Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ndugu yangu shida yote hii inakupata kwa kisa gani?

Nishakueleza mara chungu nzima.
Ikiwa unahisi historia hii niliyoandika sisemi kweli...

Siwezi kugombana na wewe kwa hilo.

Usiamini.

Mimi siko hapa kupata ushindi.

Niko hapa kueleza habari za wazee wangu na mchango wao
katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kuna watu hawakupata hata siku moja kusikia habari za Idd
Faiz wala Idd Tosiri wala vipi Nyerere alikwenda UNO.

Hawa ndiyo nawalenga humu.
Tuna watu 10,000+ wanasikiliza.

Hawa ndiyo watu muhimu sana kwangu.
 

Mohamed,
Unayosema ni kweli. History is never complete. Juzi nimesoma kitabu cha American history profesa mmoja anaelezea mchango wa kundi moja Massachussetts waliomsaidia General Washington katika harakazi za uhuru wa Marekani. Sijawahi kulisikia kundi hilo hapo awali, na historia ya Marekani ni ya miaka zaidi ya mia mbili. Kwa hiyo kwa nchi yetu na usomi wetu sishangai kabisa. Tunahitaji kitabu "A Comprehensive History of Modern Tanganyika" ambamo mchango wa wote hao uliowataja na wengine wengi akina Austin Shaba kule kusini, kwa mfano itajumuishwa na kutambulishwa.
 
Kama watu wanatukana vipi unihusishe mimi?

Mohamed,
Hupendi matusi, na hukai kimya ukisikia mtu anatukana hapa ukumbini. Sasa iweje kwenye mnakasha wako unawasikia wakimjeli Nyerere wewe ukae kimya? Hii ya Nyerere kufundishwa kuvaa suruali na wazee wako ni tusi, if you ask me.
 
Ndugu yangu Mohamed Said, nakuuliza swali wewe unaweka hadithi za alfu lela ulela?

Ulichojibu mbona hakiendani kabisa na swali nililokuuliza ndugu,

Hivi ukikiri kuwa kunamakosa katika uandishi na uelewa wako nini utapungukiwa?

Hizo unazoita Alf Lela...
Na hao niliowataja katika Alf Lela...

Ndiyo waliomfikisha Nyerere pale alipofika.
Hata baba yako juu ya yote alikaa kimya tu kuhusu watu hawa

Hakuita michango yao Alf Lela...

Chunga ulimi wako
Wajukuu wa hawa watu wengine wanafuatilia mnakasha huu...

Angalie wasije kukuoneni nyie ni wezi wa fadhila...
 
Mohamed,
Hupendi matusi, na hukai kimya ukisikia mtu anatukana hapa ukumbini. Sasa iweje kwenye mnakasha wako unawasikia wakimjeli Nyerere wewe ukae kimya? Hii ya Nyerere kufundishwa kuvaa suruali na wazee wako ni tusi, if you ask me.

Kaka Mkubwa Jasusi,
Jamaaa nachokiongea na watu anaojidai kuwatetea na imani anayodai kuitetea jitahidi kuifuatilia vizuri asili yake ni ngumu lkn ukijatahidi kwa kiasi fulani utaelewa...
Historia...inawaonyesha kama watu mabingwa wa kuchanganya uongo na ukweli na kuuamini na kuuita ukweli......pia hujitahidi sana kupindua kwa njia zilezile (uongo na ukweli) kubadili hata hadhi za watu ambao historia inawatambua kuwa walikuwa hivi wenyewe huwaita wako vile....
Ningekupa mfano...lkn mods wana ni piga ban kwa kuniita mdini!
Lkn ukweli hauta badilika......hii ndiyo tabia yao, wako hivyo kwakuwa wamefundishwa hivyo, na kiongozi wao alikuwa hivyo.....!! wanasumbua sana vichwa lkn walitabiliwa kuwa watakuja...na kazi yao ndio hiihii...watawapata wafuasi wengi tu kwakuwa kuna nguvu fulani kubwa tu inawasaidia pia ambayo pia kazi yake ni ile ile kupindua ukweli kuwa uongo uongo kuwa ukweli kwa kuingiza ukweli katika uongo!!!!

...
 

Mbona unapanga maswali ya kuulizwa Mkuu wangu?
 
Sipangi maswali.
Najaribu kuchokoza fikra ili mnakasha unawiri.

Labda nawe nikuulize ulipata kuwasikia hawa ndugu
wawili?

Idd Tosiri na Idd Faiz Mafongo?
Au Idd Tulio?

Baada ya ule ugomvi wa Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere
mwaka 1958 Sheikh Takadir alitoswa yaani alifukuzwa TANU na
nafasi yake ya uenyekiti wa Baraza la Wazee ukamwangukia Idd
Tulio.

