Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hapa anatakiwa Sheikh aingie Bungeni kama alivyo Mchungaji Msigwa. Tena sheikh awe mtu wa mbali kabisa na mfumokristo na BAKWATA.
 

Mbona jibu jepesi sana.

Hawa waliokuja kufanya mabadiliko katika jamii walikuwa kizazi cha
kwanza kuzaliwa Tanganyika.

Hawakupata kuijua nchi nyingine ila hii.

Mmojawapo ni babu yangu Salum Abdallah Mwekapopo Muyukwa
Samitungo.

Kitu kilichowafanya wao kuwa juu ni ile elimu waliyopata kutoka kwenye
shule za Wajerumani.

Kingine kuwa Wajerumani wakiwaenzi sana askari wake kwa hiyo ''social
standing'' ya wazee wetu ilikuwa juu kuliko mtu wa kawaida.

Mfano Kleist akizungumza Kijerumani na Kiingereza kaijua kupiga taipu na
kutuma ''morse signal'' akijua kuweka vitabu vya hesabu na matumizi ya
silaha mbalimbali.

Yote haya kafundishwa katika shule na jeshini.

Babu yangu Tabora Isevya alikuwa Mwafrika wa kwanza nyumba yake
kuwa na umeme, simu na bomba la maji.

Vitu kama hivi ndivyo vilivyowatambulisha katika jamii.

Hakika hii ni historia pia.

Sasa huwezi kuweka swali la dini pembeni khasa Uislam.
Kusema hivyo ni kufru.

Kubwa zaidi Wamanyema ni kabila la Waislam watupu na Dar es Salaam
walikuwa na jumuia yao Batetera Union na rais wake alikuwa Sheikh Hussein Juma.

Sasa kwa watu waliotoka bara kuja Dar es Salaam katika enzi zile ilikuwa lazima
wawe na heshima katika mila na utamaduni walioukuta mjini.
 
Wajerumani ni waDINI sana wale. Kleist alisoma na kuajiriwa vipi kule? Au wanae ndio waliouvaa Uislam ili wawapate mabinti wazuri wa Kimanyema?
 
Mkuu Mohamed Said sisi sote ni kama wewe sote tuna machungu, machungu haya yanatofautiana wengine wanalilia yaliyopita, wengine wanalilia yaliyopo na wengine wanalilia yajayo. Katika wale wanaolilia yaliyopita wanataka kutwambia waliyakosa kwa sababu....... Wale wanaolilia yaliyopo wanataka kuyatwaa sasa kwa sababu......... Wengi tunayalilia yajayo kwani yaliyopo tumeyakosa achilia mbali yale yaliyopita yote haya ni kwasababu........wenye meno wameshayala.

Tanzania ya leo ni jioni tulale tutaiona kesho tukiamka, tena tulale usingizi wa mang'amung'amu kwani kuna panya wala watu wasije tutafuna nyao za miguu yetu kwenda mbele tukashindwa. Ilitupasa sana kupigia kelele haya mauzo ya nchi, nchi yetu iko SOKONI bei yake ni siri ya MUUZAJI. Tunda hili limeiva vizuri kila MNUNUZI ANALITAKA. Nchi vipande vipande imegawanyika, ilitupasa tupigie hapo haya makelele WAUZAJI na WANUNUZI wapate KIMBIA watuachie NCHI YETU TANZANIA.
 
Je hampendi kujua nyaraka za Nyerere za enzi ya TAA na TANU
anazo nani hii leo?

Je hamtapenda kujua nini kilitokea baada ya uhuru Nyerere
alipoziomba zile nyaraka?

Wanaukumbi hamtaki kujua "kisa cha ugomvi wa nyaraka?"
Hamtapenda kujua walokuwa na nyaraka zile kwanini walikataa
kumpa Nyerere nyaraka zile za TAA na TANU?

Mkijifunga katika maswali ya kujibizana yale ya nipe nikupe

Mohamed,
Simulia basi juu ya hizo nyaraka. Na kwa nini Nyerere anyimwe nyaraka zake mwenyewe?
 
kwani hawajui hao? Ndio maana maaskofu wanapiga kelele wanaompinga wanaompinga nyerere

Acha kudandia dandia. Haya maswali tunayomuuliza MS ni yeye ndiye anayeweza kujibu kwa ufasaha na busara ya kiutu-uzima. Nyie mashabiki wake mnadandia dandia na mwishowe hata point za MS na zenyewe zinaonekana za hovyo. kaa kimya, ipo siku na wewe tutakutafutia maswali ambayo ni saizi yako.
 
