Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Naomba niulize swali dogo tu. Kama Bakwata ni chombo cha serikali, na waislamu wengi hawakitambui, inakuwaje waislamu hao hao wanataka serikali hiyo hiyo iwaanzishie mahakama ya kadhi? Ni swali dogo tu.

Jasusi,

Waislamu wanataka mahakama ya kadhi lakini hawaitaki Bakwata. Sasa hapo ni kipi kinachokuchanganya ndugu yangu?
 
Naomba niulize swali dogo tu. Kama Bakwata ni chombo cha serikali, na waislamu wengi hawakitambui, inakuwaje waislamu hao hao wanataka serikali hiyo hiyo iwaanzishie mahakama ya kadhi? Ni swali dogo tu.


Madai yetu sisi si kuitaka serikali ituanzishie mahakama ya Kadhi,mahakama ya kadhi na vitu vingine vingi tunaweza kuvianzisha sisi wenyewe na kuvisimamia,tunachopinga ni wao serikali tena mambo haya aliyapandikiza nyerere,hatutaki kutupangia mambo yetu kwa kupitia chombo chenu cha bakwata,kama vile wasivyowaingilia nyinyi kwenye mambo yenu basi nasisi wasituingilie hivyo hivyo...
 
Hakika elmu niliopata madras ni kubwa sana na imenisaidia sana kutambua hawa wasomi wa kigal******tia wanavyo shindwa ktkt mnakasha huu

Mungu awajaalie wajue njia ya haki

Hargeisa,

Salaam. Wallahi,nafurahi kufahamiana na kutambuana hapa jamvini.

Hilo jina utumialo lanikumbusha safari yangu miaka michache ilopita pale Hargeisa.

Napenda bayana zako ni kiduchu mno,lakini nasaha zako ni mwanana na hunikurubishia vicheko kila nikusomapo.

Ahsanta.
 

Mag3,

Nilishawahi kukupa tahadhari hapo awali ya kutumia lugha inayoshabihiana na umri wako. Lakini naona husikii asilan.
Kwanini usikae kitako na kubwia tumbaku huku ukimalizia pension yako kama wafanyavyo watu wazima wenzio wa kikwenu!?

Huyo alotumbukia dimbwini ni nani!? Wewe unajua nini maana ya dimbwi!? Na ukiliona dimbwi talijua!?

Nyinyi hamuwezi asilan kuona tafauti baina yetu na nilishawahi kutamka hapo awali. Kwa sababu kwa akili zako chechefu na psychology yako dhaifu, ni vigumu kuona tafauti yetu sisi. Sababu ila,dasturi na matendo yetu kwa machoni mwako tumeshabihi kama vile uwatazamapo ma-Chinese!?

Sisi ni walamba boots za Sheikh Mohammed Said,hatujui kusoma wala kuandika,tunashinda vibarazani Kariakoo kufanza majungu na mipasho,chakula chetu kikuu ni kashata na kahawa chungu,akili zetu ni za Madrassa...sasa yanini tukushughulishe wewe Mkristo mtiifu,msomi na muungwana!? Pilipili ishamba,wewe yakuwashiani!?

Taadabu nafsi yako isojua ila wala fadhila. Acha au jaribu kupunguza chuki zako binafsi kwa Sheikh Mohammed.

Wewe kama ni mtu mzima wa kikweli,yatakiwa urekebishe kashfa,fedhuli,tashtit,nakma,zilzala,kizazaa na rabsha nyinginezo nyingi hapa jamvini lakini sio ndo uwe kinara wa makhanatha.

Halafu ndo wewe ati unajinasibu umetoka kwenye family zenye maadili,na kwamba ati unatafuta amani na suluhu baina ya wa-Tanzania!? Nakuona saana kila uwekapo zile "LIKE" zako kila mara watukanapwo na kudharauliwa Waislam na Uislam.

Usinifanze nikaacha shughuli zangu,kulumbana nawe.

Natumai utajaribu kujihishimu.

Ahsanta.
 

The Big Show,

Salaam Al Akhiy. Niwie radhi,sikujua yakuwa nawewe ndo ulikua njiani pia kumnyooshea maneno huyo "Muislam".

Ahsanta.
 

Kwanza ondoa ile PAROKIA pamoja na safu ya nzima ya wakristo ambao wamewekwa pale NECTA kwa lengo moja tu kuhakikisha wanawafelisha vijana wa kiislam, ukifanya hivyo ndo utajua weledi wa watoto wa kiislam
 


Huyo ni mpuuzi tuh,kama inawezekana nawewe mwingize kwenye list yako...
Asitupotezee muda wetu hapa...
 
The Big Show,

Salaam Al Akhiy. Niwie radhi,sikujua yakuwa nawewe ndo ulikua njiani pia kumnyooshea maneno huyo "Muislam".

Ahsanta.


