gombesugu,
Yericko Nyerere siyo mtoto wa Julius Kambarage Nyerere anatumia tu hilo jina mwanzo wa mnakasha huu alikuwa anajinasibisha na Nyerere kama baba yake mzazi bahati nzuri alikuja mtoto wa kwanza wa Julius Kambarage Nyerere, Andrew Nyerere akamkana kuwa siyo ndugu yao hamjui.
Aliulizwa swali moja tu mama yako ni nani mpaka leo kimya hajajibu.
Zali la Mentali, kachafua hali ya hewa humu jamvini.
Ritz,
Salaam. Nakufahamu na nakusikiza kwa yakin. Mimi najua mengi mno wala sitie shaka. Andrew Nyerere,ni rafiki mkubwa wa Mzazi wangu,nafikiri niliwahi kusema hapo awali.
Huyo jamaa ni psychological fragile,angalia tu ile mada yake halafu ameweka Sheikh Issa Bin Ameir badala ya Sheikh Hassan Bin Ameir...kama kwenye legal technicalities basi Barrister mahiri anakwambia Case dismiss!
Hapa kilichobaki kwa ufupi ni kurembeana fedhuli na kibri kingi tu,labda zaidi wanatumia udhalimu wao wa kumuuliza makhanatha Sheikh Mohammed ili wamuumize kichwa.
Takriban yoote alozungumzia Zali la Mentali a.k.a Mchimba Chumvi,ndo yale yale alokua anadarsisha Sheikh Mohammed takriban miezi minne. Tafauti yeye Zali la Mentali kawaendesha kindava na kimchakamchaka wa nguvu,ndo maana unaona kijasho chembamba kinawabubujika.
Yule kunguni wa hoja a.k.a Abu Jahal,mimi pia nilimtoa maanani kitambo pale alipoleta ule uTarime/Ukabila wake,na ati kujaribu kumtetea Nyerere tena kwa kutumia Khadith na Qur'aan tukufu. Yule Kunguni Wallahi ni Khabith Al maar.
Nyerere aliwahi kufanza mema kiduchu,lakini dhahma wa min'karadas,dhuluma na madhila aloleta ni mengi mno pita kiasi na yanawasulubu watu wengi mno hapo Tanzania mpaka kesho.
Inastaajabisha na ni viroja pasi mfano,hao mashangingi wa shughuli kutukataza kumjadili huyo Nyerere kama vile sisi hakuwa Rais wetu!? Hawa watu maluuni saana.
Tena kama wana maarifa wampe shukran saana Sheikh Mohammed,maana najua anayo mengi lakini kahifadhi moyoni tu. Na haiingii akilini hata chembe ati watu tusimjadili Nyerere,mtu aloleta nakma na zilzala ziso mipaka hapo Tanzania na kwingineko.
Embu waambie wachungulie japo kiduchu,Biography ya JFK by Pro. Micheal O'Brien. Halafu waone huyu jamaa alivyomnyambua JFK,kuanzia Mababu na Mabibi zake woote tokea Ireland,mpaka kutaja makuwadi wake tangia Sec. School mpaka Hollywood. Kaoredhesha mpaka rangi za vichupi/bikinis walizokua wanavaa vimada wake!
Labda tafauti inakuja pale yakuwa; tamaduni za wenzetu na sisi pana khitilafa kubwa mno. Lakini tukifika hapa,itakua tunajibana soote hasa pale tunapotoa mifano mara kwa mara,na jamaa kuanza kulinganisha hapo Tanzania na nchi nyingine za ughaibuni na hasa watu na mataifa ya Magharibi. Na bila ya kufanza hivi,tutawezaje kuzungumzia History!?
Kwa kifupi,Sheikh Mohammed hakumtusi Nyerere ati kwa kusema alikua akisaidiwa kitoweo na nduguye Bwana Mshume Kiyate,hasha!
Halafu wanakuja hawa viwavi wa hoja,ati mara tunachanganya mada,mara tushawahi kujibu tuhuma za Nyerere,mara kafungueni thread nyingine. Hawaoni huyu kinyonga mwenzao anapoleta makhanatha ya hadthi za ugaidi na kutuumiza vichwa kwa kiswahili chake cha kujifunzia Secondary School. Mimi binafsi niliwahi kunena na kutahadharisha mambo kadhaa hapo awali,lakini nikaonekana mtoto wa Madrasa,halafu kajiunga only couple of weeks ago,atatwambia nini sisi mashangingi wa shughuli hii!!
Habari za Nyerere ni nyingi mno wala hazishi kwa hapa Jf hata siku moja.
Kama Jasusi ataamua kusema ukweli hapa jamvini,basi alete kisa cha Nyakyoma,Mohammed Enterprises. Hii kesi naijua kiundani na kiunagaubaga. Mzee wangu alishughulika nayo. Na kama patamwagwa vitu hapa,nami nitamwaga vitu halafu nitakupeni watu mkawaulize.
