Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Yericko Nyerere,
Nakumbushia swali langu Oscar Kambona, alikuwa na cheo gani TANU kwa faida ya wanajamvi tufahamishe.
Aliuwa Organization Secretary...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yericko Nyerere,
Nakumbushia swali langu Oscar Kambona, alikuwa na cheo gani TANU kwa faida ya wanajamvi tufahamishe.
Vipo visa na mikasa mingi ya uhuru mingine ya kuchekesha na mingine ya kuliza khasa
mtu akatokwa na machozi.
Nakumbuka Sokoine alimuweka Butiku ndani kwa kosa la kuhujumu uchumi. Nyerere akatumia mabavu kumtoa na kuamua kumkejeli Sokoine ili kuhalalisha kitendo chake cha kumtoa Butiku kwa kudai kwamba tukiwafuatilia nyie viongozi hapa ni nani atakayekuwa hana mali kama ya Butiku? Yaani kwa sababu imeangukia kwa mjomba wake basi anahalalisha kila kiongozi ni mwizi hivyo Butiku aachiwe!!!!!!!!!!!!!!!
Haikuchukua mda Sokoine akaaga dunia!!!!!!!!!!!!!
Grrrrrrrrrrrrrrrrryyyyyyyyyyyyyyyyy
Naomba niweke rekodi vema. Kwanza kabisa Mohamed hayo maneno niliyokazia kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa wewe hufanyi kama unavyomweleza RWEYE1. Nina ushahidi wa kutosha kuhusu wewe kupayuka jambo bila kupima(kumbuka lini tumeanza mnakasha na mara ngapi tumekuwa hapa JF). Kuna ushahidi wa kutosha kuwa unaongea usicho na ujuzi nacho. Sasa hapo jipime mwenyewe kuwa maneno hayo uliyosema yamekulenga au kumlenga Rweye1.Jamani bora kabisa tuache kabisa mijadala ya kijinga kijinga kama hii. Kujadiliana na mtu mwenye matatizo ya kichwa na mfadhaiko ni kupoteza muda na kuipotosha jamii. Bw. Muhamed ana ajenda potofu kabisa.
Mimi ni muislam, kama walivyo waislam wengine wengi, watu wa namna hii tunawaogopa kama ukoma kwa kuwa hawataki kukubali ukweli hata kama wanajua ukweli huo. Hawajui kuwa kinachowaangusha waislam ni watu kama yeye wenye ufinyo wa kufikiri pia na kukubali kuongozwa na watu wenye elimu finyo ambao hawawezi kubuni kwa ustadi mipango ya maendeleo kwa jamii ya waislamu.
Kumbuka wakati wa kugombea nafasi ya shekh mkuu wa bakwata ambapo alikuja kushinda mufti simba.pamoja na wagombea wengine waliokuwa na sifa kiduchu aligombea pia profesa. Kwa kuwa waisilam wana aleji ya watu wenye elimu alipata kura sufuri ktk kinyanganyiro hicho kwa kuogopa kuwa angefanya mabadiliko makubwa kama angekuwa shekh mkuu kwa kuwaengua wasio na kisomo na kuwaweka wasomi katika nafasi zote za uongozi wa bakwata.waisilam tusilaumu wakristo tujilaumu wenyewe.
Iwapo twataka maendeleo basi tuanzie kufanya mabadiliko katika mfumo wa uongozi wa bakwata. Lazima tuwe na muundo wa utumishi (scheme of service) kwa ngazi zote za uongozi wa bakwata. Muundo huu ugawanywe mara mbili, wa kiutawala na kidini.kila nafasi katika idara ya utawala itajwe elimu muafaka (elimu dunia). Viongozi wote wa kitaifa wawe na shahada (degree). Kama hili litafanyika, maendeleo yataanza kuja kwa waislam na wivu wa kijinga na infiriority complex zitaanza kupungua taratibu na watu kama bw. Mohamed wataona aibu kutuletea hadithi potofu za kulazimisha kulisha watanzania hadithi za uchafu ambazo mwisho wake ni kuleta utengano nchini.
