Kwenye post yangu
#13116 niliweka ushahidi huu ambao unadhihirisha kwamba Nyerere hakuishia Africa Mashariki tu bali aliunganisha Mfumo Katoliki mpaka Vatican. Haya ndiyo niliyoyazungumza ambayo mpaka sasa mnayakimbia kama kituo cha polisi kuyajibu:
Ni kweli wazee wa wakati ule hawakuwa wadini lakini Nyerere alikuwa mdini aliyekubuhu.
Ushahidi uliowekwa na muanzisha thread hii kwamba Askofu Maranta alikwenda kwa Sheikh Issa ili aone jinsi Kanisa linavyoweza kuingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kudai uhuru hapo mwaka 1948 na kushauriwa ajiunge kwenye vyama vilivyopo ni dhahiri kwamba Sheikh Issa alikuwa analikalibisha Kanisa kwenye African Association ambapo Masheikhs walishajitambulisha na hicho chama tangu kinaanzishwa mwaka 1929. Na inaonekana hapa kwamba mipango ya Kanisa Katoliki kuanza mikakati ya kumpandikiza Nyerere kwenye TAA ilianza kusukwa hapa kwani Kanisa halikuwa na sababu yeyote ya msingi ya kutaka kuonana na Masheikhs kujadiliana nao jinsi gani Kanisa litaingia kwenye harakati za kudai uhuru wakati Kanisa lilishafanya uamuzi kwamba hawawezi kujiunga na vyama ambavyo havina wasomi. Haiingii akili kwenda kumuona mtu ambaye tayari umeshamuhukumu kwamba hafai!!!!
Nyeree alificha makucha yake ya udini uliokubuhu wakati wa zoezi zima la yeye kuingia kwenye kwenye Siasa kupitia TAA. Makucha yake alianza kuyaanika mara baada ya kufanikiwa kujipenyeza ndani ya TAA na hatimaye kupata Urais wa nchi. Ndipo hapo Nyerere aligeuka kuwa zaidi ya Mdini. Alikuwa Mmadhehebu wa hatari sana. Alianza kuweka mikakati ya kuwapendelea Wakatoliki dhidi ya dini zingine na madhehebu mengine ya Wakristo. Akaanza mikakati ya kuuuwa Uislam.
Kitabu cha Jan P. Van Bergen kilimnukuu Nyerere akisema maslahi ya kanisa lake (Roman) yanakuja kwanza na hatokwenda kinyume na kanisa lake.
Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!
Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.
Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele:
"KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC".
Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
Mwaka 1970 Nyerere aliwaalika Ikulu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Tanzania Episcopal Conference Fr. Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa Tanzania Mgr. Giovano Cerrano na Nyerere aliwaambia wageni wake alikuwa anafanya kila liwezekanalo katika mamlaka yake kuuimarisha Ukatoliki Tanzania. Aliwaomba pia waende kuwafahamisha ma bishops kwamba ameanzisha idara ya elimu ya siasa kwenye TANU na kwamba amemteua Mkristo Reverend kuwa mkuu wa idara hiyo sio kwa sababu ya uwezo wake katika siasa bali kwa sababu ya imani yake thabiti kwenye Ukristo. Jukumu lake ni kuongoza na kudhibiti muelekeo wa kisiasa wa chama. Aliwafahamisha vilevile kwamba katika Kamati Kuu ya Chama (NEC) wajumbe wawili ni Reverends. Alisema anaamini hiyo ndio njia nzuri ya kuhakikisha kwamba chama kinapata watu wazuri!!!!!! (van Bergen, 1981:333-336).
Si ajabu kutokana na agano lake hilo hapo juu kwamba Sivalon (1992:49) anaripoti kwamba katika mwaka huo huo aliotoa ahadi Wakatoliki walikuwa asilimia 70 ya asilimia 75 ya Wakristo wote waliochaguliwa kuwa wabunge. Kati ya wabunge 108 waliochaguliwa 5 walikuwa wanaamini kwenye dini zetu za asili, 23 walikuwa wanaamini kwenye Uislam, 24 walikuwa wanaamini katika madhehebu mengine ya Kikristo yasiyokuwa Katoliki na 56 walikuwa wanaamini katika Ukatoliki. Hivyo utaona Wakatoliki walikuwa zaidi ya nusu ya wabunge wote!!!!!!!!
Nyerere ndio mtu aliyetumika na Kanisa katika mikakati yao ya kuumaliza Uislam (Crusade). Hii inadhihirishwa na mpango wake wa kufanya mapinduzi Zanzibar kwa kumtumia mtu katili na mdini mwenzake Okello ili kuusambaratisha Uislamu ambapo zaidi ya watu 20,000 waliuawa kikatili na watu wasiopungua 200 walichomwa moto kwenye tanuri wakiwa hai!!!!!
Sasa unahitaji ushahidi gani zaidi?
Hakuna haja ya kufungua thread nyingine. Fuatilia ID yangu utakuta kila thread niliyoifungua JF wameifungia isijadiliwe. Mnataka nifungue nyingine ili nayo muifungie? Tutabanana hapa hapa mpaka kieleweke.