Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Barubaru, wewe ni fundi sana wa kukimbia hoja.

Kwanza, ile ya Nyerere Mkuu Jasusi atakapoamka atakuja na zana, huwa sina shaka na maudhui yake. Tuliweke kiporo

Pili, nimekuuliza taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migogoro. Umekaa kimya.
Pengine unaunga mkono zile za Sharrif Ritz, endapo ni hivyo basi thibitisha ili tuendelee kuanzia hapo

Tatu, nimekuambia kuwa:
a) Zanzibar haina bajeti ya ulinzi na usalama tangu mwaka 1964. Kataa au kubali
b)Haina bajeti ya elimu ya juu tangia wakati huo. Kataa au kubali
c)Mishahara ya wastaafu inalipwa kutoka hazina Dar. Kataa au kubali
d) Mishahara ya SMZ inatoka Tanganyika. Kataa au kubali
e)Kwamba, wazanzibar hawajui gharama za huduma kama umeme. Kataa au kubali
f) Kwamba bajeti ya znz ni billion 630, mapato ni bilioni 120 pengo la bilioni 510 linazibwa na bajeti ya Tanganyika.
g)Kwamba ofisi ya makamu wa rais muungano inapewa hela tu(billion 32) kwa znz . Kataa au kubali
h) Kwamba znz inapata 7% ya mgao wa pato la taifa kwa kuchangia ''0'' katika pato hilo. Kataa au kubali

Sasa kama una hoja nyingine ya mgao, huu ni ukumbi iweke wazi. Hili la kusema kuna taarifa za siri si kweli.

Hoja ndizo hizo hapo juu. Ima ukabiliane nazo au ukunje jamvi kwa upande mmoja, upande mwingine ubaki ukisoma

Asante sana mkuu kwa hoja hizi mujarabu!
 
Haiwezekani,haingii akilini hata kidogo,
Mtu mzima na akili zake atoke zake kuoga na kuingia nyumba ya bui bui kubadilishia nguo zake huku akitaraji wapita njia na jirani zake wasiione aibu yake,hilo haliwezekani hata kidogo...

Kwenye bandiko lako hili kwa mtu mwenye akili timamu anang'amua wazi wazi mantiq yako..!

Pole sana...
Mkuu THE BIG SHOW, sasa hapa mchango wako ni nini sasa? sijaona ukizichambua hoja hata moja!
 
Nguruvi3,

Awali ya yote nimesikitika sana timu yangu Simba kufungwa na Yanga 2-0. lakin yote ndio mpira kuna kufunga na kufungwa. Ni wakti wa Malkia wa Nyuki na Ismail Aden Rage kujipanga upya kwa ajili ya ligi.

Mimi binafsi kama mchumi naweza kumchambua Nyerere kiuchumi zaidi kuwa ALIFELI vibaya sana na hali zote mlizonazo pamoja na rasilimali zote mumezidi kuwa masikini sababu ni SIASA za Nyerere.

Nitakupa ushuhuda nikiwa wizara ya fedha kuna fedha alikuwa analazimishwa zipelekwe kwa wapigania uhuru wa Swapo na ANC wakti wananchi wa Tz wakiwa wanakula unga wa yanga. kwa hiyo utaona alipenda sana kujipendekeza kwa nchi za nje na kulaza wananchi yake na njaa na majanga.

Alikuwa TAJIRI wa siasa lakin masikini wa uchumi na hivyo kukosa uzalendo wa kuweza kuinua uchumi wa nchi yake.

Ni yeye aliasisi Rushwa na Ulanguzi kutokana na siasa zake kiasi cha kufanya raia wake waishi kwa taabu na dhiki kubwa kukesha kwenye foleni za hata sabuni zakufulia na kuogea achilia mbali unga, mchele na maharage.

Alipiganisha vita vya Uganda kwa nia ya kumrejesha Rafiki yake Obote madarakani na kuuwa kabisa uchumi wa nchi yake na kuwaongpea mfunge mikanda ya kiuchumi kwa miezi 18 jambo ambalo ameshindwa kuwaeleza mfungue mikanda hiyo mpaka anakwenda kaburini.

Kwa vigezo hivyo nashawishika kusema kuwa hakuwa MZALENDO kwa taifa lake bali alipenda kupewa sifa binafsi.

sasa naomba uniainishie uzalendo wake uko wapi

Nguruvi nilikuwa naomba jibu huu mpini wa al Akh Barubaru je bwana mkubwa Nyerere aliyafanya hayo au utasema ni ngano za watoto wa madrasa.
 
Sawa Mzee MS; Nakukumbusha ni WEWE ULIMWONYESHA Abdul Sykes akimsengenya Nyerere kwa Swahiba wake (Mwapachu) kuwa WANGEMWACHIAJE CHAMA MTU WASIYEMJUA. Then Abdul anagombea. Then, mtoto wa mjini mwenye Benz na heshima ya wana Dar, LOST (Labda; check orodha ya voters, for Catholics!!!) Wapo wengine pia hapo awali walimwomba Nyerere kugombea kwa kumuona anafaa na kwa kuona tangu Vedasto Kyaruzi aondoke, chama kilikuwa kinadorora (Msome Seaton-wewe hujaandika). Soma yule meneja wa Arnatoglu Hall (Phombe???) anavyohaha chama kiongozwe na Julius.

Mzee MS,somewhere in life you must face it; that your Abdul was not only a backbiter but also a bad loser. No president would have kept a backbiter and double dealer in his cabinet (as you have shown him yourself!!!!) If he was any good and trustworthy as you have trumpeted in this forum, he could have not fallen from grace for others. That is the bottom line.

Wickama,
Nilipata kukueleza maana ya kusengenya katika Uislam.

Lakini inaelekea unapendezwa na kutia farka baina ya wahisani hawa wawili.
Hilo la kwanza.

Pili maneno yale ya kutoa chama kwa mtu wasiyemjua vyema alimweleza
Tewa Said Tewa si Hamza Mwapachu.

Achana na historia za Wazungu.
Mimi nakueleza maneno kutoka kwa wenye TANU yao.

Kuanzia 1950 TAA ikiwaka moto kwa yale walofanya.
Walianza na Constitutional Development Committee kwa Gavana Twining.

Ikaja safari ya Abdu Nairobi kuunganisha nguvu na Kenyatta na KAU.
Hii ilikuwa sambamba na kampeni ya kuwahamasisha wananchi majimboni
kuiunga mkono TAA.

Ikafatia safari ya Japhet Kirilo na Earle Seaton UNO 1952.

Zikaja contact na Kenneth Kaunda na Henry Nkumbula na safari ya Ally Sykes
na Dennis Phombeah Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru.

Haya yote yalisababisha wakoloni kutoa Government Circular No. 5 na 6 mwaka
1953 kuionya TAA kuwa inaingilia siasa za Tanganyika.

Hii si dalili ya chama kudorora.
Yako mengi.

Chama kilidorora 1953 mara tu Nyerere alipochukua uongozi
Alonambia haya ni Dossa Aziz.

Ukipenda nitaeleza mkasa wote In Sha Allah.

Hayo mengine ya roho mbaya ya Abdu sintoyajibu.
Wenyewe kwa wema alokuwanao walimpa jina la kupanga "The Sweet Abdu.

Una uhuru na haki ya kuamini historia uipendayo.

Mimi hapa nawapa darsa hawa watazamaji 180,000 ambao hawajapatapo kusikia
historia hii ya wazee wangu.
 
Ritz, watu wanaoishi Misiri, Libya,Algeria na Morocco ni waafrika? Je nchi hizo ni zakiafrika? ili uwe muafrika nilazima utimize vigezo gani? Serikali ya nyerere iliwateua akina Brayson na Jamal kuwa mawaziri, je hawa walikuwa waafrika? je kunatofauti kuwa Mtanganyika/Mtanzania na kuwa Muafrika?
haya ni yale baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.......
wakishinda hawa waafrika ni wakaskazini pekee
 
Mkuu THE BIG SHOW, sasa hapa mchango wako ni nini sasa? sijaona ukizichambua hoja hata moja!

Mimi nakesha hapa 24/7 na ikibid hata 365 kunyonya elimu kutoka kwa Moh Said na wengineo,na kuwabeza wengine wote wanaozuia na kukejeli elimu hii inayomwaga hapa bila tozo bila mashartii...
 
Wickama,
Nilipata kukueleza maana ya kusengenya katika Uislam.

Lakini inaelekea unapendezwa na kutia farka baina ya wahisani hawa wawili.
Hilo la kwanza.

Pili maneno yale ya kutoa chama kwa mtu wasiyemjua vyema alimweleza
Tewa Said Tewa si Hamza Mwapachu.

Achana na historia za Wazungu.
Mimi nakueleza maneno kutoka kwa wenye TANU yao.

Kuanzia 1950 TAA ikiwaka moto kwa yale walofanya.
Walianza na Constitutional Development Committee kwa Gavana Twining.

Ikaja safari ya Abdu Nairobi kuunganisha nguvu na Kenyatta na KAU.
Hii ilikuwa sambamba na kampeni ya kuwahamasisha wananchi majimboni
kuiunga mkono TAA.

Ikafatia safari ya Japhet Kirilo na Earle Seaton UNO 1952.

Zikaja contact na Kenneth Kaunda na Henry Nkumbula na safari ya Ally Sykes
na Dennis Phombeah Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru.

Haya yote yalisababisha wakoloni kutoa Government Circular No. 5 na 6 mwaka
1953 kuionya TAA kuwa inaingilia siasa za Tanganyika.

Hii si dalili ya chama kudorora.
Yako mengi.

Chama kilidorora 1953 mara tu Nyerere alipochukua uongozi
Alonambia haya ni Dossa Aziz.

Ukipenda nitaeleza mkasa wote In Sha Allah.

Hayo mengine ya roho mbaya ya Abdu sintoyajibu.
Wenyewe kwa wema alokuwanao walimpa jina la kupanga "The Sweet Abdu.

Una uhuru na haki ya kuamini historia uipendayo.

Mimi hapa nawapa darsa hawa watazamaji 180,000 ambao hawajapatapo kusikia
historia hii ya wazee wangu.

Mzee MS; Shukran kusahihisha ni Tewa, Yes. Lakini suala liko palepale, TUTAMWACHIAJE CHAMA MTU TUSIYEMJUA? This is backbiting. No pretense. Wakati huohuo ulimwonyesha pia kama mtu aliyependa chama kipate wasomi!!!! Kwa contradiction ya hizi scenes mbili unless Abdul alitaka wasomi ANAOWAJUA. Looks like this "sweet Abdul" had a problem after all, in fact hinted from your own book. Kama ile country-wise mobilization na criss crossing ya kina Nyerere hadi ana sacrifice kazi yake (1st Masters holder among Tanganyika Africans) hadi kuwa TANU hadi kupata uhuru through chama hicho ni kudorora, pia ni haki yako kuamini. BUT, this is where you at the lowest of the positions as a scholar, simulizi la MTU MMOJA (Dossa Azziz) tayari ni historia ya institution, TAA na TANU hakuna verification. Why verify given the amount of HATE you have over Nyerere and his religious orientation?

Well, we must face it now, this Sweet Abdul failed to make it into government despite his TANU card number 3 etc. Why? and strangely, his family happily still rolls in the corridors of power in this country with respect and fun. Looks like, this sweet Abdul had some problems after all. In fact the first hints are right in your book!!!!
 
Barubaru, wewe ni fundi sana wa kukimbia hoja.

Kwanza, ile ya Nyerere Mkuu Jasusi atakapoamka atakuja na zana, huwa sina shaka na maudhui yake. Tuliweke kiporo

Pili, nimekuuliza taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migogoro. Umekaa kimya.
Pengine unaunga mkono zile za Sharrif Ritz, endapo ni hivyo basi thibitisha ili tuendelee kuanzia hapo

Tatu, nimekuambia kuwa:
a) Zanzibar haina bajeti ya ulinzi na usalama tangu mwaka 1964. Kataa au kubali
b)Haina bajeti ya elimu ya juu tangia wakati huo. Kataa au kubali
c)Mishahara ya wastaafu inalipwa kutoka hazina Dar. Kataa au kubali
d) Mishahara ya SMZ inatoka Tanganyika. Kataa au kubali
e)Kwamba, wazanzibar hawajui gharama za huduma kama umeme. Kataa au kubali
f) Kwamba bajeti ya znz ni billion 630, mapato ni bilioni 120 pengo la bilioni 510 linazibwa na bajeti ya Tanganyika.
g)Kwamba ofisi ya makamu wa rais muungano inapewa hela tu(billion 32) kwa znz . Kataa au kubali
h) Kwamba znz inapata 7% ya mgao wa pato la taifa kwa kuchangia ''0'' katika pato hilo. Kataa au kubali

Sasa kama una hoja nyingine ya mgao, huu ni ukumbi iweke wazi. Hili la kusema kuna taarifa za siri si kweli.

Hoja ndizo hizo hapo juu. Ima ukabiliane nazo au ukunje jamvi kwa upande mmoja, upande mwingine ubaki ukisoma

Nguruvi3,

Ahali yangu siku zote jitahidi kuongea kwa FACT na kama zipo DATA basi ni vizuri kuzitumia.

Kwa sababu kuna wataalamu wenu wenyewe wanaolifanyia kazi basi nakupa PITIA RIPOTI ya mwaka 2010/2011 na 2011/2012 za JOINT FINANCE COMMISSION utagundua maneno yako yamesimamia wapi. Nakurahisishia pitia kwenye mtandao ipo website yao na kama unataka nakurahisishia kabisa afisi zao zipo pale SUKARI HOUSE posta dar es salaam.

Nafikiri hapo nimekurahisishia kabisa na kama utahitaji zaidi sema maana naogopa kusema mimi utasema nimekuongopea ni bora upitie taarifa zao na linganisha na maneno yako.

taarifa hizo zimeandikwa na wataalamu kutoka nchi hizo mbili zenye hisa katika BOT.

Suala la kwanza namsubiri kwa hamu jibu lako.

Ukisikia kuweweseka ndiyo huku, Mag3 kaleta jedwali lenye data ulizotuhumu kuwa si za kweli. Sasa wewe ilibidi uje na jedwali lako lenye data za kweli kupinga hoja kwa hoja. Badala yake umekurupukia name calling na accusations zisizo na mashiko. Let me tell u something openly inaonekana unasumbuliwa na kaugonjwa ambako ni mix ya ulimbukeni na inferiority complex. I could be wrong but that is the way I see it. Ndiyo maanna badala ya kujibu hoja kwa hoja lazima ulete ngoonjera ndefu ya historia ya maisha yako, familia yako which is just a b.l shyt. Lakini nadhani hiyo ndiyo namna unafikiri itafanya hoja zako ziaminike and there goes my point. You are the very person who claim to be ridiculed kwa sababu ya dini yako kwamba oooh wanywa kahawa, madrassa, na upuuzimwingine. Cha kushangaza wewe mwenyewe ni bingwa wa kuridicule others almost in every post unayotuma. Jibu hoja kwa hoja usilete vioja.

Halafu jingine naona mbonyezo like huwa unakuwewesesha mno, anyway utazoea taratibu. Demokrasia ya JF inaruhusu mtu yeyote ku-like post yeyote and they are entitled to their own reasoning.

Tuvalu

[h=3]EUROPA - European Countries - Luxembourg[/h]
[h=3]Brunei [/h]
 
Ritz, watu wanaoishi Misiri, Libya,Algeria na Morocco ni waafrika? Je nchi hizo ni zakiafrika? ili uwe muafrika nilazima utimize vigezo gani? Serikali ya nyerere iliwateua akina Brayson na Jamal kuwa mawaziri, je hawa walikuwa waafrika? je kunatofauti kuwa Mtanganyika/Mtanzania na kuwa Muafrika?

Hilo swali waulize kina Mag3, na wenzake wanaosema kuna waafrika wa Zanzibar.
 
Wickama,
Nilipata kukueleza maana ya kusengenya katika Uislam.

Lakini inaelekea unapendezwa na kutia farka baina ya wahisani hawa wawili.
Hilo la kwanza.

Pili maneno yale ya kutoa chama kwa mtu wasiyemjua vyema alimweleza
Tewa Said Tewa si Hamza Mwapachu.

Achana na historia za Wazungu.
Mimi nakueleza maneno kutoka kwa wenye TANU yao.

Kuanzia 1950 TAA ikiwaka moto kwa yale walofanya.
Walianza na Constitutional Development Committee kwa Gavana Twining.

Ikaja safari ya Abdu Nairobi kuunganisha nguvu na Kenyatta na KAU.
Hii ilikuwa sambamba na kampeni ya kuwahamasisha wananchi majimboni
kuiunga mkono TAA.

Ikafatia safari ya Japhet Kirilo na Earle Seaton UNO 1952.

Zikaja contact na Kenneth Kaunda na Henry Nkumbula na safari ya Ally Sykes
na Dennis Phombeah Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru.

Haya yote yalisababisha wakoloni kutoa Government Circular No. 5 na 6 mwaka
1953 kuionya TAA kuwa inaingilia siasa za Tanganyika.

Hii si dalili ya chama kudorora.
Yako mengi.

Chama kilidorora 1953 mara tu Nyerere alipochukua uongozi
Alonambia haya ni Dossa Aziz.

Ukipenda nitaeleza mkasa wote In Sha Allah.

Hayo mengine ya roho mbaya ya Abdu sintoyajibu.
Wenyewe kwa wema alokuwanao walimpa jina la kupanga "The Sweet Abdu.

Una uhuru na haki ya kuamini historia uipendayo.

Mimi hapa nawapa darsa hawa watazamaji 180,000 ambao hawajapatapo kusikia
historia hii ya wazee wangu.

safi sana MS mungu akubariki sisi tupo hapa kujua yaliofichwa yeye hata kama hatopenda ni bora kuelezea tu kwa faida ya wanajamvi.
 
Moja ya mambo ambayo mda mwingi nilikushauri ndugu yangu ni hilo la kuamini kila ulichoambiwa bila kufanya utafiti binafsi au shirikishi!

Tangu mwaka 1948 hadi 1953 TAA hakikuwa chama cha siasa kimantiki, kilikuwa ni chama cha harakati za haki za mwafrika wa Tanganyika,

Hilo linapatikana katika filosofia yake!

Baada ya Uchaguzi wa 1953 Anartoughulo Mnazimmoja na Mwalimu Nyerere kushika hatamu za uongozi wa TAA, chama kilianza kubadili filosofia yake kutoka kuwa cha harakati za kudai haki za weuzi, na kuwa cha harakati za ukombozi wa Tanganyika-Chama cha siasa!

Kutokana na mageuzi hayo yaliyokuwa ilikuwa ni lazima chama kibadili jina ilikiwiane na ideology yake, hivyo kikaitwa TANU!

Sasa ndugu yangu upotoshaji unaofanya katika hilo sioni sababu yake,

Kusema TAA iliyumba baada ya Mwalimu kushika madaraka ni uongo
 
Raha ya JF wakati mwingine tunaburudishana. Ngoja tupate ushairi wa T Mvungi katika kitabu chake cha CHACHUNGU TAMU, Shairi linaloitwa Unaosema ATWANA wakiamka, mjanga yu mashakani.

Kumezuka mkatao,Miaka ya thamanini,
Watu wafanya jutio,Hawasemi chini chini,
Hawasemi tena ndio,Haitoki midomoni,
Wamevumilia sana Mwisho wa uvumilivu.

Shangilio zimekwisha, Miguno imeenea,
Wasema eti ya tosha, Nguvu zimetuishia,
Miaka yakupotosha, ishirini yatimia,
Watwana wakiamka, Mjanja yu mashakani.

Na wengi walitambua, Ukweli uliofichika,
Wongo wameugundua, Hasira zimewawaka,
Hapo sasa fikiria, hilo lake patashika,

Yericko Nyerere,

Kila siku nakuanbia wewe ni mtupu sana sana kwenye historia ya Tanganyika huna unachokijua kwenye AA, TAA, TANU, unachotakiwa upinde mgongo usomeshwe historia unajipunja mengi sana kutoka kwa Mohamed Said.

Hebu msome Nyerere mwenyewe hapa chini sijui wewe na Nyerere nani anasema kweli na nani muongo wapi Nyerere kasema walianzisha chama cha harakati za mwafrika...
Julius Nyerere

'"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Moja ya mambo ambayo mda mwingi nilikushauri ndugu yangu ni hilo la kuamini kila ulichoambiwa bila kufanya utafiti binafsi au shirikishi!
Nadhani wewe ndiyo unatakiwa ufanye utafiti kabla ya kuandika hebu tuendelee kumsoma Nyerere mwenyewe hapa chini...

Julius Nyerere.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Baada ya Uchaguzi wa 1953 Anartoughulo Mnazimmoja na Mwalimu Nyerere kushika hatamu za uongozi wa TAA,
Hebu msome tena Nyerere hapa chini anavyoelezea harakati zake za kisiasa pamoja na wazee wetu ambao walikuwa na mahaba makubwa na Nyerere ingawa wewe unawaletea kejeli na dhihaka na kuwaita wazee wa vibarazani tu....

Julius Nyerere.
Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?
Mohamed Said, wala alazimishi umma wamuamini hata Nyerere mwenyewe anasema hebu msome hapa chini. hapa wanaukumbi tulizaneni mumsome vizuri Nyerere.

Julius Nyerere.

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, "Twining (Twainingi) umekwisha!" (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."'

Hizi picha za wazee wetu wakionyesha sura za bashasha pamoja na Nyerere, Sheikh Takadir kushoto kwa Nyerere kavaa kanzu na kofia kashika fimbo yake...
11.jpg

Hapa Wazee wapo uwanja wa ndege wakumuaga Nyerere akielekea UNO.
nyerere_departing_for_UNO.jpg
 
Raha ya JF wakati mwingine tunaburudishana. Ngoja tupate ushairi wa T Mvungi katika kitabu chake cha CHACHUNGU TAMU, Shairi linaloitwa Unaosema ATWANA wakiamka, mjanga yu mashakani.

Kumezuka mkatao,Miaka ya thamanini,
Watu wafanya jutio,Hawasemi chini chini,
Hawasemi tena ndio,Haitoki midomoni,
Wamevumilia sana Mwisho wa uvumilivu.

Shangilio zimekwisha, Miguno imeenea,
Wasema eti ya tosha, Nguvu zimetuishia,
Miaka yakupotosha, ishirini yatimia,
Watwana wakiamka, Mjanja yu mashakani.

Na wengi walitambua, Ukweli uliofichika,
Wongo wameugundua, Hasira zimewawaka,
Hapo sasa fikiria, hilo lake patashika,
Watwana wakiamka, Mjanja yu mashakani.

Nimekusoma mkuu naona umeenda kwenye fani yangu ila utamu umeukatisha kwa uchache wa beti
 
Mimi nakesha hapa 24/7 na ikibid hata 365 kunyonya elimu kutoka kwa Moh Said na wengineo,na kuwabeza wengine wote wanaozuia na kukejeli elimu hii inayomwaga hapa bila tozo bila mashartii...

kama unanyonya elimu usiishie kubeza yale usiyokubaliana nayo,pinga kwa kutoa hoja ili tunaojifunza tupate kitu,ikiwa huna hoja ishia kusoma ni busara zaidi.
 
Kuna habari za kusikitisha ukumbini nadhani Mohamed Said, atatuelezea Inshaalah.
 
Raha ya JF wakati mwingine tunaburudishana. Ngoja tupate ushairi wa T Mvungi katika kitabu chake cha CHACHUNGU TAMU, Shairi linaloitwa Unaosema ATWANA wakiamka, mjanga yu mashakani.

Kumezuka mkatao,Miaka ya thamanini,
Watu wafanya jutio,Hawasemi chini chini,
Hawasemi tena ndio,Haitoki midomoni,
Wamevumilia sana Mwisho wa uvumilivu.

Shangilio zimekwisha, Miguno imeenea,
Wasema eti ya tosha, Nguvu zimetuishia,
Miaka yakupotosha, ishirini yatimia,
Watwana wakiamka, Mjanja yu mashakani.

Na wengi walitambua, Ukweli uliofichika,
Wongo wameugundua, Hasira zimewawaka,
Hapo sasa fikiria, hilo lake patashika,
Watwana wakiamka, Mjanja yu mashakani.

Hehee safi mkuu,
 
Yericko Nyerere,

Kila siku nakuanbia wewe ni mtupu sana sana kwenye historia ya Tanganyika huna unachokijua kwenye AA, TAA, TANU, unachotakiwa upinde mgongo usomeshwe historia unajipunja mengi sana kutoka kwa Mohamed Said.

Hebu msome Nyerere mwenyewe hapa chini sijui wewe na Nyerere nani anasema kweli na nani muongo wapi Nyerere kasema walianzisha chama cha harakati za mwafrika...
Julius Nyerere

‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Nadhani wewe ndiyo unatakiwa ufanye utafiti kabla ya kuandika hebu tuendelee kumsoma Nyerere mwenyewe hapa chini...

Julius Nyerere.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Hebu msome tena Nyerere hapa chini anavyoelezea harakati zake za kisiasa pamoja na wazee wetu ambao walikuwa na mahaba makubwa na Nyerere ingawa wewe unawaletea kejeli na dhihaka na kuwaita wazee wa vibarazani tu....

Julius Nyerere.
Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Mohamed Said, wala alazimishi umma wamuamini hata Nyerere mwenyewe anasema hebu msome hapa chini. hapa wanaukumbi tulizaneni mumsome vizuri Nyerere.

Julius Nyerere.

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."’

Hizi picha za wazee wetu wakionyesha sura za bashasha pamoja na Nyerere, Sheikh Takadir kushoto kwa Nyerere kavaa kanzu na kofia kashika fimbo yake...
11.jpg

Hapa Wazee wapo uwanja wa ndege wakumuaga Nyerere akielekea UNO.
nyerere_departing_for_UNO.jpg

Kwa bahati mbaya sana, historia unaisimulia kwa hisia kinyume na historia hiyo inavyotakiwa kusimuliwa!

Historia hutembea na huishi kwa fact na sio hisia!

Hata uwezo wakutafsiri hiyo hotuba mpaka leo tangu ilipowekwa hapa januari umeshindwa kijana?

Narudia tena kukusihi, itendee haki jf,

Elimu yote liyoipata katika uzi huu ninakushangaa isipokuwa na mafaa kwako!
 
i

Hao wanajeshi je unajua wote walifukuzwa. Huyo wa Air force ngerengere alifukuzwa na wa china japo alikuwa mahiri sana kuongea kichina.Uliza utaelezwa.

Na hao wengine wote kama walipata degree basi wamepata degree zao baada ya baba yao kuondoka madarakani.Lakin jiulize je walisoma skuli gani za Sc na kama yupo aliyewahi kwenda High sch skuli gani?

Naomba uchunguze hilo kisha nikosoe kama nitakuwa nimenena uwongo

usitake niseme meng

The issue si kufukuzwa jeshini. The issue ni Nyerere kutosomesha watoto wake kama ulivyodai. Nakupa ushauri wa bure. Kama huna hakika na jambo afadhali unyamaze kuliko kujidhalilisha mbele ya kadamnasi kwa kusema vitu ambavyo huna hakika navyo. Anna Amesoma Carlton University, Canada mwaka 1975. Nyerere alikuwa ameondoka mamlakani wakati huo? Na Makongoro je? Magige? Madaraka? Uliwasomesha wewe baada ya Nyerere kutoka mamlakani? Andrew amesoma pale Aga Khan kabla haijabadilishwa jina na kuitwa Tambaza. Watoto wote wa Mwalimu wamesoma shule za sekondari za Tanzania. Kuna watu hapa wamesoma nao watajitokeza wakwambie. Unaniambia mimi nichunguze? Nichunguze kitu ambacho nakifahamu asilani? Nakupa ushauri wa bure. Kama huna hakika na jambo, ama uliza au kaa kimya kuliko kujiaibisha mbele ya kadamnasi kwa uwongo wa mchana kweupe.
 
Back
Top Bottom