Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

gombesugu,

..sikuwa na nia ya kukutukana. neno "kufunguka" ni msamiati ulioibuka siku za karibuni.

..kwamba sijui mambo mengi ya inner workings of our government hilo siwezi kukubishia. ndiyo maana nawasisitiza nyinyi mnaojua mtuhabarishe kwa faida ya kizazi hiki na vijavyo.

..YES, niko very interested kujua nini kilitokea ktk vita vya Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Seychelles, Comoro, na kwingineko ambako wa-Tanzania walimwaga damu.

..mwisho, sikubaliani na utamaduni wa kumaliza mambo "kistaarabu." Tujielekeze kwenye kuusema ukweli wote. Wazungu wanasema "the truth shall set u free."

cc😡Jasusi, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo
 
Last edited by a moderator:

Boksi limenibana mkuu, hilo la mgodi ilikuwa zuga tu nilikuwa namzingua mzee Saidi hahahahha!!!!!! Lakini kubwa zaidi ni kuwa mada anazotembea nazo zali la mentali bahati mbaya huwa sina ujuzi nazo na hivyo siwezi kuchangia.
 
Wickama,

Naomba kukuliza au ikibidi tufanya mnakasha mie na wewe.

Wewe unasema Waislam walitakiwa kumshukuru Benjamin Mkapa kwa nini wamshukuru?

Hivi kwako hakuna dhulma yeyote ambayo umeishaiona wakifanyiwa Waislam?

Utanisamehe mimi sio Wickama, natumaini atakujibu. Unaifahamu Muslim University of Morogoro ambayo Prof Njozi yule Mwembechai ndie makamu mkuu wa chuo? Kazi ya Mkapa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Simulizi zako gombesugu zinafanana sana na za mzee wetu Mohamed. Haziwezi kuthibitika kwa namna yoyote ile. Mwalimu, Mzena na IGP Hamza wote marehemu. Kazi kwelikweli.

WildChild,

Mbona unajidhulumu uwezo wako wa kufikiri ndugu yangu!? Au unataka kuwa miongoni mwa wale wenye kujipunja!?

Sisi tunakusaidieni informations nyingi saana ambazo kwenu nyinyi ni kama ndoto za mchana,hamfahamu na wala hamtakubali milele mpaka siku ya Parapanda.

Hivi wewe unaposikia yakuwa Serikali ni "chombo";unafikiri ni chombo kama bakuli ama sahani!?

Hivi vitu vyoote ninavyokupa vimo kwenye Archives makhususi ndani ya Idara nyeti kwenye baadhi ya Wizara/sehemu.

Tatizo ni kuwa labda huna access za watu muhimu au hizo "sehemu" huzijui!?


Mimi nimekupeni watu muhimu wengi walio hai kwanini hamwendi kuwauliza,tena nyinyi baadhi yenu nasikia ati ni Waandishi wa habari mahiri!? Tena hao watu nilokutajieni ni Wakristo wenzenu watiifu wa Mungu...acheni utoto wa kulalamika bila sababu za maana. Au na nyie mnakuwa kama watoto/watu wa Madrassa!?

Narejea tena,mfuateni Timothy Apiyo,Joseph Butiku,Sinde Warioba,Mabere Marando,Dominick Gama,John Malecela,Msangi wa PCCB/TAKUKURU,Augustine Mrema,Apson Mwalongo na wengineo wengi muwatakao nyinyi.

Na kama hamtojali akili za Madrassa basi kamuoneni Mzee KK,nasikia siku hizi yupo sana pale Mjimwema.

Vipi ile habari ya Gapex,au umetosheka kwa sababu tu mwenzenu Jasusi kaunga mkono kiduchu!? Punguzeni chuki na udini ndugu zangu.

Kamtafute pia J. Nyakyoma na Gulam Dewji kabla hawajafa ili msijesema ati tunasubiri watu wafe ndo tunaanza kutunga vitabu.

Nakuhakikishia,haya "matambara" yangu hata huyo Nyerere wako angekuwapo asingethubutu kujibu au kutia mguu wake kwenye nakma kama hizi. Labda angejitia tu "apambani za Mtonga",na kutumia zile "hekima na busara za Mwalimu" kwa kukaa kimya na kutojibu milele na milele.

