejaribu kupotosha utetezi wa Tundu Lissu kwa Lwakatare.

JOKAKUU,

Swali hilo hata Tundu Lisu kaishangaa Serikali kumkamata Lwakatare kwa ugaidi wakati sheria hiyo inawahusu Waislamu tu!
 
Kuna wakati binadamu huwa tunapitwa na jambo fulani...Unaweza kunisaidia/kunikumbusha labda ni waislam wangapi hapa Tanzania wameshafikishwa mahakamani au wameshashtakiwa kwa kutumia hii sheria ya Ugaidi?

SWEKE,
Suala sio kufikishwa au kushtakiwa! suala ni kuwa kuna sheria ya ugaidi iliyopitishwa na Bunge la Tanzania kwa ajili ya Waislamu tu! sasa kama yuko aliyekamatwa au kushtakiwa hilo unatakiwa uiulize Mahakama!
 

kwani Mufti Issa bin Shabani Simba si Muislamu?????
 
Kilicho wafanya wamarekani wavamie Iraq ni hicho cha mafuta na wewe mwenyewe umejijibu.

Mundungus Fletcher;

Mbona Marekani isivamie Venezuela nchi ya Kikristo yenye utajiri wa mafuta! nchi hiyo ni adui mkubwa na Marekani lakini subutu!
 
gombe sugu nimekukubali mkuu! Umenibania shekhe wangu mwenye uelewa mdogo wa masuala ya uchambuzi wa kisiasa,yeye anajua 2 uislam ambao wao ni asilimia 26 tu ya nchi nzima.
 

Barubari, samahani naomba unijibu hili swali; ulimaliza shule ya msingi mwaka gani?

Mimi nilimaliza Shule ya Msingi mwaka 1985 na nilitumia namba!
 

AMI,
Wenzetu Kenya sheria hii ya ugaidi haikupitishwa na bunge sababu ya uzalendo na ushupavu wa wa Kenya wa kukataa kuburuzwa na Marekani! lakini hata hivyo Shekh Robo kauwawa kwa kupigwa risasi barabarani baada ya kushinda kesi ya tuhuma za ugaidi Mahakamani! swali la kujiuliza nani kamuuwa Shekh Robo?
 
Reactions: Ami
Wacha uongo wewe, kama hakukua na vita, akina Milambo ma Mkwawa walipanuaje milki zao za utawala? au unamaanisha nini unaposema hakukuwa na vita hapo zamani?

GWALIHENZI;

Kwa hiyo Nyerere ndie alikuja kupatanisha makabila yaliyokuwa yakipigana sio? au ulimaanisha nini?
 

MZEE MWANAKIJIJI;

Haya umepata jibu lako kuhusu Balozi wako! ndio ulitaka kusema nini vile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…