Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #14,661
Wickama,
Hizo bunduki zilikuwa za Ben Bella.
Aliulizwa na Dk. Ghassany uso kwa macho.
Iweje uwape silaha watu wanaopigana na nduguzo Waarabu?
Jibu la Ben Bella ni kuwa wale walikuwa maadui zake sana
kwa kuwa walikuwa upande wa Waingereza wakandamizaji
watu.
Mohamed Said,
Nikisoma mipini yako kuhusu mapinduzi ya Zanzibar walaahi najisikia mustarehe.
Kituko Yericko naye anajitokeza kuchambua mapinduzi ya Zanzibar nabaki nacheka sawa sawa watu tunakula Mandi ya mbuzi anatokea mtu analeta ugali wa udaga na furu...ha haaa.
Ukimuuliza Yericko, John Gideon Okello amefariki lini hajui.
gombesugu,
Yaweza kuwa ni kweli ziliingizwa hizo silahala kutoka Algeria kwa Ben Bella lakini hazikutumika katika mapinduzi ya Mungu wa Afrika (Okello)Wickama,
Hilo sijui lakini za Ben Bella zilifika zikashushwa Kunduchi.
Haaaaaa; this is strange wewe tena????? Mzee MS leo masuala ya Qadar vipi? Kama wanatafuta watu ni kwamba saa hizi tayari wanasoma pages na pages za huko nyuma za miaka. Hawa wakina JF kazi yao ni kutoa address husika ya computer iliyotumika (ndio kazi ya wanachoita cookies!!!!!). MS hata uiuze, aliyeinunua mwisho wa siku atakufata na jamaa wamevaa miwani za jua. Wewe endelea, na thread wakati unasubiri Qadar Sheikh hahahahah
Ndugu yangu Mohamed Said
Hebu tumia mda kidogo kuangalia huo mkanda kisha angalia aina ya silaha zilizotumiwa!
Mimi ni mjuzi wa silaha, na ninazifahamu silaha tulizorithi toka kwa muuingereza ambozo hadi hivi hii leo zipo!
Hebu angalia video hiyo mzee wangu!
Ritz
Tungeomba utulivu na adabu katika hili,
Mimi napata elimu na ninatoa kile nilichonacho!
Nivema kutulia nakuwa msomaji ama unachochote ukijuacho juu ya hili tueleze kuliko kuleta viroja vya kutuvuruga!
Yericko,
Na wewe una deserve adabu?
Labda waseme wengine wewe kila siku unaniita mie mfuta viatu vya Mohamed Said.
Hakuna cha kujifunza kwako labda adithi za laura Bush za kuvaa suti nyekundu.
Yericko,
Nitaiangalia.
Lakini zile za Algeria zilipokelewa.
Hii ni taarifa ya kweli.
Suala la mapinduzi ya Zanzibar lina mchanganyiko sana.
Ukiangalia historia kumekuwa na resentment dhidi ya utawala wa sultan kwa miaka mingi nyuma kabla ya mapinduzi.
Mtakumbuka kuwa wakati Tanganyika wakiwa na AA na huko ZNZ ilikuwepo.
Kwa maneno mengine kulikuwa na similarities za manunguniko kutoka pande zote ambayo ni dhidi ya ukoloni. Kwa Tanganyika walikuwa Waingereza na huko visiwani Waarabu.
Migogoro ya chaguzi za Zanzibar na hata uanzishaji wa vyama vya siasa zilijikita zaidi katika damu na rangi. Kwamba wapo walioamini kuwa wanahaki ya kutawala na wapo waliopinga hilo.
Tofauti za wanazuoni kutokana na hali hiyo zinakuja katika rangi zaidi kuliko ukweli.
Ukisoma vitabu ambavyo vimeandikwa na watu wenye asili au unasaba na uarabu, mapinduzi yalikuwa haramu.
Ukisoma wengine ambao ni wazawa wa Afrika, mapinduzi yalikuwa halali.
Na tofauti hizo zipo hadi leo ndio maana tunasikia mapinduzi daima, na wengine wakisema mapinduzi ni zao la chuki la Nyerere.
Wazanzibar wenyewe hawakubaliani ndio maana nimekuwa nauliza, kama lengo la mapinduzi lilikuwa kuua Uislam, iweje ZNZ yenye 99% waislam waitukuze siku ambayo Uislam uliuawa na Nyerere?
Hapa hakuna suala la udini kwasababu wote ni waislam, lipo suala la rangi.
Sasa wanaomhukumu Nyerere ni wale wenye chuki tu na Nyerere na hivyo kutaka kumpaka matope.