Nashukuru,lakini tafadhali naomba usiniandikie tena maana nina dharura na sintapata fursa ya kukujibu.

Ahsanta.


Cc; Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3

Jitayarisheni nikipata fursa japo kiduchu I'm coming for you two ok! I will leave no stone unturned...
 
gombesugu,

..na mimi nakusubiri!!

..tayari nimetayarisha shawarma na fanta. ma-taptap nimepumzika kwa ajili ya darsa lako!! LOL!!

..ila utakapotoa majibu yako kuhusu masuala ya Msumbiji naomba "um-cc" mwana JF anayeitwa Kudi Shauri.

..huyo jamaa ana taarifa nyingi sana kuhusu zama hizo na atakuwa wa msaada mkubwa ktk mnakasha wetu.

..sisi tunachotaka ni UKWELI.
 
Boksi limenibana mkuu, hilo la mgodi ilikuwa zuga tu nilikuwa namzingua mzee Saidi hahahahha!!!!!! Lakini kubwa zaidi ni kuwa mada anazotembea nazo zali la mentali bahati mbaya huwa sina ujuzi nazo na hivyo siwezi kuchangia.

Nyambala,

Tafadhali pata fursa kidogo uje kucheka hapa jamvini!ahahaha!!

Na mimi nimeamua kuwaendea "kindava" Wazee wako Nguruvi3 na Mag3!ahahaha!! Wanajifungia ndani hapa jamvini wanachungulia tu siku hizi...njoo uje kuwapa msaada japo kiduchu!ahahah!!
 
 
Du JF kiboko, leo tunasikia mzee saidi analisema lile lile alilolokuwa akiambiwa time and again hahahah!!!!!

@ Gombesugu, huyu Nyerere unayemzungumzia ni huyu hapa chini au?



Mzee Saidi unaweza kutusimulia kisa hiki kwa mapana zaidi?

Nyambala,
Nishakwambia mara nyingi sana.

Ikiwa wewe unaona habari nilizopokea kwa wazee wangu ni uongo
basi njoo na zako zilizokuwa na ithbati.

Tatizo kubwa ni kuwa hukupata kujua ukweli, hadhi na uadilifu wa
watu hawa.

Hivi kama mimi simwamini Sheikh Hassan bin Amir au Shariff Attas
hivi nitamwamini nani katika kumjua Nyerere?

Hilo la Nyerere na benki ya Uswiss ni maarufu.
Mkasa ule alikuwa na rafiki yake Amir Jamal.
 
Wickama uko vizuri unajua nikisoma post zako naelimika sana keep it up bro.
Duh! ajabu na kweli! mimi nilidhani huwa unaelimika na post za mzee mchochezi Mohamed Said peke yake! nampa hongera sana Wickama naona anaweza kukuongoa kwenye makucha ya muovu!
 
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.
 

Mzee Saidi hoja yangu hapo kama utakumbuka umeshawahi kuambiwa mara nyingi kuhusu ujuzi wa masuala ya hapo kwetu kuwa tunayafahamu zaidi kuliko wageni wa nchi hiyo. Hilo wewe ulikuwa hulikubali sasa naona sasa hivi umekiri mwenyewe!!!!!
 

JokaKuu,

Haina neno ndugu yangu,sisi soote ni wamoja usijali.

Hapa jamvini nafikiri kila mmoja anapata kusoma kwa mwenzie,hakuna anaejua zaidi ya mwengine. Ndo maana ni vizuri pale tunapoeana fursa ya kusikizana na kuulizana maswali kwa utuvu.

Mimi binafsi nipo hapa chini ya uangalizi wa Sheikh Mohammed Said. Na namsikiza kwa utuvu uso shaka.

Ahsanta.
 
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.
Mzee Mohamed,
Mwogope Mungu wetu. Yaani Mufti, Alhad Mussa Salum,..., sio watu? Hili la kutoikubali wewe BAKWATA limekuwa neema na baraka kwa nchi yetu. Hata CCM, CHADEMA, TEC, CCT, sio sote tunazikubali taasisi na asasi hizi.
 