Huyu Idd Tulio alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnatougo
Hall.

Nyerere alipokuja kulivunja Baraza la Wazee wa TANU 1963 Idd Tulio
ndiye alikuwa mwenyekiti.

Na baraza lilivunjwa katika mkutano uliofanyika Arnautoglo Hall.

Nilitaka nihangaishe mawazo yako.

Hawa ndiyo wazee wangu.
 
Wanajamvi, kumbukeni kuwa huu ulikuwa mkutano mkuu wa TAA April 1946. Ni matarajio kuwa mkutano mkuu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka makao makuu. Kama nimeelewa vema mkutano mkuu ulihudhuriwa na Kasella, Dossa na Phombeah. Sasa soma hii tena
Mohamed:In 1946 while at Tabora, Mwapachuwas elected African AssociationSecretary with Julius Nyerere as his deputy. This was the time when theMakerere intellectuals [1] had started to show interest in theAssociation
Kumbe basi Nyerere alishaanza siasa akiwa katibu wa AA Tawi la Tabora. Kwa vile alikuwa katibu wa tawi muhimu namna hiyo vipi baadaye TAA makao makuu wasiwe wamesikia habari zake? Hapa Mohamed anakiri kuwa wanafunzi wa Makerere akiwemo Mwapachu na Nyerere tayari walikuwa katika msisimko wa kisiasa. Anaendelea
Mohamed:Abdulwahid, on the other hand, was a person of charisma, integrity, andselflessness, who soon won the confidence of the Makerere intellectuals andslowly integrated them in the politics of the municipality
Kwamba alichofanya Abdu Sykes si kuwaingiza katika siasa ili waanze kama anavyodai Mohamed katika majibu mengine bali kuwashirikisha katika siasa za jiji.
Mohamed:It became a tradition that whenever a young man from up-country came totown, he would be taken by his acquaintances to Abdulwahid’s house at Stanley Street to pay homage and receivehis first political orientation
Hapa Mohamed anamlenga Nyerere kwa kusema kila aliyetoka bara alifika kwa Abdul Sykes ili kupata ufahamu wa siasa kwanza. Alichosahu ni kuwa Nyerere huyo huyo alikuwa katibu wa AA Tabora(kwa maneno yake) na alianza siasa tangu Makerere (kwa maneno yake Mohamed).
Hakuishia hapo aliendelea kumnanga Nyerere kama hivi Mohamed anasema Ahaa1 kumbe walikuwepo akina John Rupia,Stephen Mhando katika subcommitee, sasa iweje Mohamed atambe kuwa baraza la wazee wa TANU iliyokuja baada ya TAA ilikuwa na Waislam walioleta Uhuru? Halfu hapa tunaona majina zaidi ya yale ya Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi. So far kuna Rupia, Dunstan Omar, Stephen Mhando, Clement Mtamila. Sasa inakuwaje Mohamed aseme wazee wake ni waislam na si wazee wote? Mohamed is on offensive against Nyerere, soma hii Hapo Mohamed ametumbukiza ukatoliki wa Nyerere kwanza, kisha kumwekea maneno kwa kutumia neno ''inasemekana''. Mohamed hakuwahi kumhoji Nyerere lakini alifahamu vema kuwa alikuwa mnyenyekevu wa kanisa na Serikali ili kulinda kibarua chake. Ni Mohamed huyo huyo alitueleza kuwa akiwa Makerere na Tabora Nyerere tayari alikuwa katika siasa, kwanini basi aanze kuhofia kibarua, serikali na Kanisa alipofika Dar? Maana yake ni kutaka kumshusha katika watu waliopigania uhuru kama anavyosema hapa Halafu akaendelea na chuki dhidi ya Nyerere na dini yake
Mohamed:Nyerere alijua yeye akiwa Mkristo, kamwe hangeweza kujijengea nguvu ya siasa katika mazingira yale ya Dar es Salaam ya miaka ya 1950 ambako siasa zilitawaliwa na Waislam. Kwa sababu hii, Nyerere alisita kukubali shauri la kuongoza TAA
Hapa Mohamed anasahau kuwa Dr Vedastus Kyaruzi aliwahi kuwa kiongozi wa TAA licha ya Ukristo wake. Amewasahau akina John Rupia, Stephen Mhando na Clement Mtamila kuwa kwa Nayakati fulani walikuwa viongozi katika mji ule ule ambao Nyerere asingeweza kuwa kiongozi kwa ukristo wake.

Fikiria wakati unasoma, ukimeza bila kutafuna utajikuta umemeza ''Ngano'' kama si Mashudu.
 
