Okello kaua watu wangapi, idadi niliyotoa ni makisio baada ya kuangalia namba zililzowekwa na watu mbalimbali. Okello alikuwa anatumiwa tu na Nyerere hivyo hawezi kujua kila kitu. Kuhusu Okello kulenga kuua kina nani ni kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa mahsusi kwa ajili ya kuua Uislam. Ushahidi huu ni mmojawapo wa jukumu alilopewa na Nyerere na Kanisa kuua Uislamu:
Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele:
"KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC".
Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
Kutokana na ushahidi huo, tueleze Nyerere angewezaje kubadili Tanzania kuwa katika dini ya Katoliki?
Yeye hakuwa mhubiri wa dini. Alitumia mabavu kueneza huo Ukatoliki na kati ya mabavu hayo ni mipango yake ya kuivamia Zanzibar. Sasa unapovamia Zanzibar na kuuwa watu kwa ajili ya kuendeleza Ukatoliki, ni dhahiri umelenga kuwaua Waislamu na sio Waarabu. Waliokufa kwenye mapinduzi yale sio Waarabu peke yao. Ni Wazanzibari wote. Isitoshe Waarabu ni Waislamu hivyo wameuliwa si kwa sababu ya Uarabu wao bali kwa sababu ya Uislamu wao kutokana na mkakati huu wa Katoliki wa kueneza dini yao iliyofilisika kihoja kwa kutumia mabavu.
Isitoshe, mipango hii ya kuvamia Zanzibar ilipangwa na Waingereza na Wamarekani wakati huo George Bush akiwa mkuu wa kitengo cha mashushu cha Marekani na Wamarekani walieleza wazi jinsi wanavyomtegemea Nyerere kwa kazi hiyo chafu kwani walimuona kutokana na kichwa yake kuwa mbaya basi ananafasi nzuri ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi uliotarajiwa. Na haya mataifa ya Magharibi hayakuishia hapo. Yaliweka mpaka Plan B ili kama Wazanzibar watataka kurudisha nchi yao mikononi mwo baada ya mapinduzi basi wabanwe na Nyerere ili wasiweze kufanya hivyo. Nyerere alitumia rungu hilo alilokabidhiwa na mataifa ya Magharibi kuwaua, kuwakimbiza nje ya nchi, kuwatia kizuizini, n.k