Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohammed,
Kuna tofauti gani kati ya Hassan (Kiswahili) na Ghassany (Kiarabu)? Isn't it the same name with a cultural alteration? Ndugu zetu Afrika magharibi wamezoea kuita Aminata. Waswahili tunaita Amina. Fatumata. Fatuma. etc

Jasusi,
Nilidhani umelikosea jina.

Harith ndiyo alinisindikiza VOA hapo Washington
kufanya mahojiano.

Nilikuuliza.
 

Jasusi,

Punguza munkari jitulize kunywa fundo tatu za maji kisha pumzika kidogo.

Huu ni mnakasha watu wote wapo huru kujenga hoja zao ili zijibiwe kwa hoja, unamuita Zali la Mentali, jitu hapo umeteleza.

Hebu jifunze kutoka kwa mwalimu wetu Mohamed Said, wenzako wanavyomshambulia kwa matusi, kejeli, dhihaka, lakini katulizana hana wasiwasi anafundisha tu.

Sasa nyie mtu akiwaeleza habari za Nyerere tofauti na mnazozijua nyie mnakuwa wakali.
 
Last edited by a moderator:
Zali la mentali, umesifiwa sana na wapumbavu wenzako kuwa unahoja na unaweza kuwa nyamazisha wasomi kwa huu upumbavu wako hapa. Huwezi kuleta mabadiliko kwako wewe mwenyewe wala kwa hao ambao unadhani unawasemea kwa kumtusi Nyerere! naamini hata mzee Mohamed Saidi mchochezi hawezi kuafiki hadharani matusi unayomtukana Nyerere. Hivi kwa umbumbumbu wako na mitusi yako ambayo unaiita hoja ulitegemea Nyerere angeweza kujiunga na TAA bila kuisoma katiba yake?Au kwa upumbavu wako unadhani kwamba Nyerere hakuwa anawafahamu akina Dosa kabla ya kujiunga na TAA na baadae kuiongoza? Katibiwe ugonjwa wako wa kujiamini kawa mambo ya kijinga ambayo hata huyajui. Mbona unakuwa kichekesho hapa jamvini? chuki zako binafsi dhidi ya Nyerere haiwezi kubadirisha historia ya Tanganyika! mkuu Wild Card alisha kuuliza ni nani alikuwa rais wa kwanza na wa mwisho wa TANU, hukujibu na huta kaa ujibu swali hilo kwakuwa umesheheni chuki kichwani mwako badala ya maarifa na busara.
 
Wewe ndio unayetoa malalamiko na majungu bila ushahidi. Hoja zangu zote zimejengwa kwa ushahidi ndio maana huzioni kwa sababu umezoea umbeya.
Zali la Mentali, kwa kweli hujaweka hoja hata moja tangu umeingia kwenye hili jamvi. Kilichowekwa hapa na wewe ni makelele ya mgonjwa wa akili aliyejaa chuki, kibuli, dharau na matusi dhidi ya Nyerere na sio vinginevyo. Nakushauri jirudie tu kwenye mradi wako wa kuchimba chumvi mahali ambako lugha yako inavumilika.
 
Hapa umenizindua kitu muhimu sana katika nafsi ya Nyerere.Si alikiri mwenyewe kwamba hakuwajua viongozi wake?.Ikiwa si uchizi huo ni nini?
Afadhali wewe umekiri kuwa Nyerere alijiunga na bila shaka baada ya kukaribishwa.
Tatizo umeamua kumtetea bila mafanikio kuhusu uchizi wake kama hapo juu kwa Zali.Fikiria mwenyewe ikiwa alikuwa anawajuwa akina Dosa watu muhimu katika chama mbona aliwasahau kirahisi.Ikiwa si uchizi huo ni nini?.
Yuko wapi Spike afyonze elimu na gombesugu atupe siri zaidi za Nyerere ambazo Mohammed Said alizibania kulinda heshima yake?.
 
Pongezi nyingi kwa Ritz kutuletea kichwa kama wewe hapa.
Kwa kweli ogopa sana kupingana na ukweli daima utaumbuka.Haya unayoyaeleza hapa ni ukweli wa kihistoria ambao umejaa kwenye vitabu na nyaraka vingi vikiwa havikuandikwa na waislamu.Ajabu wanatokea watu ovyo ovyo kama Mwanakijiji eti anataka kujibizana kuhusu mapinduzi ya Zanzibara wakati mwenyewe ndio kwanza anataka kusoma Kwaheri Kwaheri cha Alghassany!.
Hivi vitabu vya akina Mohammed ni historia kutokana na mahojiano ya wahusika,hivyo watu wengine ni bora wasome tu na kufyonza elimu.
 
