Spike Lee,
Karibu jamvini.
Ilm ni hidaya kutoka kwa Allah na ni amana.
Aliyekuwekeza amana yake akija una wajibika kumrejeshea.
Wengi hapa hawakuwa wanaijua historia hii ya kudai uhuru.
Kinachonisikitisha ni kuwa inawasononesha na kusababisha
hasama kitu ambacho sikutarajia.
Kuna mtu anazungumza kuhusu matamabiko.
Lakini unajua Mwafrika kuacha mila yake ni tabu...
Katika TANU ile ''inner circle'' walichokuwa wamekiweka mbele
ilikuwa tawaswul kwa kuwa hapa ni Allah mwenyewe anaombwa.
Nadhani umesoma visomo nilivyovieleza kuanzia 1948 hadi TANU
ilipokujakuchukua nchi.
Kuna mtu kafanya kebehi.
Hainishangazi hata kidogo mambo haya ili kuyaelewa inabidi uishi
ndani yake hapo ndipo utakapotambua athari yake.
Vinginevyo utaona si lolote si chochote.
Kama itakavyokuwa nimeeleza waliyofanya wazee wetu katika kuipigania
nchi yao.
Kipo kisa cha Sheikh Issa Nassir wa Bagamoyo.
Huyu alikuwa ''special body guard'' wa Nyerere.
Ukiaangalia picha ya Nyerere ile amebeba bango lililoandikwa ''Uhuru 1961,''
pembeni yake yuke Rajab Diwani na yuko Sheikh Issa Nassir pamoja na
watu wengine.
Sheikh Issa Nassir alikuwa bingwa wa ''seth habar...''
Spike Lee,
Katika vitu vilivyonipa utatanishi ilikuwa vipi nitaeleza katika kitabu ni
mikasa kama hii.
Nilifarajika sana pale Gombesugu aliponiambia kuwa ananielewa vyema kabisa
na yeye kapokea mengi katika hayo kutoka kwa babu yetu Shariff Attas.
Tushie hapa.
Sheikh Mohammed Said,
Umemtaja huyo Sheikh Nassir wa pale Bagamoyo. Ana nduguye/Cousin wake akiitwa Bwana Maembe Bin Mohammed Bin Mzaham. Huyu Bwana nae pia alikua mmojawapo wa wanaharakati vinara wa kupigania Uhuru kwa pale Bagamoyo.
Nyerere aliwahi kumtia ndani kwa takriban miaka miwili siku zile za "Uhujumu wa Uchumi". Kisa chake ati alikua na boat/mashua mbili za kuvulia samaki pale Bagamoyo!?ahaha!!
Alipotoka kizuizini huyu Bwana, haikupita muda akafariki maana alidhoofika mno na utu uzima na vitimbi vilomkuta huko jela.
Sasa ukifikiria kulikua na wale mabaniani kina J.W.Ladwa pale Upanga...walikua na visa na vitimbi viso mfano tangia "enzi ya Mwalimu" na mpaka kesho,lakini hakuna alowahi kuwakurubia wala kuwagusa asilan!?
Haina neno ndo kilimwengu.
Ahsanta.