Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu yangu labda ni speed ya Internet connectivity yako. Hiyo link ya kwanza ina picha zinabadilikabadilika, ya pili ina report ya page 12 ya tatu ina report ya pg 17, hizi report zote ni PDF. Tulia kidogo jaribu wakati Speed ni nzuri.

Mkuu Wickama,

Internet yangu iko fine kabisa hizo page nimeziweka kwenye laptop yangu kama unataka nitaziweka hapa ninavyo quote ndivyo ilivyo
 
Zumbe; Uko sawa kabisa ndugu yangu. Kuna maradhi mapya ya kudhani kuwa mikoani kulikuwa na magodoro tuu. Vichwa vyote vilikuwa kwenye familia moja. Ndio historia inayopigiwa debe hapa. Uko sawa kabisa. Hela ambazo hawa WAJANJA walizokuwa wanachota toka WANACHAMA wa mikoani (wanaita Matawi) wala hazisemwi. Ukiangalia kama Dar walipigana hata kajivita na wakoloni HAMNA, kama Dar hata wali-harass wauza watumwa HAMNA, au labda Dar wali-support vita kama Majimaji, HAMNA. Mkwawa kapigana jamaa wananunua samaki ferry. Leo ndio wanaosema eti wazee wetu mikoani walikuwa bongolala!!!!! Ila jamaa yao mmoja tuuu. Wabasema kua uyaone.
na hayo maradhi lazima yatokomezwe, la sivyo yale ya Burundi na Rwanda au korea yatatufikia.
 
Nguruvi umenisikitisha sana kwa jinsi unavyo wazungumzia wa Znz yani wewe unaposema sasa hivi hakuna tena "cold war" kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Nyerere na Karume walituunganisha kutokana na "cold war" hayo sio maneno sahihi kwa wa znz kwahiyo wazazibar walitumika kama beleshi ujenzi ukiisha linawekwa stoo na hizo cc uliowataja nikuulize unajua maana ya neno kafir? mkubwa wacha chuki na waznz haya maneno kwamba waznz ni tegemezi angeyazungumza baba yako wa taifa sio wewe nakusikitikia sana tuendelee na mnakasha. ahsante
Sheikh Farid, ahlan wahsalan muungwana.
Sina chuki na wzn kwasababu nikiwachukia lazima nianzie katika familia yetu.
Ninachofanya ni kujibu yale ambayo wznz wamekuwa wanasema miaka nenda rudi.
Wakatuita Makafir ndiyo maana tukakubali na ndio maana ya hiyo cc, kwamba ukitoka bara ''hilo chogo la kuja,kaafir huyo'' Wakatuita wanyonyanyaji, wakasema sisi wezi tunawaibia na kila aina ya fitna.

Leo Watanganyika wanaweka kila kitu mubashir mnaona ni chuki au matusi. Chuki kaanza nani?
Pili, muungano wa Nyerere ulikuwa wa Pan Afrika na ukichagizwa na nguvu ya pamoja kudhibiti madhara ya cold war pia.

Nia ilikuwa kuendelea kwa pamoja tukijisahihisha hadi kuridhiana.
Wznz wakageuza kuwa ni mradi, kila wakitaka jambo tishio tunavunja muungano.
Sasa hivi Watanganyika wanasema wala hamna haja ya kusema ondokeni tu! hata kuaga msiage mtume twitter mkishateremka Malindi.

Sasa yanazuka madai ya kugawana. Kwamba watu wagawane kisichokuwepo. Wewe una sh 24 mwenzako 1498 halafu unataka mgawane sawa. Hata hizo 24 hukuziweka katika mchango. Unadai nini kama si upungufu wa fikra.
Hatutazuia begi la mznz, lakini hakuna atakayeondoka na kingine! njia nyeupeee

Kuhusu utegemezi, ah ndugu yangu si tumeweka kila mnachotegemea?
Jana tu mumeomba mkatupe ngano bara maana hamna eneo, huo si uetegemezi.
Unaposoma bure wakati mwenzako analipa mkopo, huo si utegemezi

Nadhani ujibu kwa nukta moja hadi nyingine ukionyesha wapi si utegemezi, vinginevyo Yericko kasema mtoto aliyebebwa ana viwembe sasa ni wakati tumtue atembee mwenyewe.
 
