Nguruvi nimekusoma lakini katika mpini wako nimegundua unachuki sana na wazanzibar kwasababu point zako zote kinachokukera ni kwanini kuna mgao unaotoka Tanzania bara na kwenda Zanzibar, hata wazanzibar wakisoma hii post yako watakushangaa sana lakini nisikupinge haya ni mawazo yako na ni haki yako ya kikatiba,katiba inasema kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.Tukiridi kwenye mpini wa Barubaru kunakitu hujajibu kama sijakosea alikuuliza ilikuwaje watu wakala ugali wa Yanga na ilikuwaje Nyerere alifeli masuala ya uchumi ni hayo tu kamanda.
Sheikh Farid, wznz hawana sababu za kushangaa, wanasababu za kujibu kama kilichoelelezwa ni uongo. Kwa taarifa yako nikupe kumbu kumbu kidogo kwamba wazanzibar wanakubaliana na hoja zangu.
1. Kitendo cha wao kulalamika kuwa wanaonewa na wakati huo huo wanataka kuwa na mkataba na Tanganyika ni kuelewa fika kuwa ndani ya muungano kuna mambo yanayowasaidia sana na hivyo kuiacha Tanganyika ni muhali.
2. Kiongozi wa kuvunja muungano Maalim Seif alipoulizwa na tume ya Warioba kwanini tusikutane EAC yeye alisema muungano wa EAC ni mparaganyiko hadi sasa afadhali huu wetu na pengine tutawavutia wengine kujiunga nao.
Hapa ni kuwa anatambua wazi kuwa huu muungano ni bora hata kama anataka znz ijitenge.
3. Maalim Seif ametofautiana na sera za chama chake za serikali 3 na kuendelea na na suala la mkataba.
Amekisaliti chama anachosimamia lakini usaliti wake una mipaka, kwamba si kuvunja muungano ni muungano wa mkataba.
Kuna kitu anakiona ambacho anakifahamu kupitia mkataba znz itanufaika na wala Si Tanganyika.
4. Katika kongamano la bwawani hotel mwaka 2012, aliyewakuwa waziri katika serikali ya muungano, na mwanachama wa baraza la mapinduzi sheikh Nassor Moyo alitamka katika kipaza sauti kuwa muungano unafaida hasa za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Huyu ndiye leo anaitwa fundi seremala kisa kasema muungano una faida.
5. Tarehe hiyo hiyo, Jusa Ladhu, mbunge nguli machachari aliyehudumia bunge na baraza la wawakilishi na katibu wa CUF visiwani alisema kuwa muungano una faida kwa wznz kiuchumi, kijiografia na kielimu.
6. Mansour Himid, kindaki ndaki mwingine wa znz huru naye katika siku hiyo alisimama na kupaza sauti dunia ikamsikia akisema muungano unahitajika na wala hawataki kuvunja bali kurekebisha.
7. Tume ya Wariona imekutana na wznz na ikafikia mahali kuna vurugu. Kisa ni kundi moja likitaka muungano na lingine likitaka sultan arejee kwa kupitia mlango wa uani. Hiyo ni hiari yao, ninachosema ni kuwa uwepo wa makundi hayo unaondoa hoja yako kuwa wazanzibar wakisoma...
8. Hivi karibuni, aliyekuwa waziri kiongozi na sasa waziri katika serikali ya muungano Shamsa vua akiongea na vijana wa CCM alisema muungano una manufaa hasa katika elimu ya juu, kijiografia na kusema mafuta ambayo znz inadhani yapo ni kujidanganya maana bara wameshaanza kuvuna, kwanini wao wznz wasiwe sehemu ya uvunaji huo.
9. Rais Shein amekaririwa akisema muungano unasaidi sana znz hasa suala la ulinzi na usalama na elimu ya juu.
Akaonya matatizo yatakayotokana na kuvunjika kwa muungano.
Sasa makundi na watu hao kama wanasema nadhani ni wznz, hizi tofauti za rangi wanazijua wao.
Vinginevyo utasikia kila anayepinga muungano ni kibaraka kwasababu tu Seif kasema hata kama yeye ameshachukua kitambulisho cha muungano.
Nimeweka mambo machache ambayo mznz anaitegemea Tanganyika, nadhani tupitie moja baada ya jingine ili kuthibitisha ukweli au uongo kuliko kushangaa.
Ima wzn wanaweza kunishangaa kwasababu watajiuliza haya yote yamejulikanaje ili hali ilikuwa ni siri yao.
Kuhusu suala la njaa, nadhani kuna upungufu mkubwa wa weledi.
Mwaka 1974(sikumbuki vema) kulikuwa na njaa iliyoleta kitu kinaitwa kilimo cha kufa na kupona.
Ethiopia iliwahi kupata njaa na aliyeisalimisha mbele ya uso wa dunia ni al marhum Mohmed Amin aliyefariki kwa ajali ya ndege kule Comoro. Huyu ndiye aliionyesha dunia njaa inavyoua kule Somalia.
Mwaka juzi na jana njaa ilipiga Kenya hadi ikabidi waombe msaada wa chakula kutoka Tanzania.
Nakumbuka waziri wao alimfuata JK kule Maramba kuongea juu ya suala hili.
Malawi ilipata njaa ambayo ilibidi UN iingilie kati. Moja ya mashirika yaliyoteuliwa kusamabaza chakula ni S.S.Bkahresa.
Marekani ilikuwa na njaa mwaka jana na kufanya bei ya vyakula iongezeke.
Hali ndiyo hiyo duniani kote kuanzia mashariki hadi magharibi.
Sasa kama hoja ya Barubaru ni kuwa njaa ni kushindwa kiuchumi, nadhani nchi za jirani kama Kenya, Ethiopia, Malawi na hata Zimbabwe zimeshindwa kiuchumi. Lakini haishii hapo, je, kukiwa na balaa la njaa mahali hiyo inatosha kuwa kigezo cha kushindwa kiuchumi?
Na muhimu zaidi ni kuwa katika marais waliofuata baada ya Nyerere, nani amefanya kitu tofauti ambacho tunaweza kusema amezuia njaa.
Pengine Mkapa na Keenja walijaribu kuwa na national reserve ingawa hiyo ni bandeji na wala si matibabu.
Matibabu ni Irrigation, sasa Mwinyi, Mkapa na Kikwete combine wamefanya kitu gani ambacho Nyerere hakukifanya hasa ukizingatia kuwa wao waliikuta nchi ambayo Nyerere kajenga misingi ya baadhi ya mambo.
Misingi hiyo ni stable country as compared to our neighbors, miradi kama ya umeme wa mabwawa, miundo mbinu, huduma za afya na elimu.
Vyote hivyo havijafanywa katika kiwango cha Nyerere kwa utawala wa Mkapa, Mwinyi na Kikwete combine katika miaka zaidi ya 27.
Nadhani umeeelewa.