Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Islam gani huyu wa Upanda. Au yule mwenye duka opposite Msikiti Ngazija.

Anayeishi Ali Khan street

Barubaru,

Salaam.

Sina hakika huyu unaemzungumzia wewe. Nimjuaye mimi ni Bwana Islam jamaa zao kina Prof. Abdilrahman Babu. Mara ya mwisho nakumbuka akikaa pale Maweni Str. Upanga na alikua na Madrassa. Hiyo ya duka ni kweli,lakini nikumbukavyo duka lake lilikua ubavuni pa Al Masjid Maamur pale Malik Road Upanga.

Ni mtu mwenye bashasha mno. Nakumbuka kuna siku nilkwenda kwake kumfuata Sahib yangu mwanae Eddy Islam. Nilipobisha hodi akanifungulia yeye Sheikh Islam mwenyewe. Nikamwamkua,na nikamuuliza je Sheikh Eddy nimemkuta!?
Japo akinifahamu uzuri,lakini akanijibu;kumradhi Bwana mdogo labda umepotea njia maana huyo "Sheikh wako" Eddy hakai humu. Maana humu ndani kuna Sheikh mmoja tu,na ndie mimi.
Nami sikumwacha,nikamjibu kama Sheikh Mathias Mnyampala ali-qualify kuitwa Sheikh basi namimi kwanini nisimwite ndugu yangu Eddy Sheikh!?ahaha!! Wallahi,alicheka mno...akanambia wewe ulikua mtulivu lakini sasa umekua Maluuni saana!ahaha!!

Pale Ally Khan,kama uliwahi kuishi pia palikua na yule Mzee mstaarabu mno wa Kihaya...Mzee Bulengero,lakini alifariki kitambo maskini.
 
Kwa hiyo hizo hoja alizoziweka moja baada ya nyingine huzioni? Kama huzioni KAA KIMYA.

Kuhusu mjadala wetu, uliamua kuingia mitini baada ya kushindwa kujibu swali langu la mwisho linalohusu mantiki ya hotuba ya Nyerere. Sasa mimi nikiona mtu kaingia mitini bila kuzungumza chochote simfatilii. Najua kanielewa.

Sasa huna haki ya kusema kwamba ninarukaruka tu wakati wewe umeamua kuingia mitini. Kuendeleza malumbano yangu kupitia kwa watu wengine hakutakusaidia. Nitakushukia kama mwewe popote pale utakapoamua kuendeleza malumbano na mimi kwenye mnakasha huu.

Zali la mentali "utamshukia kama mwewe" ha ha haa...baereze baalewe wengi wameshaingia mitini CHEZEA MCHIMBA CHUMVI
 
Gombesugu,
Dk. Amour Abdallah Amour amefariki jana usiku Dar na kesho
Maziko Unguja.

Inalilah wainailaihy rajiun.

Sheikh Mohammed,

Asalaam Alaykum. Ahsanta kwa kunijuza khabari ya msiba huo mzito kwetu soote. Nimepata simanzi mno.

Tuliwahi kupata khabari mapema hapa,maana yule Aunt yangu ambae yupo hapa kwa mapumziko kiduchu alipigiwa simu toka Unguja. Inna Lillahi Wa Inna Illahi Rajiun.

Vipi Dr. Abdalllah Dahoma nae yupo,nipa salaam mno kikutana.

Shukran.
 
Zali la mentali "utamshukia kama mwewe" ha ha haa...baereze baalewe wengi wameshaingia mitini CHEZEA MCHIMBA CHUMVI

Boko Haram,

Asalaam Alaykum Al Akhiy.

Nakufuatilia bayana zako hapa jamvini. Lakini mara nyingi hufurahi unapozungumza hicho ki-Congo.
Taratibu jamaa wasije kukufuatilia makaratasi ya uraia wako!ahaha!!

Ahsanta.
 
Kwa hiyo hizo hoja alizoziweka moja baada ya nyingine huzioni? Kama huzioni KAA KIMYA.

