Wanajamvi,
Nimgeliweza kueleza mgogoro mzima wa Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere
sheikh akiwa sasa anaongoza taasisi iliyoitwa Daawat Islamiyya (Wito kwa
Waislam) yeye akiwa Mwenyekiti na Schneider Abdillah Plantan akiwa katibu.
Lakini kwa kuwa Sheikh Hassan ametukanwa hapa ninajizuia kwa ajili ya kuhifadhi
heshma ya kiongozi wetu ambaye wengi wanamuitikadi kuwa alikuwa walii.
Too late Mohamed, hoja iliyokuwepo mbele yetu ni kuwa Nyerere kwa ''udhalimu'' wake alimfukuza Sheikh Amir bila sababu. Ukaenda mbele na kumhusisha na EAMWS pale tulipouliza inawezekanaje Nyerere aamke asubuhi na kumchukia mtu aliyefanya naye kazi miaka mingi. Hakuna maelezo mengine zaidi ya kusema ukataili wa mwalimu dhidi ya wazee wako.
Leo unataka kueleza kisa baada ya kujulikana kuwa Sheikh alikuwa Msaliti.
Labda tuanzie na kwanini alikataa nafasi alizopewa na kwanini alijificha na kuendeleza siasa za pembeni.
Kuhusu Sheikh Amir kuwa Walii hilo halina tabu kama wapo walioamua kumpa hishma hiyo.
Lakini pia kuna jambo hapa, sasa kama alipewa hishma hiyo na wafuasi wake kwa taratibu za imani yao, Iweje basi wawepo watu wa kuhoji u-saint wa Nyerere anaotaka kupewa na watu wa imani yake?
Hakuna double standard kwa mtazamo wa haraka tu.
Mwisho, Sheikh kuitwa mnafiki na msaliti si tusi, kama lingekuwa tusi linalowaumiza basi msingezunguka duniani mkimsema Nyerere kuhusu viarago na pesa za vitoweo.
Kama lingekuwa linaumiza basi msingemvunjia hishma kwa kusema Laanatullah kila anapotajwa, wala asingeitwa habithi, baradhuli, mnafiki n.k.
Kwanini udhani kuwa sheik Amir anastahili hishma kuliko Nyerere wote wakiwa wanadamu, wazee na familia zao?
Hapa ndipo nasema kila siku lazima watu waangalie nyuma, pembeni na mbele.
Kurushia watu mawe ukiwa katika nyumba ya glasi si jambo jema.
Kila mzee wetu aliyepigania nchi hii na apewe heshima.
Tuache uchochezi usio na maarifa
Hii inaitwa fitna al maarifa kama anavyosema ndugu yangu Gombesugu.
Tuache haya tuangalie jamii inakwenda wapi, inahitaji nini, tufanye nini kwa pamoja na si kwa chuki na kubaguana.