Wanajamvi huyu ndugu yetu Zali la Mentali, "Mchimba chumvi" kwa kweli katumfumbua macho.

Nyerere anasema alikuwa mjumbe wa TAA na alihudhuria mkutano wa Tabora.

Cha kushangaza alikuwa hamjui kiongozi wake Katibu Mkuu wa TAA Abdul Sykes.

Kaja kufahamishwa na Kasanga Tumbo, alivyokuja Dar es Salaam, hapa napata tabu kidogo kumuelewa Nyerere.

Ni sawa sawa Mabere Marando, kajiunga Chadema lakini hamfahamu Katibu Mkuu wake wa Chadema, Dr Slaa.

Mimi nakiita ni kituko Nyerere kajiunga kwenye chama bila kuwafahamu viongozi wake.
 
Last edited by a moderator:
Ritz,Huyo Zali la Mentali ni mentali kweli. Anang'ang'ana tumjibu hoja ambazo hazipo! TAA na AA tunaweza kuiachia familia ya Sykes kwa kuwa hivo ndivyo anavyotaka ieleweke mzee Mohamed. TANU ni ya Mwalimu mwanzo hadi mwisho wake. Mwalimu alikuwa Rais wa KWANZA wa TANU na Mwenyekiti wa Mwisho wa chama hiki.
 
Last edited by a moderator:

WildCard,

Nadhani ingekuwa bora mgemjibu kusema kuwa suala la AA, TAA, mnawachia familia ya Sykes siyo jibu.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Ami
Ritz,
Post za mwenzetu Zali la Mentali ni kama gunia au belo la mitumba ya nguo. Tusaidie kuziainisha hoja zake ili tujibu tunazoweza.
 
Last edited by a moderator:

Ritz,

Hicho sio KITUKO bali ni UNAFIKI mkubwa wa kutaka kuwahadaa walimwengu wa duniyani.

Kweli tutajua mengi kutokana na mnakasha huu.


 

Hili jamvi lina Breaking News kila Upande. Kumbe kuwa na kijisehemu cha Ukurya katika maumbile yako inakupunguzia kulialia!!!!!!!! hahahahahahah. Asante Wildcard. I happen to have more of that stuff. hahahahahah. Mzee MS uliyajua haya? Sina hamu, let me laugh.
 
Last edited by a moderator:

WC,

Kwenye historia hatusemi hata siku moja baadae sana au baadae kidogo. Unatakiwa utaje miaka hapo iwe sekunde, saa, dakika au siku zote zinahishimika. Weka miaka ili ujipambanue weledi wako katika hili.

 


Nitakusaidia hapo nili Underline tu.

Nitakupa nchi jirani yako kabisa. Kenya, Uganda, Msumbiji, Zambia na nyingine nyingi sana. Ila Tanzania hususan Tanganyika ndio Serikali imewabania na kuwaundia BAKWATA.
 
Mohammed,
Kuna tofauti gani kati ya Hassan (Kiswahili) na Ghassany (Kiarabu)? Isn't it the same name with a cultural alteration? Ndugu zetu Afrika magharibi wamezoea kuita Aminata. Waswahili tunaita Amina. Fatumata. Fatuma. etc

Jasusi,



Sasa hapo huoni yakuwa unajichanganya mwenyewe!?....mfano Albert na Alberto!?...Hii kwa mwenye kufahamu ni inanyambulisha background,customs and culture ya mtajwa. Ni kama ulivyoonyesha,yakuwa jina ni moja lakini ghafla,inabainisha yakuwa huyo mtajwa anatokea pahala gani na tamaduni ipi...kama ulivyosema...Fatma kwa sisi mwambao wa East Africa lakini Bara nyinyi mnaita Fatuma...na wenzetu Afrika ya magharibi ni Fatumata kwa bara zao na halikadhalika coast zao ni Fatimata.

Tuendelee na mnakasha.
 
Wickama,
Mkurya mwanaume halii. Mkurya mwanaume hahamishii matatizo yake kwingine. Mkurya mwanaume hajui kusingizia wala kuliahirisha tatizo. Hii ni kweli pia vikabila vingi vya jamii hiyo mkoani Mara. Hawa jamaa wanakabiliana na tatizo kama changamoto.
Wakurya wengi hawakwenda shule lakini hawamlaumu Mhaya au Mchaga wa Tanzania hii.
 

