Mjadala huu kwako ni mkubwa mno, hoja za Mohamed Said zimekuwapo kwa miaka hata huyo Mwalimu alikuwa hai hakuweza kuzijibu. Kwakuwa unaoneshwa kuguswa nenda kawalete watu wenye size na Mohamed Said hasa maaskofu waje wajadiliane na wewe uchukue note book uandike nondo.
Wewe ndio unayetoa malalamiko na majungu bila ushahidi. Hoja zangu zote zimejengwa kwa ushahidi ndio maana huzioni kwa sababu umezoea umbeya.
Wickama nakuwekea kipande hiki uweze tu kujua tulikoanzia na huyu Mohamed Said na ngano zake...
- Mohamed Said: hadithi, hadithi?
- FaizaFoxy et al: Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!
- Mohamed Said: Hapo zamani za kale...
Hii ndiyo mihadhara ya hoja za nguvu aliyokuwa anayofanya Mohamed Said kutokana na eti utafiti wake wa miaka 15 hadi alipotinga ndani ya ukumbi huu na kuanza kupambana na nguvu za hoja za wana JF. Kuna watu walimeza hizi simulizi porojo mazima mazima na wanashangaa kweli tunapojitokeza watu kuupinga uongo na uchochezi wake! Walishamwamini kwani huko nyuma hakuwahi kuhojiwa hata siku moja! Mwaka 1963, chama cha siasa cha kidini AMNUT ilivunjika na ndio wengi wa wanachama wake walianza kutimkia EAMWS. Walioasi TANU kwa kumpinga Mwalimu walifanya hivyo miaka mitatu kabla ya uhuru, waliunda chama cha siasa cha kidini lakini walikataliwa na wazalendo.
Wickama nakuomba usome hicho kipande alichotoa Mohamed Said kwa utaratibu...hutashindwa kuelewa kwa nini akina gombesugu wanaandika wanayoyaandika. Wickama, tulianzia mbali, hayo ya laana ya ugonjwa wa Mwalimu yalisemwa sana na pacha wake Zali la Mentali ambaye kwa sasa ni ajabu haonekani! Nataka tu nikustue kidogo, si dini ni desturi za asili tu za watu...kuna wale utoto huuvaa kama shati hadi uzeeni...ndiyo, ndivyo walivyolelewa. Hawaoni taabu kuogea dimbwini na watoto, hawaoni taabu kukaa vibarazani na watoto kuwasengenya wasiokuwapo...babu kwa baba, baba kwa mtoto, mtoto kwa kwa mjukuu na mjukuu kwa mtukuu! Ndivyo walivyo...Dini ni kisingizio tu.
Ritz,
Asalaam Alaykum Al Akhiy.
Hawa jamaa wameshindwa kabisa kujibu hoja kali na zenye minyambulisho na zilzala za nguvu. Labda yale mawe yamekua mazito mno sasa wanaona kimulimuli,kwa hiyo tusiwalaumu sana wanaposema ati hoja za Zali la Mentali a.k.a Mchimba Chumvi hawazioni!?ahaha!!
Mimi awali nilipoingia sikujua hawa jamaa kumbe wamo hapa jamvini kwa ajili ya Crusade kama ndugunyao George Bush na wale virongwe ma-Neo Cons. Lakini kila siku zinapokwenda nabainisha mengi hapa.
Kuna wakti walikua haweshi kututajia mambo ya Tanga na Wazee wetu wa Tanga,sisi tukawa kimya tunawacheka tu...nilipowafuata kuwavuruga kila mmoja kaanza kutaja makwao na yule mwingine akaacha kabisa kumtisha Sheikh Mohammed na yale mambo ya Makorora,sasa kakimbilia kwao Kicheba na Magila.