Mzee Mohamed,

Amir Jamal alikuwa DINI gani?
 
 
Last edited by a moderator:
Utanisamehe mimi sio Wickama, natumaini atakujibu. Unaifahamu Muslim University of Morogoro ambayo Prof Njozi yule Mwembechai ndie makamu mkuu wa chuo? Kazi ya Mkapa hiyo.

Bila samahani, Unayakumbuka Mauaji ya Mwembwechai na Mauaji ya Pemba? Kazi ya Mkapa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.

Heshima kwako Mzee MS; Mi naona wao ni tuli kwa vile nyie "mbadala" mmeshakuwa wengi kiasi haina tija kwao kwamba wamjibu nani. Pia wana the largest grassroot support ambayo "mbadala" hawana. Kutokana na hili ndio maana ukifuatilia baadhi ya kauli za karibuni za misikiti na vyombo vya habari vya dhehebu moja machachari (at least waliingia wakiwa hivyo), zipo dalili njema kuwa wanaanza kuiona kweli kuwa wanawahitaji Bakwata kama partners. Sasa Masheikh wanaongea japo kwa "measured tones" kuwa "waislamu ni vizuri tukashirikiana tukawa wamoja hata kama ni kufanya kazi kwa karibu na wenzetu wa Bakwata, ni katika sunna alizoacha Mtume (saw) wetu". Kwa hiari sitalitaja. Lakini nyie tena, magwiji wa network na sensors kila mahali lazima mmeshawajua. Haya bwana, better late than never. Wanaanza kuikumbuka shuka karibu na alfajiri. Haijalishi. Time does not stop, LAKINI people age, degrade and step out for others.

Ukisema hamna watu Bakwata you could right or wrong. Inategemea aina ya ANALYSIS. Ni pale utakapo- sherehesha maana yako ya WATU ndipo tutaliweka mezani hilo. Mzee MS; mimi NAKUHISI wewe ni hostile dhidi ya Taasisi ya Bakwata (I will be glad to be wrong). Ila sijui uhasimu wako ni kwa TAASISI kama Taasisi, au ni kwa wale waliyomo ndani yake. On record ulishasema taasisi hii (Bakwata) ina ofisi kama vyoo vya serikali (tusi, au pengine utasema; Wickama, inategemea umekulia wapi) na ni kibaraka (tusi tena). Kwa hiyo mimi nakuhisi wewe na pengine sio peke yako, unaichukia sana taasisi hii. Ila sioni kama hiyo ndiyo TIBA. Wala sioni kama dawa ni kuunda taasisi mbadala kila siku. Kama kuna pa kuanzia ni kwenye attitudes za waislamu towards each other and towards taasisi kama hizi. Bila hilo, daftari la registrar litajaa hizi taasisi ambazo zitabakia dar, Tanga na Morogoro. jioni njema.
 

Wild Card,
Ndugu zangu wa Musoma hebu waulizeni wazee khabari
za Sheikh Mohamed Mvamila aliyeishi Musoma na kusomesha
dini hapo kati ya vita mbili za dunia.
 
Wickama,

Naomba kukuliza au ikibidi tufanya mnakasha mie na wewe.

Wewe unasema Waislam walitakiwa kumshukuru Benjamin Mkapa kwa nini wamshukuru?

Hivi kwako hakuna dhulma yeyote ambayo umeishaiona wakifanyiwa Waislam?

Ritz nashukuru kwa ujumbe wako; Masula ya Mkapa niliyoongelea ni yale nayoyajua mimi (1) alitoa kibali majengo ya TANESCO institute Morogoro kutumiwa kama Muslim University (2) alifanya jitihada za kujenga (kumshawishi Marehemu Gaddafi) kujenga ule msikiti wa pale Dodoma. Nikasema kwa mawili haya ilikuwa uungwana kusema shukran. Ukifuatilia threads zangu sijawahi kumkingia Mkapa kifua dhidi ya tuhuma utakazozikuta katika majadiliano mengine yanayoendelea humu. Huwa sichangii kitu kama sina data za kunitosha. I hope nimekujibu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…