Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Haahaaa safi sana mkuu,

Waliokuwa hawakuelewi sasa wamekuelewa,

Nalikusoma na kukuelewa ungali nje ya mnakasha huu, naaam nalitulia na kukujibu kwa hoja, abadani hasilani hukuthubutu kutengua medula za waungwana!
 

Mbona unamjibia kinyume wakati yeye ameshajibu ukweli halisi?
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere,

Samahani nilikuwa sijayaona majibu halisi ya Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:

Ritz,
Nakushukuru sana.
 
Swali...imedaiwa na Mohamed Said kuwa wazee wake hawakumfahamu kabla ya kukanyaga Dar es Salaaam mwaka 1952, je ni mwaka gani Dossa Aziz alikutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza?
 
Mohamed Said, hivi kweli mtu utakuwa sawa kichwani kama unaandika hivi...

Angalau leo umefunguka...

Bwana Sweke hiki kisa cha Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere hata TANU wakikiogopa
kukikhadithia.

Nakiweka hapa kwa faida ya wanaukumbi ili wajue tulikotoka:

''Baada ya kurejea kutoka Tabora, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, Elias Kassenge na Bhoke Munanka walifuatana na Nyerere kwenye ziara ya Jimbo la Mashariki kuwaeleza watu umuhimu na maana halisi ya uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Nyerere aliwafafanulia watu kile ambacho Waafrika wangepoteza endapo TANU ingesusia uchaguzi.

Lakini Sheikh Takadir alikuwa akishiriki katika mikutano ile kimwili tu; moyo na fikra zake havikuwa pale. Alikuwa na wasiwasi jinsi matukio yalivyokuwa yakitokea katika TANU na namna siasa ilivyokuwa ikichukua mwelekeo mpya.

Sheikh Takadir alikuwa anautazama kwa hofu uongozi wa Wakristo katika TANU ambao ulikuwa ukielekea kuchukua uongozi baada kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria.

Kwa sababu ya yale masharti magumu ya uchaguzi, TANU ilibidi itazame nje ya uongozi wake ili kupata wagombea uchaguzi wenye sifa zilizohitajika kugombea uchaguzi dhidi ya UTP.

TANU iliwachagua Julius Nyerere, Chief Abdallah Said Fundikira, John Ketto, Nesmo Eliufoo, John Mwakangale, Lawi Sijaona, Paul Bomani na George Kahama kusimama kama wagombea wa TANU. [1]

Baadhi ya hawa walikuwa watu ambao hawakuinukia katika TANU au harakati za siasa. Sheikh Takadir alihofu kuwa hawa Wakristo walioelimishwa na wamisionari na ukuzingatia kuwa walikuwa watu wapya katika harakati, mara watakaposhika madaraka watafanya juhudi kudumisha hali ile ile ya ukoloni, wakiwa hawana dhima ya kuongoza harakati kufikia lengo lake lake lililokusudiwa.

Sheikh Takadir alikuwa kiongozi wa kwanza katika TANU kuwatanabaisha Waislam kuhusu hatari hii mpya iliyokuwa ikiwabili.

Sheikh Haidar Mwinyimvua, mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU na mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU katika mwaka 1958 na aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sheikh Suleiman Takadir, anakumbuka jinsi Sheikh Takadir ghafla alipotoa dukuduku lake kwa Nyerere, dukuduku ambalo lilionekana lilikuwa halina sababu:

''Ilikuwa katika ofisi ya zamani ya TANU tukisubiri kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Ghafla tu Sheikh Takadir alisimama wima akishikilia fimbo yake ya kutembea akimuelekezea Nyerere huku akisema, ''Huyu mtu katu hatakuja kutujali sisi atakuja kuwajali ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta''

Sheikh Takadir alirudia maneno haya mara mbili. Sisi sote katika kile chumba cha mkutano tulipigwa na butwaa kutokana na maneno yale.

Nilimwona Nyerere akilia.

Nyerere alitugeukia sisi na kutuuliza, ''Je, Sheikh Suleiman amesema maneno yale kwa niaba yenu?''

Tulijibu kwa pamoja kuwa hatukuwa na habari kuhusu shauri lile; na mkutano ukavunjika hapo hapo.

Sheikh Takadir alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kumuunga mkono Nyerere na alikuwa ameifanyia kampeni TANU kwa bidii kubwa, akihutubia mikutano jukwaa moja na Nyerere.