Kwa wale wa Mara na Tarime,nanyi pia nakuja hukohuko na nitaanza kwa kukuonyesheni ya kuwa huyo Nyerere wenu kaanza kula fadhila za Wazee wetu toke pale Musoma kwa Mzee Makongoro na Masheikh wengine wengi tu huko mabara. Nina tambara chafu saana la Nyerere alowafanyia kina Issa Makongoro na Sheikh Abdallah Mwita. Kwa hakika yule mtu alikua hakumbuki kabisa fadhila. Kila nikisoma hiyo hotuba ya upuuzi aloiweka huyo Yericko hapo juu,basi Wallahi nakumbuka jinsi gani Nyerere alishindwa hata kwenda mazikoni/msibani kwa Sheikh mohammed Yahya Ramia pale Bagamoyo. Alipopashwa habari na AbdilRahman Ramia,akadai ati yuko very busy kwenye simu na yule "changumemenya" Samora Machel!? Sijawahi kusikia maongezi ya simu ya siku nzima!? Na kuwasahau walokuweka na kukufadhili kwenye hayo madaraka!?
Leo hao jamaa ati wanamzoma Rais Al Jamuhuriya Al Maaruf Mrisho Bin Khalfan Kikwete,ati anasafiri sana. Embu wajaribu kupiga hesabu ya trip za huyo "Mwalim wao"!? Kuna trip nyingine alikua analazimisha huku anaambiwa kuwa ndege bado iko Government Hanger ina khitilaf. Chief Engineer wa Serikali yake takriban miaka 20 Mohammed "Babu" Mwita(mnywa kahawa,mtoto wa Kariakoo,mtu wa akili za Madrassa),alikua analalamika kuwa huyu Mzee Nyerere,iko siku atatufanya tufie angani maana anaingilia sana mambo asoyajua na mkaidi wa kusikiliza Wataalamu. Kwa issue hii,wale wajuba na mpendao kujipunja kamuulizeni Mkristo mwenzenu mtiifu Mzee Newa maana ndiye aliekua Pale Civil Aviation miaka mingi .
Jamaa naona kila habari tukiwapa hawazikubali,ati kwa sababu tu kuwa wao walikua hawazijui na wanajaribu kuzitia tashtit. Ndo maana Sheikh Mohammed huwauliza ,haya mambo mtayajuaje kwani nyinyi ni wageni na pia Wazee wenu ni wageni?
Nipo hapa leo, napitia ule utumbo wao wa W'end. Naona hamna lolote la maana zaidi ya matusi ya yule Kiroboto wao. Najua wale Manyangumi wa hoja wametahayari,pale The Big Show a.k.a The King Of Kings alipowaambia kuwa wanashinda hapa na kulala hapa hapa jamvini!ahaha!!
Naona yule kunguni wa hoja a.k.a Abu Jahal,ati anahangika kuingia kwenye "google search" na kupata fadhaa mbona hizi details hazipatikani!?ahaha!!...hawa jamaa kweli hamna kitu!
Tuendelee na mnakasha.
Cc; Ami
Sitie shaka nakuwekea vitu vipya na vya ndani every time...I never break my promises.
Wickama,
Nimekuelewa.
Lugha inashabihiana na utamaduni.
Kuna wakati nilikuwa natumia usafiri wa ofisi na jamaa ofisini.
Hawa jamaa wote wanatoka bara.
Tunapita Kariakoo.
Nawaona jamaa zangu.
Katika mila zetu aliyepanda chombo ndiye aula zaidi kutoa salamu.
Mimi nikifanya hivyo lakini kwa sauti ya juu kidogo.
Nasema, ''Abdallah Hashim Asalaam Aleikum.''
Hawa jamaa zangu wananiuliza (wamekereka kidogo) ''Why are you
shouting?''
Nami nawajibu, ''I am not shouting that is how we salute each other
short of that I would be considered snobbish.''
Hawaelewi.
Basi mie nikawa nawaambia, ''Nyie maadam mmekuja kuishi huku kwetu
lazima mjifunze na mila zetu.''
Walikuwa hawapendi wakichomwa sana na maneno yangu na katika wale
wengine ni wakubwa zangu katika kazi.
