Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Jasusi,

Nilistaajabu,pale ulipokawia kunijibu maana nilihisi ya kuwa kwa hili usingenacha asilan. Lakin haina neno ndo kuelekezana kulivyo. Haina haja ya kufanza pupa na vishindo.
I suspect the main difference between us is that;you are making suggestion while I'm presenting a fact before you.
I'm pretty dismayed that, in your "analysis" you managed to reduce the very complex subject of Civil Rights Movement and Blacks struggle in Amerika during 60's into a very simple term.
Do you sincerely think that quick phone call you mentioned in your "analysis" did manage to solve everything like a click of an eye!? NO! I mean a big NO!

I never understood why many people(in your case Catholic) have been so fascinated by the criminal,Anti-Amerika,racist and unpatriotic Kennedy family!? Probably it's the same reason they love Bill Clinton;they favour style over substance.

Katika hiyo point yako ya mwanzo,inaashiria yakuwa unakubali kuwa Nyerere na Mugabe walifanza udhalim na unyama uso kifani dhidi ya raia wasio na hatia hapo Matabeleland,wengi wao wakiwa ni watoto,wanawake na vikongwe kama nilivyodai.
Lakini justification yako ni kwamba "War is brutal"!.
Na pia unadai,kama mimi namlaumu Nyerere na Mugabe kwa unyama ule,basi unanitaka lazim pia nimlaumu Joshua Nkomo!? Sasa huoni yakuwa hapa unani-blackmail kihoja ndugu yangu!?
Kwa kifupi,hoja yangu bado inasimama palepale,na umeipa nguvu zaidi kwa kuthibitisha japo huku ukiniwekea masharti yakuwa lazim nimlaumu na J. Nkomo.

People always seems to forget that it was Bobby Kennedy then the Attorney General,who had Martin Luther King Jr wiretaped,attempted to set him with hookers and had him jailed. The Kennedy's used the full power of the government to try destroy him and only sided with him when they realised and saw how powerful the Civil Rights Movement was and used him for political gain.
I think it was his daughter or niece who had said that Kennedy basically traded releasing MLK from jail for his endorsement.

Do you remember Jackie Kennedy a racist!? When she made comments about MLK that were more offensive and vitriotic!?

JFK,among many other things also failed to invite Sammy Davis Jr to his inaugural ball,despite the fact that Sammy Davis Jr worked extremely hard in the electoral campaign of 1960 to get him elected!?

Hapa inashabihiana na ile ya Nyerere kushindwa asilan kuhakikisha mwenyeji wake na mwanaharakati mwenzie Abdilwahid Sykes anahudhuria zile sherehe za makabidhiano ya nchi na wakoloni siku ya Uhuru. Matokeo yake maskini Abdilwahid Sykes ikamlazim akasikilize sherehe zile kwenye radio chumbani kwa Mamiye pale Kipata!!

Are you aware that Bobby Kennedy authorised J. Edgar Hoover, then FBI Director to spy on Martin Luther King Jr. private life!?

I'm sure you remember how Ted Kennedy supported pro-abortion laws that killed estimated 50 million Amerikan babies,many of them blacks.

When Ted Kennedy murdered Mary Jo Kopechne,he was not the first to commit murder. There are credible allegations that his two elder brothers murdered more people,including Marilyn Monroe.

Their Father,Joe Kennedy,was a major Amerikan organised crime boss,in the same league as Al Capone,Meyer Lansky,Luck Luciano and John Gotti. He made much of his money as a bootlegger during the prohibition era. Joe Kennedy was also a pro-Hitler and pro-Nazi anti-semite,when he served as a US Ambassador to Britain.

It should not suprise you Jasusi,that during the JFK term in office,Kennedy brothers did business with an old business partner of their daddy,the Mafia boss,Sam Giancana. The same Mafia business partner of Joe Kennedy,enabled him to steal the election in Chicago from Richard Nixon in 1960.