Vinginevyo basi ZNZ yote siku moja ingesema hakuna mapinduzi wala siku ya mapinduzi wala sherehe za mapinduzi kwasababu ni haram.
Hilo halitokei kwasababu Mapinduzi ni ya wazanzibar na wanayaona ni halali kwa mtazamo wa sehemu fulani ambayo ni kubwa ya jamii hiyo.
Hawa wanaosema Nyerere alifanya hivyo kuua Uislam, hawajibu hoja kuwa kwanini basi Nyerere huyo huyo aunge nkono Palestina na Polisario.
Kwanini basi Nyerere huyo huyo aondoe nduguze kule Msumbiji, Botswana, Namibia na ku-abolish apartheid kama lengo lilikuwa kuua uislam EAC ili ukristo ushamiri kwingine Afrika mashariki au Afrika yote?

Kama kawaida yako Mzee Mohamed. Huyu bwana angekuwa Muislam bila shaka yoyote simulizi zako zingekuwa tofauti kabisa! Kwa kuwa ni Mkristo lazima aondolewe awekwe Kassim, Ali,...,
DINI yako imekudhibiti sana. Kumbuka tu kuwa Mungu hana DINI.
Mkuu hili hata asubuhi leo tulipoanza mjadala huu nilieleza mtazamo wangu kulingana na maandiko mengi niliyosoma pamoja na kuziangalia video hasa ile ya mapinduzi ya Okello, nilisema wazi kuwa katika mijadala iliyotanda siku ya mapinduzi haikuwa DINI bali Rangi, Kabila na mengineyo,
Lakini utata umeibuka hapa hasa baada ya Ndugu yetu Mohamed Said kusema Okello hakufanya chochote bali mapinduzi yaliongozwa na Kasim Hanga akiwa sambamba na Oscar Kambona,
Mimi namuona Okello kuwa ndie muasisi wa mapinduzi, na anasema wazi katika kitabu chake,
Sasa tunahitaji fikra mpya ili kuliweka sawa hili, lakini pia mimi nilionya kuweka mbele itikadi za kiroho itatuondolea uwepo katika mada hii!
Inahitaji ustahimilivu wa kweli ili kung'amua!
Suala la mapinduzi ya Zanzibar lina mchanganyiko sana.
Ukiangalia historia kumekuwa na resentment dhidi ya utawala wa sultan kwa miaka mingi nyuma kabla ya mapinduzi.
Mtakumbuka kuwa wakati Tanganyika wakiwa na AA na huko ZNZ ilikuwepo.
Kwa maneno mengine kulikuwa na similarities za manung'uniko kutoka pande zote ambayo ni dhidi ya ukoloni. Kwa Tanganyika walikuwa Waingereza na huko visiwani Waarabu.
Migogoro ya chaguzi za Zanzibar na hata uanzishaji wa vyama vya siasa zilijikita zaidi katika damu na rangi. Kwamba wapo walioamini kuwa wanahaki ya kutawala na wapo waliopinga hilo.
Tofauti za wanazuoni kutokana na hali hiyo zinakuja katika rangi zaidi kuliko ukweli.
Ukisoma vitabu ambavyo vimeandikwa na watu wenye asili au unasaba na uarabu, mapinduzi yalikuwa haramu.
Ukisoma wengine ambao ni wazawa wa Afrika, mapinduzi yalikuwa halali.
Na tofauti hizo zipo hadi leo ndio maana tunasikia mapinduzi daima, na wengine wakisema mapinduzi ni zao la chuki la Nyerere.
Wazanzibar wenyewe hawakubaliani ndio maana nimekuwa nauliza, kama lengo la mapinduzi lilikuwa kuua Uislam, iweje ZNZ yenye 99% waislam waitukuze siku ambayo Uislam uliuawa na Nyerere?
Hapa hakuna suala la udini kwasababu wote ni waislam, lipo suala la rangi.
Sasa wanaomhukumu Nyerere ni wale wenye chuki tu na Nyerere na hivyo kutaka kumpaka matope.
Vinginevyo basi ZNZ yote siku moja ingesema hakuna mapinduzi wala siku ya mapinduzi wala sherehe za mapinduzi kwasababu ni haram.
Hilo halitokei kwasababu Mapinduzi ni ya wazanzibar na wanayaona ni halali kwa mtazamo wa sehemu fulani ambayo ni kubwa ya jamii hiyo.
Hawa wanaosema Nyerere alifanya hivyo kuua Uislam, hawajibu hoja kuwa kwanini basi Nyerere huyo huyo aunge nkono Palestina na Polisario.