Mungu tuepushe na watu kama hawa ambao muda wote wanupoteza kwa kutoa hadithi na mihadhara potofu badala ya kuwafungua macho waislamu kujitambua na kuanza harakati za kupambana na ujinga na umasikini na wakati mwingine hata kwa kushirikiana na hao anaowaona "wabaya wake" yaani wakristo ili kuchota kwao mema yanayoweza kutusaidia.
Mtoto wa kihaya (zamani) akipelekwa kuanza shule mara ya kwanza huambiwa afanye urafiki na mwanafunzi mwenye akili sana darasani sio kufanya urafiki na zezeta anayekuwa wa mwisho darasani kila mara. Hiyo ni mila ya kihaya ambayo sasa imeanza kutoweka na ndio maana elimu bukoba imeshuka.
Wahaya wa enzi hizo waliamini kuwa ukifanya urafiki na mwanafunzi mwelevu na wewe automatically utakuwa kama yeye angalau kwa kiasi fulani. Mimi nadhani bw. Mohamed ni mtu wa asili ya pwani.
Nawaombeni waislamu tuwapuuze na kuwaogopa watu kama mohamed. Tushirikiane kwa karibu sana na wakristo ili tuweze kupata nafasi ya kujifunza/kuiga mipango yao mizuri.naamini tukionyesha wema kwao nao watarudisha wema kwetu at the end of the day watoto wetu ndio watakao kuwa wa kwanza kufaidika na kuujenga/kuukuza uislamu.wabillah taufiq-shukranRweye,
Kwa kuwa umejinasibu kwa Uislam nami nitazungumza na wewe kwa maneno yake Allah SW.
Uislam ni tabia njema.Waislam hawapayuki hupima kila jambo na Allah katuonya tusizungumze
kitu tusichokuwa na ujuzi nacho.Ina l'muuminina ikhwan.Muislam nduguye Muislam yaani Waislam wote ni ndugu.
Mbona sioni tabia hii kwako na hii ni post yako ya pili tu naisoma?Nakuona umeingia na mashambulizi moja kwa moja.
Vipi utamnusuru nduguyo Muislam kama Allah alivyoagiza ikiwa Uislamwako ndiyo huu ninaoshuhudia?
And you call this logic? Or facts? It is simply uwongo, with a capital UWONGO. Butiku hajawahi kuwekwa ndani na Sokoine. I know, because Butiku is my brother in law. Unakuja huku unajaza ----- wa uwongo na kuuita logic halafu unataka watu wenye akili timamu wachangie? Shame on you!
Naomba niweke rekodi vema. Kwanza kabisa Mohamed hayo maneno niliyokazia kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa wewe hufanyi kama unavyomweleza RWEYE1. Nina ushahidi wa kutosha kuhusu wewe kupayuka jambo bila kupima(kumbuka lini tumeanza mnakasha na mara ngapi tumekuwa hapa JF). Kuna ushahidi wa kutosha kuwa unaongea usicho na ujuzi nacho. Sasa hapo jipime mwenyewe kuwa maneno hayo uliyosema yamekulenga au kumlenga Rweye1.
Nikirudi kwa Rweye1, naona ameingia kwa ghadhabu kidogo kama ilivyo kwa mtu mwingine.
Anayedhani kuwa yupo mtimilifu basi na atuambie! Lakini katika aliyoongelea ukiacha yale aliyoghadhabika kuna mambo muhimu kayasema ambayo nilitaraji yatajibiwa kwa hekima zile zile zitokanazo na hoja zake.
Kinyume chake ameshambuliwa, eti kwa kusema yeye ni Mwislam. Mohamed hakuna mtu anayeweza kujinasibu katika imani. Imani ipo kwa mtu na wala si chama cha siasa, mpira au mdumange.
Yeye akisema ni mwislam basi hilo ni baina yake na Mola wake.
Unaposema anajinasibu hapo unahalifu na kupoteza busara.
Kwani wewe ni nani hadi uweze kujua mwislam au mwingine awaye?