In your "analysis" you also you ignored the fact JFK himself,voted against the 1957 Civil Rights Law pushed by Republican President D. Eisenhower.
JFK also opposed the 1963 March on Washington by Dr. Martin Luther King Jr. A march that was organised by a black Republican A. Philip Randolph. I bet you didn't know that either!?

Kwa kifupi ,kwa mtu yeyote anaejua kiundani mambo ya Nyerere na JFK,hatopata tabu ya kujua ya kwamba hao wawili walikua ni Wakatoliki hatari saana,ambao waliweza kufanza lolote,chochote na pahala popote bila ya kufuata sharia asilan.

Halafu unashangaa ati Nyerere hawezi kuzungumza Internal Affairs za nchi nyingine na huyo criminal JFK!? Huyo Nyerere unataka ahusike na mangapi ya Internal Affairs za watu!? Embu chungulia tena japo kiduchu habari za hizi nchi halafu umuone huyo Nyerere na kuhusika kwake; Somalia,Ethiopia,Zimbabwe,Comoro,Seychelles,Uganda,Mozambique,Algeria,Nigeria /Biafra na kwingineko kwingi mno.

Pia usisahau zogo na vitimbi vya Nyerere na wale "Wanae Matapeli" kina Museveni,Yusuf Kirunde Lule,Godfrey Binaisa,Milton Obote na gangs zao. Halafu ndugu yangu Jasusi,unataka kuniwekea Premiere League isokua na maana yoyote. Hiyo yakuwa Nyerere kuwa anaingila/anazungumzia Internal Affairs ya nchi za watu ni mojawapo ya sifa zake kubwa.

Huo mkutano wa JFK na Nyerere;palizungumzwa vitimbi vingi mojawapo ni masuala/mipango yalohusu yale maafa na mauaji ya Zanzibar,pia jinsi ya kuwadhibiti Patrice Lumumba na Eduardo Mondlane bila ya mkono wa Amerika kujitokeza au kujionyesha dhahiri!!

Yasemekena yakuwa wewe ni mwandishi wa habari mahiri,basi nakuomba ndugu yangu, pia kipata wasaa pitia sources zako upya na pia haya hapa chini:

  • The Sins of The Father: Joseph P. Kennedy and the Dynasty He founded. Grand Central Publishing 1996 by Ronald Kessler.
  • JFK Biography by Prof. Michael O'Brien.
  • The Kennedy Men: The Three Generations of Sex,Scandals and Secrets. 1996 by Nellie Bly.
  • Barack Obama: The making of the Man by D. Maraniss.
  • Kwaheri Ukoloni! Kwaheri Uhuru! Dr. Ghassany.
  • www.cbs.com/stories/2011/09/12/earlyshow/main20104707.shtml.

Shukran.

Cc; Ritz,Ami,Nyambala,JokaKuu,Uthman
 
Ivi ata iyo st. 10 alifika? @ wildcard

Kuenda shule sio tija. Yuko Bakhresa hapa anawaajiri watu wenye PhD wamfanyie shughuli zake. Bill Gates anawaajiri ma engineer wenye PhD kwenye kampuni yake ya Microsoft.

Elimu ya Nyerere haikumsaidia kitu kwani alikubali kutumika na Wakoloni kama Condom na kuuza uhuru wetu ili kuendeleza maslahi yao chini ya mfumo wa Ukoloni Mamboleo.
 

Sheikh Mohammed,

Al Akhiy,Wallahi nakusikiza kwa utuvu na uadilifu uso kifani, na nakufahamu kwa yakini iso shaka.

Nami pia Allahmdulillahi,nilipata fursa ya kusikia mambo kiduchu toka kwa baadhi ya Wazee wetu hasa Babu Shariff Abdallah Al Attas. Kanieleza mengi na nimejifunza mengi toka kwake na kwa Wazee wetu wengine walotangulia.