Kuhusu mjadala wetu, uliamua kuingia mitini baada ya kushindwa kujibu swali langu la mwisho linalohusu mantiki ya hotuba ya Nyerere. Sasa mimi nikiona mtu kaingia mitini bila kuzungumza chochote simfatilii. Najua kanielewa.

Sasa huna haki ya kusema kwamba ninarukaruka tu wakati wewe umeamua kuingia mitini. Kuendeleza malumbano yangu kupitia kwa watu wengine hakutakusaidia. Nitakushukia kama mwewe popote pale utakapoamua kuendeleza malumbano na mimi kwenye mnakasha huu.

Katika swali lako kwangu kuhusu mantiki uliyodai nimeiweka juu ya majibu yangu kwako juu hotuba hiyo, sikukujibu baada ya kubaini kasoro za kiuelewa wa baadhi ya misamiati ya lugha adhimu ya kiswali!

Kwanza ili twende sawa naomba tuwekane sawa juu ya hili,

1) Unajua maana ya MANTIKI na husimama wapi katika hoja?

NB:

Kile nilichokijibu pale awali hakikuhitaji matumizi ya MANTIKI,

Nilipigwa butwa pale ulipohoji kuwa ni mantiki gani niliyotumia kujibu vile!

Napenda mjadala wa adabu na staha,

Haya tusonge ndugu!
 
Wapo wanaoziamini hizi hadithi za Mohamed Said kama ndio ukweli...tazama tu listi ya wanaozichangamkia, humo humkosi Ritz et al. Hao wazee wa Mohamed Said hakuna hata mojawapo aliyeziongoza AA, TAA wala TANU, huo ndio ukweli. Yuko mojawapo aliyetaka kushindana na Mwalimu Nyerere katika kuiongoza TANU ilipoanzishwa lakini hakuweza kuambulia hata kura za waswahili wenzake wa Gerezani, huo pia ndio ukweli. Majuha kama kawaida yao wanalishwa uwongo na wao wanaitikia hewala bwana, hakuna utumwa unaozidi utumwa wa akili. Huyu Mohamed Said si lolote, si chochote bali mchochezi...anashinda kwa uchochezi, anakula kwa uchochezi na anaishi kwa uchochezi.

Kwa wanajamvi wapya hebu msomeni huyu jamaa anavyowatukana wazee wetu.

Cc... gombesugu.
 
Last edited by a moderator:
Boko Haram,

Asalaam Alaykum Al Akhiy.

Nakufuatilia bayana zako hapa jamvini. Lakini mara nyingi hufurahi unapozungumza hicho ki-Congo.
Taratibu jamaa wasije kukufuatilia makaratasi ya uraia wako!ahaha!!

Ahsanta.

Gombesugu, waaleykum salaam ndugu yangu hayo ni maneno tu al akhiy wakinifuatilia sana nafanya hijra mbona mtume alifanya hijra kutoka Makka akaenda madina na kuna maswahaba walikuja mpaka Afrika hapo Ethiopia mimi hilo halinibabaishi mkubwa.
 
gombesugu,

Ndugu yangu umemitajia hao Masheikh umenikumbusha mbali sana nimeudhulia madrasa yao mwengine saizi wameishatangulia mbele ya haki.

Tuzidi kuwaombea dua Allah hawafanyie wepesi Ishaalah... kwa kumalizia nakuwekea maneno machache kuhusu wanafiki walivyoelezewa.

