Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hapana si nyumba hii.

Nyumba iliyojengwa na Kleist na wenzake iko pale Mtaa
wa Lumumba.

Pale palipoandikwa "Hapa ndipo ilipozaliwa TANU 7 Julai 1954."

Katika mambo ya kusikitisha mle ndani hakuna kumbukumbu yoyote
ya wazalendo walojenga nyumba ile.

Historia yote imefutwa.

Katika kitabu changu ipo picha ya ufunguzi wa jengo lile mwaka1933.

Yuko Gavana Ronald Cameron, Kleist Sykes, Mashado Plantan, Mwalimu
Mdachi Shariff na wengineo.
 
Historia haijafutwa labda walisahau kuweka kumbukumbu
 

Mkubwa kuna uwezekano ukatuwekea hiyo picha hapa ukumbini.
 
Ni kweli hii ni historia ya wazee wangu.
Hili nalikubali siku zote halina shaka.
kuna hili mzee ms kuwa nyerere alikuja mshamba anavaa kaptula na wazee wako ndo walio mfundisha kuvaa suluali.
Je? Ni kweli? Huwa najiuliza mwalim kasomea uingereza kwa wavaa suti iweje aje afundishwe kuvaa na watu wa kariakoo?
 
Angeileta "historia" hii bila DINI za watu hawa, mzee huyu alikuwa amefanyakazi nzuri tu. Mwambie akubali kuondoa dini kwenye hawa waliosahaulika. Ni wengi na wa dini zote na kabila nyingi tu. Wala asisikie ukakasi kwa ukatoliki wa Mwalimu. Tuwe na DINI zetu kwa maisha ya nje ya dunia hii kama yapo!
 
kuna hili mzee ms kuwa nyerere alikuja mshamba anavaa kaptula na wazee wako ndo walio mfundisha kuvaa suluali.
Je? Ni kweli? Huwa najiuliza mwalim kasomea uingereza kwa wavaa suti iweje aje afundishwe kuvaa na watu wa kariakoo?
Kwani mtu akitaka kukutukana atakuchagulia tusi? Mwalimu alikuja Dar akiwa amesoma Makerere na Edinburgh lakini bado Kariakoo ya Kimanyema ilimbabaisha!
 
Hii picha mohamed said hawezi kuitafutia ujiko kama alivyozea maana inamsuta yeye mwenyewe...si ajabu alikuwa nayo lakini hakuitoa kwa sababu haionyeshi kutengwa kwa waislam na Nyerere mara baada ya uhuru...
Waislam wa mzee wetu Mohamed Said sio hawa waliofanyakazi na Mwalimu hadi mwisho wa UONGOZI wake. Mzee Mohamed anao Waislam wake ambao anadai Mwalimu aliwasahau. Anao Waislam wake ambao hawajawahi kuutumikia huu MfumoKristo wa Mwalimu. Hao ndio Waislam HALISI.
 

Ni changamoto kwako kuandika historia isiyokuwa na dini ya wazee wa sehemu tofauti ndani ya Tanzania na kuifunika kabisa historia ya Mohamed Said ambayo ina dini ya uislam fanya hivyo mkuu.
 
Ni changamoto kwako kuandika historia isiyokuwa na dini ya wazee wa sehemu tofauti ndani ya Tanzania na kuifunika kabisa historia ya Mohamed Said ambayo ina dini ya uislam fanya hivyo mkuu.
Wazee wa kunisimulia kama yeye alivyosimuliwa hawapo tena! Historia nilioisoma shuleni inatosha kabisa. Hata Mzee wetu huyu mtafiti sana ameshindwa kuibadili akaegemeza simulizi zake kwenye dini.
 
Wazee wa kunisimulia kama yeye alivyosimuliwa hawapo tena! Historia nilioisoma shuleni inatosha kabisa. Hata Mzee wetu huyu mtafiti sana ameshindwa kuibadili akaegemeza simulizi zake kwenye dini.

Kwa kweli narudia kusema mimi sina ugomvi na historia
uliyosoma shule ambayo unasema inakutosha.

Siwezi kukulazimisha usome historia nyingine.

Lakini ikiwa utabaki na historia hiyo utakuwa umepunjika sana.

Utapunjika kwa sababu kuna mambo mengi muhimu na ya kusisimua
katika historia wewe yatakupita.

Historia ya uhuru ilikuwa na ''drama'' zake.

Mathalan nafasi ya askari wa KAR waliopigana Burma kuja kuwa msingi
wa kuanzisha chama cha siasa.

Haya yalitokea 1938 -1945.

Mgomo wa makuli wa 1947 na nafasi ya Abdulwahid na AA katika harakati zile.
Mgogoro wa Ardhi ya Wameru na nafasi ya TAA Political Sub Committee.

Kuja kwa Nyerere 1952 na ule uchaguzi wa Abdu na Nyerere wa 1953.
Kuasisiwa kwa TANU 1954

Kuundwa kwa Baraza la Wazee 1955 na safari ya Nyerere UNO 1955.
Urafiki kati ya Mzee Mshume Kiyate na Nyerere.

Joto la Kura Tatu na ugomvi wa Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere 1958.

Mengi, mengi, mengi utayakosa.

Uchaguzi ni wako kubaki huko uliko au kutoka gizani na kusoma kile usichokijua.
 
Yote haya yameandikwa na watu mbalimbali ingawa sio kwa mfumo wa kuandika vitabu. Mengi nimeyasoma kama makala kwenye magazeti yetu na machapisho mbalimbali.