Ndo maana,niliwahi kusikitika hapa jamvini,kuhusu Nyerere yakuwa alishindwa hata kwenda pale Bagamoyo kumzika Mzee wake na Mwanaharakati mwenzie Sheikh Mohammed Yahya Ramia!?

Lakini haina neno ndo kilimwengu...

Shukran.
 
WildCard,

Ushangai Freeman Mbowe darasa la 7 anawangoza nyie wasomi wa vyuo vikuu.

Akili ndogo inaongoza akili kubwa.

Wapi na wapi msomi wa Chuo Kikuu anaongozwa na darasa la 7 tena DJ.
Ah! Huyu bwana ni fomu six. Alikuwa Hull kipindi flani sijui kama ali-graduate. Wanaofahamu upande wa pili wa Abdu wanajua kwa nini hakuendelea na shule. Hili mzee wetu Mohamed hatakaa aliseme. Anammwagia misifa tuuu!
 

Katika kuonyesha umedhamiria kutugawa kidini,

Visa vya matambiko alivyofanyiwa Mwalimu Nyerere umeviacha vingine kwa maksudi tu na kuvitaja vile vya mashehe,


Mfano tambiko lililomchukua Mwalimu Nyerere siku 14 nyumbani kwa chifu Adam Sapi pale Kalenga,

Tambiko la chifu Fundikila wa unyamwezi lililochukua siku 7,

Je lile la Chifu Mazengo la siku 7,

Na mengine mengi sana!

Tena kwa kufafanua zaidi nikuwa lile Tambiko la Kalenga Iringa kwa chifu Adam Sapi lilikuwa ni maalumu kwaajili ya kumlinda Nyerere na MAPINDUZI ya aina yoyote ile, yawe ya ndani au nje ya nchi, na hili lilifanyika baada ya kutokea waasi ndani ya TANU waliokuwa wanataka kupindua uongozi wa TANU ya Nyerere!

Waasi hao sio wengine bali ni akina Abdul Sykes, Shehe Bin Amir, Shehe Takadir na wengine wengi ambao Mzee Mohamed Said anawalilia leo hii!
 
Ikiwa ni hivi, kwa kweli wazee hawa wamepigania UHURU! Visomo, matambiko, Ibada; malazi, maharage, maandazi kwa Mwalimu...., kwa kweli wamepigana!

Tunawahitaji wazee kama hawa sasa hivi ambapo risasi, mabomu, moto umeanza kuwakia makanisa, misikiti. Mzee Mohamed, natumaini unaweza kurithi mikoba ya wazee wako hawa. Unajua walichokifanyia nchi hii.
 

Ajabu ni kuwa leo Mohamed Said anapigania ukombozi wa nchi kidini wakati wa zee wake walipigania ukombozi wa taifa huru bila kuweka udini au ubora mimi!
 

Ritz,

Al Akhiy.

Nimealikwa huko Kicheba na Magila,kwa hiyo nitakapokuja holiday safari hii italazim twende soote mie na wewe. Maana kwa hizo habari nisikiazo za hicho Chama cha Kisiasa anachoshirikiana nacho Muheshimiwa Nguruvui3, Wallahi napata shaka na woga hata kwenda huko Kicheba peke yangu!aahaha!!

Al Akhiy,dasturi yako si nzuri ya kunitamanisha vyakula vinono kama hivyo na mimi bado niko kibaruani na kipande changu cha sandwich...utanifanza nitoroke hapa kibaruani!ahaha!!

Shukran Al Akhiy na mkae salama Insha Allah.
 

Wild Card,

Fikra yako kuwa Abdu Sykes hana mchango katika TANU ni jambo ambalo
watazamaji watajiamulia wao wenyewe kwa kuwa wewe umetoa fikra zako
kwa yale mie niliyosema.

Ndiyo nikasema hapana ugomvi tuache historia hizi zote mbili zisomwe na
pasiwe na bughudha.

Wenye uamuzi wa mwisho ni wasomaji.
 