Juu ya hayo mie si mtu wa kujidhalilisha na walikuwa wakisema sana nawapa
hii nawaambia, ''Haya ni mafunzo katufunza Mtume SAW.''
Ilikuwa raha sana.
Hawa jamaa hawatanisahau.
Walikuwa wakati mwingine wakisema, ''Mohamed sisi hatujapatapo kukutana na
Mswahili wa aina yako.''
Sasa sijui ile ilikuwa ''compliment'' au nini.
Wickama,
Mimi nimekuelewa na mimi nakuomba unielewe.
Uingereza (Kuleta makomandoo wa kurejesha utawala haramu wa Nyerere baada ya kukataliwa na Wazalendo wakati wa mapinduzi ya 1964)
Sikutaka kujibizana na huyu jamaa anajiita Zali la Mentali kwa sababu kwanza naona uelewaji wake wa masuala ni wa ajabu sana. Mfano ni hicho kipande nilichonukuu hapo juu kutoka kwa bandiko lake. Kwa hiyo ule uasi wa 1964 ulikuwa ni juhudi za wazalendo kukataa utawala haramu wa Nyerere? Hao wazalendo walikuwa ni akina nani? Na je, uasi uliofanyika wakati huo huo Kenya ulikuwa pia ni juhudi za wazalendo kuukataa utawala wa Kenyatta? Kwa sababu Waingereza vile vile walisaidia kuuzima ule uasi, lakini tofauti na Tanganyika, waliweka kambi za kudumu za kijeshi Kenya. Utajibizanaje na jitu la maoni kama haya?
jokaKuu,'
Hii ya Kitwana Kondo kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya serikali ya Mwinyi ni kweli kabisa. Mzee Bomani aliwahi kulalamika kuwa baraza la mawaziri lilikuwa likipitisha uamuzi lakini baada ya Kitwana Kondo kukutana na Mwinyi wanasikia yanayotangazwa na RTD ni tofauti na yale waliyokubaliana.
Gombesugu umenikumbusha mbali kuhusu huyu bwana mkubwa zamani makureish walikuwa wanamuita abul hakam(baba wa hekima)siku moja walikuwa wamekaa pale darul Nadwa wanapanga jinsi ya kumuua mtume Mohamad (s.a.w)Abul hakam akawambia makifiri wenzake wa kikureish ongeeni taratibu MUNGU WA MUHAMAD ASIJE AKATUSIKIA ndio tangu siku hiyo mtume akampa jina la ABUU JAHAL(BABA WA WAJINGA)hata hapa wapo wengi watu hao!
mkuu anajua sana huyu ila anajifanya haelewi ....damu nzito kuliko maji .. mohd said anagusa pasipotakiwa ..
Gombesugu,
Huwezi kujua mapenzi ya Hamza Aziz kwangu.
Sote tumezaliwa Kipata na sote tukipenda muziki
wa Nat King Cole.
Juu ya tofauti wa umri wetu tukizungumza as equals.
Akinitania kwa mke wangu, "Mohamed you have taste
for good looking ladies..."
Nami huwa simwachi namjibu namwambia, "I have picked
that from you!"
Tena akinitania hivi mbele ya binti zake kwenye diner table.
Akiwa na jambo zito tunakwenda kwenye majlis yake pwani
tunaangalia bahari.
Kwenye kibanda kile ndipo Hamza Aziz alikuwa anafunguka khasa.
Sasa baadae nikajajua kwa nini tukiwa ndani ni maskhara na tukiwa
majlis ni serious business.
Ndani mwake nahisi alikuwa na hofu ya bugs.
Sasa baada ya kukusoma ndiyo inanijia wazi kabisa.
Ikajanipitikia kuwa Hamza Aziz alikuwa anataka niyajue baadhi ya mambo
asije kwenda nayo kaburini.
Hiyo bugging kanipa mkanda mzima lakini siyo hiyo album yako....
Nimeburudika pia na showdown yake ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU...
Akanambia yote chanzo ilikuwa yeye kukataa kumkamata Sheikh Hassan
bin Amir.