Kwanini basi Nyerere huyo huyo aondoe ''nduguze'' kule Msumbiji, Botswana, Namibia na ku-abolish apartheid kama lengo lilikuwa kuua uislam EAC ili ukristo ushamiri kwingine Afrika mashariki au Afrika yote?
Yaweza kuwa ni kweli ziliingizwa hizo silahala kutoka Algeria kwa Ben Bella lakini hazikutumika katika mapinduzi ya Mungu wa Afrika (Okello)
Kumbuka katika baadhi ya machapisho yanasomeka kuwa hata Muingereza alipoamua kuondoa askari wake katika vituo, aliondoka na funguo za ghala la silaha, hivi Okello alikuwa na Silaha kama kumi tu alizonyang'anya kwa baadhi ya askari waliosalia!
Ukini uliza mimi mpaka sasa namuona Okello ndie Mwanamapinduzi halisi wa Zanzibar pamoja na mauaji yote aliyoyaendesha!
Nguruvi,
Kusema siyo kuwa ndiyo iwe kweli.
Hawakupanga mapinduzi Umma Party ya kina Babu aje
apange Okello?
Jeshi lile la Kipumbwi likilishwa na nani na nani alilidhamini
kuja kuipigia kura ASP kisha kuja kufanya mapinduzi?
Aliyewaruhusu kuvamia Zanzibar kutoka Kipumbwi ni nani?
Yericko Nyerere, mimi mwanzoni nilidhani porojo za huyu mwenzetu zingeishia tu hapa bara lakini duh, uongo una sifa moja mbaya, ukiachwa unaenea kama upepo vile. Ona sasa porojo zimevuka bahari hadi kutua kwenye visiwa vya karafuu. Mimi hapa nabaki nacheka tu...namkumbuka Abdulrahman Babu akipiga tusker zake pale Dar es Salaam Club, akitaka apewe microphone apande stejini atoe burudani akiimba wimbo wa "soul"...baadaye sana nawaona wasaidizi wake wakimshauri kuwa saa ya kuondoka imetimia (wakati huo ni saa tisa usiku hivi) aweze kuwahi ofisini asubuhi...hiyo ni miaka ya 1960s baada ya Muungano!Mkuu hili hata asubuhi leo tulipoanza mjadala huu nilieleza mtazamo wangu kulingana na maandiko mengi niliyosoma pamoja na kuziangalia video hasa ile ya mapinduzi ya Okello, nilisema wazi kuwa katika mijadala iliyotanda siku ya mapinduzi haikuwa DINI bali Rangi, Kabila na mengineyo,
Lakini utata umeibuka hapa hasa baada ya Ndugu yetu Mohamed Said kusema Okello hakufanya chochote bali mapinduzi yaliongozwa na Kasim Hanga akiwa sambamba na Oscar Kambona,
Mimi namuona Okello kuwa ndie muasisi wa mapinduzi, na anasema wazi katika kitabu chake,
Sasa tunahitaji fikra mpya ili kuliweka sawa hili, lakini pia mimi nilionya kuweka mbele itikadi za kiroho itatuondolea uwepo katika mada hii!
Inahitaji ustahimilivu wa kweli ili kung'amua!
Yericko,
Kuna mashujaa wengine hujapata kuwasikia.
Hebu soma hapa chini kisha tuendelee na darsa:
''Jina la huyu mzee wangu ni Mohamed Omar Mkwawa.
Ilikuwa katika barza yetu ya kawaida ya kunywa kahawa na kula pweza huku tukijadili historia ya Tanzania ambako siku moja Mzee Mkwawa alinambia, Mohamed nataka nikuambie kitu. Unajua mimi nimehusika sana katika mapinduzi ya Zanzibar?
Nilimuangalia Mzee Mkwawa kwa makini. Fikra yangu ya utafiti na uandishi ishashtuka haipo tena usingizini. Mzee Mkwawa aliendelea, Mimi ndiye niliyekuwa nikiwavusha Wamakonde kutoka Kipumbwi kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP na wakati wa mapinduzi mie ndiye niliyewavusha Wamakonde kwenda kuipindua serikali ya Jamshid.
Sasa moyo wangu ukaanza kudunda kwa nguvu. Naisemesha nafsi yangu, Huyu mzee anajua uzito wa maneno haya? Tuishie hapa.
Kuanzia siku ile nikawa sasa namtazama Mzee Mkwawa kwa jicho jingine na heshima yangu kwake ikawa imepanda maradufu. Nilikuwa nimeshatambua kuwa Mzee Mohamed Omari Mkwawa alikuwa mmoja wa wanahistoria waliosahaulika katika historia ya Tanganyika na Zanzibar...
