Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee Mwanakijiji. Nakumbuka suali langu la kwanza wakati naingia kwenye mnakasha huu lilielekezwa kwako. Mbona hukunijibu?
Mzee Mwanakijiji, nilijua kimya chako kina mshindo lakini naona umeamua kufanya la maana kabisa...iko siku Mohamed Said alijaribu kupotosha ukweli katika maandishi ya John Iliffe ambayo tayari yako in black and white, ndipo nilipom"right off" kabisaa na toka siku hiyo kwangu ni mtu wa umbea na uchochezi tu, period. Hamna cha utafiti wala historia...tatizo lililomo humu ni kuwa kuna watu hawahangaiki kutafuta hivyo vitabu na kuvisoma!
Mtu unaambiwa kitabu cha Kivukoni hakijamtaja Abdulwahid Sykes na wewe kama vuvuzela vile unakurupuka na kuufanya wimbo! Kumbe kama ungefanya jitihada kidogo tu ukitafute kitabu ujisomee mwenyewe, hungekubali kudanganyika kirahisi hivyo...lakini wako watu humu, mmh! Yaani hata katika kunukuu yaliyoandikwa tayari mtu anaamua kuchakachua kwa malengo ya ajabu kabisa lakini the gullible gobble it all too hyperdeliciously without question!
mkuu kuna wajuzi wa dhihaka humu wameenda mbali na kudai ni bora Yeriko afuate nyendo zako tu za utunzi wa "ngano" za mapenzi. Sijui ni kipi kawaza aliyenena hivi. Ila ninaomba kujua toka kwako unahisi Ndg. Yeriko yupo sahihi katika hili mpaka uandishi wake??
mmmh kwani na wewe unapata wapi nguvu ya kuamini hivyo vitabu unavyoendelea kuvisoma? Na ukumbuke pia ni rahisi kuukana ukweli ili kuhalalisha uongo....! binafs nina uthibitisho wa anayoyasema Mohamed Said
Mwenzenu nipo namalizia vitabu vyote muhimu katika somo hili:
Baada ya kummaliza John Iliffe katika A Modern History of Tanganyika na Modern Tanzanians na pia Tanganyika Under German Rule namsoma Judith Listowell sasa hivi. Pamoja na hao nasoma Tanganyika Under International Mandate, Tanzania Education Since Uhuru, TANU Yajenga Nchi: Political Development in Rural Tanzania na vingine vingi. Naweza kusema kwa uhakika wa asilimia 100 Bw. Mohammed Said ameokoteza okoteza taarifa mbalimbali akazipamba kwa lugha na masimulizi ya wazee wake na kuziita historia na akaziuza na bahati mbaya sana zimeaminiwa na wengi.
Denoo49,
Huyu ndugu yangu aandike review ya kitabu changu aonyeshe
''kuokoteza'' kwangu.
Insha Allah nitamjibu uso kwa macho.
Hebu na tuangalie kila kichwa kwa upana wake, tujiulize hivi kuna uzima?Barubaru,
Huyu mtoto huenda ana matatizo na nasema hili kwa huzuni kubwa sana.
Kaanza na kujinasibisha kuwa kazaliwa na....naogopa hata kutaja jina.
Sasa anasema kaalikwa Pentagon kama bingwa wa ugaidi na anataja majina
ya watu wa huko.
Anasema Balozi wa Marekani ndiye anasimamia kitabu chake.
Anaweka kitabu hapa jamvini nacho si kitabu si chochote.
Hapo mtu huna budi ila kwenda kwenye kichwa chake.
Huyu mtoto ni mzima?
Naomba mwenye weledi anieleze kama dini ya Uislam zaidi ya imani ina nembo na kama kiswahili ndio nembo ya ukanda huu wa Afrika Mashariki.Mohamed Said😛amoja na Uislam ikazuka lugha ya Kiswahili, lugha ianyozungumzwa Afrika ya Mashariki na ya Kati na utamaduni wa Kiswahili ambao unanasibishwa na Uislam.Nembo ya Muislam katika Afrika ya Mashariki na Kati ni kuikubali lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya asili
Sensa hiyo ya 1957 ilifanywa na taasisi gani! Pili, kila waislam 3 wakristo walikuwa 2! katika nchi yenye hindu, atheist, Pagans huwezi kuondoa kundi moja ukabaki na data sahihi. Mohamed kageuza sensa hiyo(kama ilikuwepo na hajawahi kueleza) kuwa ilikuwa sensa ya wakristo vs Waislam, kuna tatizo hapa, wajanja wanakitazama kichwa chako kwa shauku, tuendeleeMohamed Said:Kutokana na sensa ya mwaka 1957, kwa kila Waislam watatu walikuwepo Wakristo wawili
Sheikh, hapa ni suala la hesabu na stat. Ni ngumu sana kukuelewesha lakini ngoja tujaribu kuingia kichwani mwako. Namba ya waislam au wakristo inaweza kuwa imebaki pale pale, pengine sensa ilifika mahali ambako ile ya awali haikufika. Baada ya uhuru uhamasishaji ulikuwa mkubwa. Kwa hesabu ni kuwa umeongeza idadi na hiyo inaathiri percentage hata kama namba zimebaki kama zilivyo. Kuna mengine lakini hilo tu ni kwa kuanzia kuingia kichwani, sasa tuingie kichwani kujua kama ni mzima?Mohamed Said:Kwa wakati ule hii ilionyesha kuwa Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi katika nchi zote Kusini ya Ikweta. Lakini katika sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili na Waislam asilimia thelathini na Wapagani asilimia thelathini na saba. Sensa hii inaonyesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania. Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislam wamepungua nchini au kwa nini ghafla Wapagani wameongozeka katika nchi ya waumini
In other words,kulikuwa na sensa ya mwaka 1957, 1967 na 1970! Hapo ndipo ninaposema tusitishe haraka sana zoezi la kuingia vichwani mwa watu.Mohamed Said:Upo ushahidi kuwa mwaka 1970, ilipobainika kuwa Waislam ni wengi Tanzania serikali iliiamrisha Idara ya Takwimu kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970
Judith Listowell anaeleza vizuri tu kuhusu Sheikh Takadir -ambao kina Ritz wanaamini Mohammed Said ni wa kwanza kumtaja!!