Kwani cheti cha uislam kinatolewa wapi na kwa rekodi gani kiasi cha kusema huyo anajinasibu!
Jamani imani ni kitu rahisi ukikielewa na ni kigumu sana ukiimba tu.
Nasema ni kiugumu sana ukiimba kwasababu maoni ya Mohamed ni kuwa Rweye1 alitakiwa amuunge mkono ili akamilike na awe ndugu. Mohamed anasahau kuwa tofauti ya mitazamo ni shemu ya Uislam.
Kama isingekuwa hivyo leo tusingekuwa na Sunni, Shia, Kadiani,Bohora, Ismailia n.k.
Hata katika wale waliotangulia bado kuna mahalifa na masheikh wakubwa waliotofautiana sana kimitazamo.
Ndiyo maana tumekuwa tunasikia kuwa jambo lina utata kutokana na tafsiri na mitazamo.
Mohamed alikataa kutoa kauli juu ya DVD ya Ilunga na kulipeleka suala hilo ''kwa maulamaa''.
Hapa ni wazi kuwa alikuwa na mtizamo tofauti na waislam wengine waliodhani kuwa Ilunga hakufanya jambo zuri.
Juu ya yote na mitizamo yote tofauti bado kila mmoja amebaki kuwa mwislam.
Leo kwanini Rweye1 aonekana kituko eti kwasababu amepingana na Mohamed.
Kinachotisha sana ni Mohamed kutumia maneno ya Mwenyezi kwa namna atakayo.
Hili la Mwislam kumnusuru mwenzake nalo linahitaji kuangaliwa.
Labda naomba msaada kwa Mohamed na vijana wake wanieleze, hivi akitokea Mwislam anamnajisi mwanamke kwa nguvu(kubaka) na mwanake huyo si Mwislam, je huyu mwislam aliyeona hilo anatakiwa amnusuru nani?
Nadhani tatizo la kutaka kumeza tu ni kubwa kuliko linavyoonekana.
Lazima kuwe na mawazo tofauti ili kuleta akhili na fikra zaidi.
Nadhani ndio maana kuna watu wanaamua tu Ijumaa maandamano na bila kufikiri watu wanaunga tela kwasababu kutofautiana na wenye Uislam ni kuukana Uislam.!
Jamani hili nalo linahitaji elimu yoyote zaidi ya akili za kawaida za mwanadamu?
Na mwisho, nawashangaa sana wale wanaosema Mufti Simba hana elimu ya dini. Nakumbuka na nasimama kusahihishwa kuwa wakati wa sheikh Hemed, huyu alikuwa katika kamati ya maulamaa.
Sasa sijui watu wanataka kusema au kuuambia nini ulimwengu kuhusu hili.
Kitu kimoja nilichosoma magazetini ni kuwa mufti Simba alisimamama na kusema Ponda hana elimu ya dini hata kidogo.
Hakuna aiyesimama kuhoji elimu yake wala ku-challenge maneno yake.
Sasa kama Ponda ni kiongozi kwanini mufti anayesemwa hana elimu ya dini awe dhalili licha ya yeye kuthibitisha kuwa Ponda ni mweupe.
Hebu angalieni mnasema nini kwanza, kupayuka au kusema mtu asicho na ujuzi nacho imekatazwa kama alivyosema Mohamed. Naona watu mnasema kila jambo hadi mengi yasiyofaa.
Msioongee hata yale ya chumbani kwenu.
Busara ipo wapi?
Ndio tatizo la kuoga dimbwini na watoto, mwishowe inakuwa vigumu kuwatenganisha kwa nasaba. Mtu akikusimulia jambo la kipuuzi lisilo na chembe ya ukweli na wewe ukalimeza fasta fasta, maana yake ni kwamba unapoteza uwezo wa kupima siyo kwa yake unayoyasikia tu bali yake unayoyanena pia.And you call this logic? Or facts? It is simply uwongo, with a capital UWONGO. Butiku hajawahi kuwekwa ndani na Sokoine. I know, because Butiku is my brother in law. Unakuja huku unajaza ----- wa uwongo na kuuita logic halafu unataka watu wenye akili timamu wachangie? Shame on you!
