gombesugu, sitaweza kutoa majibu kwa maswali yote uliyoniuliza kwa sababu tu ya muda; wakati mwingine majukumu mengine yanatutinga. Usione ajabu
Mag3 kuonekana yuko "
on line" ukafikiri nipo muda wote, hapana, wakati mwingine sihangaiki hata ku"
sign out" kwa sababau sitaki taabu ya ku"
log in and out" ninapopata kamuda ka kuchungulia humu.
gombesugu, labda huna muda mrefu ndani ya jukwaa hili lakini hayo mambo ya kukashifiana katika imani zetu
please count me out. Ninao ndugu na marafiki wa karibu sana ambao si wa imani yangu na nisingependa kujiingiza katika malumbano yanayoweza kuathiri mahusiano yetu. Hata hivyo nafurahi sana kwamba katika huu mjadala pamoja na kujua msimamo wangu na kuyasoma maandishi yangu, wananiunga mkono kwa kupinga upotoshaji unaofanywa na baadhi ya Watanzania wakisukumwa zaidi na chuki zao walizorithi kutoka kwa wazee wao. Wanatambua kwamba hujuma na ufisadi uliotamalaki nchini na unaotudidimiza kama taifa hauna rangi, dini, ukabila wala jinsia. Bahati mbaya wapo wenzetu ambao wameamua kutumia kalamu zao kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu kwa mgongo wa dini...hawa lazima wapigwe vita bila kujali ni wa dini gani, Al Akhiy
Mohamed Said akiwa ni mmoja katika watu hao hatari.
Mimi ni mtu wa kwanza humu jamvini kumwita
Mohamed Said mpuuzi kwani pamoja na kujua hatari ya mbegu anayojaribu kuipandikiza, anashindwa kutambua madhara yake. Kwa sasa tunaanza kuona hizo mbegu zikichipua...kwa mfano, ukipata muda ukasikiliza mahubiri ya Sheikh Ilunga au Sheikh Ponda, utadhani wanasoma neno kwa neno aloandika huyo Al Akhiy. Mimi pia ni mtu wa kwanza humu jamvini kumwita Mohamed Said mchochezi na muongo kwani pamoja na kuhubiri chuki, hata siku moja hajawahi kushiriki wanafunzi wake wanapotekeleza kwa vitendo hizo sera zake za chuki.
Bahati mbaya watetezi wakubwa wa mahubiri yake ya uongo, wanakesha humu wakitudhihaki wengine eti mbona hatuandiki vitabu? Pamoja na kutoa data kuonesha kuwa maandishi yake siyo sahihi, utetezi unaotolewa ni wa kunukuu hayo hayo maandishi yake tunayoyapinga. Wapo ambao wako humu wakidai wanafyonza ilmu, lakini cha ajabu ni kama vile wamejifungia ndani ya box na elimu tunayoitoa kwa maandishi kupinga madai potofu ya mwalimu wao, je hawayaoni na kuyasoma?
gombesugu, mimi ni mmoja wa watu waliokukaribisha ulipojiunga na JF tarehe
4th April 2013, hadi sasa unatimiza mwezi moja na nusu, kwa kuamini kuwa ungesimamia ukweli na kuutetea bila woga. Nadhani wakati huo hukufahamu kuwa iko dhana imepadikizwa humu kwamba asiyekubaliana na Al Akhiy
Mohamed Said bado hajakamilika kiimani. Nina ushahidi wa Waislaam tena safi tu ambao badala ya kutulia na kufyonza ilmu anayotoa mwalimu wakajaribu kuyakosoa, looo! Eti wanaoiendesha serikali wanatekeleza maagizo ya Kanisa, BAKWATA inaendeshwa kwa mfumo Kristo, wakuu wote wa idara nyeti za serikali wana utii kwa mfumo Kristo...!
gombesugu, hata mara moja wewe hujawahi kumpinga huyu bwana, je si kweli? Huo uthubutu huna Al Akhiy!
gombesugu, baada ya kudumu humu jamvini kwa muda mrefu wengi wetu hivi sasa, pamoja na kutokukutana wala kufahamiana, lakini tunaelewana kwa misimamo yetu. Mimi, Mag3, hata ukipitia post zangu zote (na sasa zinafikia zaidi ya elfu tatu) msimamo wangu ni kuwa
adui nambari wani wa taifa hili ni CCM, period. Naamini kuwa CCM ilipofikia haiwezi ikabadilika na kama kungekuwa na uwezekano taifa hili, chini ya utawala wa CCM, lingezidi kudidimia ila tumegota
chini kabisa,
We are at the very bottom na CCM imeamua kupiga kambi hapo hapo!
CCM imetuzalia akina
Mohamed Said,
ZeMarcopolo, bunge, polisi, mahakama, shule za kata, Sheikh Ilunga, the Chenges, TANESCO, kung'oana kucha na vidole ...wewe acha tu, hata nataka kulia! Mtu yeyote ambaye katika hali kama hii ana jeuri ya kukitetea hiki chama cha Maovu, hastahili heshima yoyote ile kutoka kwangu. Sasa
ZeMarcopolo kutuita eti vijana wa BAVICHA na wewe ukampa "like"!...hiyo BAVICHA ndio nini na ina uhusiano upi na tusoipenda CCM! Aah, ni vijana wa Chadema! Kweli
gombesugu, na wewe unaamini mimi ni Chadema? FYI Al Akhiy hata
Ritz, ni mkereketwa na mtetezi mkuu wa CCM inayoendeshwa kwa mfumo Kristo, upo?
Hapo umeongea na hayo ndiyo maneno, siyo kudai source! Tunapompinga Al Akhiy Mohamed Said tunaweka kwa maandishi what should be, hatuombi source;