Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee Mwanakijiji. Nakumbuka suali langu la kwanza wakati naingia kwenye mnakasha huu lilielekezwa kwako. Mbona hukunijibu?
Zali wa Mentali,
Judith Listowel kamtaja Sheikh Suleiman Takadir lakini
kama ilivyo kawaida ya waandishi Wazungu yeye kwa
bahati mbaya kaparazia juu juu.
Hakumueleza Sheikh Takadir kama ilivyostahili kwa maana
ya kueleza historia yake nzimna baina yake na Nyerere
walipoanza kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mimi ndiye niliyekuja kumueleza Sheikh Takadir kwa urefu
na kueleza chanzo cha ugomvi wake na Nyerere mwaka
1958.