Gombesugu,
Mie ninachoshukuru ni kuwa JF kwa hisani kubwa wamenipa fursa
ya kusikilizwa na watu zaidi ya 180,000 na wenye uwanja wanasema
uzi kama huu haujapatapo kutokea.

Naamini kuna wengi walikuwa hawajasikia TANU iliundwa vipi na akina
nani walikuwa mstari wa mbele.

Nashukuru nimejifunza mengi kwa ndugu zangu ambao imewawia tabu
kuamini mengi niliyowafunulia.

Hata hivyo nimesikitishwa na kejeli, ghadhabu, vitisho na matusi ya dhahiri.
Kama itakavyokuwa namshukuru Allah kwa kuniwezesha kuyasema yote
niliyosema.
 
WildCard,

Ushangai Freeman Mbowe darasa la 7 anawangoza nyie wasomi wa vyuo vikuu.

Akili ndogo inaongoza akili kubwa.

Wapi na wapi msomi wa Chuo Kikuu anaongozwa na darasa la 7 tena DJ.

RITZ:

Unayosema ni sawa kabisa akili ndogo inaongoza akili kubwa! ndio maana wanataka kumburuza Profesa Baregu ajiondoe tume ya Katiba, lakini Profesa kashtuka kumbe alikuwa anaongozwa na akili ndogo ya ma DJ wa darasa la 7 au form 6 kama anavyodai WILDCARD!!!
 
Gombesugu, sijui kuna vitimbwi gani nimefanya hadi Ritz akakudokeza pembeni nawe usinijulie kulikoni. Huo kama si usenganyaji kama alivyosema Wickama sijui ni nini na kama ndio basi mumetoka nje ya dini

Mimi huwa namwambia mtu kile ninachotaka kumwambia na si kile anachotaka kusikia.
Husema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kama shubiri.
Hukubali mapungufu na udhaifu kwa kutambua kuwa mtimililifu ni mwenyezi peke yake.

Ni lazima watu waelewe kuwa Uislam si chama cha siasa au cha mpira.
Dini ni imani na hivyo inahitaji akhili kuielewa.
Nimeambiwa nimeishiwa hoja na al maarufu Big show nikasema basi japo nitie senti sumuni.
Natahayari kusoma matusi, kadhia eti kwasababu sijasema kile watu wanachotaka kusikia.

Ukitaka kusikia unachotaka kusikia msome Mohamed Said. Hakika hutakiwa kuwa na akili, unatakiwa kuwa na macho na mdomo wa kumaka! leso ya kujifuta jasho na maji endapo utapata mghafla katika vile vitokavyo ndani ya mwili.

Hoja yangu si kutetea BAKWATA, ni kuonyesha kwa uwazi kuwa si kweli kwa anayesema haiungwi mkono.
Mimi nimetembea nchi hii sana nakuhakikishia kuwa maustadhi, maalim au masheikh ni wafuasi wazuri wa BAKWATA.
Ina watu nyuma yake ima ukubali au ukatae lakini huo ndio ukweli.

Nimeseme pia kuwa hizi taasisi zingine zina matatizo sana. Ipo ya mali za waislam na ipo ya haki za waislam.
Zote hizo zinafanya kazi Kariakoo na zinajihusisha na kiwanja cha Ng'ombe na nyumba za wakfu.

Kiwanja kiliuzwa na maalhaji kikanunuliwa na maalhaji wote waislam, sasa akina Mohamed, Ponda na Ilunga wanawatoa watu katika ukweli wanasema ni mfumokristo.

Kama utaweka akili zako pembeni, hewalaaa!!!! hilo ndilo unataka kuliskia, vinginevyo ukweli ni kuwa hujuma zimefanywa na waislam wenyewe kwa wenyewe. Sasa leo watu wanahamasisha kuua watu wengine kwa tatizo lililo uvunguni mwa kitanda chao! Uislam hausemei kuwa unatakiwa kuidanganya jamii, hawa ni wachumia tumbo.