Yericko,
Tuendelee na darsa letu la historia ya mapinduzi ya Zanzibar na nakuomba uangalie wapi utampachika ''Field Marshal Okello'' katika nyavu hizi abaki salama bila ya kujifungafunga:
Kitu kimoja mashuhuri kwa mashujaa wa harakati za siasa katika Tanzania ni kuwa takriban wote wana hali ngumu sana za maisha. Sikujua vyema hali ya Mzee Mkwawa hadi nilipofika nyumbani kwake na Dkt Ghassany.
Utu uzima na udhaifu wa maisha ulikuwa umempiga barabara. Nilimjulisha Dkt Ghassany kwa Mzee Mkwawa na kuwaacha waendelee na maongezi yao. Niliporudi mchana kumchukua Dkt Ghassany rafiki yangu alinambia nimuache nije jioni kumfuata. Niliporudi jioni nilimkuta Dkt Ghassany amechoka na uso umesawijika.
Tukiwa ndani ya gari yangu tunaondoka nikamuuliza kulikoni. Dkt Ghassany akanambia maneno ambayo hadi leo yamebaki kichwani mwangu,Mohamed ufunguo wa kitabu changu anao Mzee Mkwakwa na kama nisingeonana nae utafiti wangu wote wa kabla ungelikuwa hauna maana yoyote.
Dkt Ghassany alikuwa amechukuliwa na Mzee Mkwawa katika safari ya zaidi ya nusu karne. Mzee Mkwawa akimshika mkono kwanza kumpeleka Pemba ambako akiwa kijana wa kiasi cha miaka 25 akifanya kazi ya uashi. Huo ndio ulikuwa wakati wa siasa za ASP na Hizbu zimepamba moto.
Mzee Mkwawa alikuwa mmoja wa wachezaji wa ngoma ile hata kama alikuwa anatoka Tanganyika. Dkt Harith akavushwa na kuletwa pwani ya Kipumbwi na Sakura ambako Mzee Mkwawa alikuwa akisimamia kambi ya mafunzo iliyokuwa msituni ya wakata mkonge wengi wao wakiwa Wamakonde, kambi ambayo ilitoa askari waliotumika kuipindua serikali ya Mohamed Shamte 12 Aprili 1964.
Dkt Ghassany hakuwa amejitayarisha kwa haya. Alishangwazwa na uwezo wa kumbukumbu wa Mzee Mkwawa, akitaja majina na mahali na akirudia mazungumzo neno kwa neno kati yake na maofisa wa serikali ya Tanganyika kutoka vyombo vya usalama waliomtia katika operesheni maalum ya kuipindua Zanzibar kutoka Tanganyika.
Majina ya Abdulla Kassim Hanga, Jumanne Abdallah, Ali Mwinyi Tambwe, Victor Mkello, Oscar Kambona na wengine yakawa yanadondoka moja baada ya lingine. Taarifa hizi ndizo zilizommaliza Dkt Ghassany na kumsawajisha uso.
Mimi binafsi nilipigwa na butwaa. Nilibaini kama alivyobaini Dkt Ghassany kuwa Mzee Mkwawa alikuwa hazina na tulikuwa tumevumbua mgodi wa dhahabu. Kazi yetu sasa ilikuwa kuchimba tu. Kumekuwa na uvumi kwa miaka mingi katika duru za wanasiasa wapya na wa zamani na katika wanafunzi wa historia ya Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Ali Mwinyi Tambwe alihusika sana katika kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar lakini hakuna aliyejuwa ni kwa kiwango gani na alihusika vipi.
Lakini zito ni kuwa yeye mwenyewe akiudhika sana mtu akimuuliza habari zile. Kwa nini ilikuwa hivyo? Kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru cha Dkt Ghassany kilikuja kutoa majibu. Hakuna binadamu apendae historia yake ihusishwe na mauaji na dhulma na kufutwa kwa nchi yake.
Kwa kipindi cha takriban miaka saba Dkt Ghassany alikuwa akija Tanga kwa mahojiano na Mzee Mkwawa na katika kipindi hicho Mzee Mkwawa alitupeleka Kipumbwi na Sakura na kutuonyesha sehemu zile ambazo walikuwa na kambi na wakifanya mazoezi ya kivita na matumizi ya silaha.
Mkahawa ambao wale wakata mkonge walikuwa wakila chakula cha usiku kabla ya kuvushwa kwa vyombo vya bahari kwenda Unguja bado upo hadi leo ingawa kwa sasa kijumba kile hakitumiki tena kama mkawaha. Endapo itakuja siku serikali ya Zanzibar itataka kuhifadhi historia ya Mapinduzi ya Zanzibar bila shaka moja ya vitu vitakavyokuwa katika makumbusho ni picha ya hicho kibanda.''