Nani Mnafiki – Kilugha Na Kidini

Katika kamusi la lugha ya kiarabu, neno ‘Mnafiki’ maana yake ni mtu mwenye kigeugeu au mwenye kuwa na sura mbali mbali: Leo hivi kesho vile. Katika dini, neno ‘Mnafiki’ maana yake ni yule anayejidhihirisha kuwa ni Muislam na kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), wakati undani wake ni kafiri na adui wa Mwenyezi Mungu na adui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Baada ya tafsiri hii fupi ya nani Swahaba na nani Mnafiki, tutakubaliana kuwa maneno hayo mawili hayawezi kuwa na maana moja, (hayawezi kwenda sambamba) Kilugha wala Kidini. Kwa sababu Swahaba ni yule aliyemuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akafariki dunia akiwa Muislam, wakati Mnafiki ni mwenye kujidhihirisha kama ni Muislam wakati ndani ya nafsi yake ni kafiri. Kwa hivyo haiwezekani Swahaba akawa Mnafiki na wala Mnafiki hawezi akawa Swahaba. Sasa Mtu anaweza kuuliza: 'Vipi tutaweza kutofautisha baina ya Swahaba na Mnafiki?' Majibu: Mnafiki ana sifa na alama maalum tulizojulishwa katika Qur-aan na katika Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na kwa ajili hiyo tunaweza kutofautisha baina yake na Swahaba. Wanafiki ni watu; ‘Wanaoeneza ufisadi ardhini, kuifanyia istihzai dini, kuwafanyia istihzai wacha Mungu, ni wavukaji mipaka katika kufanya maasi wenye kuununua upotofu (upotevu) kwa uongofu, wavivu katika kufanya ibada, hugeuka geuka, mara Waislamu mara makafiri, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَلِكَ لاَ إِلَى هَـؤُلاء وَلاَ إِلَى هَـؤُلاء “Wanayumba yumba baina ya huku (kwa Waislam) na huko (kwa makafiri). Huku hawako wala huko hawako),” An-Nisaa-143 Na katika sifa za wanafiki pia ni; ‘Kuwa hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Akhera na kwamba Waislam wanapopata kheri yoyote au mafanikio, wao wanahuzunika, na hufurahi pale Waislamu wanapopata tabu au wanapokumbwa na masaibu au mitihani. Huchukizwa na kutoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na hufurahi wanaporudi nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) peke yake vitani. Wameingia katika dini kwa ajili ya kujikinga wasiambiwe kuwa wao ni makafiri, na wanapenda kuwadhuru Waislam na kuwafarikisha. Na katika sifa za unafiki ni kuwa; wanaiahirisha Swalah mpaka nyakati zake za mwisho na hawahudhurii Swalah za jamaa na kwamba wanaionea uzito kabisa Swalah ya Alfajiri na ya ‘Ishaa’. Hizi ni baadhi tu ya sifa za Wanafiki Alizozitaja Mwenyezi Mungu katika Qur-aan tukufu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) katika mafundisho yake. Bila shaka Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni watu walio mbali kabisa na sifa hizi. Hawa ambao Mwenyezi Mungu Amewaambia: كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ

Ritz,

Asalaam Alaykum. Wallahi hii Fatwa uloiweka hapa ni nzito kwa wenye kujua. Mimi nilipoiona nalipatwa na kisunzi.

Naomba umsamehe yule Abu Jahal,maana tayari keshadhurika kitambo kama tulivyoona vile vitimbi vyake hapa jamvini. Maana ana maradhwi,na maradhwi yake ni makubwa mno kwa wenye kujua na kutambua.

Ahsanta.
 
Kwa wanajamvi wapya hebu msomeni huyu jamaa anavyowatukana wazee wetu.

Cc... gombesugu.

Ritz,

Alaa! Kumbe ulo "ustaarabu" woote wa Nguruvi3 na Mag3 khabari zao ndo hizi. Lakini haina neno wenzao wanayaona. Tukisema sisi tunaambiwa watu wa Madrassa hatwishi kulalama.

Jana nilimwandikia Nguruvi3,na nilimzungumza khabari hizi za matusi japo kiduchu. Nina imani amenifahamu.

Shukran.

Cc; Ami,Nguruvi3,Mag3
 
Kwa wanajamvi wapya hebu msomeni huyu jamaa anavyowatukana wazee wetu.

Cc... gombesugu.

Kusema ukweli kwenu ni kuwatusi hao wazee/waasi?

