Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Vipo visa na mikasa mingi ya uhuru mingine ya kuchekesha na mingine ya kuliza khasa
mtu akatokwa na machozi.

Kweli huyo mzee naye alikuwa na matatizo. Hivi leo ukikutana na mtu ambaye una uhakika mnafahamiana au mmewahi kukutana baada ya miaka mingi akakuuliza "nikumbushe aisee tulikutana wapi" wewe na kisirani chako unasema 'hatujawahi kukutana" huku ukijua mmewahi kukutana!

Ukisoma simulizi lako hili unaweza kuona baadhi ya wazee wako walivyokuwa na kinyongo kisicho na sababu. Nyerere angekuwa hataki kumkumbuka asingemuuliza!!! Na mzee huyo kwa kuamua kusema uongo kwa sababu kazira inasikitisha. NI mfano mbaya kwa marafiki. Miye kuna watu sijawaona kwa miaka naweza hata kuwa nimewasahau kwa majina na wengine siwezi kukumbuka tulikutana wapi lakini nikikutana nao wala sioni haya kuwauliza na wakiwa waungwana watanikumbusha.

Mifano mingine ni aibu tu kwa hao wazee.
 

And you call this logic? Or facts? It is simply uwongo, with a capital UWONGO. Butiku hajawahi kuwekwa ndani na Sokoine. I know, because Butiku is my brother in law. Unakuja huku unajaza ----- wa uwongo na kuuita logic halafu unataka watu wenye akili timamu wachangie? Shame on you!
 
Naomba niweke rekodi vema. Kwanza kabisa Mohamed hayo maneno niliyokazia kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa wewe hufanyi kama unavyomweleza RWEYE1. Nina ushahidi wa kutosha kuhusu wewe kupayuka jambo bila kupima(kumbuka lini tumeanza mnakasha na mara ngapi tumekuwa hapa JF). Kuna ushahidi wa kutosha kuwa unaongea usicho na ujuzi nacho. Sasa hapo jipime mwenyewe kuwa maneno hayo uliyosema yamekulenga au kumlenga Rweye1.

Nikirudi kwa Rweye1, naona ameingia kwa ghadhabu kidogo kama ilivyo kwa mtu mwingine.
Anayedhani kuwa yupo mtimilifu basi na atuambie! Lakini katika aliyoongelea ukiacha yale aliyoghadhabika kuna mambo muhimu kayasema ambayo nilitaraji yatajibiwa kwa hekima zile zile zitokanazo na hoja zake.

Kinyume chake ameshambuliwa, eti kwa kusema yeye ni Mwislam. Mohamed hakuna mtu anayeweza kujinasibu katika imani. Imani ipo kwa mtu na wala si chama cha siasa, mpira au mdumange.
Yeye akisema ni mwislam basi hilo ni baina yake na Mola wake.
Unaposema anajinasibu hapo unahalifu na kupoteza busara.

Kwani wewe ni nani hadi uweze kujua mwislam au mwingine awaye?
Kwani cheti cha uislam kinatolewa wapi na kwa rekodi gani kiasi cha kusema huyo anajinasibu!
Jamani imani ni kitu rahisi ukikielewa na ni kigumu sana ukiimba tu.

Nasema ni kiugumu sana ukiimba kwasababu maoni ya Mohamed ni kuwa Rweye1 alitakiwa amuunge mkono ili akamilike na awe ndugu. Mohamed anasahau kuwa tofauti ya mitazamo ni shemu ya Uislam.
Kama isingekuwa hivyo leo tusingekuwa na Sunni, Shia, Kadiani,Bohora, Ismailia n.k.

Hata katika wale waliotangulia bado kuna mahalifa na masheikh wakubwa waliotofautiana sana kimitazamo.
Ndiyo maana tumekuwa tunasikia kuwa jambo lina utata kutokana na tafsiri na mitazamo.

Mohamed alikataa kutoa kauli juu ya DVD ya Ilunga na kulipeleka suala hilo ''kwa maulamaa''.
Hapa ni wazi kuwa alikuwa na mtizamo tofauti na waislam wengine waliodhani kuwa Ilunga hakufanya jambo zuri.

Juu ya yote na mitizamo yote tofauti bado kila mmoja amebaki kuwa mwislam.
Leo kwanini Rweye1 aonekana kituko eti kwasababu amepingana na Mohamed.