Halikadhalika alikuwa amesaidia kufutilia mbali Ukristo wa Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam kiasi kwamba watu mjini Dar es Salaam hawakumnasibisha Nyerere na Kanisa Katoliki ila na TANU kama chama cha wananchi.

Wadhifa wa Sheikh Takadir mwenyewe kama mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU ulikuwa wa heshima kubwa.

Haikuwa kwamba wale wote waliokuwemo ndani ya chumba kile hawakuelewa kile alichodokeza Sheikh Takadir.

Walielewa kila neno alilotamka na maana yake halisi hasa kwa uongozi wa TANU. Kile ambacho hawakufahamu, kutambua au kusadiki kilikuwa ule ukweli kuwa Nyerere, mtoto wao mpendwa na kiongozi wao, iko siku moja atawageuka Waislam na kuwatazama kama adui zake na mahasimu kwa imani yake ya Kikristo.

Lakini kwa wakati ule hili lilikuwa wazo lililokuwa mbali sana na lisilokuwa na maana yeyote kwao.

TANU na chama kilichotangulia, African Association, hazikuundwa kwa ajili ya masilahi ya kikundi fulani pamoja na ukweli kuwa Waislam ndiyo waliounda vyama hivyo viwili na kuviongoza.

Sheikh Takadir alikuwa ametonesha jambo nyeti sana. Njia pekee ya kuzuia mgogoro huu mpya usikue ilikuwa kwa Nyerere kuthibitisha kuwa Waislam watatendewa haki baada ya uhuru kupatikana.

Kwa wakati ule, umoja wa wananachi ulikuwa muhimu kwa ajili ya harakati.

Umoja wa Watanganyika ukawa ndiyo hoja kuu ya Nyerere katika hotuba zake zote kuanzia mkasa wa Takadir utokee na alishikilia hoja ya umoja katika kila hotuba yake hadi kufikia uchaguzi wa kura tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU iliamua kuunda kamati ya haraka haraka kwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kumuuliza kwa nini alimshutumu Nyerere. Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo walikuwa Idd Faiz, Mwenyekiti wa Halmashauri ya TANU, Idd Tulio na Jumbe Tambaza.

Sheikh Takadir aliiambia kamati hiyo kuwa Nyerere alikuwa akitumia sharti la elimu katika uchaguzi wa kura tatu ili kuwaweka Wakristo wenzake madarakani kwa hoja kwamba wanazo zile sifa zitakiwazo kushika majukumu ya serikali.

Kisha Sheikh Takadir akarudia tena maneno yale yale aliyomwelezea Nyerere, neno kwa neno, akiongeza kwamba hana majuto yoyote kwa msimamo wake huo.

Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Idd Tulio walisimama na kuondoka kimya kimya. Matokeo yake ikawa Sheikh Takadir kufukuzwa kutoka TANU kwa kuanzisha suala la udini, ambalo lilidhaniwa lingewagawa wananchi.

Idd Tulio akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kushika nafasi ya Sheikh Takadir.

Idd Tulio alikuwa kati ya watu waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU pale Ukumbi wa Arnatouglo.

Kuingizwa kwa watu kama Eliofoo, Mwakangale, Sijaona, Bomani, Kahama na wengine katika Baraza la Kutunga Sheria ili kuwakilisha TANU kuliwatia wasiwasi idadi kubwa ya wanachama Waislam waliokuwepo makao makuu ya TANU.

Lakini kwa hakika viongozi hawa walikuwa wazalendo wakiwakilisha sehemu muhimu nchini Tanganyika ambazo kwa mfano wale kutoka vyama vya ushirika kama Bomani kutoka Jimbo la Ziwa, walijitoa mhanga sana katika harakati.

Hakuna namna ambayo Nyerere angeweza kuwakwepa kwa hofu ya kuujaza uongozi katika TANU na Baraza la Kutunga Sheria na Wakristo.

Kwa upande mwingnine halikadhalika haikufikiriwa kuwa ni lazima kuwa na uwakilishi ulio sawasawa baina ya Waislam na Wakristo katika TANU au katika Baraza la Kutunga Sheria.

Wakati ule tatizo la udini lilikuwa halijulikani kabisa.''

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
 
Mohamed ndio maana kuna akina James H. Chase, Mario Puzo n.k.
Ni kweli kabisa ni ngumu kwa watu wengine kuandika kitu katika ''genre'' isiyokuwepo.
Mfano mtu ataandikaje Non-Fiction na Fiction kwa wakati mmoja?