WildCard,

Mie ni mtani wangu tunapenda kutaniana mimi sina ukurya ingiwa nimeishi nao na ni marafiki zangu mwaka jana nilikwenda Tarime kumzika rafiki yangu Masubo, alikuwa mfanyabiashara pale Mwanza.

Napafahamu vizuri Musoma, Mkendo Kati, Kawawa, Karume, Makoko, Majita, Tarime, Shirati, Bunda, Sirari, Lamadi, juzi Nguruvi3, kataja daraja la lililowasumbua Wataliana nimekumbuka mbali sana watu walikuwa wanasema pale kuna mizimu inabidi wachinje ng'ombe wamwage damu, ha haa ha.

Kaka nashukuru Tanzania nimetembea kwingi...ukifika Tarime likizo msalimie Zakaria.
 

Ritz nashukuru; Najua mlikuwa mnatoana jasho na Wildcard nilijiingiza kwenye mtaa wa utani wenu ili nicheke kidogo. Mi nyumbani ni pale Starehe street Tarime mjini. Japo pia kwa vile Mara unaijua vizuri tunatokea maeneo ya Kuruya uelekeo wa ziwani. Pale mjini nilisomea kwa miaka michache pale Sabasaba primary school (muda mwingi nimekulia MOshi). Classmates ni kina Mwita Mantago (alikuwa meya wa Tarime hivi karibuni), wakina Macharia-wakikuyu hawa walikuwa na hotel (then ni Kilimambogo nadhani). Kuna wakina Paulo Mganda (ana dispensary yake huyu kwa sasa). Wakati huo huyu Zacharia unayemsema hajainuka. Walikuwa ndio wakina Gachuma, Chambiri ndio wababe wa biashara. Tarime ya wakati huo ilikuwa na timu ngumu ya football ikiitwa Mori FC (wakiwamo kina akina Nashon, Abdallah, kaka yake bubu mmoja mchoma mishkaki, Hamad-kipa huyu kama Pondamali). Siku wakipambana na timu ya kutoka Musoma (Maji, wakina Nyitara na striker mwingine hatari kwa mashuti-mjaluo yule bwana simkumbuki jina kwa sasa-huenda ni Ouma) Mji unasimamisha shughuli. Mara nyingi hata FFU toka Musoma walikuwa wanakuja kupunguza hamasa!!!! Wazee wa kiislamu waliobebea walikuwa wakina mzee Idd Akilimali (marehemu sasa), Mzee Juma Mtongoli (naye marehemu kwa sasa). huyu Mtongoli alikuwa jirani yetu (nyumba inayofuata na alikuwa rafiki yangu sana japo mimi ni mtoto). Kila nikifika likizo lazima nikishatua mizigo yangu marehemu mama ananipa UPDATEs za Mzee huyu, then naenda kumsalimu. Miaka hiyo nilipiga sana picha naye, bila kujua baadae zingeifaa familia yake. Majuzi tuu ndio nilizi scan picha zake na kumtumia binti yake anasomea PhD ya hali ya hewa Norway kwa sasa!!!!!! picha za baba yao after nearly 35 years. Mzee Akilimali alikuwa rafiki sana na marehemu mama. Ila watoto wake kina Daudi hao walisoma na kaka zangu. Umetaja kisa cha daraja la mto mara-kirumi. "Mzimu" wa pale kirumi ulikuwa unasubiriwa sana kunako miezi ya mwisho mwisho wa mwaka. Miezi kama hiyo palitumbukia gari ya breweries pale. Ni zamani wakati wa ferry. Mwanzoni, askari (FFU) walipalinda sana ili watu wasijaribishe kuzamia hadi kunako shehena yenyewe. Lakini jinsi matumaini ya kulitoa yalivyozidi kufifia taratiibu wakaanza kuwaachia wapiga mbizi wa kisimbiti na kikiroba (wenyeji hawa) kuzamia kujaribisha "bahati yao". Sijui kama walikuwa wanabahatisha au kukosa. Itatosha kusema kila mtu (askari ni mtu pia) alikuwa na mapenzi na bia za bure. I mean kama unazipata. Afterall huenda lori na "shehena yake" lilikuwa limekatiwa bima au siyo???? Kwa hiyo Ritz, dunia ilishaanza kuwa a small village tangu miaka hiyo. Shukran kwa response yako. Msalimu Wildcard.
 