Kinachotisha sana ni Mohamed kutumia maneno ya Mwenyezi kwa namna atakayo.
Hili la Mwislam kumnusuru mwenzake nalo linahitaji kuangaliwa.

Labda naomba msaada kwa Mohamed na vijana wake wanieleze, hivi akitokea Mwislam anamnajisi mwanamke kwa nguvu(kubaka) na mwanake huyo si Mwislam, je huyu mwislam aliyeona hilo anatakiwa amnusuru nani?

Nadhani tatizo la kutaka kumeza tu ni kubwa kuliko linavyoonekana.
Lazima kuwe na mawazo tofauti ili kuleta akhili na fikra zaidi.

Nadhani ndio maana kuna watu wanaamua tu Ijumaa maandamano na bila kufikiri watu wanaunga tela kwasababu kutofautiana na wenye Uislam ni kuukana Uislam.!
Jamani hili nalo linahitaji elimu yoyote zaidi ya akili za kawaida za mwanadamu?

Na mwisho, nawashangaa sana wale wanaosema Mufti Simba hana elimu ya dini. Nakumbuka na nasimama kusahihishwa kuwa wakati wa sheikh Hemed, huyu alikuwa katika kamati ya maulamaa.
Sasa sijui watu wanataka kusema au kuuambia nini ulimwengu kuhusu hili.

Kitu kimoja nilichosoma magazetini ni kuwa mufti Simba alisimamama na kusema Ponda hana elimu ya dini hata kidogo.
Hakuna aiyesimama kuhoji elimu yake wala ku-challenge maneno yake.

Sasa kama Ponda ni kiongozi kwanini mufti anayesemwa hana elimu ya dini awe dhalili licha ya yeye kuthibitisha kuwa Ponda ni mweupe.

Hebu angalieni mnasema nini kwanza, kupayuka au kusema mtu asicho na ujuzi nacho imekatazwa kama alivyosema Mohamed. Naona watu mnasema kila jambo hadi mengi yasiyofaa.
Msioongee hata yale ya chumbani kwenu.

Busara ipo wapi?
 

Kama sio Butiku, aliyewekwa ndani katika mazingira haya niliyoyaelezea ni nani? Tujulishe basi kwani tukio hilo lilitokea hilo halina ubishi.
 
Jana nimebahatika kuisikiliza vyema taarifa fupi (KUNTU) iliyotolewa na mlezi wetu mkuu wa kiroho KARDINALI) ya kuujulisha umma ni nini kilichotokea kupitia chombo chake cha habari TUMAINI. Tunashukuru kwa taarifa yake hiyo ambayo kwa jinsi ilivyotolewa, nina hakika ilifanyiwa kazi ya kina kabla ya kuletwa hadharani.

Kwanza kabisa nashawishika kwa ukurasa wa awali kukubaliana na taarifa yake hiyo kutokana na imani yangu kuu kwake, na inavyojulikana kwa wachache kuwa kada ya UPAPA na UKARDINALI ni kada ambazo wanaozifikia pia wamepitia mambo ya kiintelijensia!

Tunashawishika kuamini hivyo kutokana na jinsi kiongozi huyu wa kiroho ambavyo ameweza kutoa ripoti yake ya kiintrijensia ndani ya chini ya masaa 24! Amesema suala hili lisihusishwe kwa aina yoyote ile na dini au itikadi ya uislamu bali waliofanya kitendo hicho ni WAKRISTO tena wa KANISANI hapo! Na kwa msisitizo akasema kuwa anao uhakika wa kile anachokisema!

Sasa inamaana kwa uweza wa kimungu ambao mtumishi huyu anao na ule wa uintelijensia alionao ameweza kuwasaidia hata polisi wetu kumaliza kazi ya upelelezi katika muda mfupi sana! Sasa kuna haja gani ya kuleta tena CIA? Na kama amesisitiza kuwa taarifa yake aliyoitoa ndiyo ya mwisho, kuna haja gani ya kuwashikilia hao watu wengine, si yeye apelike hiyo ripoti yake polisi ili kazi iwe fupi na amani irejee mioyoni mwa watu na kukata vilimilimi vya watu wengine ambao wanataka kupata umaarufu kupitia SAGA hilo?!

Lakini tukija katika upande wa pili, Je, hatuoni kuwa mtumishi wetu huyu amewahi saaaaaaaaaaaaaaana kutoa ripoti yake hiyo ambayo inaonekana kama hitimisho la SAGA lenyewe?!