Hivi Mohamed, wale Wapare waliopambana na mkoloni wao hawakushiriki katika mapambano ya uhuru?

Pili,kuna post yako umetaja majina ya akina Abdu Sykes, Nyerere, Mhando, Dunstan Omar, Dosa Azizi na wengine ukasema walikuwa wanakaa katika barza ya mtaa wa Stanley kujadili Mustakabali wa Tanganyika.
Narudia, Mstakabali wa Tanganyika.

Hapo nyuma ukurusa wa 67 umesema baraza la TANU lilikuwa na Waislam watupu.
Halafu kuna mahali umetaja wazee wako wasiotajwa lakini walishiriki sana kwasabau ya uislam.

Katika idadi ya wazee wako sijaona jina la Vedastus Kyaruzi hata kama aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa chama kwa nyakati fulani. Sijaona jina la Paul Rupia au Boman achilia mbali akina Matola n.k.

Hivi huoni kuwa kile unachokipinga ndicho unachokifanya kama Mwanakijiji alivyowahi kusema?
Kwamba unaacha majina kwa mtindo ule ule wa wazee wako kusahulika.
Hivi mtoto wa Bomani au Rupia kweli anaweza kusoma kitabu chako na kuhisi wazee wao wameheshimiwa?

Lakini pia hebu tueleze, Abdul Sykes aliwahi kwenda lini Songea kukutana na Ali Songea Mbando.
Lini aliwahi kwenda Mbeya au Kilimanjaro? Kama hakuwahi kwenda( na assume tu) unawezaje kuandika historia ya wazee wako waislam halafu ukasema ni ya Tanganyika?

Tatu, umesema Abdul Sykes alimtaka sana Nyerere kwa usomi wake. Wakati huo huo unasema alitoka kijijini na hakuna aliyemjua hadi kufundishwa kuvaa ''nguo''.

Tena siku za nyuma uliweka picha ya kuonyesha jinsi alivyokuwa na kaptura.
Well, Labda nikuulize wakati Nyerere anaingia Dar es salaam yeye na Mshume Kiyate nani alikuwa na ufahamu zaidi wa dunia hii?

Nne, hivi wakati Nyerere anaingia Dar na kuingizwa katika siasa na Abdul, ina maana alikuwa hajui lolote kabisa kuhusu siasa?

Samahani hizi ni hoja na sikuona namna ya kuzipanga kwa namna unayotaka. Twende hivyo hivyo ilimradi kila mmoja aelewe na aweze kujibu au kutoa maoni. Natumaini pia hakuna neno ngano mahali popote na hutakwazika.

Inshallah Mzee Said ukumbi wako.
 
Swali...imedaiwa na Mohamed Said kuwa wazee wake hawakumfahamu kabla ya kukanyaga Dar es Salaaam mwaka 1952, je ni mwaka gani Dossa Aziz alikutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza?

Julius Nyerere alikutana na Dossa kwa mara ya kwanza 1946 Dodoma kwenye mkutano
wa African Association.
 

Nakushauri usome kitabu changu.

Inaelekea hujakisoma kitabu changu maana ungesoma usingesema
hayo yote.

Sasa hatuwezi kujadili kitu ambacho wewe hukijui.

Wanaukumbi hili swali nisaidieni na nyinyi kujibu.
 
Nakushauri usome kitabu changu.

Inaelekea hujakisoma kitabu changu maana ungesoma usingesema
hayo yote.

Sasa hatuwezi kujadili kitu ambacho wewe hukijui.

Wanaukumbi hili swali nisaidieni na nyinyi kujibu.
Kama sijui si ndio wakati unjiuze?
Mohamed, nimesoma vitabu vyako version zote, na kama unadhani nahitaji kurudi kusoma sasa unafanya nini hapa ukumbini?

Kilichokuudhi ni swali kuwa, wazee wako walikaa na Nyerere kujadili mustakabali wa Tanganyika.
Halafu wewe huyo huyo unasema walikaa waislam watupu! Mohamed not everyone is a zombie or nincompoop!

Na mwisho sikuuliza swali nimeuliza maswali.
 