Unajifanya mjuvi ilihali hujui kitu,

Unaleta kejeli na matusi mwisho unaomba kupewa darasa?

Nakujuza kuwa mzee wetu Shehe Issa Bin Amir amefariki 26 januari 1953 akiwa na umri wa miaka 107!

Hoja zingine zote naomba uzijibu kwa swali hili,

1) Je Mwalimu Cesil Matola alikuwa na Umri gani 1929 wakati anakuwa rais wa KWANZA wa AA?

2) Ally Ramadhan alikuwa na umri gani wakati anachaguliwa kuwa Muweka hazina wa kwanza wa AA?

3) Klest Sykes alikuwa na umri gani wakati anachaguliwa kuwa katibu mkuu wa AA?

Ukijibu haya naomba jibu na hili:

Je unadhani Shehe Issa Bin Amir alikuwa na umri gani mpaka viongozi wa AA wakamheshimu na kutumia hekima zake?!

Tumia akili unayofundwa kila siku hapa jf
Yericko Nyerere,

Wanaukumbi ndiyo wataamua, wapi nimeleta matusi na kejeli naona "mipini" imekuchanganya sana nionyeshe wapi nimekutukana? kwa faida ya Wanaukumbi nashindilia Mpini mwingine halafu utasema matusi.

Nakujuza kuwa mzee wetu Shehe Issa Bin Amir amefariki 26 januari 1953 akiwa na umri wa miaka 107!
Wanaukumbi nadhani mnajionea wenyewe hapa anatujuza kuwa huyo Sheikh Issa amefariki mwaka 1953 hapa chini baada ya kufa akafufuka...waalahi bayana zako ndiyo zinakutukanisha na mimi siwezi kukaa kimya umekutana na kichwa cha madrassa mnywa Gahawa, haha haa aaa Shariff gombesugu, upo Alhy Baabu soma chini hapa.
Mnamo tarehe 7/7/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)

Sheikh Issa Bin Amir amefariki mwaka 1953 halafu alifanya mkutano na Nyerere mwaka 1954...ha ha haaa
gombesugu, Jasusi, Kadogoo,
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa mbinafsi na mbora mimi kamwe huwezi kuandika historia ya nchi inayohusu makabila zaidi ya 120 na inayohusi imani zaidi ya tano nchini!

Utabaki na kikundi cha wanafiki na wafitini tu ndio wataokuunga mkono!

"Kikundi cha wanafiki na wafitini" ha ha haa...mnafiki ni wewe unaoyejinasibisha na baba ambae si wako halafu unajifanya mjanja, ntakupa kisa kimoja ndani ya Quran kuna bwana mmoja alikuwa anaitwa Walid bin Mughira huyu mzee Mughira alikuwa anapesa sana na kipindi hicho mtoto wa kiume mkubwa ndio alikuwa anarithi mali sasa huyu mzee Mughira jongoo lilikuwa halipandi mtungi mama yake Walid akapiga mahesabu akafikiria nani atarithi mali ya mzee Mughira ikabidi akazae nje ya ndoa ndio akapatikana Walid bin Mughira lakini kumbe walid sio mtoto wa mzee Mughira na hilo swala walid alikuwa halijui,walid alikuwa nimfanya biashara mkubwa sana pale Makka kwasababu alirithi mali ya mzee Mughira basi siku moja akawa anapita nje ya nyumba ya mtume Mohamad(s.a.w)anasoma suratul kalam akasikiliza ikafika sehemu mwenyezi mungu anamwambia mtume usimti mtu mwenye kuapa apa hovyo,mtu mwenye kujiona,mtu muongo ilipofika pale inaposema baada ya hayo yote mtu mwenyewe ni wa nje ya ndoa,baada ya yote Walid akiangalia sifa zote zilizo tajwa anazo ila hiyo moja ndio ikamtatiza,ikabidi amtafute mama yake amuulize Muhamad nimemsikia anasoma Quran sifazote alizozitaja ninazo ila moja tu ndio sijamuelewa mama yake akamuuliza ni ipi akamwambia amesema mimi mtoto wa nje ya ndoa mama yake akamwambiani kweli wala hajakosea akamueleza issue yote ilivyo kuwa ikabidi walid awe mpole, na ndio maana uislamu umepinga mtu kujinasibisha na baba ambae si wake ahsante tuendelee na munakash.cc Mohamed Said,Ritz Gombesugu,Big Show
 