WildCard,

Nadhani ingekuwa bora mgemjibu kusema kuwa suala la AA, TAA, mnawachia familia ya Sykes siyo jibu.

Ritz,

Asalaam Alaykum Al Akhiy.

Hawa jamaa wameshindwa kabisa kujibu hoja kali na zenye minyambulisho na zilzala za nguvu. Labda yale mawe yamekua mazito mno sasa wanaona kimulimuli,kwa hiyo tusiwalaumu sana wanaposema ati hoja za Zali la Mentali a.k.a Mchimba Chumvi hawazioni!?ahaha!!

Mimi awali nilipoingia sikujua hawa jamaa kumbe wamo hapa jamvini kwa ajili ya Crusade kama ndugunyao George Bush na wale virongwe ma-Neo Cons. Lakini kila siku zinapokwenda nabainisha mengi hapa.

Kuna wakti walikua haweshi kututajia mambo ya Tanga na Wazee wetu wa Tanga,sisi tukawa kimya tunawacheka tu...nilipowafuata kuwavuruga kila mmoja kaanza kutaja makwao na yule mwingine akaacha kabisa kumtisha Sheikh Mohammed na yale mambo ya Makorora,sasa kakimbilia kwao Kicheba na Magila.

Kwa wale wa Mara na Tarime,nanyi pia nakuja hukohuko na nitaanza kwa kukuonyesheni ya kuwa huyo Nyerere wenu kaanza kula fadhila za Wazee wetu toke pale Musoma kwa Mzee Makongoro na Masheikh wengine wengi tu huko mabara. Nina tambara chafu saana la Nyerere alowafanyia kina Issa Makongoro na Sheikh Abdallah Mwita. Kwa hakika yule mtu alikua hakumbuki kabisa fadhila. Kila nikisoma hiyo hotuba ya upuuzi aloiweka huyo Yericko hapo juu,basi Wallahi nakumbuka jinsi gani Nyerere alishindwa hata kwenda mazikoni/msibani kwa Sheikh mohammed Yahya Ramia pale Bagamoyo. Alipopashwa habari na AbdilRahman Ramia,akadai ati yuko very busy kwenye simu na yule "changumemenya" Samora Machel!? Sijawahi kusikia maongezi ya simu ya siku nzima!? Na kuwasahau walokuweka na kukufadhili kwenye hayo madaraka!?

Leo hao jamaa ati wanamzoma Rais Al Jamuhuriya Al Maaruf Mrisho Bin Khalfan Kikwete,ati anasafiri sana. Embu wajaribu kupiga hesabu ya trip za huyo "Mwalim wao"!? Kuna trip nyingine alikua analazimisha huku anaambiwa kuwa ndege bado iko Government Hanger ina khitilaf. Chief Engineer wa Serikali yake takriban miaka 20 Mohammed "Babu" Mwita(mnywa kahawa,mtoto wa Kariakoo,mtu wa akili za Madrassa),alikua analalamika kuwa huyu Mzee Nyerere,iko siku atatufanya tufie angani maana anaingilia sana mambo asoyajua na mkaidi wa kusikiliza Wataalamu. Kwa issue hii,wale wajuba na mpendao kujipunja kamuulizeni Mkristo mwenzenu mtiifu Mzee Newa maana ndiye aliekua Pale Civil Aviation miaka mingi .

Jamaa naona kila habari tukiwapa hawazikubali,ati kwa sababu tu kuwa wao walikua hawazijui na wanajaribu kuzitia tashtit. Ndo maana Sheikh Mohammed huwauliza ,haya mambo mtayajuaje kwani nyinyi ni wageni na pia Wazee wenu ni wageni?

Nipo hapa leo, napitia ule utumbo wao wa W'end. Naona hamna lolote la maana zaidi ya matusi ya yule Kiroboto wao. Najua wale Manyangumi wa hoja wametahayari,pale The Big Show a.k.a The King Of Kings alipowaambia kuwa wanashinda hapa na kulala hapa hapa jamvini!ahaha!!

Naona yule kunguni wa hoja a.k.a Abu Jahal,ati anahangika kuingia kwenye "google search" na kupata fadhaa mbona hizi details hazipatikani!?ahaha!!...hawa jamaa kweli hamna kitu!

Tuendelee na mnakasha.


Cc; Ami

Sitie shaka nakuwekea vitu vipya na vya ndani every time...I never break my promises.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…