Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JokaKuu,

I can confirm without knowing you and where you are /your location that,you know nothing about the Government inner workings and its system.

Una maana ipi unaposema "nifunguke zaidi"!? Haya kwetu ni matusi yaso kiasi ndugu yangu. Au ndo Kiswahili cha kisasa na cha mjini!?

Masuala ya Nyakyoma na Mohammed Enterprises,tayari nilishamalizana na Jasusi(ambaye kwa sababu mzijuazo wenyewe ndie mnaemuamini zaidi kuliko mimi wa Madrassa).

Pia lile suala la Mzee KK ,Jasusi alitumia ustaarabu na kuniepushia Premier League na nyinyi. Jasusi amekuthibitishia tena akakupa na mfano wa matamshi ya Mzee Paul Bomani.

Inaelekea umevamia hoja zangu kwa pupa. Hayo mambo ya Meli ya SMZ mbona nilikupa kiduchu tu. Nina mengi saana. Pale nilikua tu naonyesha ukaidi wa Nyerere kiduchu tu kwa kutokufuata kwake Sharia/Ushauri,kama ulipata wasaa wa kuangalia zile points zangu kwa kina!?

Habari za Mozambique,nakusihi fanya sabra tuimalize shughuli hii. Halafu nikupe darsa,nitakuanzia tangia kifo cha Eduardo Mondlane pale D'Salaam,Internal struggle na mtafaruku ndani ya Frelimo,kuhusishwa kwa Nyerere kwenye kifo cha Mondlane,ukaribu na prefference/choice ya Nyerere kwa Samora Machel,unyama na ushenzi uso mfano ulofanywa na Majeshi ya Tanzania dhidi ya wananchi na raia wasio na hatia wa Mozambique,mkono wa Nyerere/influence na jinsi alivyosababisha RENAMO na FRELIMO kuendeleza vita na khitilafu baina yao na mengineyo mengi.

Nina picha nipo pale Estadio da Machava formerly known as Estadio Salazar 1975. Wanajamvi,niwieni radhi ningeiweka hapa lakini ni group photograph na wahusika wengine itakua si busara asilan kuwaanika hapa.

Ile habari ya sheikh Yahya Hussein uliyoitaka ni ndefu mno na mambo ni mengi saana. Ule ulikua ni mfano tu wa hoja. Nakuongezea tena kiduchu. Sheikh Yahya Hussein,ni mmojawapo wa Watanzania wachache mno,waliokua wanamsaidia Nyerere dhidi ya makaburu wa South Afrika ndani ya South Afrika.
Sheikh Yahya Hussein, kwa kutumia influence na connection yake kwa King wa Swaziland,alifungua "offices" ndani ya South Afrika miji tafauti,Lusaka na London ili kuwasaidia ANC kama alivyotaka na kuomba Nyerere. Nafikiri wengi wenu mnakumbuka jinsi gani ilikua ni risk kubwa mno kufanza mambo hayo wakati huo wa vikwazo dhidi ya Makaburu na kama je kama Makaburu wenyewe wangemgundua!? Sheikh Yahya Hussein ni katika Watanzania wachache wakti huo alokua na passports za UK,Swaziland,Kenya...na zoote hizo alipewa na Marais/Wafalme wa nchi hizo mkononi mwake.

Kama unahitaji tena hizi "habari za vinyozi wa Kipata na Mkunguni";nifahamishe nami tajaribu kutafuta fursa. Itanilazim siku nyingine nikuonyeshe kwanini nilisema Nyerere alikosa fadhila au kumkumbuka Sheikh Yahya Hussein!?

Ahsanta na tuendelee na mnakasha.
gombesugu,

..sikuwa na nia ya kukutukana. neno "kufunguka" ni msamiati ulioibuka siku za karibuni.

..kwamba sijui mambo mengi ya inner workings of our government hilo siwezi kukubishia. ndiyo maana nawasisitiza nyinyi mnaojua mtuhabarishe kwa faida ya kizazi hiki na vijavyo.

..YES, niko very interested kujua nini kilitokea ktk vita vya Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Seychelles, Comoro, na kwingineko ambako wa-Tanzania walimwaga damu.

..mwisho, sikubaliani na utamaduni wa kumaliza mambo "kistaarabu." Tujielekeze kwenye kuusema ukweli wote. Wazungu wanasema "the truth shall set u free."

cc😡Jasusi, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo
 
Last edited by a moderator:
Nyambala,

Mbona umeadimika ndugu yangu na kuniacha kwenye hii bahari ya Manyangumi peke yangu mimi mgeni hapa jamvini!?