Ili uwe na qualification ya kujadiliana na mimi naomba kujua kama uliwahi kusoma kitabu cha Mohamed Said au kitabu chochote kinachozungumzia historia ya Uhuru wa Tanganyika!
Na pili naomba kujua kama uliwahi kusoma kitabu chochote kinachozungumzia ugaidi!
Hama hakuna basi huna vigezo vya kuamatana nami, na kuanzia sasa wewe Boko Haram na The Big Show sitawajibu chochote mpakaba muwe na vigezo hivyo hapo juu!
Wanajamvi,
Naomba mtu yeyote aliyekisoma kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na chuo cha Kivukoni authibitishie UMMA kama kitabu hicho kimewataja Abdul Sykes, nk!
Madai ya Mohamed ni kuwa hakijamtaja Abdul Sykes!
Na mimi nasema katika kitabu cha TANU kutoka Kivukoni, Abdul Sykes katajwa tena katajwa kiweledi kabisa
Kwa faida ya wanajamvi tuwekee basi ivyo vipande unavyosema katajwa kwingi wanajamvi wasome.
Bahati mbaya ndugu yangu ninatumia simu ya kiganjani,
Ningaliileta hapa hiyo nakala laini,
Nipatapo mda wakuketi katika kidadavuzi nitaitupia hapa ndugu!
Lakini fahamu kuwa kivukoni hakijamwacha mtu kama Mohamed Said anavyouaminisha umma
Wanajamvi hata kama ni uongo, ni heri uongo wenyewe uwe na nyama na si mifupa mitupu kama aliyoweka hapa Al Akhiy Mohamed Said. Mwaka 1945, Mwalimu Nyerere akiwa tayari ni kiongozi wa AA Tabora, nani alimjua Abdulwahid Sykes zaidi ya kuwa mtoto wa baba, Kleist Sykes. Abdulwahid Sykes alikuwa nani ndani ya AA mwaka 1946? Abdulwahid Sykes alikuwa nani ndani ya AA mwaka 1947? Ni mwaka 1948 ndio Abdulwahid anakuja kusikika akiwa miongoni mwa walioshiriki katika mapinduzi ya kuung'oa uongozi wa TAA kwa kutumia masumbwi! Huu mwamko sana sana uliletwa na wasomi wanaharakati kutoka Makerere!It was an Englishman, Brendon Grimshaw, the editor of Tanganyika Standard, who published a fitting obituary to Abdulwahid describing him as: ‘one of the architects of the independence movement and one of the men who helped launch President Nyerere on his political carrier...'
Mohamed Said najua ungependa sana umdhalilishe Mwalimu Nyerere lakini uongo mwingine hata haufai. Hao certain members of the TANU leadership unaodai walisikika wakilalama ndio akina nani? Na hao waliowasikia na baadaye kukueleza ndio kina nani? Mbona simulizi zako zingine zinakuwa mno kama za mtaani halafi unadai ni matokeo ya utafiti wa miaka 15! Jaribu kuona aibu japo kidogo Al Akhiy Mohamed Said, unawaangusha vijana wako wanaoingia humu kufyonza ilmu kama Spike Lee. Naomba uwaeleze wanajamvi jitihada za Abdulwahid Sykes toka chama cha kwanza cha siasa kinaasisiwa mwaka 1954 hadi tunapata uhuru mwaka 1961.It is said that this recognition of Abdulwahid as one of the founding fathers of the nation became a focus of attack from certain members of the TANU leadership. They were overheard grumbling in the corridors of the TANU headquarters in Dar es Salaam that Ally and Abbas Sykes were trying to glorify their elder brother.
