Sina kinyongo na michango yenu hapa,
Kila hoja hapa inajibiwa sawa na ujazo wake!
Uchezi wa Mohamed Said upo wazi na tumeueleza tangu post ya mwanzo kabisa!
Ikiwa hujauona naomba nikupe kwakifupi tu!
1) AA iliasisiwa na Klest Sykes, Ni UONGO.
Ukweli nikuwa iliasisiwa na mwalimu Cesil Matola
2) Kuwa Mwalimu rejea kutoka Scotland alisema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika TAA, Ni UONGO.
Ukweli nikuwa mwalimu ameeleza wazi katika hotuba ya muago kwa wazee wa dar kuwa Abdul alikuwa katibu mkuu wa TAA.
3) Kuwa TANU iliasisiwa BAMA na Abdul Sykes, Ni UONGO,
Ukweli nikuwa TANU imeasisiwa tarehe 7/7/1954 pale Mtaa mpya leo pakiitwa Lumumba chini ya Julius Kambarage Nyerere
4) Kuwa Balozi wa USA aliwahi kulihutubia Bunge la Tanzania 2003, Ni UONGO
Ukweli nikuwa balozi wa USA nchini hajawahi kulihutubia bunge la nchi hii, zaidi ya kisemina cha wabunge wa CCM tu cha kushinikiza upitishwaji wa sheria ya ugaidi nchini kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Pius Msekwa.
Hayo bado hujaona uchochezi wa Mohamed Said?
Yericko,
Ukiwa utajituliza na kuacha jeuri tunaweza tukafanya mnakasha mzuri
wenye adabu na heshima.
Bahati mbaya naona mjadala umeteka hisia zako pakubwa sana.
Suala AA kuasisiwa na Kleist si mimi nilosema hilo.
Hilo kalisema yeye mwenyewe Kleist katika kumbukumbu alizoacha na
baadhi ya nyaraka hizo zimehifadhiwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
East Africana.
Ikiwa utapenda fika hapo chuoni kasome ''The Life of Kleist Sykes,'' pia
ukipenda soma Iliffe (ed) ''Kleist Sykes The Townsman,'' katika Modern
Tanzanians.
Yote hayo kaandika mjukuu wa Kleist, Daisy Sykes akisaidiwa na baba yake
Abdu Sykes kabla hajafariki mwaka 1968.
Hilo la Nyerere kusahau cheo cha Abdu tulikubaliana kuwa utaleta audio.
Mimi nitazungumza kuhusu hilo In Shaa Allah baada ya kusikiza hiyo audio.
Nilikuwa sitaki kusema lakini nitakupa kitu kidogo.
Shariff Attas na Nyerere wakifahamiana vyema pale Sokoni Kariakoo na hadi
nyumbani kwa Abdu Sykes pale Mtaa wa Aggrey.
Walikuwa na kawaida ya kula chakula cha mchana pamoja Shariff Attas na Nyerere
nyumbani kwa Abdu.
Abdu alikuwa harudi nyumbani kula kwa hiyo Shariff Attas na Nyerere kila siku walikuwa
wakiongozana kwenda kula chakuka cha mchana pamoja nyumbani kwa Abdu.
Baada ya uhuru kupatikana iko siku Nyerere akakutana na Shariff Attas pale New
Street Ofisi ya TANU.
Nyerere katika kusalimiana na Shariff Attas alimuuliza Shariff Attas ikiwa wanafahamiana.
Shariff Attas alimjibu Nyerere kuwa hawajapatapo kukutana.
Nyerere alikuwa kamsahau rafiki yake wa zamani Shariff Attas.
Ni kisa kirefu lakini hapa hakuna haja ya mimi kukieleza.
Ama hilo la kuwa Nyerere ndiye aliyeasisi TANU New Street na kuwa TANU haina historia
yoyote na Abdu na Vita Kuu Vya Pili mimi halinipi tabu wala sitakubishia una haki ya kusema
unachoamini.
Hilo la Balozi wa Marekani na kuhutubia Bunge unaweza kufanya tafsiri upendayo lakini ukweli
ni kuwa alikuwapo bungeni na aliwasilisha mada juu ya ugaidi.
Mwisho nakusihi uwe mtulivu tufanye mnakasha wa heshima.