Mzee Mohamed Said inaonyesha kitabu chako baada ya kusimuliwa na mtu mmoja tu wa ukoo wa akina Sykes ukaenda kujifungia ndani tayari kwa kuandika kitabu
 
Ni kweli Dar es Salaam kwa wakati huo wa harakati za kudai uhuru ilikuwa "predominantly Moslem" lakini pia tusisahau kuwa idadi ya wakaazi wa Dar es Salaam ilikuwa ni chini ya watu 120,000 (laki moja na ishirini) wakati idadi ya Watanganyika ilikuwa zaidi ya watu 8,000,000 (milioni nane!) Hivyo pamoja na TANU kuanzishwa Dar es Salaam, ili iweze kuonekana inawakilisha Watanganyika, ilibidi wapatikane watu kutoka nje ya Dar es Salaam kama Chief Abdallah Said Fundikira (Jimbo la Magharibi), John Ketto, Nesmo Eliufoo (Jimbo la Kaskazini), John Mwakangale (Jimbo la Nyanda za juu Kusini), Lawi Sijaona (Jimbo la Kati), Paul Bomani (Jimbo la Ziwa) na George Kahama (Jimbo la Ziwa) na kadhalika. This was just common sense stepping in.

Hawa watu hawakuokotwa tu, tayari walikuwa viongozi, wasomi na wenye ushawishi mkubwa katika sehemu walizotoka na watu waliwakubali bila kujali dini zao. Kwa jinsi ile ile Mwalimu alivyoweza kuchaguliwa kuwa Raisi wa TANU ndivyo hivo hivyo kiongozi wa kwanza wa tawi la TANU Moshi Jimbo la Kaskazini alichaguliwa Muislaam Mzee Yussuf Ngozi katika eneo ambalo lilikuwa "predominantly Christian" Hatukatai kuwa watu kama Abdulwahid Sykes hawakutoa mchango mkubwa katika harakati za wakati huo, tunachopinga ni upotoshwaji wa makusudi wenye lengo la kupandikiza chuki na uhasama unaofanywa na mchochezi Mohamed Said.

Naomba kwa ufahamisho tu nidokeze kuwa Mohamed Said ni mdogo sana kwangu kiumri na hivyo wakati mambo mengi anayohadithia ni ya kusimuliwa, mimi mengi niliyashuhudia kwa macho yangu. Kati ya waliosisi TANU, tisa kati ya 20 walikuwa wakazi wa Dar es Salaam, lakini wako pia ambao pamoja na kushiriki kikamilifu walikuwa kwenye utumishi ndani ya serikali ya ukoloni na haikuwa rahisi kujitokeza wazi wazi. Katika njama zake Mohamed Said anachanganya mambo mawili...UdaresSalaam na Uislaam na mpaka wakati atakapoweza kufunguka macho na kutenganisha tofauti hii, maandishi yake kwetu wengine yatabaki kama porojo tu.

Sasa wanajamvi, hebu angalieni huu mtiririko;
Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere katika siasa za Dar es Salaam hadi Abdu alipomleta ofisi ya TAA New Street. Hiki wala si kitu cha kificho watu wote wa Dar es Salaam katika harakati zile za 1950 wanajua.
Hapana inawezekana huko alikotoka alifanya makubwa. Lakini kwa Dar es Salaam ambako ndiko hasa siasa zilikuwa kali hakuna aliyepata kusikia jina la Nyerere.
Swali...imedaiwa na Mohamed Said kuwa wazee wake hawakumfahamu kabla ya kukanyaga Dar es Salaaam mwaka 1952, je ni mwaka gani Dossa Aziz alikutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza?
Julius Nyerere alikutana na Dossa kwa mara ya kwanza 1946 Dodoma kwenye mkutano wa African Association.
Ukiwa muongo na mchochezi, yabidi utunze kumbu kumbu.
 
Mzee Mohamed Said inaonyesha kitabu chako baada ya kusimuliwa na mtu mmoja tu wa ukoo wa akina Sykes ukaenda kujifungia ndani tayari kwa kuandika kitabu

Hapana mtu wa kwanza kunipa habari za uhuru alikuwa baba yangu na wakati ule
kwa kweli nilikuwa na umri mdogo sana.

Wala haukunipitia kama itakuja siku yale mazungumzo yetu yatakuja kuwa chanzo
cha historia.

Baba yangu akiniambia habari za Dar es Salaam ya 1930s wakati yeye ni mtoto akiishi
Kipata na wazazi wake mkabala na nyumba ya Kleist Sykes.

Akinieleza jinsi yeye na Abdu walivyokuwa wakimsaidia bibi yangu Bi Zena bint Farijallah
kutwanga chenga za vitumbua vyake.