Angalia kiwanja cha Kibaha cha shule ya ufundi, mafisadi ni waislam hadi mradi ukaondolewa, leo watu wanatafuta sababu za kimaaluni kwa kusema eti ni mfumokristo.

Hilo ndilo mnataka kusikia, kwa anayeijua nchi hii kuanzia Shirati Mission, Magila mission, Ujombani Tanga kule TAMTA, Nakapanya, Mikindani, Kwa mtipura na mfenesini, anayeishi Takadir street na mwenye mtazamo mpana atakuambia kuwa hilo si kweli, kiwanja kimefanyiwa fitna na waislam wenyewe hakuna mfumokristo, hilo la mfumo ni kutaka kufurahisha nafsi zenu kwa kuwafanya majuha.

Kwa msingi huo ndio maana nasema wakati umefika wa kutenga mambo mawili.
1. Viongozi wa imani
2. Viongozi wa taasisi.

Viongozi wa imani wasimamie mambo ya ilm ya dini na wale wa taasisi wasimamie mambo yanayohusu maendeleo kwasababu dunia ya sasa intawaliwa na weledi wa mchanganyiko wa mambo na hivyo kuhitaji watu wenye weledi.

Kinyume chake utaendelea kusikia hoja za msingi zikijengwa na watu wasioweza kuzisimamia na hivyo kupoteza maana iliyokusudiwa. Mathalan, kama suala la kadhi ni la kiimani basi suala hilo lielezwe kwa mtazamo wa kiimani likisimamiwa na viongozi wenye weledi wakisaidiana na viongozi wa imani.

Kwa sababu ya mapungufu kadha wa kadha, hoja nzito kama hiyo imeshikwa na washabiki ambao si viongozi wa imani au viongozi wa taasisi wenye weledi. Utashangaa watu kudai mahakama ya kadhi kwasababu kuna MoU na si kwasababu ya imani. Tatizo hapa ni watu wa kujenga hoja ya kimantiki.

Na wala haina maana hakuna watu wenye uwezo huo. la hasha! wapo maelfu lakni wao wamechuakua back seat na kuachia issue kama hiyo kwa wasio na upeo wa aina yoyote iwe ilm ya dini au nyingine zaidi ya kuwa fanatics.

Niseme kuwa nitawaeleza watu ninachotaka kusema hata kama ni kichungu na sitawapendeza watu kwa kuwadumaza kifikra. EAMWS inayopigiwa kelele haijulikani kwanini haikurudi Momabasa ilikoanzia na kujenga chuo hypotthetical hadi watu watumie muda mwingi kufunga akili zao kwa kitu cha kufikirika na wasifanyie kazi uhalisia wa hali iliyopo.
How many times watu wanajadili kuhusu MMU?


Kuna maembe matamu sana kutoka Mtindiro, nikipata wasaa nitakutumia kwa pakacha.
Kule wanapopoa maembe maana warabai kazi yao ndaza!

Karibu bonde ni kwema
 

I almost began to take you seriously mpaka pale uliposema kuwa Nyerere alizungumza na Kennedy juu ya kumdhibiti Lumumba. Nyerere amekutana na Kennedy 1963. Lumumba ameuawa 1960. This simple fact makes everything you are claiming to be another njozi. Kuhusu Matabeleland, sina fact kuwa majeshi yetu yalishiriki. What I was saying is that if they took part Joshua Nkomo is as much to blame as anyone else. Hata ungekuwa wewe Mugabe usingeruhusu nchi iwe na majeshi mawili independent of each other. Na kuhusu racism ya Marekani every white person at one time or another has been a racist, kwa hiyo matamshi ya Jacqueline Kennedy hayana mshiko.
By the way, hivyo vitabu vyote nimevisoma ila tu kile cha Dr. Ghassan sikuweza kuendelea baada ya ukurasa wa kwanza kwa njozi zake kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.
 