Nina mengi...
Hawa ndugu zetu ni wageni katika mambo haya.
Hao walikuwa wazee wetu walioipigania nchi hii kuitoa mikononi mwa Waingereza.
Sheikh Mohammed,
Asalaam Alaykum Al Akhiy. Wallahi nipa fursa ya kunipokelea bayana yangu chechefu kwako.
Nahisi huyo "Abdallah Hashim" hapo,itakuwa ni Abdallah Hashim wa Sheikh Hashim Haji Abdallah!ahaha!!
Awali ulitaja habari za Al Marhum Maulana Sheikh Al Khalifa Hassan Bin Ameir. Nafurahi kukujuza yakuwa mimi nilikutana mara kadhaa na kupata baadhi ya habari zake toka kwa Bwana Haytham pale Portsmouth England. Huyu Bwana ameoa mmoja kati ya mabint wa Sheikh Hassan Bin Ameir.
Pale Portsmouth ,nilikutana na jamaa wengi walokimbia yale maafa ya 1964.
Yupo pia,Shariff Ibn Maashar,Sheikh Suleiman,Sheikh Hassan wa Kiembe Samaki na Al Sahib Muhammad Yahya Al Alawy na wengineo wengi wamefariki maskini.
Pia niliwahi kupata fursa ya kualikwa Iftaar Ramadhan moja na Khalifa Jamshid Bin Abdallah. Ni mtu mwenye staha na asopenda kunena mengi.
Waingereza hawana maana chembe. Wale jamaa zao walotoka zile Empire ziloangamia kule Romania,Greek na Russia ati wamewaweka kule Fulham,Kingston Upon Thames,Kensington na Belgravia,lakini huyu jamaa yetu wamemtupa pale Portsmouth.
Naona jamaa zako wamepatwa na Kibuki hapa jamvini,lakini haina neno Zali la Mentali atawaletea "chano" chao!
Ahsanta.
Ps; Kule kwenye ile List ya Wazee wetu nimekumbuka Sheikh Muharam alokua Imam wa Msikiti wa Mwinyikheir Akida pale Bibi Titi Bint Mohammed Road,Sheikh Digira alokua Imam wa msikiti w Makonde pale mtaa wa Nyamwezi na Sheikh Maalim Mohammed Mwita nafikiri alikua pale Al Masjid Badawy opposite na Soko Mjinga Kisutu.
Salaam Sheikh Islam wa pale Maweni Street Upanga...nilikua sana kwenye Madrasa yake na baadae pale Al Masjid Maamur Malik road. Vipi nduguyo Bwana Jidawy alokua Cargo Manager pale Lufthansa,naye pia salaam mno.
Jasusi,
Wewe umepokea kwa Judith Listowel.
Mimi nimekaa na Sheikh Haidar Mwinyimvua.
Sheikh Haidar Mwinyimvua ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wazee.
Halikadhalika alikuwa rafiki wa Sheikh Suleiman Takadir kisha wote ni
wa TANU Mvita Branch moja ya matawi yaliyokuwa na nguvu Tanganyika
nzima.
Wazungu waijue historia ya TANU kunishinda mie mjukuu wa mashujaa hawa?
Huo ni muhali.
Three things sum up Mwalimu Julius Nyerere for me. Sometime in the mid sixties a Swiss bank wrote offering to keep his money in a secret coded account at extremely generous interest rates.
It was a prudent proposition seeing that African governments were at the time falling to military coups at the rate of about one every six months. But far from jumping at the offer, the president published the letter in the national newspapers with the memorable declaration that he had no money to hide and that the little that he had could only be banked in Tanzania where it belonged.
Wickama,
Mkurya mwanaume halii. Mkurya mwanaume hahamishii matatizo yake kwingine. Mkurya mwanaume hajui kusingizia wala kuliahirisha tatizo. Hii ni kweli pia vikabila vingi vya jamii hiyo mkoani Mara. Hawa jamaa wanakabiliana na tatizo kama changamoto.