Naomba niweke rekodi vema. Kwanza kabisa Mohamed hayo maneno niliyokazia kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa wewe hufanyi kama unavyomweleza RWEYE1. Nina ushahidi wa kutosha kuhusu wewe kupayuka jambo bila kupima(kumbuka lini tumeanza mnakasha na mara ngapi tumekuwa hapa JF). Kuna ushahidi wa kutosha kuwa unaongea usicho na ujuzi nacho. Sasa hapo jipime mwenyewe kuwa maneno hayo uliyosema yamekulenga au kumlenga Rweye1.
Nikirudi kwa Rweye1, naona ameingia kwa ghadhabu kidogo kama ilivyo kwa mtu mwingine.
Anayedhani kuwa yupo mtimilifu basi na atuambie! Lakini katika aliyoongelea ukiacha yale aliyoghadhabika kuna mambo muhimu kayasema ambayo nilitaraji yatajibiwa kwa hekima zile zile zitokanazo na hoja zake.
Kinyume chake ameshambuliwa, eti kwa kusema yeye ni Mwislam. Mohamed hakuna mtu anayeweza kujinasibu katika imani. Imani ipo kwa mtu na wala si chama cha siasa, mpira au mdumange.
Yeye akisema ni mwislam basi hilo ni baina yake na Mola wake.
Unaposema anajinasibu hapo unahalifu na kupoteza busara.
Kwani wewe ni nani hadi uweze kujua mwislam au mwingine awaye?
Kwani cheti cha uislam kinatolewa wapi na kwa rekodi gani kiasi cha kusema huyo anajinasibu!
Jamani imani ni kitu rahisi ukikielewa na ni kigumu sana ukiimba tu.
Nasema ni kiugumu sana ukiimba kwasababu maoni ya Mohamed ni kuwa Rweye1 alitakiwa amuunge mkono ili akamilike na awe ndugu. Mohamed anasahau kuwa tofauti ya mitazamo ni shemu ya Uislam.
Kama isingekuwa hivyo leo tusingekuwa na Sunni, Shia, Kadiani,Bohora, Ismailia n.k.
Hata katika wale waliotangulia bado kuna mahalifa na masheikh wakubwa waliotofautiana sana kimitazamo.
Ndiyo maana tumekuwa tunasikia kuwa jambo lina utata kutokana na tafsiri na mitazamo.
Mohamed alikataa kutoa kauli juu ya DVD ya Ilunga na kulipeleka suala hilo ''kwa maulamaa''.
Hapa ni wazi kuwa alikuwa na mtizamo tofauti na waislam wengine waliodhani kuwa Ilunga hakufanya jambo zuri.
Juu ya yote na mitizamo yote tofauti bado kila mmoja amebaki kuwa mwislam.
Leo kwanini Rweye1 aonekana kituko eti kwasababu amepingana na Mohamed.
Kinachotisha sana ni Mohamed kutumia maneno ya Mwenyezi kwa namna atakayo.
Hili la Mwislam kumnusuru mwenzake nalo linahitaji kuangaliwa.
Labda naomba msaada kwa Mohamed na vijana wake wanieleze, hivi akitokea Mwislam anamnajisi mwanamke kwa nguvu(kubaka) na mwanake huyo si Mwislam, je huyu mwislam aliyeona hilo anatakiwa amnusuru nani?
Nadhani tatizo la kutaka kumeza tu ni kubwa kuliko linavyoonekana.
Lazima kuwe na mawazo tofauti ili kuleta akhili na fikra zaidi.
Nadhani ndio maana kuna watu wanaamua tu Ijumaa maandamano na bila kufikiri watu wanaunga tela kwasababu kutofautiana na wenye Uislam ni kuukana Uislam.!
Jamani hili nalo linahitaji elimu yoyote zaidi ya akili za kawaida za mwanadamu?
Na mwisho, nawashangaa sana wale wanaosema Mufti Simba hana elimu ya dini. Nakumbuka na nasimama kusahihishwa kuwa wakati wa sheikh Hemed, huyu alikuwa katika kamati ya maulamaa.