Hata Lema naye darasa la 7 akili ndogo inaongoza akili kubwa.
 

Nguruvi3,
Tuongee ukweli,namm ni miongoni mwa wale ninaokuheshim sana,tena sana,napata raha sana unapojaribu kuingia kwenye vikao vyetu vya gahawa na kuongea kwa lugha zetu na kufuata muktadha stahiki,ila tatizo lako unayumba yumba sana,pia unajifanya unaujua sana uislam,,ah yawezekana unaujua kweli kwani siku hizi kila jambo ukiliamulia kulisoma na kulipa juhud utalielewa tuh,insha allah nakuombea dua usiwe mwenye kufa ila ufe hali ya kuwa umekuwa muislam,,
"walaa tamutunaa ila wa'antum muslimuun",,insha allah nakuombea sana...

Naomba nikuulize kitu kimoja,jumuiya zenu za kikristo zilivoundwa zilikua zina mkono wa serikali katika kuundwa kwake??
Kama hapana,iweje sasa serikali hiyo hiyo ichukue jukumu la kuiunda bakwata ilie kiwe chombo kinachosimama kwa niaba ya waislam na kufuata matakwa ya serikali??nyerere dhamira yake ilikua nini??

Na kwanin hakuthubutu kufanya hayo kwenu nyinyi na jumuiya zenu??,kipi alikiogopa??

1.viongozi wa imani kwetu sisi ni kina ponda...

2.viongozi wa taasisi kwetu sisi ni hao kina SIMBA,lakini kwa kuwa taasisi hizo zimeundwa na serikali ili zisimamie mfumo kristo sisi hatuna haja nazo,wala hatuna haja nao...

wao kivyao na bakwata yao/yenu,sisi kivyetu na uislam wetu,hata mkituita Extrimists sawa tuh,kwani tunakosa nini??

hayakuwa haya maisha ya dunia ila ni kitu chenye kupita tuh,mungu muumba wa mbingu na ardhi ndiye mwenye kwenda kutuhukum na tutafaham huko baina ya haqi na batwil,,

tuvute subira tuh,muda wetu wa kuondoka hapa dunian ukifika mbivu na mbichi itajulikana...
 