Je ni uongo?

Haya nitajie kati ya wanaoitwa wazee wenu ambae aliwahi kuongoza AA, TAA, TANU ama CCM katika ngazi ya Urais au Uenyekiti ambayo ndio ngazi kuu ya uongozi wa kichama!

Narudia tena kukwambia hao wazee walikuwa waasi wa serikali mpya ya Mwalimu Nyerere, na walionja nguvu ya dola huru ya Mwalimu!
 
Last edited by a moderator:
Unatisha watu! period.
Kwamba mtu asipokubali uongo,fitna na uzushi atakuwa amekufur! Mzee Said sijui unasimamia Uislam kwa kuzua uongo ili iweje.

Narudia tena kukwambia nawe uwe msikivu!
Kifo ni ahadi ya mja na mola wake.
Si wewe unayeamua nani afe kwa njia gani. Kifo kinakuja kadri mtu alivyopangiwa.

Unawatisha akina Gombesugu hata kufikia mahali pa kusema ''ni makosa madogo''
Wasomi wanaogopa kuongoza taasisi za waislam kwasababu ya vitisho vyenu. Na wewe na akina Ilunga na Ponda ni tatizo kabla ya kuongelea tatizo.Sasa hivi mupo bize mkiongoza itikafu ili kudhuru wanadamu wenzenu.

Kifo hapangi Mohamed Said, msitishwe! huyu anawatisha kwa mbinu za zamani.
Huyu ni mwanadamu tu asiwatishe jamani. Angekuwa mwadilifu kiasi hicho asingepokea tiketi ya ndege akabeba mfuko wenye nyaraka za uongo na kulala nao five star Ibadan! Tumeonyesha mara ngapi fitna ya mzee Said!

Siwezi kufanya utafiti wenye majibu kuwa kifo ni kazi ya mwenyezi mungu.
Siwezi kumhukumu mwanadamu mwenzangu kama ufanyavyo wewe! hili la wewe kujifanya nabii unalitoa wapi Mohamed!

Kila mtu atakwenda mbele ya haki na kuhesabiwa amali zake yeye na si kutokana na Mohamed Said asemavyo.

Usirudie tena kutisha watu!

Nguruvi3,

Salaam ndugu yangu. Nalikua napitia baadhi ya majambo hapa jamvini,ndipo ghafla nikakumbana na hii bayana yako.

Yaelekea huo "mkoba wa Ibadan" umekuchoma mno ndugu yangu. Maana huishi kuutaja!?ahahaa!

Ahsanta.
 
Kusema ukweli kwenu ni kuwatusi hao wazee/waasi?

Je ni uongo?

Haya nitajie kati ya wanaoitwa wazee wenu ambae aliwahi kuongoza AA, TAA, TANU ama CCM katika ngazi ya Urais au Uenyekiti ambayo ndio ngazi kuu ya uongozi wa kichama!

Narudia tena kukwambia hao wazee walikuwa waasi wa serikali mpya ya Mwalimu Nyerere, na walionja nguvu ya dola huru ya Mwalimu!

Yericko akiongea Mag3 yeye hatukani lakini Zali la mentali akiongea unamwambia aongee kwa staha "mkuki kwa nguruwe"na katika huu mnakasha unajifanya unatetea utaifa lakini si kweli wewe ni "DOUBLE FACE"
 
U double face upo sehemu gani ndugu?

Nguruvi3 ametukana nini hapo?
 
Kwa hiyo hizo hoja alizoziweka moja baada ya nyingine huzioni? Kama huzioni KAA KIMYA.

Kuhusu mjadala wetu, uliamua kuingia mitini baada ya kushindwa kujibu swali langu la mwisho linalohusu mantiki ya hotuba ya Nyerere. Sasa mimi nikiona mtu kaingia mitini bila kuzungumza chochote simfatilii. Najua kanielewa.

