Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
Kadogoo,
Yule alikuwa akiitwa Malekia ambae alikuwa akivaa sare za jeshi
nadhani ni huyu unaemkusudia.
Kadogoo; Nimekulia Moshi. Mzee Malekia wakati tunakua (tukiwa wadogo) tuliambiwa alirukwa akili through mambo ya WWII (vita kuu ya Pili). Walikuwa yeye na mwingine anaitwa Micheal (huyu alikuwa amejaza misuli na mara nyingi akijishughulisha kwenye bustani ya manispaa au mara nyingine utamkuta karibu na mnara wa saa. Mzee Malekia binafsi nilimwona akitunza sana mabustani na maua pale kwenye mnara na alikuwa akikukuta unatupa takataka ovyo basi ni yeye na wewe. Lakini pia ilikuwa ni baadhi ya siku. Siku zingine ndizo hizo alizokuwa anavalia zile sare za Jeshi na Kutembea mjini amebeba misalaba, au baadhi ya kama zana. The last time i was in Moshi niliuliza sana habari zake (huu ni mwaka jana around
around april). Niseme kuwa nilijawa na utata kama yupo hai au keshakufa, huyo niliyeonyeshwa kuwa ndiye Malekia nilimkuta jirani na duka moja yanatazamana na soko kuu lakini huu upande unaozitizama TAXI. Hakuwa yule wa zamani (kama ni yeye). Huyu alikuwa mchafu, mchovu, hoi, kalala kwenye baraza ya hilo duka hapo nje. Nilijizuia sana kulia pale mbele ya wenzangu. As tiny boys we loved this Mzee so much. Mzee Maiko niliambiwa alishafariki.