Nilifikiri mnafahamiana na yule jamaa Zali la Mentali,maana nasikia nae anafanya kazi za kwenye migodi kama wewe. Lakini yeye ni Mchimba Chumvi...sijui wewe mwenzetu wachimbani!?
Haina neno tuendelee na mnakasha.

Boksi limenibana mkuu, hilo la mgodi ilikuwa zuga tu nilikuwa namzingua mzee Saidi hahahahha!!!!!! Lakini kubwa zaidi ni kuwa mada anazotembea nazo zali la mentali bahati mbaya huwa sina ujuzi nazo na hivyo siwezi kuchangia.
 
Wickama,

Naomba kukuliza au ikibidi tufanya mnakasha mie na wewe.

Wewe unasema Waislam walitakiwa kumshukuru Benjamin Mkapa kwa nini wamshukuru?

Hivi kwako hakuna dhulma yeyote ambayo umeishaiona wakifanyiwa Waislam?

Utanisamehe mimi sio Wickama, natumaini atakujibu. Unaifahamu Muslim University of Morogoro ambayo Prof Njozi yule Mwembechai ndie makamu mkuu wa chuo? Kazi ya Mkapa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Simulizi zako gombesugu zinafanana sana na za mzee wetu Mohamed. Haziwezi kuthibitika kwa namna yoyote ile. Mwalimu, Mzena na IGP Hamza wote marehemu. Kazi kwelikweli.

WildChild,

Mbona unajidhulumu uwezo wako wa kufikiri ndugu yangu!? Au unataka kuwa miongoni mwa wale wenye kujipunja!?

Sisi tunakusaidieni informations nyingi saana ambazo kwenu nyinyi ni kama ndoto za mchana,hamfahamu na wala hamtakubali milele mpaka siku ya Parapanda.

Hivi wewe unaposikia yakuwa Serikali ni "chombo";unafikiri ni chombo kama bakuli ama sahani!?

Hivi vitu vyoote ninavyokupa vimo kwenye Archives makhususi ndani ya Idara nyeti kwenye baadhi ya Wizara/sehemu.

Tatizo ni kuwa labda huna access za watu muhimu au hizo "sehemu" huzijui!?


Mimi nimekupeni watu muhimu wengi walio hai kwanini hamwendi kuwauliza,tena nyinyi baadhi yenu nasikia ati ni Waandishi wa habari mahiri!? Tena hao watu nilokutajieni ni Wakristo wenzenu watiifu wa Mungu...acheni utoto wa kulalamika bila sababu za maana. Au na nyie mnakuwa kama watoto/watu wa Madrassa!?

Narejea tena,mfuateni Timothy Apiyo,Joseph Butiku,Sinde Warioba,Mabere Marando,Dominick Gama,John Malecela,Msangi wa PCCB/TAKUKURU,Augustine Mrema,Apson Mwalongo na wengineo wengi muwatakao nyinyi.

Na kama hamtojali akili za Madrassa basi kamuoneni Mzee KK,nasikia siku hizi yupo sana pale Mjimwema.

Vipi ile habari ya Gapex,au umetosheka kwa sababu tu mwenzenu Jasusi kaunga mkono kiduchu!? Punguzeni chuki na udini ndugu zangu.

Kamtafute pia J. Nyakyoma na Gulam Dewji kabla hawajafa ili msijesema ati tunasubiri watu wafe ndo tunaanza kutunga vitabu.

Nakuhakikishia,haya "matambara" yangu hata huyo Nyerere wako angekuwapo asingethubutu kujibu au kutia mguu wake kwenye nakma kama hizi. Labda angejitia tu "apambani za Mtonga",na kutumia zile "hekima na busara za Mwalimu" kwa kukaa kimya na kutojibu milele na milele.

Nashukuru,lakini tafadhali naomba usiniandikie tena maana nina dharura na sintapata fursa ya kukujibu.

Ahsanta.


Cc; Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3

Jitayarisheni nikipata fursa japo kiduchu I'm coming for you two ok! I will leave no stone unturned...
 
gombesugu,

..na mimi nakusubiri!!

..tayari nimetayarisha shawarma na fanta. ma-taptap nimepumzika kwa ajili ya darsa lako!! LOL!!

..ila utakapotoa majibu yako kuhusu masuala ya Msumbiji naomba "um-cc" mwana JF anayeitwa Kudi Shauri.

..huyo jamaa ana taarifa nyingi sana kuhusu zama hizo na atakuwa wa msaada mkubwa ktk mnakasha wetu.