Nguruvi umemaliza kasi; kwenye kusoma na aelewe. Nimesema hapo juu hoja zote za Bw. Said zinasimama na kuanguka na mwaka 1953. Hivi kuna mtu amewahi kuuliza wakati Nyerere anaondoka kwenda Uingereza masomo aliondokea mji gani?
 

Mkuu, I respect you, umemwanika vizuri sana huyu mchochezi asiyejua hata kanuni za uongo
 
Sina ugomvi na uchambuzi wako.
Hatuwezi sote tukaona mambo kwa jicho moja.

Kinachonistaajabisha ni hizi hamaki mlokuwanazo
katika mjadala huu.

Lugha za "uongo," "uchochezi" hakika si maneno ya
kiungwana.

Sasa mbona hamgusi kwa kina Idd Faiz, Idd Tosiri na
Idd Tulio?

Hamna maswali kwa watu hawa?

Hampendi kujua kile kisichojulikana na wengi?

Hampendi kuwajua marafiki wa Nyerere katika siku zile
ngumu na za hatari za mwanzo 1955.

Mbona hamshangazwi kuwa mashujaa hawa hawajaenziwa
hadi leo?

Hampendi kujua nini ilikuwa hatima yao katika TANU?

Je hampendi kujua nyaraka za Nyerere za enzi ya TAA na TANU
anazo nani hii leo?

Je hamtapenda kujua nini kilitokea baada ya uhuru Nyerere
alipoziomba zile nyaraka?

Wanaukumbi hamtaki kujua "kisa cha ugomvi wa nyaraka?"
Hamtapenda kujua walokuwa na nyaraka zile kwanini walikataa
kumpa Nyerere nyaraka zile za TAA na TANU?

Mkijifunga katika maswali ya kujibizana yale ya nipe nikupe
mtapitwa na mengi.
 
Naomba mimi ndugu zangu msinihusishe na hii historia ya ''kaptula.''
Kwa kweli hainipendezi na inanivunjia muruwa wangu.

Nihusisheni na historia ya kudai uhuru hilo ndilo somo ninalojua.
mzee ms hivyo vyote vinaendana na simulizi zako haviachani. Na huku mitaani ndo simulizi kwa wale wanaopokea kila neno litamkwalo na mtu wa imani yake wala usikataee.
Na kama hilo jambo halipo ungeliandika kwenye kitabu chako kulikanusha.
 
Shukran kwa darsa na majibu yako muruwa kabisa. Kwani naona kama sasa hakuna masuala bali zimebaki kejeli. Ahsantum
 
Ahali yangu Mohamed Said. Mimi nakuomba kwa hishma na taadhima kubwa unipe machache kidogo kuhusu MZEE ALI MPIMA ( watoto zake Mbaraka, na dadaye Nuru maarufu kama Nuru Jongoo) anayekaa pale kona ya Livingstone na Mkunguni. Vile vile hicho kisa cha kunyimwa Docs za TAA na TANU ili tujifunze mengi kutokana na historia ya Tanganyika. Hakika Mola akubariki sana kwa ilmu unayo tu darsisha hapa.
 
Nguruvi3 asante sana kwa jinsi ulivyochambua,hakika nimeona jinsi mzee MS anavyojichanganya! Hata kama mzee unataka kuwaenzi wazee wako usipotoshe historia utatuchanganya
 
mzee Mohamed Said,

kwanza Assalam Alykum

Natumai hali yako ni murwa

Swali kwa hao wanaoita kitabu chako Alf Lela... Ni akina nani walimsaidia Hayati Mwalimu Julius Nyerere mpaka Tanganyika inapata Uhuru? Katika orodha yenu, mnawatambua wazee aliyowataja mzee [MENTION]Mohamed Said [/MENTION]au la?

Naomba majibu
cc Barubaru Do santos Ritz
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi umemaliza kasi; kwenye kusoma na aelewe. Nimesema hapo juu hoja zote za Bw. Said zinasimama na kuanguka na mwaka 1953. Hivi kuna mtu amewahi kuuliza wakati Nyerere anaondoka kwenda Uingereza masomo aliondokea mji gani?
mzee mwankijiji natumia kamchina ningekugongea like.
 
kaka Do santos mpaka sasa ninasubiri kwa hamu lakini huyu kijana anakwepa kwepa tu
Alitaka kutuhadaa tu hawezi kujibu kwani sakata lile limetungiwa kitabu maalum kabisa nanimwe utawaona akina Murtaza lakha na Issa Shivji walivyokuwa wanawaenyesha akima Mhavile na wengine wengi. Ok vuteni subra labda anakusanya data.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…