Mzee wangu Mohamed Said,

Kwanza, kama mtu hawezi kuona uzito wa Oxbridge, haina haja kujibizana naye. Kitabu kinamiaka 15. Kimepitiwa na magwiji wa vyuo vikuu duniani. Lakini bado mtu kichwa chake kizito kutambua hilo

Pili, nimeuliza swali, je wale mnaompinga mzee wetu Mohamed Said na kitabu chake, wanakubali au wanakataa kuwepo kwa wazee aliyowataja katika kupigania uhuru wa Tanganyika? Hakuna jibu nimepata mpaka sasa

Tatu, Yericko Nyerere, umetupa ahadi ya kutaja majina ya wahaini ambao wamepewa ubalozi nje, mpaka sasa hakuna jibu.

Cc Ritz Do santos
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Mohamed Said, bado nakusubiri kujua nyaraka za Nyerere za enzi ya TAA na TANU,
anazo nani hii leo?
 

well stated,thank you
 
Mohamed,
Si kweli kwamba EAMWS ilipigwa marufuku Tanzania kwa sababu ilitaka kujenga chuo. Hili umelirudia mara kadhaa kwa dhana kwamba uongo ukirudiwa mara kwa mara watu wataanza kuamini kuwa ni kweli. EAMWS ilipigwa marufuku baada ya kuingilia mambo ya siasa. EAMWS ilitumika kuchanga fedha ili Nyerere aondolewe uongozi wa TANU. Hilo katu hautalisema. Zilichangwa fedha kwa ushawishi wa Tewa Said Tewa. Na pia hujataja mchango wa Adam Nasib. Unamfahamu huyu Muislamu mzalendo? Hujatuambia juu ya Iringa National Islamic Conference ya 1968. Hujataja kauli ya Sheikh Abeid Karume, makamu wa kwanza wa rais wa Tanzania, kwamba EAMWS ilikuwa inafuata siasa zinazopingana na TANU na AFP. na kuonya juu ya "religious pretenders from outside," na kuwataka uongozi wa Waislamu ukabidhiwe mikononi mwa watu wenyewe. Hebu tuambie ni waziri gani aliyetangaza Desemba 20 1968 kupigwa marufuku kwa EAMWS nchini Tanzania. Hakuwa Muislamu huyu?
 
Nacheka peke yangu.

Kwanini mnaamini kuwa ninazo taarifa hizo wakati nikikuwekeeni
habari za wazee wangu mnaita porojo?
 
Nimekutia hamu?
Vipi kuhusu nyaraka muhimu za kihistotria zilozotoweka?

Hutaki kujua vilevile?
 
Nacheka peke yangu.

Kwanini mnaamini kuwa ninazo taarifa hizo wakati nikikuwekeeni
habari za wazee wangu mnaita porojo?

Katika maelezo yangu huko nyuma nilisema wazi kuwa, kujua habari ni hatua moja, na kuamini habari hizo ni hatua nyingine.

Sisi tumekuomba utujuze, kazi ya kuamini tuachie wenyewe!
 
Hiyo ndiyo ilikuwa propaganda na uongo uliotengenezwa na akina Rashid Kayugwa
aliyekuwa akiongoza operesheni ile.

Huyu alikuwa mtu wa Usalama wa Taifa.

Iko siku akaisikia Qur' an inasomwa Allah anatoa ahadi zake kwa wale watakaosimama
kuipigania dini yake.

Nini yatakuwa malipo yao.

Na wale watakaompiga vita Allah nini utakuwa mwisho wao.

Kainamisha kichwa chini machozi yanambubujika.

Kakumbuka alowatendea askari wa Allah Sheikh Hassan bin Amir na Waislam walokuwa
pamoja na yeye.

Akajitazama hali yake.

Mfumo umemtumia kuhujumu Uislam kisha ukamtupa.

Kayugwa kabla hajafa akawaeleza Waislam fitna yote ile na wahusika wake.
Kisha akaomba Allah amuwie radhi kwa yale alotenda.

Ndugu yangu tunajua mengi sana.
 
Nyerere alikuwa Mkatoliki alieijenga tz kwa misingi ya kikatoliki
 
Katika maelezo yangu huko nyuma nilisema wazi kuwa, kujua habari ni hatua moja, na kuamini habari hizo ni hatua nyingine.

Sisi tumekuomba utujuze, kazi ya kuamini tuachie wenyewe!

Unaweza ukapewa. ukasema naomba tarehe. ukipewa tarehe unaweza ukasema naomba mtunzi. ukipewa mtunzi utasema nataka cover, ukipewa cover utasema jina la page. yaan utataka mtu mpaka mwisho wa dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…