Na, Je, kama itatokea ikaja kuapatikina ripoti nyingine tofauti na hii tuliyoaminishwa na mtumishi wa mungu, Je, tutamwamini nani?

Maswali yapo mengi sana kuliko yale ya papo kwa papo ya Waziri mkuu, lakini katika hili nafikiri TAFAKARI ya kina ilitakiwa ichukuliwe kabla ya taarifa hii kutolewa.

Mliokuwa mnahamu ya kunywa damu ya Waislamu kwenye hili jambo mnasemaje kuhusu kauli hii ya Pengo? Kwa nini Pengo anaingilia kazi za mahakama na kutoa hukumu kabla hata mahakama haijamaliza kazi yake? Kwa nini aseme kwamba ushahidi aliyopewa yeye anauamini na kwamba hakuna kitu kitakachobadilisha uelewa wake wa suala hilo zaidi ya ushahidi aliopewa na watu wake? Kama anajua kila kitu kwenye ugaidi huu, kwa nini asifunguke na kuelezea wazi magaidi ni kina nani?

Kiu ya kunywa damu za watu wasio na hatia inawasumbua mpaka mnaanza kunywa damu zenu wenyewe kwa wenyewe makanisani. Magaidi wakubwa nyinyi. Hamfai kabisa kukabidhiwa dhamana kwenye jamii.

YERICKO ongezea hiki kipande cha ugaidi kwenye kitabu chako kabla hujakifungua rasmi.
 


Nilijua tu Nguruvi3 lazima utakuja kuichukua hoja ya huyu bwana Rweye1,,
usipate shida na sisi nguruvi3,na wala usiumie sana kutaka kutusemea,mufti simba na bakwata yake isikughulishe sana,we kama unaona ana ilm kisa alikua katika barza la maulamaa na mufti hemed ibn jumaaa sawa,ila kama mtu ana ilm ya dini kisha anaitumia kwa maslahi ya tumbo lake basi haina maana ya ilm yake,

hakuna ataepoteza uislam wake eti kwa kmpinga Moh Said,ila tunaona ni busara aje apinge kwa hoja kama unakuja ww ili tuchambue na tupimie uzito wa hoja zenyew na sio kupinga tuh kutokana na hisia binafsi,sawa?
 
Ndio tatizo la kuoga dimbwini na watoto, mwishowe inakuwa vigumu kuwatenganisha kwa nasaba. Mtu akikusimulia jambo la kipuuzi lisilo na chembe ya ukweli na wewe ukalimeza fasta fasta, maana yake ni kwamba unapoteza uwezo wa kupima siyo kwa yake unayoyasikia tu bali yake unayoyanena pia.

Kwa sasa ni vigumu kumtofautisha Mohamed Said na Ritz, gombesugu na Kadogoo, zomba na Zali la Mentali au Barubaru na THE BIG SHOW! Wote wamejitupa dimbwini wakiamini wanaoga na kwamba watatoka humo wametakata! Kipi cha kushangaza hapa...humo hakuna tena cha mzee na mtoto!

zali la Mentali darsa limemkolea kisawasawa kama ilivyowakolea Sheikh Ilunga na Sheikh Ponda, umbea na uchochezi wa mwalimu wao Mohamed Said umewaingia kweli kweli, atasita vipi naye kuzua la kwake? Kwa nini mtoto asione fahari kuchafuka kama humo dimbwini wazee hawabanduki?
 

Nguruvi3,

Umemsikia Kadinal Pengo na sakata la bomu Arusha.

Wewe ulisema Mohamed Said anahusika na matukio ya Zanzibar na Arusha.

Busara yako ipo wapi?
 
Last edited by a moderator:

Mimi nimeelezea hilo tukio na nimetaja Butiku na nikaelezea mazingira yaliyovyokuwa kwenye sakata lile kadri nilivyoweza kuyakumbuka kwa kuelezea ukweli kwamba aliyemtia ndani alikuwa Sokoine na majibu ya Nyerere yalikuwa vipi katika kuutetea uhujumu uchumi ule.

Sasa mtoto mdogo ni wewe ambaye baada tu ya kusikia Jasusi kasema nini unaingia kichwa kichwa na kutoa hukumu yako ya kijinga isiyokuwa na ushahidi wowote wa kunihukumu mimi kwa niliyoyasema.

