Nafikiri kiswahili tu hapo kina mapungufu lakin kuzungumza na wabunge katika semina ina nguvu sana kuliko kulihutubia Bunge. Kwani katika semina unapewa nafasi ya kuuliza masuala na hata kujadiliana kitu ambacho katika kuhutubia upati nafasi hiyo ya kuulizana maswali na mtoa mada.
All in all alisema na wawakilishi wa wananchi katika kufanya lobbing ili muswada wake wa Ugaidi upite kilainiiii.Poleni sana.
Barubaru inaweza kuwa wewe umeona kiswahili kina mapungufu pengine kwa weledi wako au kiingereza hakikueleweka kwa weledi wako.
Hakuna anayekataa uwepo wa balozi maeneo ya bunge kwasababu si yeye wa kwanza.
Kwa jinsi Mohamed alivyoiweka, wale watu wa Ibadan walishangaa kuona balozi amepewa hadhi kiasi hicho.
Labda unikumbushe, Dr Salimin Amour komandoo alihutubia lini bunge la JMT!
Wilcard amesema kuwa hana kumbu kumbu za balozi yoyote kuhutubia bunge na sikumbuki balozi yoyote.
Mohamed ameiweka hiyo akifahamu kuwa watu wa Ibadan Nigeria hawawezi kuwa na muda wa kutafuta taarifa za nchini kwetu ndogo kama hizo wakati huo akilenga kundi analolitaka la ''kumeza'.
Yeye amekubali kuwa taarifa hiyo aliipata mahali kadhaa na bila kuifanyia tahmini akaibeba kama ilivyo.
Kilichomsukuma ni utamu wa taarifa hiyo uliopelekea yeye kuibeba nzima nzima kwasababu ilikuwa ni sensational news.
Nikukumbushe kuwa huko nyuma Mohamed aliwahi kutueleza kuwa maulidi ya Tabora 1988 yalihudhuriwa na makamu wa Rais bw. Kawawa. Hapa napo alitaka kuonyesha umuhimu wa tukio hilo kwa kutumia jina la makamu wa rais.
Ndivyo alivyoitumia hotuba ya Rehani Waikela(moto wa waislam) ukiwaka katika kuleta hisia kwa kizazi hiki kuwa moto unaweza kuwashwa. Akazidi kumnanga Nyerere kwa kisa cha Warioba asiyejulina na bila credential kuwa waziri mkuu.
Hebu pitia alichoandika Mohamed na kule alikonukuu habari hiyo ya Ibadan.
Utaona wazi kuwa amepindisha ukweli kwasababu Mohamed anakijua kiingereza sidhani kama angelifanya kosa kubwa kiuandishi kama hilo. It was a calculated move to instigate the public.
Huyu ni mtafiti ambaye paper na vitabu vyake amevifanyia utafiti kama anavyodai na vimehaririwa kwahiyo vipo sahihi na si muhimu JF free for all kuvifanyia critic kama anavyodai.
Sasa hapa ndipo tunauliza, je, kabla ya kwenda Ibadan alifanya kautafiti kujua bunge letu linakaa wakati gani na lina taratibu gani katika uendeshaji wake! Hata forgery zina taratibu zake, huwezi andika cheque terehe 37 April 2013!!
Hili linakwenda mahali ambapo mtu atajiuliza, hivi yale yaliyoko kwenye shajara za familia ya Sykes yamechukuliwa kwa uadilifu na ukamilifu wake?
Kama haiwezekani kupata kumbu kumbu za mwaka 1988 au 2003 kwa usahihi, usahihi wa kile tusichokiona kinachosemwa ni ukweli mtupu unatoka wapi.
Hata pale alipoelezwa kuwa huenda ilikuwa semina, Mohamed kwa ima kutojua au kwa jeuri ya kuwa na vitabu katika vyuo mbali mbali alikuja kwa jeuri, bunge lilikaa tarehe kadha wa kadha!
Siyo suala la ubishi au kuchukua phrase moja na kuifanya mada, ni suala la validity and integrity za information zake ambazo hakuna shaka kuwa zinamuondolea msomaji yoyote mashaka juu ya maandiko ya Mohamed.