Si sahihi misahama hiyo kudhibitiwa na BAKWATA.Hilo ni jukumu la serikali husika. Ninachoelewa ni kuwa misaada hiyo lazima ipitie taasisi zinazojulikana na zilizosajiliwa na kama BAKWATA ndiyo inayojulikana, hilo si tatizo la serikali ni tatizo la waislam kwasababu wale BAKWATA ni waislam unless usimame hapa na kusema siyo.
Misamaha ya kodi inatumiwa vibaya na watu wa dini, narudia dini zote isipokuwa wapagani na wasioamini.
Nakaumbuka kama si Rais JK ni Mkapa aliwahi kuonyesha misaada hiyo inavyokuwa misused na taasisi.
Kwamba magari yanaingia kama ya taasisi za dini kumbe ni ya watu binafsi.
Siku zote huwa nasema misamaha ya kodi lazima iwe na udhibiti wa hali ya juu sana ili kuzuia kufujwa na baadhi ya watu. Nimekonyesha kuwa misamaha inayotolewa lets say kwa BAKWATA hutumika kwa waislam kwahiyo hakuna sababu ya kusema hilo ni jambo la uonevu.
Ndivyo ilivyo kwa imani zingine na ndio sababu nasema misamaha ni ukwepaji kodi isipokuwa ile inayodhibitiwa kikamilifu.
Umeongelea kwanini kuwe na udhibiti. Kuna jambo unalosahau hapa. Kauli na matendo ya watu vinatosha sana kuwa na shuku juu ya misaada. Nimekuuliza hivi ukisikia Maliki ametoa dollar milioni 1 kwa ajili ya maendeleo kupitia wanafunzi wake utakuwa na imani kweli. Wanafunzi hao ndio wanasema ''tafuta mtu fulani ua kwa siri'', ndio hao wanakuwa wazushi kila alfajiri hadi isha wakienda hadi China si kuitafuta elimu bali kueneza chuki na uongo.
Si kweli kuwa kuna udhibiti kwa waislam. Hivi karibuni kuna taasisi imejenga misikiti 700, visima na maji mbona hawakudhibitiwa? Kuna akina African Muslim agency na World muslim league mbona hawakuwahi kudhibitiwa.
Nenda ndani ya baadhi ya taasisi hizo uone uchafu unaofanyika halafu urudi na kuniambia hiyo ni sehemu ya Uislam.
Na mwisho huko nyuma uliongelea TAMPRO. Nadhani hii taasisi inapoteza maana yake kwa namna fulani.
Wao kama professionals wanapaswa waongoze waislam katika mambo mengi badala ya kukaa pembeni na kuwaachia wahuni wachache.
Haiwezekani siku ya Ijumaa igeuzwe siku ya fujo na maandamo bila sababu za maana wala za msingi.
Ni hawa ninaoita wahuni ndio wameshika usukani wa kupotosha watu.
TAMPRO inapaswa itumike kama msaada mzima wa kuchukua ajenda na kuziangalia, kuzitathmini na kuzifanyia kazi kiweledi bila tafrani.
Sijui hebu nieleweshe viongozi wa TAMPRO ni akina nani ili niweze kuielewa vema
Anyway ni maoni tu.
Ukisema BAKWATA ni tatizo nitakuuliza WML ilifanya nini na iliondokaje, maana mzee mzima hakujibu!
Sitetei BAKWATA ninachosema hapa ni kuwa tatizo linaonekana kama BAKWATA lakini ni zaidi ya hapo na ni kubwa sana
Mzee Mwanakijiji, nilijua kimya chako kina mshindo lakini naona umeamua kufanya la maana kabisa...iko siku Mohamed Said alijaribu kupotosha ukweli katika maandishi ya John Iliffe ambayo tayari yako in black and white, ndipo nilipom"right off" kabisaa na toka siku hiyo kwangu ni mtu wa umbea na uchochezi tu, period. Hamna cha utafiti wala historia...tatizo lililomo humu ni kuwa kuna watu hawahangaiki kutafuta hivyo vitabu na kuvisoma!
Mtu unaambiwa kitabu cha Kivukoni hakijamtaja Abdulwahid Sykes na wewe kama vuvuzela vile unakurupuka na kuufanya wimbo! Kumbe kama ungefanya jitihada kidogo tu ukitafute kitabu ujisomee mwenyewe, hungekubali kudanganyika kirahisi hivyo...lakini wako watu humu, mmh! Yaani hata katika kunukuu yaliyoandikwa tayari mtu anaamua kuchakachua kwa malengo ya ajabu kabisa lakini the gullible gobble it all too hyperdeliciously without question!
Pamoja na hilo neno (in red) kutokueleweka, Al Akhiy Mohamed Said, ikiwa ni kweli Abdulwahid Sykes ndiye aliyemwingiza Mwalimu Nyerere kwenye siasa, unaweza sasa kutoa majibu yanayoeleweka kuhusu haya uliyoyakwepa hapo nyuma?Mohamed Said said:Abdulwahid Sykes was one of the architects of the independence movement and one of the men who helped launch President Nyerere on his political carrier...