Nguruvi3,

..nadhani wa-Znz wanafikiri bado tuko ktk zile zama za utumwa.

..wanafikiri Tanganyika, na wa-Tanganyika ni mali yao.

..nimesoma ile thread ya faida za gesi kusini, na misaada inayotolewa na makampuni ya utafiti wa mafuta kwa wananchi wa kusini.

..hebu tulinganishe mapesa yanayochotwa Tanganyika kwenda Zanzibar, na kile wanachopewa wananchi wa kusini na makampuni ya gesi na mafuta.

..Wananchi wa kusini wanataabika wakati serikali yao inachota mapesa na kuwapelekea wa-Zanzibari. Bilioni 32 alizopewa Dr.Bilali kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar zingepelekwa kusini wananchi wa huko wasingekuwa wanalalamika kwamba serikali yao imewatupa.

cc: THE BIG SHOW, gombesugu, Kadogoo, Jasusi
JokaKuu!
Ninachofahamu mimi kutoka kwako ni kuwa unajaribu kuwaonyesha wana ukumbi hasara za Muungano kwa Watanganyika na athari zake mbaya ikiwemo ukwamishaji wa "maendeleo" ya Mtanganyika kama vile Kusini.

Umetuonyesha huko nyuma pia kuwa upo mstari wa mbele katika kuwazindusha Watanganyika kuhusu hasara wanazozipata kutokana na Muungano.Ulitufahamisha vilevile kuwa Watanganyika wamechelewa katika kuzidai haki zao zinazohodhiwa na Muungano.

Unaweza kutuelezea ni sababu zipi unafikiria zilimchelewesha Mtanganyika kuzinduka katika kudai haki yake?
Ni matumaini yangu kuwa kuelewa kwa Mtanganyika wapi alijikwaa kutakuja kumsaidia sana mbeleni.
*Si lazima JokaKuu yoyote anaweza kujimwaga na kutupatia tathmini yake.
 
na hayo maradhi lazima yatokomezwe, la sivyo yale ya Burundi na Rwanda au korea yatatufikia.

Nashukuru Zumbe; Sielewi mtu utakavyowadanganya wale wazee pale stendi Mlalo, au Bumbuli kuwa Nyerere hakuwa lolote katika kuikomboa nchi toka kwa wakoloni. Eti mkombozi wa kweli alikuwa mtu mwingine na huyo ndiye baba halisi wa taifa, ndiye aliyeunda TANU, nk. Labda vizazi vinavyokuja. Lakini kama ni wale wazee wa kisambaa wa kule Kwemakame, hawatakusikiliza. Ushahidi umesheni kuwa waliishi kama watanganyika na kila mtu na dini yake. Familia ni nyingi wazazi ni dini tofauti na watoto, kwa hii EFFORT ya DIVIDE AND MISRULE umefikia wakati wa kila mmoja kuwa mwangalifu sana. Siku zote wadanganyifu huwa wana maneno matamu. Ujinga walionao ni pale wanaposhindwa kujua kuwa zikianza risasi mtaani, hata binti/baba yake yatampata.
 