Nilikuuliza maswali mengi wakati najibu hoja zako moja baada ya nyingine. Ukaingia mitini. Baada ya kujibu maswali uliyoulizwa ndio uingie kwenye mjadala mwingine unakimbilia kwenye mjadala mwingine tena mikono mitupu bila hata hoja ya msingi. Sasa kama huu sio utoto ni nini? Acha utoto.
 

Wanajamvi naona kiongozi wa kundi la Wakistu kwenye huu mnakasha Mag3, kawataja Waislam watupu vichwa vya madrassa ni fahari kubwa kwetu kuwekwa kundi moja na Mwalimu wetu Mohamed Said,

Wanajamvi mtajiuliza kwa nini huyu kiongozi hakuwataja Wakirsto wenzake tafakari.

Utakuja na kila kauli bado Mohamed Said atabaki kuwa bingwa wenu kwenye historia ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Samahani sana Ritz, sikujua kama wote niliowataja ni Waislaam watupu. Huo uwezo wa kumtambua mtu ni dini gani kwa kusoma jina Ritz au Zali la Mentali sinao...hicho labda ni kipaji walichojaaliwa wachochezi kama mwalimu wako wa darsa! Nimeambiwa anacho pia kipaji cha kutambua yupi ni Muislaam wa kweli!
 

Kapokea na kumeza mazima kama mamba kashindwa hata kuhoji.

Umeishaona wapi kiongozi wa kuwangoza Waislam anachaguliwa na watu 20 tena wamejifungia ukumbini kama mkutano wa kitchen party.
 

The beareved begins the wailing latter others join...ha haa haaa ha.

Cc.. gombesugu,
 
Last edited by a moderator:


Wewe mimi nishakuwia radhi tokea mda mrefu sana,kila mtu humu ana list yake nadhani,
katika list ya watu vihiyo mimi ninayo wawili tuh,
wa kwanza ni wewe Mag3,na wa pili ni yule msukuma mkokoteni,,
Matusi yako mimi sina aleg nayo,nazid kukupuuza tuh,pole sana...
 
Kama sio Butiku, aliyewekwa ndani katika mazingira haya niliyoyaelezea ni nani? Tujulishe basi kwani tukio hilo lilitokea hilo halina ubishi.
Unajua nini? Ungeanza kusema kuwa ulisikia fununu. Hapa JF ni kisima cha knowledge. Nina hakika angejitokeza mtu kuunga mkono fununu zako au kuziweka sawa. Sasa ngoja nikueleze sasa ninayoyafahamu mimi. Marehemu Sokoine alikuwa na ushahidi kuwa Cleopa Msuya ni mla rushwa. Alipeleka vijana wake kufanya msako nyumbani kwake. Msuya akampigia Mwalimu simu na kumwambia kama ameruhusu asachiwe nyumbani kwake basi kwanza amfukuze kazi kwa sababu itakuwa fedheha kwa waziri kufanyiwa msako nyumbani kwake. Mwalimu akamwambia Sokoine wamwache Msuya. Hakuna mtu aliyewekwa kizuizini aliyekuwa "prominent" katika serikali, as far as I know. Nina hakika kuna wengine waliokuwa karibu zaidi na tukio wakaja na picha kamili.
 
Kapokea na kumeza mazima kama mamba kashindwa hata kuhoji.

Umeishaona wapi kiongozi wa kuwangoza Waislam anachaguliwa na watu 20 tena wamejifungia ukumbini kama mkutano wa kitchen party.

Ritz,
Msome Zitto Kabwe hapo chini:
TAIFA LINA NYUFA

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:

“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias”

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki “hate speeches”. Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

 
Moh Said,
Ndug Zitto kamaliza kila kitu,ametumia lugha yenye kueleweka sana,
Huo ndio ukweli tunaousema...
 

Sikusikia fununu. Nilisikia mwenyewe na maneno ya Nyerere kumtetea Butiku niliyasikia mwenyewe. Bado nina kumbukumbu ya tukio hilo. Watakaoweza kulikumbuka tukio hilo watachangia.
 

Mohamed Said,

Nimemsoma Zitto Kabwe hakihotubia bunge kaongea maneno mazito sana utadhani naye anafyonza Ilm kwenye huu Mnakasha.

Humu jamvini watu wanataka kuwapangia Waislam waongozwe na Bakwata ambayo ni chombo cha serikali.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…