Sasa huna haki ya kusema kwamba ninarukaruka tu wakati wewe umeamua kuingia mitini. Kuendeleza malumbano yangu kupitia kwa watu wengine hakutakusaidia. Nitakushukia kama mwewe popote pale utakapoamua kuendeleza malumbano na mimi kwenye mnakasha huu.
Yerico ameishiwa kabisa na hoja,ndio maana akajitoa kimasomaso kwa kutubembeleza tujadili mradi wake wa kitabu cha ugaidi kinachofadhiliwa na Marekani.Lakini naona watu tumemuelewa bado tunapiga za mgongoni mpaka ainue mikono kuwa hakuna uchochezi wa Mohammed bali ilikuwa ni uzushi wake tu.Na akiri kuwa alitumwa kutaka kupotosha ukweli.
Masheikh zangu wa Upanga,kariakoo na kwengineko endeleeni kumkaba nasi vijana wenu twaona juhudi zenu.Allah tawalipa katika dunia na akhera kwa kutetea ukweli.
 
Katika swali lako kwangu kuhusu mantiki uliyodai nimeiweka juu ya majibu yangu kwako juu hotuba hiyo, sikukujibu baada ya kubaini kasoro za kiuelewa wa baadhi ya misamiati ya lugha adhimu ya kiswali!

Kwanza ili twende sawa naomba tuwekane sawa juu ya hili,

1) Unajua maana ya MANTIKI na husimama wapi katika hoja?

NB:

Kile nilichokijibu pale awali hakikuhitaji matumizi ya MANTIKI,

Nilipigwa butwa pale ulipohoji kuwa ni mantiki gani niliyotumia kujibu vile!

Napenda mjadala wa adabu na staha,

Haya tusonge ndugu!

Katika hotuba yake aliuliza nani wanaongoza TAA baada ya kurudi kutoka masomoni na baada ya kuwa Pugu. Kuuliza suali hilo ina maana alikuwa hawajui ni nani viongozi wa TAA. Sasa alipokuwa Pugu alikuwa amesimama shughuli za siasa za TAA mpaka afikie kiasi cha kutowajua ni nani wanaongoza chama kilekile alichoamua kujiunga nacho tangu yuko Makerere?
 
Yerico ameishiwa kabisa na hoja,ndio maana akajitoa kimasomaso kwa kutubembeleza tujadili mradi wake wa kitabu cha ugaidi kinachofadhiliwa na Marekani.Lakini naona watu tumemuelewa bado tunapiga za mgongoni mpaka ainue mikono kuwa hakuna uchochezi wa Mohammed bali ilikuwa ni uzushi wake tu.Na akiri kuwa alitumwa kutaka kupotosha ukweli.
Masheikh zangu wa Upanga,kariakoo na kwengineko endeleeni kumkaba nasi vijana wenu twaona juhudi zenu.Allah tawalipa katika dunia na akhera kwa kutetea ukweli.

Sina kinyongo na michango yenu hapa,

Kila hoja hapa inajibiwa sawa na ujazo wake!

Uchezi wa Mohamed Said upo wazi na tumeueleza tangu post ya mwanzo kabisa!

Ikiwa hujauona naomba nikupe kwakifupi tu!

1) AA iliasisiwa na Klest Sykes, Ni UONGO.

Ukweli nikuwa iliasisiwa na mwalimu Cesil Matola

2) Kuwa Mwalimu rejea kutoka Scotland alisema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika TAA, Ni UONGO.

Ukweli nikuwa mwalimu ameeleza wazi katika hotuba ya muago kwa wazee wa dar kuwa Abdul alikuwa katibu mkuu wa TAA.

3) Kuwa TANU iliasisiwa BAMA na Abdul Sykes, Ni UONGO,
Ukweli nikuwa TANU imeasisiwa tarehe 7/7/1954 pale Mtaa mpya leo pakiitwa Lumumba chini ya Julius Kambarage Nyerere

4) Kuwa Balozi wa USA aliwahi kulihutubia Bunge la Tanzania 2003, Ni UONGO

Ukweli nikuwa balozi wa USA nchini hajawahi kulihutubia bunge la nchi hii, zaidi ya kisemina cha wabunge wa CCM tu cha kushinikiza upitishwaji wa sheria ya ugaidi nchini kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Pius Msekwa.