Zumbe; Uko sawa kabisa ndugu yangu. Kuna maradhi mapya ya kudhani kuwa mikoani kulikuwa na magodoro tuu. Vichwa vyote vilikuwa kwenye familia moja. Ndio historia inayopigiwa debe hapa. Uko sawa kabisa. Hela ambazo hawa WAJANJA walizokuwa wanachota toka WANACHAMA wa mikoani (wanaita Matawi) wala hazisemwi. Ukiangalia kama Dar walipigana hata kajivita na wakoloni HAMNA, kama Dar hata wali-harass wauza watumwa HAMNA, au labda Dar wali-support vita kama Majimaji, HAMNA. Mkwawa kapigana jamaa wananunua samaki ferry. Leo ndio wanaosema eti wazee wetu mikoani walikuwa bongolala!!!!! Ila jamaa yao mmoja tuuu. Wabasema kua uyaone.
Zumbe mkuu, kuna watu walipinga ukoloni hadharani. Kuna kitu kinaitwa kodi ya Mbiru, wapare wanakifahamu sana ukisoma historia. Tena kiliwahi kuwa na tamthilia RTD nyakati hizo.
Hayo hayasemwi yanasemwa ya familia moja iliyokuja kuikomboaTanganyika.

Wickama, tena hao waliokuja kuikomboa Tanganyika ni hao hao walikuja na Wajerumani wapigane dhidi ya Watanganyika.
Leo tunaambiwa huko bara watu walikuwa wamelala usingizi wa pono, wakitafuna dodo na ng'ongo kama si kugigina vibanda meno na mahiza! Jamani.

Hizo pesa za matawi hazisemwi kwasababu ukizisema si Nyerere alikuwa katibu Tabora!! Sasa hapo utakuwa umeondoa maana nzima ya Nyerere kufundishwa siasa alipokuja Dar na kukutana na wakombozi.

Utakuwa umeondoa maana halisi ya Nyerere kuwa na mchango maana yeye aliletwa na wamishenari kufundisha, tena si mkatoliki?

Kwahiyo naomba msiongelee mambo ya matawi, mtatia maji katika wine! chonde chonde waungwana acheni ngano iumuke wanaomeza wameze.
 
Mbona kwangu inafunguka picha hiyo Nyerere na Ally Sykes mwaka 1958

Hata mimi kwangu haifunguki. Ila kuna notification kuwa THE ADMINISTRATOR MAY HAVE REMOVED THE CONTENT au kama hivyo. Huenda ndio censorship tena au watarekebisha, kwa vile wanauliza kama unadhani ni vyema!!!!
 
Barubaru,
Nina hakika. Anna alikuwa Canada 1974-1977. Nilimtembelea mara kadhaa pale. Madaraka vile vile alisoma Canada lakini sina hakika jina la chuo. Na si kila mtu aliyesomea nje alishindwa kujiunga UDSM. Mimi nimesomea nje wakati kaka zangu wawili walisoma UDSM. Barubaru, wewe ni msomi, tena nasikia una Phd. Sasa kwa watu kama wewe mnategemewa kuwa wabobeaji kwenye utafiti na ukileta habari hapa ziwe za uhakika siyo zile za kijiweni . Na kuhusu tv ya Mwalimu hayo unayosema ungo mkubwa nyumbani kwake ni hadithi nyingine ya kijiweni. TV ya Mwalimu aliyokuwa nayo alinunuliwa na balozi Bomani baada ya ziara yake hapa Marekani 1977. Kuna video nyingi zilirekodiwa na vipindi mbalimbali wakati wa ziara hiyo na Mzee Bomani akasuggest kununua TV hiyo pamoja na video hizo ambazo zilikuwa kwenye American system NTSC. Haikuwa tv ya kuangalia matangazo hata kidogo. Haya, lete stori nyingine ya kijiweni kuhusu Mwalimu nikuweke sawa.

Jasusi,

Kwanza niliweka nia nikuwekee hapa ukukmbini watu wote kutoka Tanzania waliopitia Carleton University lakin nimepata ushauri toka kwa wengi nisiweke hapa lakin kama utapenda naweza nikaku PM wote uangalie kama Huyo Anna yupo.