Sasa sijui watu wanataka kusema au kuuambia nini ulimwengu kuhusu hili.
Kitu kimoja nilichosoma magazetini ni kuwa mufti Simba alisimamama na kusema Ponda hana elimu ya dini hata kidogo.
Hakuna aiyesimama kuhoji elimu yake wala ku-challenge maneno yake.
Sasa kama Ponda ni kiongozi kwanini mufti anayesemwa hana elimu ya dini awe dhalili licha ya yeye kuthibitisha kuwa Ponda ni mweupe.
Hebu angalieni mnasema nini kwanza, kupayuka au kusema mtu asicho na ujuzi nacho imekatazwa kama alivyosema Mohamed. Naona watu mnasema kila jambo hadi mengi yasiyofaa.
Msioongee hata yale ya chumbani kwenu.
Busara ipo wapi?
Ndio tatizo la kuoga dimbwini na watoto, mwishowe inakuwa vigumu kuwatenganisha kwa nasaba. Mtu akikusimulia jambo la kipuuzi lisilo na chembe ya ukweli na wewe ukalimeza fasta fasta, maana yake ni kwamba unapoteza uwezo wa kupima siyo kwa yake unayoyasikia tu bali yake unayoyanena pia.
Kwa sasa ni vigumu kumtofautisha Mohamed Said na Ritz, gombesugu na Kadogoo, zomba na Zali la Mentali au Barubaru na THE BIG SHOW! Wote wamejitupa dimbwini wakiamini wanaoga na kwamba watatoka humo wametakata! Kipi cha kushangaza hapa...humo hakuna tena cha mzee na mtoto!
zali la Mentali darsa limemkolea kisawasawa kama ilivyowakolea Sheikh Ilunga na Sheikh Ponda, umbea na uchochezi wa mwalimu wao Mohamed Said umewaingia kweli kweli, atasita vipi naye kuzua la kwake? Kwa nini mtoto asione fahari kuchafuka kama humo dimbwini wazee hawabanduki?

Samahani sana Ritz, sikujua kama wote niliowataja ni Waislaam watupu. Huo uwezo wa kumtambua mtu ni dini gani kwa kusoma jina Ritz au Zali la Mentali sinao...hicho labda ni kipaji walichojaaliwa wachochezi kama mwalimu wako wa darsa! Nimeambiwa anacho pia kipaji cha kutambua yupi ni Muislaam wa kweli!Wanajamvi naona kiongozi wa kundi la Wakistu kwenye huu mnakasha Mag3, kawataja Waislam watupu vichwa vya madrassa ni fahari kubwa kwetu kuwekwa kundi moja na Mwalimu wetu Mohamed Said,
Wanajamvi mtajiuliza kwa nini huyu kiongozi hakuwataja Wakirsto wenzake tafakari.
Utakuja na kila kauli bado Mohamed Said atabaki kuwa bingwa wenu kwenye historia ya Tanganyika.
Nilijua tu Nguruvi3 lazima utakuja kuichukua hoja ya huyu bwana Rweye1,,
usipate shida na sisi nguruvi3,na wala usiumie sana kutaka kutusemea,mufti simba na bakwata yake isikughulishe sana,we kama unaona ana ilm kisa alikua katika barza la maulamaa na mufti hemed ibn jumaaa sawa,ila kama mtu ana ilm ya dini kisha anaitumia kwa maslahi ya tumbo lake basi haina maana ya ilm yake,
hakuna ataepoteza uislam wake eti kwa kmpinga Moh Said,ila tunaona ni busara aje apinge kwa hoja kama unakuja ww ili tuchambue na tupimie uzito wa hoja zenyew na sio kupinga tuh kutokana na hisia binafsi,sawa?
Samahani sana Ritz, sikujua kama wote niliowataja ni Waislaam watupu. Huo uwezo wa kumtambua mtu ni dini gani kwa kusoma jina Ritz au Zali la Mentali sinao...hicho labda ni kipaji walichojaaliwa wachochezi kama mwalimu wako wa darsa! Nimeambiwa anacho pia kipaji cha kutambua yupi ni Muislaam wa kweli!