Nyerere alimshangaza saana Zacharia Maftah(former Director of Anti Corruption Squad),alipoamua ghafla kuhamisha file ya Nyakyoma ipelekwe kwa Abdallah Nungu(alikua Mwenyekiti wa Tume Ya Kudumu ya Uchunguzi Wa Viongozi). Alifanya kusudi kumuokoa nduguye Nyakyoma kwani alijua yakuwa Maftah ilikua anamfunga miaka mingi saana. Wakati Maftah anaifata ile file kwa Abdallah Nungu,ati anaambiwa file imeitwa State House na iko mikononi kwa Mwalimu. File inatoka kwa Nyerere tayari imenyofolewa makaratasi ushahidi takriban woote haumo. Huyo ndiye Nyerere. Matokeo yake akamzidshia utajiri uso kifani Mohammed Enterprises na kufa kwa Gapex maskini mpaka kesho!
Kwa wale wajuvi msokubali hoja za watu wa Madrasa,tafadhali kawaulizeni Joyce Shundi(Kamanda wa Takukuru Dar),Zacharia Maftah, Mzee Butiku au Timothy Apiyo na wengineo wengi walio sehemu nyeti za Serikali. Hawa woote nawajua na nawaheshimu vizuri mno ni Wakristo watiifu tu.
Nyerere alikua analazimisha kwa kibri na kuchukua meli ya kiraia ya Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar,ili akamsaidie rafiki yake Samora dhidi ya Renamo pale Mozambique. Ile meli ilikua inabebeshwa silaha nyingi na za hatari,Wanajeshi na ndani yake kulikua na wafanyakazi wa kiraia wa kawaida kabisaa. Hawa wafanyakazi woote mpaka Captain walikua tu wanapewa taarifa masaa machache kabla ya safari na bila ya kufahamishwa destination mpaka wafike Dar port ndio wanashtukizwa. Hapa kama kuna wataalamu wa Maritime Insurances,pia mtashangaa hiyo meli ilikua inachukua cover ipi na hao wafanyakazi wa kiraia ndani yake walikua wako-covered kivipi!? Hiyo meli imenusurika mara kadhaa na mizinga ya Renamo.
Nyerere,alimstaajabisha mpaka Mzena(Usalama wa Taifa enzi ya Mwalimu),pale alipoamrisha IGP wake Hamza Aziz awekwe chini ya surveillance bila ya ushahidi au sheria yoyote. Ndio maana ile siku Hamza Aziz alipopata accident,alipokwenda kumuona Nyerere huku anajitafunatafuna,ndipo Nyerere alipomwambia Hamza kabla hujasema lolote fungua hiyo bahasha hapo. Ndani ya ile bahasha palikua na photographic evidence,inamounyesha sura halisi ya Hamza Aziz,gari yake na mpaka plate numbers. Picha ile ilipigwa na Mzungu mmoja ati alikua akifanya kazi pale BP - Kurasini!?
Kwa masuala haya muulizeni Mzena mwenyewe kama yuhai. Mkitaka zaidi nitakupeni majina ya watu makhusus tena Wakristo wenzenu mkaulize.
Kuna jamaa mmoja hapa,nae alikuja na hoja yake mbuzi kutaka kuonyesha ati "vitimbi" vya Sheikh Yahya Hussein. Kuna mengi saana pita kiasi...lakini chukua hii tu kiduchu.
Sheikh Yahya Hussein,alishughulika saana kumsaidia Nyerere kuzima lile jaribio la mapinduzi la 1982. Sheikh Yahya Hussein alitumia saana influence na connections zake kwa Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy, Kenyatta,Moi,Njonjo,Usalama wa Taifa wa Kenya na wengineo wengi mno pale Kenya ili kuleta habari huku na kule na pia kuwakamata na kuwarejesha nchini baadhi ya watuhumiwa. Na kuna vitu vingi mno in between vilikua vinafanyika. Ukitaka zaidi nitakufungulia kwa undani,halafu nitakuonyesha udhaifu,Ukabila na roho mbaya ya Nyerere uko wapi.
Halafu,anakuja yule Mrema, mtu mgeni kabisa wa politics za Mzizima na Kariakoo kumkamata Sheikh Yahya Hussein bila ya jambo lolote la maana. Mpaka Lawrence Gama(former DG Usalama wa Taifa na nyadhifa nyingine nyingi tu hapo Tz,pia Jasusi ataeleza alimuoa nani ndani ya family ya Nyerere),alisikitika saana upumbavu wa Mrema kuingilia vitu alivyokua havijui. Kumbe Mrema alikua hajui maskini yakuwa anamfanyia Kitwana Kondo kazi yake,ambae wakati huo ndio alikua Rais wa nchi kuliko huyo Mwinyi mwenyewe. Kitwana Kondo alinyang'wanya mke na Sheikh Yahya Hussein during 60's.
Hizi habari kwa undani muulizeni Dominick Gama au Sinde Warioba. Maana nasikia Mzee Gama Lawrence amefariki. Na kwa wale wa Chadema,kamuulizeni Mabere Marando na atakufahamisheni yeye wakati huo alikua nani!? Au Shahidi X...Mzee Maige!
Kwa hiyo msione watu tumekaa kimya,ati mkafikiri tumevamia tu hili jamvi au hatujui mambo au huyo Nyerere wenu hatumjui au mambo nyeti takriban yoote, ati kwa sababu tu ni watoto wa Mdarasa. Tunafanya staha tu kiduchu. Kwa sababu wengi hawa ni Wazee wetu kama anavyosema Sheikh Mohammed Said. Hiyo nchi sisi wengine ni haki yetu na tuna uchungu nayo kupita hivyo mnavyohisi.
Ahsanta.
Cc: The Big Show