Lakin unapoandika kitu hakikisha kuwa una yakini nacho kama mimi ninavyoyakinisha. Kumbuka kuwa enzi hizo ili mtu aende CHUO KIKUU ilimpasa kwanza amalize Form four na kisha aende form six na kisha apite JKT. au apitie Adult chances ambazo nina hakika yeye hajapita huko.Sa

Sasa hebu dadavua kidogo kuwa je aifanikiwa kupata maksi za kutosha kwenda form six. je alisoma skuli gani na JKT alipitia wapi kama huu msema kweli?

Nitakuongezea moja hapo yule mtoto wake uliyesema alikwenda Airforce China. Je unajua kuwa alikuwa form four akaenda kusomea kozi ya urubani ambazo colifications zake zilihitaji form six. Na wote aliokuwa nao walikuwa form six yeye pekee ndio alikuwa form four? Na alikuja baada e alishindwa masomo hayo. Je nae alipitishwa kinamna hiyo au ... Je nalo hili unalikataa?

Kwa kuwa najua mengi sana kwa sababu nilikuwa karibu na familia hiyo nilipokuwa Tz. napenda kukwambia Nyerere alipenda sana vijana wake wasome lakin ...

Nilichokubainishia hapa alipenda watoto wa wengine wapite njia sahihi yeye wake walipita njia za mkato japo wengi hawakufanikiwa kufika. Ndio maana tunasema hakuwa mwadilifu.

Kuhusu PhD yangu isikutie khofu kwani nimeipata kihalali kabisa toka Mtendeni skuli Dar, Tambaza, Ilboru, JKT Ruvu, UDSM(Tz). Carleton Univ(Can), Na Sofia Univ (Jpn).tafuta tu jina la Dr Hamza Yousuf Al-Naamaniy

Tuendelee na mnakasha kwani tutaingilia siri za ndani za familia hii ambazo si vizuri kuzianika hapa.

Pole sana

Zumbe mkuu, kuna watu walipinga ukoloni hadharani. Kuna kitu kinaitwa kodi ya Mbiru, wapare wanakifahamu sana ukisoma historia. Tena kiliwahi kuwa na tamthilia RTD nyakati hizo.
Hayo hayasemwi yanasemwa ya familia moja iliyokuja kuikomboaTanganyika.

Wickama, tena hao waliokuja kuikomboa Tanganyika ni hao hao walikuja na Wajerumani wapigane dhidi ya Watanganyika.
Leo tunaambiwa huko bara watu walikuwa wamelala usingizi wa pono, wakitafuna dodo na ng'ongo kama si kugigina vibanda meno na mahiza! Jamani.

Hizo pesa za matawi hazisemwi kwasababu ukizisema si Nyerere alikuwa katibu Tabora!! Sasa hapo utakuwa umeondoa maana nzima ya Nyerere kufundishwa siasa alipokuja Dar na kukutana na wakombozi.

Utakuwa umeondoa maana halisi ya Nyerere kuwa na mchango maana yeye aliletwa na wamishenari kufundisha, tena si mkatoliki?

Kwahiyo naomba msiongelee mambo ya matawi, mtatia maji katika wine! chonde chonde waungwana acheni ngano iumuke wanaomeza wameze.

Nguruvi; Umegusa kitu sikuwahi kukiwaza hivi kama Julius Nyerere baba yake angekuwa kafika hapa nchini kama mamluki wa kijerumani kuja kuwatwanga wakina Kimweri kule Lushoto, kisha na huu Ukatoliki wake!!! Aiseeeeeeee, PANGECHIMBIKA Ndugu yangu
 
Nashukuru Zumbe; Sielewi mtu utakavyowadanganya wale wazee pale stendi Mlalo, au Bumbuli kuwa Nyerere hakuwa lolote katika kuikomboa nchi toka kwa wakoloni. Eti mkombozi wa kweli alikuwa mtu mwingine na huyo ndiye baba halisi wa taifa, ndiye aliyeunda TANU, nk. Labda vizazi vinavyokuja. Lakini kama ni wale wazee wa kisambaa wa kule Kwemakame, hawatakusikiliza. Ushahidi umesheni kuwa waliishi kama watanganyika na kila mtu na dini yake. Familia ni nyingi wazazi ni dini tofauti na watoto, kwa hii EFFORT ya DIVIDE AND MISRULE umefikia wakati wa kila mmoja kuwa mwangalifu sana. Siku zote wadanganyifu huwa wana maneno matamu. Ujinga walionao ni pale wanaposhindwa kujua kuwa zikianza risasi mtaani, hata binti/baba yake yatampata.
afanaleki, tena wale wazee ukiwaletea uongo kama huu wa MS walahi watakutemea mate yaliyojaa ugoro mdomoni,
 