..sisi tunachotaka ni UKWELI.
 
Boksi limenibana mkuu, hilo la mgodi ilikuwa zuga tu nilikuwa namzingua mzee Saidi hahahahha!!!!!! Lakini kubwa zaidi ni kuwa mada anazotembea nazo zali la mentali bahati mbaya huwa sina ujuzi nazo na hivyo siwezi kuchangia.

Nyambala,

Tafadhali pata fursa kidogo uje kucheka hapa jamvini!ahahaha!!

Na mimi nimeamua kuwaendea "kindava" Wazee wako Nguruvi3 na Mag3!ahahaha!! Wanajifungia ndani hapa jamvini wanachungulia tu siku hizi...njoo uje kuwapa msaada japo kiduchu!ahahah!!
 
gombesugu,

..na mimi nakusubiri!!

..ila utakapotoa majibu yako naomba kuhusu masuala ya Msumbiji "um-cc" mwana JF anayeitwa Kudi Shauri.

JokaKuu,

Mbona unaanza kunitisha kunitajia majina ya wachezaji wa kulipwa!?...haina neno na mimi nakutangulizia Sheikh Mohammed Bin Said. Kazi kwako!

Halafu vipi yakhe,waanza kunita mrongo hata mnakasha hatujaanza!?
 
Du JF kiboko, leo tunasikia mzee saidi analisema lile lile alilolokuwa akiambiwa time and again hahahah!!!!!

@ Gombesugu, huyu Nyerere unayemzungumzia ni huyu hapa chini au?



Mzee Saidi unaweza kutusimulia kisa hiki kwa mapana zaidi?

Nyambala,
Nishakwambia mara nyingi sana.

Ikiwa wewe unaona habari nilizopokea kwa wazee wangu ni uongo
basi njoo na zako zilizokuwa na ithbati.

Tatizo kubwa ni kuwa hukupata kujua ukweli, hadhi na uadilifu wa
watu hawa.

Hivi kama mimi simwamini Sheikh Hassan bin Amir au Shariff Attas
hivi nitamwamini nani katika kumjua Nyerere?

Hilo la Nyerere na benki ya Uswiss ni maarufu.
Mkasa ule alikuwa na rafiki yake Amir Jamal.
 
Wickama uko vizuri unajua nikisoma post zako naelimika sana keep it up bro.
Duh! ajabu na kweli! mimi nilidhani huwa unaelimika na post za mzee mchochezi Mohamed Said peke yake! nampa hongera sana Wickama naona anaweza kukuongoa kwenye makucha ya muovu!
 
Haki ya Mungu; ya leo kali. Hii mada inanipasua mbavu. Sasa Wilcard, lawama iwe ndani ya mapimo. Sio umlaumu mtu mwingine weeeeeeeeeeee kwa shamba lako kutopata mahindi mengi tangu mwaka 1974 huku walilima na hulitunzi ipasavyo!!!! Au ndio tena nyumba yako haipati wapangaji? Jamani majirani wabayaaaaaaaaa. kumbe wewe mwenyewe kelele tupu mpaka mtaani wanawatonya watafuta vyumba. Imagine wewe ni hizooooo tuuu kila mwaka? Karo za watoto zinasubiri wewe unalia na lawama za mahindi yako? Kama umeoa dada zangu wa kikurya tegemea yeye ndie atakuanzishia hiyo mijeledi (hahahahahahaha.......).

Ni kama hili la Bakwata, Lawamaaaaaaaaaa, vibaraka haooooooooo; ofisi zenu kama vyoo....; Sawa, wenzao Bakwata tuliiiiii, "Mkisusa sisi twala". Like a video game.
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.
 
Nyambala,
Nishakwambia mara nyingi sana.

Ikiwa wewe unaona habari nilizopokea kwa wazee wangu ni uongo
basi njoo na zako zilizokuwa na ithbati.

Tatizo kubwa ni kuwa hukupata kujua ukweli, hadhi na uadilifu wa
watu hawa.

Hivi kama mimi simwamini Sheikh Hassan bin Amir au Shariff Attas
hivi nitamwamini nani katika kumjua Nyerere?

Hilo la Nyerere na benki ya Uswiss ni maarufu.
Mkasa ule alikuwa na rafiki yake Amir Jamal.

Mzee Saidi hoja yangu hapo kama utakumbuka umeshawahi kuambiwa mara nyingi kuhusu ujuzi wa masuala ya hapo kwetu kuwa tunayafahamu zaidi kuliko wageni wa nchi hiyo. Hilo wewe ulikuwa hulikubali sasa naona sasa hivi umekiri mwenyewe!!!!!
 
gombesugu,

..sikuwa na nia ya kukutukana. neno "kufunguka" ni msamiati ulioibuka siku za karibuni.