Hayo bado hujaona uchochezi wa Mohamed Said?
 
Kusema ukweli kwenu ni kuwatusi hao wazee/waasi?

Je ni uongo?

Haya nitajie kati ya wanaoitwa wazee wenu ambae aliwahi kuongoza AA, TAA, TANU ama CCM katika ngazi ya Urais au Uenyekiti ambayo ndio ngazi kuu ya uongozi wa kichama!

Narudia tena kukwambia hao wazee walikuwa waasi wa serikali mpya ya Mwalimu Nyerere, na walionja nguvu ya dola huru ya Mwalimu!

Yericko,

Sasa huoni yakuwa kuna wakati unajichanganya mwenyewe!? Nahisi hii "definition ya matusi" ni pale tu inapoku-suit wewe!?
Nakukumbusha yakuwa; hapa baadhi yetu tunatoka katika matabaka,makabila,mila,dasturi na tamaduni tafauti.

Hapo awali hapa jamvini palikua na kishindo na kebehi kadhaa dhidi ya Sheikh Mohammed,yakuwa kwanini kataja kuwa Nyerere alikua akisaidiwa kitoweo na Mshume Kiyate na pia kwanini alitaja yakuwa Nyerere alikua hana pa kulala ikalazim asaidiwe chumba cha Abbas Sykes,alikua hana uwezo akitembea kwa miguu tokea Pugu mpaka Kariakoo,akasaidiwa baiskeli na mengineyo machache ambayo hata huyo Nyerere mwenyewe aliwahi kutamka hadharani. Wewe na jamaa zako wengi mlihamaki pasi mfano.

Kama una maarifa,hishma,na mapenzi makubwa mno kwa Nyerere kiasi cha kumnasibisha na Unabii... basi tafadhali nakusihi ndugu yangu punguza nyendo zako. Maana hapa dignity ya huyo Nyerere unazidi kuididimiza kila kukicha.

Unamzidisha ukiwa na machungu hata huyo Mama Maria. Maana hishma na mapenzi yoote alokua nayo kwa Mzazi mwenzie Nyerere,lakini sasa wewe umejitokeza na umeonyesha yakuwa Nyerere kumbe alikua si Mkristo mtiifu wala hakuwa mwanandoa muadilifu na pia alikua na Vimada na umezaliwa wewe mtoto wa nje ya ndoa!?

Ndugu yangu Yericko,kama utatumia ustaarabu japo kiduchu basi wahurumie ndugu zako wa Mama mwingine(Andrew Nyerere na wenzie). Najua wanateseka na kupata uchungu mkubwa kwa jinsi wewe unavyosababisha "kumuanika" Mzazi wao hapa jamvini.

Natumai utanifahamu japo kiduchu.

Tuendelee na mnakasha.

Cc;Ami,JokaKuu,Nguruvi3,Mag3,Barubaru,Jasusi,Boko Haram,Kadogoo,Zali la Mentali,Ritz,The Big Show,Sheikh Mohammed Said,Sideeq,Uthman

Ps;
Nakuhakikishia wewe humjui Rais Nyerere kiundani kama wamjuavyo baadhi ya Wanajamvi hapa! Kumbuka yakuwa Nyerere alikua ni Rais wa nchi,kwa hiyo kuna vitu vingi mno wewe "mwanafamilia" huwezi kuvijua alotenda "Mzazi wako".
 
Sina kinyongo na michango yenu hapa,

Kila hoja hapa inajibiwa sawa na ujazo wake!

Uchezi wa Mohamed Said upo wazi na tumeueleza tangu post ya mwanzo kabisa!

Ikiwa hujauona naomba nikupe kwakifupi tu!

1) AA iliasisiwa na Klest Sykes, Ni UONGO.