Sasa katika kumbukizi hizi za utoto wake akawa ananihadithia hali ilivyokuwa Vita Vya Pili
vilipoanza Ulaya na nini kilitokea Dar es Salaam.

Vijana kukamatwa kwenda ''mpakani" kadi za ''ration'' ya chakula kwa ajili ya uhaba
uliotokana na vita.

Mambo mengi na mimi nilikuwa msikilizaji mzuri.
Haya yote kwenye diner table usiku.

Sasa katika maelezo haya baba bila kujitambua akanambia siku moja, ''Unajua Mohamed
hata hii TANU wanayosema kaanzisha Nyerere uongo mtupu. TANU kaanzisha Abdu tena
vitani Burma.''

Wakati ule kwangu wala hakikuwa kitu cha kunifanya nitafakari. Baba anaendelea, ''Tena
unajua mimi mara ya kwanza nakutana na Nyerere ilikuwa pale nyumbani kwa Abdu Stanley
sasa kuja kusikia kuwa hii TANU kaanzisha Nyerere na huyu mtu hapa si kwao katoka bara
nashangaa.''

Huyu baba yangu.

Nilipoingia Chuo Kikuu sasa mazungumzo yote ya utoto na baba yangu yakawa yananijia nikisikia
walimu wakisomesha ile historia rasmi asiyotajwa Abdu wala Mzee Kleist.

Ndipo nikawa nasema namwambia mwalimu wangu darasani, '' Mwalimu Nyerere hakuanzisha TANU
mimi baba yangu alikuwapo na Nyerere anakujapale kwa Abdu baba yangu anamuona na Abdu tayari
alikuwa rais wa TAA chama alichoasisi baba yake Mzee Kleist. Mimi hawa ni wazee wangu nasema
jambo ninalolijua.''

Kitu kikubwa sasa kilichonisaidia ni kule kuaminiwa na nyaraka za akina Sykes.
Hapo nikawa nimevumbua mgodi wa dhahabu.

Kazi yangu ilikuwa kuuliza maswali, maswali, maswali...

Lakini turudi kwa Bwana Ally Sykes.

Unadhani kuna mtu hivi sasa au hata hapo nyuma anyoijua TANU kushinda Ally Sykes?
Iwe kuwa habari atakazonipa Ally Sykes ziwe na shaka?

Wewe unae?
 

Si kama kuniita muongo nitatahayari.
Kama muongo si mimi.

Waongo watakuwa wazee wangu walionisomesha historia hii.

Kukuonyesha kama ninayokueleza nayajua vyema hebu sikiliza
haya maneno.

Wewe unasema kuwa kulikuwa wengine walioshiriki kuasisiTANU
lakini waliogopa kujitokeza.

Kama unawajua mbona hujawataja?

Sasa msikilize Mohamed Said Mchochezi ninavyochochea.

Watu ambao wangelikuwa katika waasisi wa TANU lakini hawakuwepo
kwa sababu isingewezekana wote wahudhurie mkutano ule kwanza
ni babu yangu Salum Abdallah. (Ukitaka nitakupa habari zake. Kwa ufupi
alikuwa mfadhili wa TAA na askari wa mstari wa mbele Tabora).

Mwingine ambae angekuwapo pale New Street ni Ali Migeyo kutoka Bukoba.
Mwingine Dk. Michael Lugazia.

Mwingine ni Hamza Mwapachu alikuwa Nansio ''kifungoni'' kama Dk Kyaruzi
alivyopenda kusema.

Sheikh Hassan bin Amir na ile kamati ya TAA Political Subcommittee hawa
walikuwa kamati ya ndani wapishi wa mambo.
Je unataka nikutilie na akina Idd Faizi Mafongo na ndugu yake Idd Tosiri?
Mbona historia hii imesheheni mambo mengi tu?

Unadhani Idd Faiz aliaminiwa kuweka fedha za TANU na Al Jamiatul Islamiyya
bure bure?

Unadhani Idd Faiz aliaminiwa kufanya mipango ya safari ya Nyerere UNO hivi hivi?

Unaweza kuwa wewe ni mkubwa kwangu lakini hao niliokutajia mmoja ni baba yake
Maulid Tosiri rafiki yangu toka utoto na leo tunaishi jirani na mwingine ni baba yake
Faiz kaka yangu kanitangulia miaka miwili kuzaliwa.

Sasa ikiwa hii historia ni porojo sasa si basi kwani pana nini?
Iache ibaki porojo.

Sijamlazimisha mtu kuniamini.