Ndio tatizo la kuoga dimbwini na watoto, mwishowe inakuwa vigumu kuwatenganisha kwa nasaba. Mtu akikusimulia jambo la kipuuzi lisilo na chembe ya ukweli na wewe ukalimeza fasta fasta, maana yake ni kwamba unapoteza uwezo wa kupima siyo kwa yake unayoyasikia tu bali yake unayoyanena pia.
Kwa sasa ni vigumu kumtofautisha Mohamed Said na Ritz, gombesugu na Kadogoo, zomba na Zali la Mentali au Barubaru na THE BIG SHOW! Wote wamejitupa dimbwini wakiamini wanaoga na kwamba watatoka humo wametakata! Kipi cha kushangaza hapa...humo hakuna tena cha mzee na mtoto!
zali la Mentali darsa limemkolea kisawasawa kama ilivyowakolea Sheikh Ilunga na Sheikh Ponda, umbea na uchochezi wa mwalimu wao Mohamed Said umewaingia kweli kweli, atasita vipi naye kuzua la kwake? Kwa nini mtoto asione fahari kuchafuka kama humo dimbwini wazee hawabanduki?
Unajua nini? Ungeanza kusema kuwa ulisikia fununu. Hapa JF ni kisima cha knowledge. Nina hakika angejitokeza mtu kuunga mkono fununu zako au kuziweka sawa. Sasa ngoja nikueleze sasa ninayoyafahamu mimi. Marehemu Sokoine alikuwa na ushahidi kuwa Cleopa Msuya ni mla rushwa. Alipeleka vijana wake kufanya msako nyumbani kwake. Msuya akampigia Mwalimu simu na kumwambia kama ameruhusu asachiwe nyumbani kwake basi kwanza amfukuze kazi kwa sababu itakuwa fedheha kwa waziri kufanyiwa msako nyumbani kwake. Mwalimu akamwambia Sokoine wamwache Msuya. Hakuna mtu aliyewekwa kizuizini aliyekuwa "prominent" katika serikali, as far as I know. Nina hakika kuna wengine waliokuwa karibu zaidi na tukio wakaja na picha kamili.Kama sio Butiku, aliyewekwa ndani katika mazingira haya niliyoyaelezea ni nani? Tujulishe basi kwani tukio hilo lilitokea hilo halina ubishi.
Kapokea na kumeza mazima kama mamba kashindwa hata kuhoji.
Umeishaona wapi kiongozi wa kuwangoza Waislam anachaguliwa na watu 20 tena wamejifungia ukumbini kama mkutano wa kitchen party.
Unajua nini? Ungeanza kusema kuwa ulisikia fununu. Hapa JF ni kisima cha knowledge. Nina hakika angejitokeza mtu kuunga mkono fununu zako au kuziweka sawa. Sasa ngoja nikueleze sasa ninayoyafahamu mimi. Marehemu Sokoine alikuwa na ushahidi kuwa Cleopa Msuya ni mla rushwa. Alipeleka vijana wake kufanya msako nyumbani kwake. Msuya akampigia Mwalimu simu na kumwambia kama ameruhusu asachiwe nyumbani kwake basi kwanza amfukuze kazi kwa sababu itakuwa fedheha kwa waziri kufanyiwa msako nyumbani kwake. Mwalimu akamwambia Sokoine wamwache Msuya. Hakuna mtu aliyewekwa kizuizini aliyekuwa "prominent" katika serikali, as far as I know. Nina hakika kuna wengine waliokuwa karibu zaidi na tukio wakaja na picha kamili.
Ritz,
Msome Zitto Kabwe hapo chini:
TAIFA LINA NYUFA
NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.
Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:
Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias
Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni irresponsible vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.
NDUGU KABWE Z. ZITTO
Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-point fingers kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-expose, tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa Agent Provacateur, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni very irresponsible tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia grievances zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu honest discussions miongoni mwetu kama wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki hate speeches. Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na hate speeches nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.