Ukweli nikuwa iliasisiwa na mwalimu Cesil Matola

2) Kuwa Mwalimu rejea kutoka Scotland alisema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika TAA, Ni UONGO.

Ukweli nikuwa mwalimu ameeleza wazi katika hotuba ya muago kwa wazee wa dar kuwa Abdul alikuwa katibu mkuu wa TAA.

3) Kuwa TANU iliasisiwa BAMA na Abdul Sykes, Ni UONGO,
Ukweli nikuwa TANU imeasisiwa tarehe 7/7/1954 pale Mtaa mpya leo pakiitwa Lumumba chini ya Julius Kambarage Nyerere

4) Kuwa Balozi wa USA aliwahi kulihutubia Bunge la Tanzania 2003, Ni UONGO

Ukweli nikuwa balozi wa USA nchini hajawahi kulihutubia bunge la nchi hii, zaidi ya kisemina cha wabunge wa CCM tu cha kushinikiza upitishwaji wa sheria ya ugaidi nchini kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Pius Msekwa.

Hayo bado hujaona uchochezi wa Mohamed Said?[/QUOTE]

Yericko,

Kumbuka katika "mada/shutuma" zako ulidai ni "uchochezi na uhaini"!?....nime-bold hapo juu kukuonyesha yakuwa "mashtaka" yako mbona yamepungua au umepatwa na mtafaruku kiduchu!?
 
Katika hotuba yake aliuliza nani wanaongoza TAA baada ya kurudi kutoka masomoni na baada ya kuwa Pugu. Kuuliza suali hilo ina maana alikuwa hawajui ni nani viongozi wa TAA. Sasa alipokuwa Pugu alikuwa amesimama shughuli za siasa za TAA mpaka afikie kiasi cha kutowajua ni nani wanaongoza chama kilekile alichoamua kujiunga nacho tangu yuko Makerere?

Nikuweke sawa kwenye maelezo yako,

Sio kwamba mwalimu aliishi Pugu ndipo akaenda masomoni, la hasha bali aliishi Tabora ndipo akaenda masomoni na aliporejea ndipo alifikia Shule ya Mtakatifu Frances pale Pugu na alidumu kwa mwaka mmoja tu na nusu kisha akaachana na kufundisha!

Akiwa pugu hajawahi kuwa kiongozi wa chama chochote bali alijihusisha na shughuli za kisiasa kwa kuja kuzifanyia Dar!

Hoja yako kuu ni kuwa iweje mwanachama na kiongozi kanda ya mashariki ya chama cha TAA aliyesafiri nje ya nchi ndani ya miaka mine tu aliporejea akaanza kuulizia wanaokiongoza chama chake kitaifa?

Jibu langu nikuwa, ndani ya kipindi ambacho Mwalimu yupo Masomoni, serikali ya kikolini ilikuwa inavisambaratisha vyama vya harakati za ukombozi,

Hivyo TAA ilikuwa imekumbana na zengwe hilo baada ya rais wake msomi na daktari wa kwanza kabisa Mtanzani Vedasto Kyaruzi kuhamishwa kituo chake chakazi na kupelekwa Kahama,

Katika anga za harakati za kimataifa TAA ilikuwa imeparaganyika.

Ndiomaana msomi na muhitimu wa kwanza wa PHD ya uchumi Tanganyika/Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliporejea ilikuwa kwanza kuulizia habari za chama alichokiacha miaka mitatu minne iliyopita!

Na katika kuuliza alianza na "nani wanakiongoza chama sasa hivi?"

Ndipo akaambiwa jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes,

Kumbuka katika kpindi hicho mtu huyu aitwae Abdul Sykes alikuwa si mzoefu kwa siasa za Nyerere zaidi ya Dosa Azizi na wengineo kama Dr Kyaruzi nk!

Bila shaka kwakifupi umenipata na ndio MANTIKI ya hotuba ya Mwalimu Nyerere.
 
Back
Top Bottom