Last edited by a moderator:
Nikiiona hii picha nakumbuka mbali sana kuhusu unyama aliofanyiwa Kambona yeye pamoja na ndugu zake. In his address to the Press in London in 1991 Kambona recalls the events. " Mr Nyerere was staying with me in my cramped student accommodation. We discussed how he could avoid returning to Tanganyika to face his supporters empty handed. I managed to persuade him to state at a press conference at the East Africa House in Marble Arch that ‘The White Settlers in Tanganyika were the most reasonable in East Africa.' He agreed to do this on condition that I would suspend my law studies in London and return to Tanganyika to give him support before the National Executive Committee of TANU when he defended the "most reasonable statement." Following the first elections under universal suffrage, TANU won every seat but one. TANU formed the first government under Self Rule, with Julius Nyerere as the Chief Minister. It was also during the preparations that Kambona married Flora Moriyo from Kilimanjaro, during a trip to London in November 1960 to finalize the details of independence with the British Government. The ceremony was held at St Paul's Cathedral, London and Julius Nyerere led the young bride to the alter. Kambona was appointed the Minster for Education. He later held posts as the Minister for Home Affairs, Minister for External Relations and Defense, the first Chairman of the OAU Liberation Committee and Chairman of the Drafting Charter of the OAU and finally Minister for Regional Administration. In 1964 Kambona played a crucial role in the unification of Zanzibar and Tanganyika along side President Nyerere, President Karume and Chief Minister Hanga after the Zanzibar revolution. He was also the main negotiator between the government and the rebellious army leaders in 1964, when soldiers from the Colito Barracks staged a mutiny. Nyerere and Kawawa were both led into hiding in Kigamboni. After three days of negotiations, Kambona consented to speed up the process of Africanisation within the army. In an interview with London's Daily Telegraph, Kambona said, "after I had calmed down the soldiers, I went to fetch the other leaders in my Land Rover to bring them back to the city." The mutiny was eventually put down by the British Army and Nyerere praised Kambona for his bravery and loyalty. After the mutiny, differences between Kambona and Nyerere began to appear. Nyerere wanted to introduce a one party system into Tanzania to strengthen state security. Kambona argued against the move claiming that it would inhibit people's freedom and progress towards democracy. However, Kambona was defeated in parliament. He refused to sign the bill. In 1967 after a trip to China in 1965, Nyerere impressed with Mao's style of communism wanted to adopt the same system under the guise of Ujamaa. The main doctrine behind Ujamaa was the relocation of peasants into village communes and the nationalization of all industries and property. Kambona did not agree with the policies arguing that they would rather increase poverty and state control over the people. He resigned from the Government and the party and later Kambona with his family fled to neighbouring Kenya and then UK were he was granted political asylum. Immediately Kambona's properties were confiscated. His two brothers and were detained without trial and put in prison for over ten years. Other family members were harassed and detained. Some were falsely accused of plotting to overthrow the Tanzanian Government and were tried and imprisoned by the Government. Most famous of these were Bibi Titi who fought alongside Nyerere in the independence movement and was head of the woman's wing and also Michael Kamaliza, the former trade unionist and TANU member and government Minister. Other family members included Gray Mattaka, John and Elia Chipaka and Prisca Chiombola. Kambona was also accused of being the ring leader of the plotters while in London and was tried in absentia. The accused finally appealed to the East African High Court and were acquitted. Though they were later rounded up by the Tanzanian government and thrown into jail again. Kambona was also accused of stealing millions of public funds which he rejected out rightly in a press statement issued on 6th September in London, 1967. The allegations claimed that "Kambona was found with a lot money when searched at Nairobi Airport". However in his press statement, Kambona challenged the Tanzanian government to request the Kenyan authorities to ‘substantiate the allegations" which they never did. In London Kambona led a tough life in exile under considerable financial constraints. However in 1982, his two brothers were eventually released from detention after the intervention of New Zealand Prime Minister Robert Muldoon. In 1990 anticipating changes in Tanzania, Oscar Kambona formed the Tanzania Democratic Alliance, an umbrella organization bringing together the various pro democracy parties. When a multi party system was introduced in 1992 Kambona requested to return to Tanzania. The Tanzanian government refused claiming that he was not a citizen. Kambona appealed to the British Government to give him a travel document to enter Tanzania. The Tanzanian authorities claimed that they would arrest him immediately upon entry. Nevertheless, on 5th September 1992, Kambona made the courageous journey back to Tanzania and triumphantly entered Tanzanian soil. No authorities were present to arrest him, though he was given only three months to sort out his nationality question. On returning to Tanzania Kambona found that the progress towards democracy was disappointingly slow. After experiencing several strokes Oscar Kambona died in London in 1997 where he was receiving medical attention. In a twist of fate his younger brother Ottini Kambona also died at the same time from heart failure. Kambona is survived by his wife and two children. His eldest son Mosi Kambona was murdered in London in unexplained circumstances.
 
Mnaikataa BAKWATA kama watu wanavyoikataa CCM. BAKWATA ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo ili mradi itaendelea kuongozwa na wasio wafiaDINI


Vyovyote vile,ikibidi iongoze hata dunia yote hii hiyo bakwata,sisi tutazid tuh kuipuuza na kuiacha ijifie zake kama muasisi wake alivojifia na kuzikwa,na i am telling you,hata ikifa sasa wataosononeka baina yetu na nyie mtakuwa nyie kwa kuwa mna maslahi nayo...

Sisi muongozo wetu tunaujua ni Qur'an na Sunnah za kipenz chetu Muhammady s.a.w,

Bakwata nani anaitafakari bakwata?
 