..kwamba sijui mambo mengi ya inner workings of our government hilo siwezi kukubishia. ndiyo maana nawasisitiza nyinyi mnaojua mtuhabarishe kwa faida ya kizazi hiki na vijavyo.

..YES, niko very interested kujua nini kilitokea ktk vita vya Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Seychelles, Comoro, na kwingineko ambako wa-Tanzania walimwaga damu.

..mwisho, sikubaliani na utamaduni wa kumaliza mambo "kistaarabu." Tujielekeze kwenye kuusema ukweli wote. Wazungu wanasema "the truth shall set u free."

cc😡Jasusi, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo

JokaKuu,

Haina neno ndugu yangu,sisi soote ni wamoja usijali.

Hapa jamvini nafikiri kila mmoja anapata kusoma kwa mwenzie,hakuna anaejua zaidi ya mwengine. Ndo maana ni vizuri pale tunapoeana fursa ya kusikizana na kuulizana maswali kwa utuvu.

Mimi binafsi nipo hapa chini ya uangalizi wa Sheikh Mohammed Said. Na namsikiza kwa utuvu uso shaka.

Ahsanta.
 
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.
Mzee Mohamed,
Mwogope Mungu wetu. Yaani Mufti, Alhad Mussa Salum,..., sio watu? Hili la kutoikubali wewe BAKWATA limekuwa neema na baraka kwa nchi yetu. Hata CCM, CHADEMA, TEC, CCT, sio sote tunazikubali taasisi na asasi hizi.
 
Nyambala,
Nishakwambia mara nyingi sana.

Ikiwa wewe unaona habari nilizopokea kwa wazee wangu ni uongo
basi njoo na zako zilizokuwa na ithbati.

Tatizo kubwa ni kuwa hukupata kujua ukweli, hadhi na uadilifu wa
watu hawa.

Hivi kama mimi simwamini Sheikh Hassan bin Amir au Shariff Attas
hivi nitamwamini nani katika kumjua Nyerere?

Hilo la Nyerere na benki ya Uswiss ni maarufu.
Mkasa ule alikuwa na rafiki yake Amir Jamal.
Mzee Mohamed,

Amir Jamal alikuwa DINI gani?
 
gombesugu,

..na mimi nakusubiri!!

..ila utakapotoa majibu yako naomba kuhusu masuala ya Msumbiji "um-cc" mwana JF anayeitwa Kudi Shauri.

JokaKuu,

Mbona unaanza kunitisha kunitajia majina ya wachezaji wa kulipwa!?...haina neno na mimi nakutangulizia Sheikh Mohammed Bin Said. Kazi kwako!

Halafu vipi yakhe,waanza kunita mrongo hata mnakasha hatujaanza!?
gombesugu,

..u must have misunderstood what i wrote.

..Masuala ya Msumbiji siyafahamu, kwa hiyo siwezi kukuita mrongo.

..Ila ungesema kuhusu masuala ya namba za mtihani; kwamba kabla ya Prof.Malima kulikuwa hakuna namba, hapo ningekuita mrongo kwasababu nimefanya mitihani ya kitaifa mara 3, na zote nilitumia namba siyo jina.

..nimekushauri um-cc Kudi Shauri kwasababu naamini na yeye ana uelewa fulani kuhusu Msumbiji. U may end up exchanging notes, and even forge a friendship.
 
Last edited by a moderator:
Utanisamehe mimi sio Wickama, natumaini atakujibu. Unaifahamu Muslim University of Morogoro ambayo Prof Njozi yule Mwembechai ndie makamu mkuu wa chuo? Kazi ya Mkapa hiyo.

Bila samahani, Unayakumbuka Mauaji ya Mwembwechai na Mauaji ya Pemba? Kazi ya Mkapa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Wickama,
BAKWATA ni tuli kwa kuwa hakuna watu.