Naam,
Waleykhum salaam,huyo kanjanja sijui katokea wapi,na anajinasibu na uislam huku akishindwa kujua changamoto kuu zinazowakabili waislam ndann ya nchi hii,wa ajabu sana,kweli tutashuhudia mengi kwenye mjadala huu...
Me naona Yericko angeufunga tuh kwani sasa naona joto ya jiwe imekuwa kubwa hadi anakuja kushutumiwa kuwa mwanzilishi wa mjadala huu ni Moh Said,hana analoliongea la maana,haeleweki hoja yake ipo wapi,yeye anasimama hapa na kudhani sisi tupo hapa kujenga na kushabikia chuki na farki baina yetu na ndugu zetu wa upande wa pili,kwa maana hiyo basi hata hao kina Invisible walioamua kuupa heshima mjadala huu yeye anawaona wapuuzi hivi nadhani,ni mtu wa sampuli ya ajabu sana,,tena sana...
 
Last edited by a moderator:
Naomba niulize swali dogo tu. Kama Bakwata ni chombo cha serikali, na waislamu wengi hawakitambui, inakuwaje waislamu hao hao wanataka serikali hiyo hiyo iwaanzishie mahakama ya kadhi? Ni swali dogo tu.

waarabu wana usemi the right question is usual better than the right answer for a wrong question.

labda na mimi nikuulize kutokana na ufahamu wako. Je mahakama ya Kadhi inahusiana nini na suala la Bakwata?

 

The Big Show,

Haya yote yaliwezekana kwa kuwa wazee wetu walipogeukiwa na kusalitiwa walikaa kimya
na mmoja mmoja wakafa na wakaingia kaburini na historia zao.

Sisi tumethubutu kufungua vinywa vetu na kusema ukweli.
Ndiyo haya unayoyaona hapa JF hivi sasa.

Kila tulisemalo kwao ni kitu cha ajabu.

Kuna kioja na ajabu kama kuandika historia ya TANU ukamuacha Mshume Kiyate?
Wanataka waandike historia ya TANU kwa kuwaruka wana TANU.

Itawezekana wapi?
Twendenao taratibu In Sha Allah.
 

Wimana,

Nashukuru ndugu yangu kwa bayana yako hii na hishma ulonipa. Najua Shariff Ritz,alishakupa jibu japo kiduchu(lakini lazim niseme ukweli lile jibu la Ritz kwako,limenivunja mbavu mno!).

Inanilazim nikueleze kiduchu kwa hishma unipayo mara kadhaa hapa jamvini,na kama fikra zangu zipo sahihi naamini hujawahi kunitusi katika majadiliano yetu kiduchu tulowahi kufanza mimi nawe.

Pole pia kwa masikitiko na hiyo huruma ilokupata dhidi ya hoja yangu dhaifu. Haina neno ndo kilimwengu kila mwana-Adam ana udhaifu wake wala hakuna alokamilika baina yetu.

Hiyo kwangu haikua hoja asilan,ilikua ni marembesho ya khadithi zetu za vibarazani baina yangu na Sheikh Mohammed. Kama umeshabaini,mara nyingi kuna Wazee wetu ndo huwa tunakumbushana. Labda ndo kwa bakhti mbaya nikatia ile issue ilokusibu.

Hizo habari za "Uhujumu wa Uchumi",nami pia nazijua kwa kina na vitimbi/vituko vyake takriban vyoote. Na yule baniani J.W.Ladwa nae namjua vizuri mno na mpaka kwake nikifika. Kama uliangalia ile post yangu kwa makini, kuhusu J.W.Ladwa;hapana sikumlaumu Nyerere tu peke yake. Nilitaja yakuwa huyo jamaa vitimbi na vurugu zake bado zipo na zinaendelea mpaka kesho. Hapo nilimaanisha yakuwa awamu zoote za "Viongozi" hazijamshughulikia kwa kina!?

Natumai majibu yangu japo kiduchu yatakuridhisha ndugu yangu. Nachelea tusiweke malumbano yaso tija hapa jamvini.

Ahsanta kwa kunisikiza na kunikubalia huo uchechefu wangu.
 
Swadakta bw. Sideeq!
Sasa kama hayo maneno ndivyo yalivyo kwanini Wickama na Rweye1 wanapomzuia Mohamed asidhulum waonekane kuwa waovu?

Nadhani unajua jinsi gani Mohamed anadhulumu vijana na watu waliokuwa hawafahamu baadhi ya mambo.
Miaka 15 andhulum watu huoni hilo ni tatizo na ni wakati sasa waislam wamsaidie ndugu asidhulum zaidi
Amedhulum upotoshaji,amedhulumu Kusengenya, kusema uongo na hata kusafiri nchi za mbali akiwa amekumbatia mikoba.
Hataki kuacha dhulma Abdan.

Sasa watu wakimzuia asitende hayo yeye anawakashf ikiwa tena ni dhulma nyingine.
Hebu isadie jamii yako kwa kusimama na maneno haya na ukweli maana Mohamed undugu anaosema ni ule wa kukubali hii tamthlia ambayo imepoindwa pondwa na sasa imebaki kuwa simulizi tamu baina ya isha na Maghribi.

Wickama na Rweye1, msijisikie wanyonge wala kupata fadhaa, kumbe kazi mnayofanya ya kuzuia dhulma ipo katika Sahhih al Bukhar.
Basi mtayakuta mafungu yenu mema mbele kwa kusema na kuzuia dhulma.