Mzee Mohamed, usidhani ni wewe tu uliyejaliwa kuyafahamu haya.
Mimi nimekunywa chai na Padre John Sivalon, M.M., mara kadhaa. Huyu pamoja na ukatoliki wake unaelekea kumkubali sana. Labda kwa kuwa ni mzungu, Mmarekani.
 
Kwani mtu akitaka kukutukana atakuchagulia tusi? Mwalimu alikuja Dar akiwa amesoma Makerere na Edinburgh lakini bado Kariakoo ya Kimanyema ilimbabaisha!

Hayo maneno yanasemwa sana lakini watu wanapoghadhibika.

Ni kukosa adabu na ustaarabu kutoa maneno kama hayo ya
kudhalilisha watu.

Kila mahali watu kama hao wasema ovyo huwezi kuwakosa.

Uniform aliyokuwa akivaa Abdu Sykes kama Market Master
pale Sokoni Kariakoo ilikuwa kaptula stockings na shati jeupe.

Waafrika wengi walikuwa wakivaa hivyo haikuwa kioja kwa Nyerere.
Lakini kama ulivyosema akutukanae hakuchagulii tusi.

Sasa nareja kwako.

Umeandika ukiwa na hasira moyoni kama vile mimi ndiye niliyokuwa
nafanya kashfa zile.

Hapa ndipo nisemapo jifunzeni utulivu katika majadiliano.
 

Haya ndiyo majibu ya nasaha nilizokupa?
 
Katika vitu ambavyo ninaweza kuvidhibiti sana ni hasira. Nikasirikie nini sasa! Haunifahamu, sikufahamu. Hata Mwalimu amefariki hanifahamu kabisa ingawa nilimfuatilia sana tu.

Nachukia mno mtu akileta masuala binafsi kama DINI kwenye mambo yetu sote kama hii HISTORIA ya TANGANYIKA. Mtu wa namna hiyo namwona kama aliyefilisika kwa hoja. Anatafuta "legitimacy" kwa nguvu. Anatafuta kuungwa mkono kwa njia yoyote ile. DINI, kokote ilikokomaa sana, hakuna AMANI.
 
Ni changamoto kwako kuandika historia isiyokuwa na dini ya wazee wa sehemu tofauti ndani ya Tanzania na kuifunika kabisa historia ya Mohamed Said ambayo ina dini ya uislam fanya hivyo mkuu.

Hawawezi kwa kuwa hawana hiyo historia.

Kuwapa changamoto hiyo ni sawasawa
kuwaambia Wachina waandike historia
ya ''holocaust.''

Sasa Wachina wataanzia wapi wakati
historia hiyo ni ya Wayahudi?

Ile historia ya uhuru wa Tanganyika
Allah alijaalia iwe ya Waislam.

Sasa si unaona matatizo haya?

Tovuti ya Baba wa Taifa inasema Nyerere
kaasisi TANU Pugu.

Mwanae anasema hiyo tovuti ni ya mitaani
haina uhusiano wowote na Baba wa Taifa.

Ana maana tovuti ya Baba wa Taifa inapotosha.

Inapotosha kweli lakini mbona mmekuwa kimya siku
zote?

Sasa swali la kujiuliza ni hili yaani Nyerere kakosa
hadhi kiasi mtu yoyote anaweza akachezea
jina lake?

Tovuti hiyo ilipokuwa inapotosha taarifa za
Baba wa Taifa wahusika walikuwa wapi?

Hakika ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji
 
Haya ndiyo majibu ya nasaha nilizokupa?
Nasaha zako Mzee wangu unazichanganya na maneno makali mno; unapomwambia mtu huna adabu, asiyefunzwa na mamaye, na lugha kama hizo, nashindwa kuelewa kama ni nasaha kweli kutoka kwa mtu kama wewe!
 

Inawezekana kweli hukuwa na hasira nisamehe ndugu yangu.

Mimi nitafute uhalali wa nini kwa kutaka nini na kwa nani.
Nitafuta kuungwa mkono na nani na kwa lipi?

Hii historia ndiyo ilivyo hivyo hivyo huwezi kuibadili.

Sheikh Hassan bin Amir alikuwapo, Sheikh Suleiman Takadir,
Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Mohamed Yusuf Badi na masheikh wengi tu
walikuwa TANU mstari wa mbele.

Ali Migeyo, Dharura bint Abdulrahman, Mama bint Maalim, Halima Selengia,
Amina Kinabo,Zena Maua, Abdallah Rutababzibwa, Sued Kagasheki, Hawa
Bint Maftah, Tatu bint Mzee, Shariffa, Bint Mzee Msham Awadh, Rajab Sisso...

Hawa hamuwajui lakini walikuwapo na walikuwa mstari wa mbele kupambana
na ukoloni.

Baraza la Wazee wa TANU lilikuwapo na walikuwa Waislam watupu.
Haya yote ni ukweli wa historia haukwepeki.

Wenye kufilisika ni wanasiasa mimi sijafilisika chochote kwani mimi si mwanasiasa.
 
Wazee wa kunisimulia kama yeye alivyosimuliwa hawapo tena! Historia nilioisoma shuleni inatosha kabisa. Hata Mzee wetu huyu mtafiti sana ameshindwa kuibadili akaegemeza simulizi zake kwenye dini.

Duh

Kijana unatisha.

Huishughulishi akili yako kujua zaidi. Ushaiwekea kikomo. Umekunywa nusu karne na mawazo yako ndo haya, nakuonea huruma wewe na vizazi vyako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…