Ila ninalotaka kukusitizia ni hili huwezi kuyajua haya kunishinda.

Pili huo Udaresalaam ndiyo ilikuwa TANU yenyewe.

Na huo Uislam unaokuchoma ndiyo uliokuwa unapambana na ukoloni.
Jina la kitabu changu halikuficha hilo.
 
Si kama kuniita muongo nitatahayari.
Kama muongo si mimi. Waongo watakuwa wazee wangu walionisomesha historia hii...
Kwa nini Julius Nyerere alihudhuria mkutano wa African Association Dodoma mwaka 1946? Kama nani? Akitokea wapi? Je, hakuna mjumbe/wajumbe kutoka Dar es Salaam aliyehudhuria/waliohudhuria mkutano huo? Kama wapo inakuwaje mwaka 1952 (miaka sita baadaye) unadai hakuna hata mmoja kati ya wazee wako wa Dar es Salaam aliyewahi kumsikia Julius Nyerere? Kwa nini unadai kuwa safari ya kisiasa ya Nyerere ilianzia 1953? na aliingizwa katika siasa na kina Sykes? Je uko tayari kukiri kuwa ujio wa Mwalimu ndiko kulileta mwamko, msisimko na mawazo mapya ndani ya TAA? Je uko tayari kukiri uwongo ambao umekuwa ukiueneza kwa chuki kwa watu ambao hawaijui historia sahihi? Do you know even the meaning of the word "truth"?
 

Mag3, mzee mwenzangu ni lazima tuseme jambo moja wazi sana na ni la kweli. Hoja zote dhidi ya Nyerere ambazo Bw. Said amezijenga katika maandishi yake yote zinasimama na kuanguka na mwaka 1953. Kwa sababu kwa maelezo yake ni wakati huu Sykes na wengine wanamtambua Nyerere kwa ukaribu na kumpa nafasi ya uongozi na hatimaye TANU inazaliwa mwaka 1954 wakati wa uongozi wa Nyerere.

Kutokana na hili Bw. Said hawezi kamwe kukubali ukweli wa kihistoria - kumbuka yeye si mwanahistoria na sijui kama kajifunza kanuni za uandishi wa kihistoria - kuwa Nyerere aliingia kwenye siasa za Tanganyika kabla ya kuanza kazi Dar kama mwalimu na kabla ya kuja kuwa mkazi wa Dar. Kama Nyerere alianza siasa na harakati zake kabla ya 1953 hoja zote za kuwa ni wazee wa Kiislamu wa Dar ndio walimuingiza Nyerere kwenye siasa zinaanguka.

Bw. Said hayuko tayari zianguke na hivyo hawezi kurudi nyuma ya 1953.

Lakini it makes sense.

Kama wazee wake wengi wa Dar hawakumjua Nyerere kabla ya 1953 masimulizi yao kwa Bw. Said ni LAZIMA yaanzie mwaka 1953 kwani wao kutomjua kabla ya hapo kuliwafanya waamini kuwa Nyerere hakuwa yoyote wala lolote kabla ya kuja Dar. Ndio maana ya lile simulizi lao ambalo wapo wanaamini kuwa Nyerere alifundishwa kuvaa suruali alipokuja Dar japo historia inaonesha alianza kuvaa mavazi haya shule ya msingi Misenyi huko!

Kama Nyerere alianza siasa na harakazi zake kabla ya kuja Dar mwaka 1953 basi wazee wa Dar hawawezi kujipa credit ya kumuingiza Nyerere kwenye siasa mwaka huo na hivyo hoja nzima ya kuwa wao ndio walimfundisha siasa kijana huyu msomi zinaporomoka kama kumomonyoka kwa biskuti kwenye kikombe cha chai.
 
Na sasa tunaanza kugundua kwamba Dosa Aziz alifahamiana na Nyerere mwaka 1946. Kwa hiyo Nyerere alipokuja Dar-es-Salaam 1952 hakuwa mgeni sana kwa wana harakati. In fact tayari alikuwa mwenzao ila tu kwamba hakuwa mtu wa Dar-es- Salaam. Very interesting.
 
Huko Dodoma, mwaka 1946 Nyerere alifuata nini na alihudhuria kama nani.

Nahisi mzee sasa hajui hata cha kudanganya, kila uongo wake unagonga ukuta!

Ataendelea kuwaburuza wenye akili mgano tun nao wakielevuka wanakana na kumchukia kupita kiwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…