Heshima kwako Mzee MS; Mi naona wao ni tuli kwa vile nyie "mbadala" mmeshakuwa wengi kiasi haina tija kwao kwamba wamjibu nani. Pia wana the largest grassroot support ambayo "mbadala" hawana. Kutokana na hili ndio maana ukifuatilia baadhi ya kauli za karibuni za misikiti na vyombo vya habari vya dhehebu moja machachari (at least waliingia wakiwa hivyo), zipo dalili njema kuwa wanaanza kuiona kweli kuwa wanawahitaji Bakwata kama partners. Sasa Masheikh wanaongea japo kwa "measured tones" kuwa "waislamu ni vizuri tukashirikiana tukawa wamoja hata kama ni kufanya kazi kwa karibu na wenzetu wa Bakwata, ni katika sunna alizoacha Mtume (saw) wetu". Kwa hiari sitalitaja. Lakini nyie tena, magwiji wa network na sensors kila mahali lazima mmeshawajua. Haya bwana, better late than never. Wanaanza kuikumbuka shuka karibu na alfajiri. Haijalishi. Time does not stop, LAKINI people age, degrade and step out for others.

Ukisema hamna watu Bakwata you could right or wrong. Inategemea aina ya ANALYSIS. Ni pale utakapo- sherehesha maana yako ya WATU ndipo tutaliweka mezani hilo. Mzee MS; mimi NAKUHISI wewe ni hostile dhidi ya Taasisi ya Bakwata (I will be glad to be wrong). Ila sijui uhasimu wako ni kwa TAASISI kama Taasisi, au ni kwa wale waliyomo ndani yake. On record ulishasema taasisi hii (Bakwata) ina ofisi kama vyoo vya serikali (tusi, au pengine utasema; Wickama, inategemea umekulia wapi) na ni kibaraka (tusi tena). Kwa hiyo mimi nakuhisi wewe na pengine sio peke yako, unaichukia sana taasisi hii. Ila sioni kama hiyo ndiyo TIBA. Wala sioni kama dawa ni kuunda taasisi mbadala kila siku. Kama kuna pa kuanzia ni kwenye attitudes za waislamu towards each other and towards taasisi kama hizi. Bila hilo, daftari la registrar litajaa hizi taasisi ambazo zitabakia dar, Tanga na Morogoro. jioni njema.
 
Kwa wale wa Mara na Tarime,nanyi pia nakuja hukohuko na nitaanza kwa kukuonyesheni ya kuwa huyo Nyerere wenu kaanza kula fadhila za Wazee wetu toke pale Musoma kwa Mzee Makongoro na Masheikh wengine wengi tu huko mabara. Nina tambara chafu saana la Nyerere alowafanyia kina Issa Makongoro na Sheikh Abdallah Mwita. Kwa hakika yule mtu alikua hakumbuki kabisa fadhila. Kila nikisoma hiyo hotuba ya upuuzi aloiweka huyo Yericko hapo juu,basi Wallahi nakumbuka jinsi gani Nyerere alishindwa hata kwenda mazikoni/msibani kwa Sheikh mohammed Yahya Ramia pale Bagamoyo. Alipopashwa habari na AbdilRahman Ramia,akadai ati yuko very busy kwenye simu na yule "changumemenya" Samora Machel!? Sijawahi kusikia maongezi ya simu ya siku nzima!? Na kuwasahau walokuweka na kukufadhili kwenye hayo madaraka!?

Gombesugu,
Mwalimu alimheshimu sana Chief Makongoro. Hata huyu kijana wa Mwalimu, Charles Makongoro, ameitwa jina hilo kwa heshima ya huyu mzee. Katika familia ya Mwalimu ni Charles huyu ndie kaoa binti safi wa Kiislam anayeitwa Aisha ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Achana na akina Issa matapeli hawa.

Wild Card,
Ndugu zangu wa Musoma hebu waulizeni wazee khabari
za Sheikh Mohamed Mvamila aliyeishi Musoma na kusomesha
dini hapo kati ya vita mbili za dunia.
 
Wickama,

Naomba kukuliza au ikibidi tufanya mnakasha mie na wewe.

Wewe unasema Waislam walitakiwa kumshukuru Benjamin Mkapa kwa nini wamshukuru?

Hivi kwako hakuna dhulma yeyote ambayo umeishaiona wakifanyiwa Waislam?

Ritz nashukuru kwa ujumbe wako; Masula ya Mkapa niliyoongelea ni yale nayoyajua mimi (1) alitoa kibali majengo ya TANESCO institute Morogoro kutumiwa kama Muslim University (2) alifanya jitihada za kujenga (kumshawishi Marehemu Gaddafi) kujenga ule msikiti wa pale Dodoma. Nikasema kwa mawili haya ilikuwa uungwana kusema shukran. Ukifuatilia threads zangu sijawahi kumkingia Mkapa kifua dhidi ya tuhuma utakazozikuta katika majadiliano mengine yanayoendelea humu. Huwa sichangii kitu kama sina data za kunitosha. I hope nimekujibu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom