Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mohamed Said,

Hajui anachoandika ni wakumuhurumia tu, Nyerere mwenye ameelezea jinsi alivyoishi na hawa wazee, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Suleiman Takadir, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Omar Londo, Rajabu Diwani, Mshume Kiyate, Bibi Tatu bint Mzee, Asha Ngoma, Bibi Hawa bint Maftah, Bibi Khadija bint Kamba, Said Chamwenyewe, na wengine wengi.

Hizi habari za mwaka 1952 watu walivyokuwa waungwana leo mwaka 2013 tunawaongelea wengine wanawakejeli na kuwadhihaki lakini leo historia inawakumbuka hawa wazee wazalendo.
 
Last edited by a moderator:

Nitagusia mambo matatu tu katika hili bandiko lako. Kwanza kuhusu vita ya Matabeleland hakuna siri kuwa Tanzania iliunga mkono ZANU-PF. Ni Zanu-PF ambayo ilibeba mzigo mkubwa wa ukombozi wa Zimbabwe. Joshua Nkomo alikuwa akiepewa silaha na Warusi lakini jeshi lake lilikuwa halipigani . Jiulize ni kwa nini?

Na baada ya mauaji ya Chimoia, nina hakika unaifahamu hii stori, kwenye mkutano uliofanyika Msumbiji chini ya uenyekiti wa Samora, Nyerere alimkasirikia sana Kaunda na Urusi ikafika point ya kumwambia Kaunda awaambie Russians to go to hell. Aliuliza hizo silaha Nkomo anazopewa ni za kazi gani kama hawezi kuwasaidia wenzake ambao wanauawa kila kukicha na jeshi la Ian Smith. It seems Nkomo alikuwa anasubiri resolution ya Zimbabwe imalizike ndipo atumie silaha zake. Kwa lengo lipi? Yaani wewe umeshaona wapi nchi inapata uhuru ikiwa na majeshi mawili? Haiwezekani. Ni kweli vita ya Matabeleland ilikuwa brutal, lakini war is brutal. Kwa baadhi yetu hatukushangazwa na vita ya Matebeleland. If you blame Nyerere and Mugabe, an equal blame should be put to Joshua Nkomo.

Pili, umezungumzia Nyerere/Kennedy na Jewish lobby. It is highly unlikely for Julius Nyerere to talk to a foreign leader about an internal affair. Hapa nitakuomba unipe uthibitisho. Kilichojadiliwa katika mkutano wake na Kennedy mwaka 1963 lilikuwa suala la kuipa silaha Afrika kusini. Kennedy was the first American president to stop arms to South Africa. And this was in 1963. This leads me to my third point.

In 1960, while campaigning for the presidency, John Kennedy made a phone call to Martin Luther King, Sr., the father of Martin Luther king jr. who had been jailed due to his civil rights campaign. That phone changed the history of American politics. The majority of black Americans up to this point were Republicans and voted Republican because of the history of Abraham Lincoln. But news spread throught black churches about this young catholic candidate who called papa King.

We all know what happened in the election results and this was the beginning of black American's shift to the Democratic party. On civil rights, it was the work started by Kennedy, and his support to Martin Luther King, jr. that led to the landmark 1965 civil rights legislation which was championed by his successor, Lyndon Johnson.
 

Ritz,
Ikiwa wanahistoria wa hapa nyumbani hawatafiti habari za wanaTANU wa mwanzo
kuiunga TANU mkono pale sokoni Kariakoo kwa sababu tu wanataka kuwakwepa akina
Abdu Sykes, Shariff Attas, Mshume Kiyate na wengineo sasa watamfikiaje Nyerere?

Hiyo TANU ni akinanani walikuwa wanachama wa mwanzo?
Si watu wa Dar es Salaam ndiyo walioanza mapambano na Muingereza katika TAA?

Sasa hiyo TANU ilizuka?

Ndiyo nikasema tunaweza tukawa na historia mbili za TANU na pasiwe na kubughudhiana.
Historia ya Chuo Cha Kivukoni iwepo pamoja na hii yetu msomaji mwenyewe aamue ipi kwake
inamkalia sawa.
 
MOHAMED SAID; lakini hii historia ya kivukoni inamapungufu! nadhani kitabu chao kinahitaji kufanyiwa sahihisho ili taifa letu liweze kuwa na historia iliyokamilika! kuendelea kusomwa kitabu cha kivukoni ni muendelezo wa kukaririsha wa tz historia batili! au labda naelewa tofauti?
 
As much as you people want to prove me wrong kwa kejeli na dhihaka, I will bring this to the light.

Lazima uelewe kuwa Mohamed ameonyeshwa kuwa mzigo aliobeba umeandikwa na mtu mwingine.
Hicho ndicho chanzo cha yeye kushindwa kuelewa tofauti ya ''Addresing na addressed''.
Mwanakijiji ameeleza vizuri sana.Mohamed amekiri kuwa kwa ''taarifa' alizokuwa nazo habari ndivyo kama alivyosema.

Pili, kwa kutambua maudhui ya alichokisema tulimwambia Mohamed asiseme ''kahutubia'' bunge bali semina au kinginecho.
Mohamed akaja na tarehe 15 May 2003. Tena akisema kama tungefanya tafiti tusingeuliza swali la namna hiyo.
Hakuishia hapo akazidi kutoa kashfa na kejeli kwa kutambua kuwa alikuwa sahihi.
Sasa ninyi mnaosema kuhusu maudhui, mnasema kitu gani wakati mhusika ametoa tarehe?

Tatu, katika mada yake kuna tukio na wahusika. Tukio ni kuhutubia bunge, wahusika ni wabunge na balozi.
Kwa mtu mwenye weledi lazima atajiuliza wanaofanya tukio hilo liwe katika mizania iliyopo ni akina nani?

Jibu ni wabunge na balozi. Mohamed kumtaja balozi na bunge haikuwa bahati mbaya ilikuwa ni makusudi kuonyesha sheria hiyo kandimizi kwa waislam ilivyoshiinikizwa.

Nne, kwavile bunge halikukaa siku hiyo na kwavile balozi hakuhutubia bunge, maudhui yote yanakuwa hayana maana.
Hayana maana kwasababu tukio limekosa viunganisho viwili muhimu, bunge na balozi.
Kwamba hakuna uhusiano wa dhahiri kati ya sehemu hizo mbili katika tarehe 15 May 2003.

Tano, tumeona mada halisi iliyoandikwa ambayo Mohamed ameinukuu. Technically hata kama ametaja aliponukuu, hapa jamvini amekuja na hoja kuwa ni paper yake na wala hakusema sehemu ya paper yake alinukuu kutoka kwa bwana fulani.
Hilo halina tatizo, tatizo linatokea pale ambapo anabeba dhamana ya maneno yale ambayo ni Tarehe 15 May 2003.

Mwisho, bila yeye kufanya utafiti kuhusu taratibu za bunge na itifaki za kibalozi, Mohamed akabeba mkoba hadi Ibadan akakalisha watu kitako na kueleza kisicho cha kweli. Kisicho cha kweli kwasababu leo watu wa Ibadan wanajua kuwa balozi anaweza kuhutubia bunge la Tanzania kitu ambacho hakijawahi kutokea.

Kwa mfano rahisi sana wa mitaani, mbunge X alimtukana mwenzake Z wakiwa katika baa wanakunywa.
Hilo ni tukio litakaloandikwa katika vijarida vya udaku. Lakini Mbunge X aliposema 'F' ndani ya bunge basi bunge zima lilizizima na nchi nzima kulaani. Kwanini? Jibu ni kuwa ametumia tukio(mkutano wa bunge) na wahusika(wabunge) ndani ya bunge(eneo) kusema neno baya.No one is talking about his/her topic any more.

Huu ni mwendelezo wa exaggerations za Mohamed (rejeeni post 13112 ya Mag3 ).
Sijui kwanini hamuoni mantiki iliyopo.

Mohamed amekashfu sana sisi wengine kuwa mahakimu kiruka, hatukafanya tafiti japo kidogo, atatuweka kwenye kundi alisoloweza kulisema n.k. Mbona hamjamtaka aombe radhi kuhusu hayo baada ya ukweli kujulikana mnajitahidi kushambulia walioweka ukweli wazi.

Mkoba wa Ibadan una tarehe Baru baru acha utetezi wa mitaani, mwenye mada hakuja na utetezi alikuja na tarehe tena akiwa ame-bold kuonyesha msisitizo na uhakika.

Nafikiria Mtu aseme Rais Mandela wa Nigeria amehutubia UN mjini Carcas venezuela kuhusu Malaria, ati tukubali tu kwasababu kuna neno malaria! Hell no!
 

Msiwe na hofu, mvua zinazoendelea zinanifanya nizidi kuwa shambani, neema ya kuvuna maji ya mvua na kutayarisha mashamba inanifanya niwe na muda kidogo wa kuingia JF, InshaAllah mashamba yatakuwa sawa na ntarejea jamvini, kwa sasa ni kuchungulia na kuondoka.

Wapayukaji naona mpaka leo darsa limewaingia, mmeshindwwa kuja na hoja kama kilivyo kichwa cha mada.
 

Kadogoo,
Kitabu changu ndicho kilichosahihisha kitabu cha Kivukoni.

Lakini si unaona jinsi kitabu changu kilivyowaumiza ndugu
zetu kiasi cha kufikia kurusha matusi mazito kwa hamaki?
 

Zomba,
Karibu sana jamvini.

Jamvi lilichafuka vibaya sana kiasi cha kuogofya.
Yaliwekwa matusi makubwa lakini hali imetulia.

Imekuwa kawaida sasa kujirudia na kupita njia tuliyopita.

Kubwa zaidi ni kuwa clip ya hotuba ya Nyerere hadi leo haijapatikana.

Hilo la kwanza.

Kubwa la pili na kidogo limepandisha ghadhabu ni kisa cha Shariff Attas
na Nyerere.

In Sha Allah taratibu utayaona yaliyoko lakini lengo nashukuru limefanikiwa pakubwa.

Wengi sasa wamesikia upande mwengine wa historia ya TANU.
Ni juu yao sasa kuchagua ipi chuya na upi mchele.
 

Wanajamvi,

Hebu msomeni hapa chini huyu Mchochezi anamaanisha nini na hapo juu anapinga nini?

Nilishasema ukiwa muongo jiandae kuutetea uongo huo kwa gharama yoyote!

Hasa utetezi unakuwa mgumu pale unapowadanganya werevu!

Haya chini ni maneno ya Mohamed Said juu ya Shariff Attass


 

zomba,

Karibu tena jamvini.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed,
Hatutakuwa na historia mbili za TANU au nchi hii. Ulichokiandika wewe sio historia ya TANU. Ni maoni yako tu. Historia ya Taasisi kubwa kama TANU haiwezi kuandikwa na mtu mmoja kwa kutumia vikabrasha flani, akaingiza na DINI yake humo, kisha akajiita ana "authority" ya Watanzania wote!

Uzuri mmoja wa TANU haikupata kuongozwa na kiongozi mwingine yeyote zaidi ya Mwalimu. Ngonjera nyingine zote za AA, TAA unaweza kuzinyumbulisha unavyotaka. Ukifika tarehe 7.7.1954 utaanza na Mwalimu hadi tarehe 5.2.1977 ilipotoweka rasmi duniani.

Historia isiyoambatana na tarehe hiyo itakuwa ni hadithi au msahafu.
 

Kila mtu ana mtazamo wake lakin mimi naamini kwa wasomi wote hatuwezi hukumu Kitabu kwa jalada lake. Kwani wasomi tunajikita katika maudhui aliyomo na sio kichwa cha habari.

Pole sana

 
Kadogoo,
Kitabu changu ndicho kilichosahihisha kitabu cha Kivukoni.

Lakini si unaona jinsi kitabu changu kilivyowaumiza ndugu
zetu kiasi cha kufikia kurusha matusi mazito kwa hamaki?
Kitabu chako kimesahihisha jambo lipi kwenye kitabu cha Kivukoni? Tarehe iliyozaliwa TANU imebadilika ikawa ile ya Burma? Rais wa KWANZA wa TANU sio Mwalimu tena?