Leo nimekumbuka wali wa nazi na tui zito kwenye mharagwe.
Bonde kwema karibuni muoe.
 
Nguruvi3,

Ndugu yangu hayo maneno yako ulikuwa unamlenga nani kama siyo Mohamed Said.

Hakuna tatizo kama unayakana maneno yako.

Tuendelee na mnakasha tusemezane...

Ritz,

Salaam Al Akhiy.

Wallahi nina shauku na hamu iso kifani yakuona Muheshimiwa Nguruvi3,hapo atakuja kujibu kivipi au kutoa excuse ipi!? Maana yeye ni "Vunja Mifupa" bingwa wa PR!ahaha!!

Najua lolote atakalosema kujibu "mpini" huu ulomnasa nao,basi Wallahi nitavunjika mbavu kwa kucheka...maana siku hizi naanza kumjua taratibu!ahaha!!

Navuta sabra kiduchu maana itakua kazongwa na mishughuliko labda!?

Ahsanta.
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Mimi suali langu kwako ni kiduchu na wala sitagusia asilan hiyo "Fatwa" yako ulotoa.

Hivi ni kwanini wanapoingia watu wapya hapa jamvini,na wakiyakinisha kuwa hawakubaliani na hoja za Sheikh Mohammed Said na wanampinga vikali na khasa pale wasemapo yakuwa ati wao pia ni "Waislamu"; mbona nyinyi nyoote huwa hamleti zile shutuma na tashtit ya kumshuku huyo mtu/mwanajamvi mpya kwa multiple IDs!?

Hayo mambo mlinifanzia mimi takriban wiki nzima wakti najiunga hapa jamvini/JF,na hata Zali la Mentali nae pia yalimsibu!?

Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu.

Ahsanta.
 
Ritz, gombesugu, Mohamed Said, Zali la Mentali,....

Hakuna tatizo la ELIMU kwenye mila, desturi na tamaduni za Kiislam? Nimeona juzi kwenye Tv kule Tunduru wazee wengi wa Kiislam( kama majina ni utambulisho tosha) wamefikishwa mahakamani kwa kuwatoa watoto shule hasa za sekondari.
 
Last edited by a moderator:
waarabu wana usemi the right question is usual better than the right answer for a wrong question.

labda na mimi nikuulize kutokana na ufahamu wako. Je mahakama ya Kadhi inahusiana nini na suala la Bakwata?

Barubaru,
Baada ya kumsoma Zitto inaonekana kuna consesus miongoni mwa waislamu kuwa serikali ilifanya makosa kuanzisha Bakwata kama kweli Bakwata ilianzishwa na serikali. That being the case, kitu rahisi ni kuvunjwa kwa Bakwata na kuwaachia waislamu wajiendeshee mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na serikali ikiwa pamoja na mahakama ya kadhi. Au kuna kitu ninachokikosa hapa?
 

The Big Show,

Haya yote yaliwezekana kwa kuwa wazee wetu walipogeukiwa na kusalitiwa walikaa kimya
na mmoja mmoja wakafa na wakaingia kaburini na historia zao.

Sisi tumethubutu kufungua vinywa vetu na kusema ukweli.
Ndiyo haya unayoyaona hapa JF hivi sasa.

Kila tulisemalo kwao ni kitu cha ajabu.

Kuna kioja na ajabu kama kuandika historia ya TANU ukamuacha Mshume Kiyate?
Wanataka waandike historia ya TANU kwa kuwaruka wana TANU.

Itawezekana wapi?
Twendenao taratibu In Sha Allah.
 

Wild Card,
Hilo linaelezeka bila hofu yoyote.

Hukusikia wanasema hawana fedha za kulipa ada?

Iweje hali iwe hivyo?
Hujajiuliza hilo?
 
Kaka Jasusi

Taasisi na asasi zote NCHI hii zinaanzishwa kwa idhini na baraka za serikali. Ndivyo ilivyoanza BAKWATA enzi hizo wakati kulikuwa shughuli pevu na ngumu sana kuliweka TAIFA pamoja. Hata kama akina Mzee Mohamed watataka EAMWS irudi, itabidi serikali iridhie. Wanashindwa nini hadi sasa mimi sielewi.

Wala akina Mzee Mohamed wasije wakadhani wanaweza kuanzisha chombo kimoja kikawaunganisha WAISLAM wote. Tunawafahamu ndugu zetu hawa. Wasitudanganye ndugu zetu hawa. Hili tu la kutaka kuiondoa BAKWATA ni shughuli nzito.
 
Wild Card,
Hilo linaelezeka bila hofu yoyote.

Hukusikia wanasema hawana fedha za kulipa ada?

Iweje hali iwe hivyo?
Hujajiuliza hilo?

Mzee Mohamed,
Wazee haohao walipigwa faini ya laki moja au kwenda jela miezi sita wakalipa faini ile! Faini ile ni kubwa kuliko karo ya shule za kutwa kwa mwaka. Lipo tatizo Mzee Mohamed. Tatizo hili lipo pia kwa baadhi ya makabila nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…