WildCard,

Hayo mambo mbona yalikuwepo...
Ikiwa ni hivi, kwa kweli wazee hawa wamepigania UHURU! Visomo, matambiko, Ibada; malazi, maharage, maandazi kwa Mwalimu...., kwa kweli wamepigana!
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, "Twining (Twainingi) umekwisha!" (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.
 
Last edited by a moderator:
Nafyonza Ilm tu hapa nachukuwa data na facts tu za uhuru wetu wa Tanganyika makapi yote na matusi nayaacha, nafyonza jamami Mzee Said, mimi natoka tarudi tena kufyonza Ilm.
 

Nguruvi3,

Thank kwa comment zako.

Tatizo lako unamtazama kwa upande mmoja tu na sio pande zote.

Waarabu ndio maana tunasema SWADAKA Inaanzia nyumbani. Huwezi hata siku moja kumsaidia jirani yako chakula wakti familia yako inalala na njaa.

labda weka jadwali vizuri uone. Enzi za mkoloni hakukuwa na Rushwa na sharia zilizopo zilisimamiwa vizuri. Hakukuwa na upungufu wa vitu madukani na hivyo haikuwahi tokea ULANGUZI ambao ulisababishwa na watu wachache kujilimbikizia mali na kuwauzia wengine kwa bei ya juu. Muendelezo wa tarbia hii ndio leo mnaita UFISADI.

Jiulize wa waTz hawa hawa ambao wakati wa mkoloni hawakutenda haya leo hii wamekuwa vinara wamejifunza wapi?

Mimi naamini wazi kuna kusoma na kuelimika. Mtu yoyote aliyeelimika anakuwa na swifa kuu 3. ya kwanza anapenda kujifunza, Anapenda kushauriwa na mwisho kuwa na maamuzi kutokana na ushauri.

Mimi siwezi sema mengi lakin Mzee Mtei anaweza kuwaeleza nini alishauriwa kuhusu uchumi wa nchi yeye aliamua kufanya kisiasa. Mfano mdogo tu ni makao makuu kuwa Dodoma.

Lakin mimi naamini maji yanafuata mkondo. Nikimkumbuka mchezaji wangu wa pamba Khalfan Ngasa, Khalid Bitebo, Hussein masha na wengine Leo hii kuna Mrisho Ngasa, Kulikuwa na Aboubakar Salum ''Sure boy '' wa yanga leo kuna Salum Aboubakar na hata Mcha Khamis wa Miembeni Znz leo kuna hamis Mcha. Kuna Maalim Ali H Mwinyi leo kuna ...

Kwa maana kua ukiona mtoto anatukana ujue kafunzwa na wazazi wake. je nao aliwafunza nini wanae. je uoni kuwa kuna tatizo hapo.

ndio maana kama mchumi na niliyewahi fanya kazi tanzania naweza sema kwa kinywa Kipana kabisa kuwa Nyerere alikuwa tajiri sana kisiasa lakin alikuwa masikini sana wa kiuchumi na hilo ndio dimbwi lililowatumbukiza wa Tz mpaka leo ni masikini japo muna resource zote.

kama ufisadi nae alikwisha ufanya. Jiulize kwanini alikataa kukaa IKULU na kuamua kukaa nyumbani kwake msasani. je ujui kuwa fedha za wananch
zilitumika katika kuijenga na hata kuiweka nyumbaile vizuri kulingana na hadhi ya Rais. je huo sio ufisadi pia .

na huu umasikini au madhila mnayopata hayataweza kwisha kama mtataka kuyatatua kisiasa lazima mfate nyayo za KAGAME. kwa kuwa wachapa kazi, kuhishimu taaluma na kusimamia sharia zenu bila kuangalia nani ni nani katika jamii. Ukweli na uwazi ndio silaha kubwa

Nguruvi3.
Tiugusie bonde

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…