Kuna anayemfahamu Abdu?
 

Asante sana kiongozi ubarikiwe mara elfu!
 

Yericho.

Nilipo Underline.

Naomba unifafanulie hapo, yaani TAA iliposhinda uchaguzi na Nyerere kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu wa kwanza tanganyika. Je ni sahihi kweli. Jiulize TAA ilishinda uchaguzi mwaka gani? na Nyerere kuwa waziri mkuu wa Kwanza tanganyika mwaka gani?

Nyerere alikuwa haruhusiwi kula ovyo na ndiyo maana Shariff Attas
alikuwa kivuli chake wakenda kula pamoja
.

Ina maana umeelewa kuwa Sharif Attas alikuwa mpambe wake hapo au alifanya hivyo wakiwa wanaenda kula nje ya nyumbani kwake Nyerere?.

Soma vizuri kisha tupe darsa kidogo hapo.


Lakin la mwisho Je Nyerere katika kumbukumbu zake alizoandika aliwahi hata siku moja kumtaja Mshume Kiate?

nasubiri majibu yako
 
Barubaru,

Kina Munif umeoa kwao Allah hawazidishie mara ya mwisho nimeonana na Mzee Islam wakati wanakaa Aggrey pale msikinitini Qibratein. Nyumba yao mtaa wa Aggrey na nyamwezi.

Ritz


Munif sio jina lao. Hilo jina walilipata wakiwa kule Ngerengere morogoro likiwa na mana Mwaminifu. Kwani yeye na kaka yake walikuwa na bakery kubwa ya mikate na biashara zao huko na kuwa wakawa wanaweka amana za watu kwa uaminifu mkubwa ndio wakapewa jina hilo la MUNIFU.

Ahsantum
 

Wild Card,
Lakini tayari sasa zipo historia mbili.

Unaona hapa kuna yenu mnayoitetea na mimi naeleza historia ya TANU kama
nilivyopokea kutoka kwa waasisi wake ambao wengine ni wazee wangu.

Tuvumiliane kwa hapa tulipofika.
Unajua kutokana na historia hii yangu imepatikana " Sheikh Hassan bin Amir Award?"

Tuzo hii inatolewa kila mwaka sasa yapata miaka zaidi ya 15.
 

Kwanza niseme ni TANU na sio TAA, nimakosa ya kiuandishi tu,

Ndio Mwalimu Nyerere alikuwa waziri mkuu wa kwanza, tena wakuchaguliwa sio wa mapinduzi au wakuteuliwa!

Hilo la pili kwa maneno ya Mohamed Said inamaana Shariff Attas alikuwa ni mlinzi wa Mwalimu Nyerere, (food tester)

Lamwisho ni ndio, Mshume Kiyate katajwa sana katika masimulizi na mafunzo na Mwalimu Nyerere,

Tafuta machapisho yake yahusuyo historia yake utawakuta watu wote aliowataja Mohamed Said na wengine wengi tu hawajatajwa na Mohamed!

Watanzania wenzangu mpende kusoma historia ya nchi hii,

Inashangaza sana watu kuja hapa jf nakuona kama mambo haya ni mageni,

Huku akina Mohamed Said wakijinasibu kuwa wao tu ndio wanaijua historia ya Tanganyika/Tanzania!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mrehemu Marehemu Mzee Julius Nyerere
 

Barubaru,
Ahsante ndugu yangu.

Bubu alisema kwa uchungu wa mwanae.
Hili nikilisitiri lakini nitalisema leo.

Mshume Kiyate kalazwa Muhimbili mahatuti.

Anamuuliza mwanae Kiyate, "Mmempelekea
Nyerere taarifa mie nimelazwa?"

Jibu ni kuwa taarifa zilikwenda.

Nawaachia wanaukumbi mmalizie kisa hiki.

PS:
Barubaru hebu muulize huyo kijana wapi tukasome habari
za Mshume Kiyate zilizoadikwa na Nyerere?

Kama kipo kitabu atufahamishe pia au kama nyaraka zipo
Nyerere Foundation atujuvye au East Africana, Maktaba ya
Chuo Kikuu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…