Wakurya wengi hawakwenda shule lakini hawamlaumu Mhaya au Mchaga wa Tanzania hii.
GOmgesugu,
..hebu tuliza munkari.
..siyo vizuri kutoa kauli za hasira namna hiyo.
..pamoja na hayo, kuna mambo umeyaandika hapo ningependa ufunguke zaidi.
..haswa suala la Hamza Aziz[r.i.p], Shekhe Yahya, Kitwana Kondo, Nyakyoma, na Mohamed Enterprise.
..kuna mahali unadai Kitwana Kondo alikuwa na nguvu kuliko Raisi Mwinyi!! WHAAAT!!?? R U KIDDING ME!!?
NB:
..kuhusu suala la meli ya SMZ kutumika kwa shughuli za KIJESHI, naomba uzingatie kwamba ULINZI na USALAMA ni masuala ya MUUNGANO.
..zaidi, naomba nitahadharishe kwamba Samora Machel hakuwa mkatoliki, bali Wareno aliokuwa akipigana nao ndiyo majority Wakatoliki. pia uzingatie kwamba Wareno walikuwa sehemu ya NATO.
..Umemlaumu Mwalimu Nyerere kwa kumsaidia Samora Machel. Je, una mtizamo gani kuhusu Raisi Mwinyi kumsaidia Joaquim Chissano baada ya Samora kuuwawa??
cc: Nguruvi3, Jasusi, Wickama
Du JF kiboko, leo tunasikia mzee saidi analisema lile lile alilolokuwa akiambiwa time and again hahahah!!!!!
@ Gombesugu, huyu Nyerere unayemzungumzia ni huyu hapa chini au?
Mzee Saidi unaweza kutusimulia kisa hiki kwa mapana zaidi?
Wanalia na BAKWATA wakati sheria za NCHI hii haziwazuii kuanzisha taasisi nyingine huru ya Kiislam hata kama ni kuirudisha EAMWS! Badala yake wanamtumia Sheikh Ponda kuvamia viwanja vya watu na kujenga msikiti wa mahema na kuuita wa Sheikh Amir!Mzee Mohamed anajua sana "brainwashing"Haki ya Mungu; ya leo kali. Hii mada inanipasua mbavu. Sasa Wilcard, lawama iwe ndani ya mapimo. Sio umlaumu mtu mwingine weeeeeeeeeeee kwa shamba lako kutopata mahindi mengi tangu mwaka 1974 huku walilima na hulitunzi ipasavyo!!!! Au ndio tena nyumba yako haipati wapangaji? Jamani majirani wabayaaaaaaaaa. kumbe wewe mwenyewe kelele tupu mpaka mtaani wanawatonya watafuta vyumba. Imagine wewe ni hizooooo tuuu kila mwaka? Karo za watoto zinasubiri wewe unalia na lawama za mahindi yako? Kama umeoa dada zangu wa kikurya tegemea yeye ndie atakuanzishia hiyo mijeledi (hahahahahahaha.......). Ni kama hili la Bakwata, Lawamaaaaaaaaaa, vibaraka haooooooooo; ofisi zenu kama vyoo....; Sawa, wenzao Bakwata tuliiiiii, "Mkisusa sisi twala". Like a video game.
Mazuri ya Mwalimu mzee wetu hakuyaona. Kama aliyaona, hayakumbuki. Kama anayakumbuka, asingeweza kuyasimulia. Ataonekana anaji-contradict na pia agenda yake kuu ya kulipa kisasi kwa Mwalimu haitatimia. Mtu MDINI kama Mwalimu asingeweza kuwa muadilifu kiasi hiki.Du JF kiboko, leo tunasikia mzee saidi analisema lile lile alilolokuwa akiambiwa time and again hahahah!!!!!
@ Gombesugu, huyu Nyerere unayemzungumzia ni huyu hapa chini au?
Mzee Saidi unaweza kutusimulia kisa hiki kwa mapana zaidi?