gombesugu,JokaKuu,
I can confirm without knowing you and where you are /your location that,you know nothing about the Government inner workings and its system.
Una maana ipi unaposema "nifunguke zaidi"!? Haya kwetu ni matusi yaso kiasi ndugu yangu. Au ndo Kiswahili cha kisasa na cha mjini!?
Masuala ya Nyakyoma na Mohammed Enterprises,tayari nilishamalizana na Jasusi(ambaye kwa sababu mzijuazo wenyewe ndie mnaemuamini zaidi kuliko mimi wa Madrassa).
Pia lile suala la Mzee KK ,Jasusi alitumia ustaarabu na kuniepushia Premier League na nyinyi. Jasusi amekuthibitishia tena akakupa na mfano wa matamshi ya Mzee Paul Bomani.
Inaelekea umevamia hoja zangu kwa pupa. Hayo mambo ya Meli ya SMZ mbona nilikupa kiduchu tu. Nina mengi saana. Pale nilikua tu naonyesha ukaidi wa Nyerere kiduchu tu kwa kutokufuata kwake Sharia/Ushauri,kama ulipata wasaa wa kuangalia zile points zangu kwa kina!?
Habari za Mozambique,nakusihi fanya sabra tuimalize shughuli hii. Halafu nikupe darsa,nitakuanzia tangia kifo cha Eduardo Mondlane pale D'Salaam,Internal struggle na mtafaruku ndani ya Frelimo,kuhusishwa kwa Nyerere kwenye kifo cha Mondlane,ukaribu na prefference/choice ya Nyerere kwa Samora Machel,unyama na ushenzi uso mfano ulofanywa na Majeshi ya Tanzania dhidi ya wananchi na raia wasio na hatia wa Mozambique,mkono wa Nyerere/influence na jinsi alivyosababisha RENAMO na FRELIMO kuendeleza vita na khitilafu baina yao na mengineyo mengi.
Nina picha nipo pale Estadio da Machava formerly known as Estadio Salazar 1975. Wanajamvi,niwieni radhi ningeiweka hapa lakini ni group photograph na wahusika wengine itakua si busara asilan kuwaanika hapa.
Ile habari ya sheikh Yahya Hussein uliyoitaka ni ndefu mno na mambo ni mengi saana. Ule ulikua ni mfano tu wa hoja. Nakuongezea tena kiduchu. Sheikh Yahya Hussein,ni mmojawapo wa Watanzania wachache mno,waliokua wanamsaidia Nyerere dhidi ya makaburu wa South Afrika ndani ya South Afrika.
Sheikh Yahya Hussein, kwa kutumia influence na connection yake kwa King wa Swaziland,alifungua "offices" ndani ya South Afrika miji tafauti,Lusaka na London ili kuwasaidia ANC kama alivyotaka na kuomba Nyerere. Nafikiri wengi wenu mnakumbuka jinsi gani ilikua ni risk kubwa mno kufanza mambo hayo wakati huo wa vikwazo dhidi ya Makaburu na kama je kama Makaburu wenyewe wangemgundua!? Sheikh Yahya Hussein ni katika Watanzania wachache wakti huo alokua na passports za UK,Swaziland,Kenya...na zoote hizo alipewa na Marais/Wafalme wa nchi hizo mkononi mwake.
Kama unahitaji tena hizi "habari za vinyozi wa Kipata na Mkunguni";nifahamishe nami tajaribu kutafuta fursa. Itanilazim siku nyingine nikuonyeshe kwanini nilisema Nyerere alikosa fadhila au kumkumbuka Sheikh Yahya Hussein!?
Ahsanta na tuendelee na mnakasha.
..sikuwa na nia ya kukutukana. neno "kufunguka" ni msamiati ulioibuka siku za karibuni.
..kwamba sijui mambo mengi ya inner workings of our government hilo siwezi kukubishia. ndiyo maana nawasisitiza nyinyi mnaojua mtuhabarishe kwa faida ya kizazi hiki na vijavyo.
..YES, niko very interested kujua nini kilitokea ktk vita vya Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Seychelles, Comoro, na kwingineko ambako wa-Tanzania walimwaga damu.
..mwisho, sikubaliani na utamaduni wa kumaliza mambo "kistaarabu." Tujielekeze kwenye kuusema ukweli wote. Wazungu wanasema "the truth shall set u free."
cc😡Jasusi, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo
Last edited by a moderator: