gombesugu, sitaweza kutoa majibu kwa maswali yote uliyoniuliza kwa sababu tu ya muda; wakati mwingine majukumu mengine yanatutinga. Usione ajabu
Mag3 kuonekana yuko "
on line" ukafikiri nipo muda wote, hapana, wakati mwingine sihangaiki hata ku"
sign out" kwa sababau sitaki taabu ya ku"
log in and out" ninapopata kamuda ka kuchungulia humu.
gombesugu said:
Napenda kukuuliza masuali japo kiduchu. Wakati Mtume Muhammad na Allah walipokua anatukanwa kwa maneno machafu yaso kiasi wewe binafsi uliandika chochote japo kukemea au kumstaajabu huyo mtukanaji!?
gombesugu, labda huna muda mrefu ndani ya jukwaa hili lakini hayo mambo ya kukashifiana katika imani zetu
please count me out. Ninao ndugu na marafiki wa karibu sana ambao si wa imani yangu na nisingependa kujiingiza katika malumbano yanayoweza kuathiri mahusiano yetu. Hata hivyo nafurahi sana kwamba katika huu mjadala pamoja na kujua msimamo wangu na kuyasoma maandishi yangu, wananiunga mkono kwa kupinga upotoshaji unaofanywa na baadhi ya Watanzania wakisukumwa zaidi na chuki zao walizorithi kutoka kwa wazee wao. Wanatambua kwamba hujuma na ufisadi uliotamalaki nchini na unaotudidimiza kama taifa hauna rangi, dini, ukabila wala jinsia. Bahati mbaya wapo wenzetu ambao wameamua kutumia kalamu zao kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu kwa mgongo wa dini...hawa lazima wapigwe vita bila kujali ni wa dini gani, Al Akhiy
Mohamed Said akiwa ni mmoja katika watu hao hatari.
gombesugu said:
Mtu mzima mwenzio Sheikh Mohammed Said anapotukanwa na kupewa kashfa za hali ya juu na vijana ambao wengine labda yaweza kuwa hata ni wajukuze,wewe ulishawahi kukemea!? Mifano kadhaa,ni kwamba wewe binafsi unajumuika nao au kuanzisha hilo zogo dhidi ya Sheikh mohammed.
Mimi ni mtu wa kwanza humu jamvini kumwita
Mohamed Said mpuuzi kwani pamoja na kujua hatari ya mbegu anayojaribu kuipandikiza, anashindwa kutambua madhara yake. Kwa sasa tunaanza kuona hizo mbegu zikichipua...kwa mfano, ukipata muda ukasikiliza mahubiri ya Sheikh Ilunga au Sheikh Ponda, utadhani wanasoma neno kwa neno aloandika huyo Al Akhiy. Mimi pia ni mtu wa kwanza humu jamvini kumwita Mohamed Said mchochezi na muongo kwani pamoja na kuhubiri chuki, hata siku moja hajawahi kushiriki wanafunzi wake wanapotekeleza kwa vitendo hizo sera zake za chuki.
Bahati mbaya watetezi wakubwa wa mahubiri yake ya uongo, wanakesha humu wakitudhihaki wengine eti mbona hatuandiki vitabu? Pamoja na kutoa data kuonesha kuwa maandishi yake siyo sahihi, utetezi unaotolewa ni wa kunukuu hayo hayo maandishi yake tunayoyapinga. Wapo ambao wako humu wakidai wanafyonza ilmu, lakini cha ajabu ni kama vile wamejifungia ndani ya box na elimu tunayoitoa kwa maandishi kupinga madai potofu ya mwalimu wao, je hawayaoni na kuyasoma?
gombesugu said:
Kuhusu baadhi yenu, kuhisi yakuwa kila anaemkubali Sheikh Mohammed ni mbumbumbu na hajui atendalo; nilishawahi kujitetea. Sina sababu ya kujichosha au kukuchosha wewe pia kwa kujieleza.Tafadhali kipata fursa pitia bayana zangu za awali japo kiduchu. Lakini kwa kifupi tu,kwangu mimi hiyo itakua ni kinyume na dasturi yangu na pia kinyume na maadili ya taratibu za kibarua/field yangu.
gombesugu, mimi ni mmoja wa watu waliokukaribisha ulipojiunga na JF tarehe
4th April 2013, hadi sasa unatimiza mwezi moja na nusu, kwa kuamini kuwa ungesimamia ukweli na kuutetea bila woga. Nadhani wakati huo hukufahamu kuwa iko dhana imepadikizwa humu kwamba asiyekubaliana na Al Akhiy
Mohamed Said bado hajakamilika kiimani. Nina ushahidi wa Waislaam tena safi tu ambao badala ya kutulia na kufyonza ilmu anayotoa mwalimu wakajaribu kuyakosoa, looo! Eti wanaoiendesha serikali wanatekeleza maagizo ya Kanisa, BAKWATA inaendeshwa kwa mfumo Kristo, wakuu wote wa idara nyeti za serikali wana utii kwa mfumo Kristo...!
gombesugu, hata mara moja wewe hujawahi kumpinga huyu bwana, je si kweli? Huo uthubutu huna Al Akhiy!
gombesugu said:
Unajua jana kule kwenye ile Thread ya "CCM imeshindwa kulinda tembo hata Kiswahili"? Niliona mchango wako kiduchu. Lakini mbona ZeMarcopolo alipotoa hoja kuhusu vijana wa Bavicha;wewe badala ya kumjibu kwa ustaarabu na utulivu kama mtu mzima na mmojawapo ya waadilifu/wawakilishi wa Chadema humu JF...ukamwita mbwa na mpaka picha ukamwekea ya mbwa wawili mmoja ukamwita Marco na mwengine Polo!?
gombesugu, baada ya kudumu humu jamvini kwa muda mrefu wengi wetu hivi sasa, pamoja na kutokukutana wala kufahamiana, lakini tunaelewana kwa misimamo yetu. Mimi, Mag3, hata ukipitia post zangu zote (na sasa zinafikia zaidi ya elfu tatu) msimamo wangu ni kuwa
adui nambari wani wa taifa hili ni CCM, period. Naamini kuwa CCM ilipofikia haiwezi ikabadilika na kama kungekuwa na uwezekano taifa hili, chini ya utawala wa CCM, lingezidi kudidimia ila tumegota
chini kabisa,
We are at the very bottom na CCM imeamua kupiga kambi hapo hapo!
CCM imetuzalia akina
Mohamed Said,
ZeMarcopolo, bunge, polisi, mahakama, shule za kata, Sheikh Ilunga, the Chenges, TANESCO, kung'oana kucha na vidole ...wewe acha tu, hata nataka kulia! Mtu yeyote ambaye katika hali kama hii ana jeuri ya kukitetea hiki chama cha Maovu, hastahili heshima yoyote ile kutoka kwangu. Sasa
ZeMarcopolo kutuita eti vijana wa BAVICHA na wewe ukampa "like"!...hiyo BAVICHA ndio nini na ina uhusiano upi na tusoipenda CCM! Aah, ni vijana wa Chadema! Kweli
gombesugu, na wewe unaamini mimi ni Chadema? FYI Al Akhiy hata
Ritz, ni mkereketwa na mtetezi mkuu wa CCM inayoendeshwa kwa mfumo Kristo, upo?
gombesugu said:
Yale majedwali yako nimeyaona ndugu yangu,lakini nimeshikwa na vijishughuli kiduchu. Kipata fursa Insha Allah takuandikia. Nimependa tumewasiliana,nami binafsi tajifunza kwa mazuri ulonayo.
Shukran.
Hapo umeongea na hayo ndiyo maneno, siyo kudai source! Tunapompinga Al Akhiy Mohamed Said tunaweka kwa maandishi what should be, hatuombi source;
Akidai kuwa Kleist Sykes ndiye muasisi wa AA mwaka 1929 tunamwambia hapana, Raisi muasisi ni Cecil Matola.
Akidai kuwa Abdul Sykes ndiye aliasisi TANU mwaka 1954 tunamwambia hapana, Raisi muasisi ni Mwalimu Nyerere.
Akidai kuwa Prof. Malima ndiye aliasisi namba kwenye mitihani, tunamwambia hapana, huo ni uongo.
Akidai kuwa balozi wa Marekani alihutubia bunge la Tanzania, tunamwambia hapana, huo ni uongo, hilo halikutokea.
Akidai kuwa kitabu cha Kivukoni cha historia ya TANU hakiwataji wazee wake, tunamwambia huo ni umbea.
Akidai akidai, akidai...
Hayo tuyaache, ninasubiri kwa hamu hilo jedwali lako. Mimi nina jedwali linaloonesha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwezi Julai mwaka 1963
jimbo kwa jimbo...