Wanajamvi,
Nimgeliweza kueleza mgogoro mzima wa Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere
sheikh akiwa sasa anaongoza taasisi iliyoitwa Daawat Islamiyya (Wito kwa
Waislam) yeye akiwa Mwenyekiti na Schneider Abdillah Plantan akiwa katibu.

Lakini kwa kuwa Sheikh Hassan ametukanwa hapa ninajizuia kwa ajili ya kuhifadhi
heshma ya kiongozi wetu ambaye wengi wanamuitikadi kuwa alikuwa walii.
Too late Mohamed, hoja iliyokuwepo mbele yetu ni kuwa Nyerere kwa ''udhalimu'' wake alimfukuza Sheikh Amir bila sababu. Ukaenda mbele na kumhusisha na EAMWS pale tulipouliza inawezekanaje Nyerere aamke asubuhi na kumchukia mtu aliyefanya naye kazi miaka mingi. Hakuna maelezo mengine zaidi ya kusema ukataili wa mwalimu dhidi ya wazee wako.

Leo unataka kueleza kisa baada ya kujulikana kuwa Sheikh alikuwa Msaliti.
Labda tuanzie na kwanini alikataa nafasi alizopewa na kwanini alijificha na kuendeleza siasa za pembeni.

Kuhusu Sheikh Amir kuwa Walii hilo halina tabu kama wapo walioamua kumpa hishma hiyo.
Lakini pia kuna jambo hapa, sasa kama alipewa hishma hiyo na wafuasi wake kwa taratibu za imani yao, Iweje basi wawepo watu wa kuhoji u-saint wa Nyerere anaotaka kupewa na watu wa imani yake?
Hakuna double standard kwa mtazamo wa haraka tu.

Mwisho, Sheikh kuitwa mnafiki na msaliti si tusi, kama lingekuwa tusi linalowaumiza basi msingezunguka duniani mkimsema Nyerere kuhusu viarago na pesa za vitoweo.

Kama lingekuwa linaumiza basi msingemvunjia hishma kwa kusema Laanatullah kila anapotajwa, wala asingeitwa habithi, baradhuli, mnafiki n.k.

Kwanini udhani kuwa sheik Amir anastahili hishma kuliko Nyerere wote wakiwa wanadamu, wazee na familia zao?

Hapa ndipo nasema kila siku lazima watu waangalie nyuma, pembeni na mbele.
Kurushia watu mawe ukiwa katika nyumba ya glasi si jambo jema.

Kila mzee wetu aliyepigania nchi hii na apewe heshima.
Tuache uchochezi usio na maarifa

Hii inaitwa fitna al maarifa kama anavyosema ndugu yangu Gombesugu.
Tuache haya tuangalie jamii inakwenda wapi, inahitaji nini, tufanye nini kwa pamoja na si kwa chuki na kubaguana.
 
Nguruvi; Umegusa kitu sikuwahi kukiwaza hivi kama Julius Nyerere baba yake angekuwa kafika hapa nchini kama mamluki wa kijerumani kuja kuwatwanga wakina Kimweri kule Lushoto, kisha na huu Ukatoliki wake!!! Aiseeeeeeee, PANGECHIMBIKA Ndugu yangu
Kimweri alimzuia nyerere na timu yake kupanda milima ya Lushoto akidhani ni mamluki wa wakolini, wake zake kimweri ndo walienda kuondoa mawe bara barani ili nyerere aweze kupita.
 
Back
Top Bottom