Nguruvi umenisikitisha sana kwa jinsi unavyo wazungumzia wa Znz yani wewe unaposema sasa hivi hakuna tena "cold war" kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Nyerere na Karume walituunganisha kutokana na "cold war" hayo sio maneno sahihi kwa wa znz kwahiyo wazazibar walitumika kama beleshi ujenzi ukiisha linawekwa stoo na hizo cc uliowataja nikuulize unajua maana ya neno kafir? mkubwa wacha chuki na waznz haya maneno kwamba waznz ni tegemezi angeyazungumza baba yako wa taifa sio wewe nakusikitikia sana tuendelee na mnakasha. ahsante
Sheikh Farid,
Nakuelewa kiundani hayo majonzi yakupatayo. Unajua hawa
Nguruvi3 na JokaKuu,mimi binafsi ni kati ya jamaa ninaowaheshimu mno.
Ndo maana huwa napata huzuni wakija na matendo au kauli za ajabu ajabu na zenye kuonyesha chuki baina ya
WaTanzania. Wapo jamaa wanaweza kuzungumza chochote na lolote hapa jamvini sisi tukadharau. Lakini hawa JokaKuu na Nguruvi3 nafikiri wanashindwa kujua yakuwa kuna wengine tunathamini michango yao hapa jamvini.
Yaani tokea ije khabari ya Zanzibar
"wamefunguka" kikweli! kwa hili inanilazim nimsifu ndugu yangu
Mag3,japo anachangia lakini kauli zake zimekua ni adilifu mno.
Halafu
Nguruvi3,kama dasturi yake anatoa excuse yakuwa kwenye
Family tree yake pia kuna
Waislamu na WaZanzibary. Ananikumbusha hawa jamaa zetu wa
Kizungu huku...wakianza kushutumiwa ubaguzi wa rangi,basi ghafla wataanza kutaja nasaba na ku-count how many
Cousins and Black friends they have!ahaha!!
Hayo uyazungumzayo hapo juu,ndo mpaka leo yanaleta zogo na utata mwingi kule kwenye zilizokua
Eastern Block Countries. Kwa mfano mpaka kesho
Poland ana hasama kubwa mno na
Russia. Kwamba anahisi kumbe
USSR walikuwa wala sio ndugu au marafiki wa kweli bali tu ni wanafiki na wazandik walikua wakiitumia Poland as a
"buffer Zone"!
Sasa hapa ndo
Nguruvi3 na JokaKuu unaona language watumiayo ina dalili zoote za hayo. Kingine labda wasichofahamu ni kuwa;lolote litakalotokea na kuvunja Muungano huo basi hakuna ati atakaekua
"mshindi wa kudumu" kati ya Tanganyika au Zanzibar.
Mimi binafsi,sisemi wala sioni ubaya wa kuzungumzia haya matata ya Muungano kwa kina. Tatizo tujiepushe na hizo
colourful languages. Hazijengi bali zinabomoa tu!
Embu fikiria,
JokaKuu amefikia ati mpaka ya kusema sisi huku Bara
Wazungu hawana ubaya na sisi lakini
Waarabu tu ndio tunawaona wabaya kwa ile biashara ya Utumwa!? Hapa napata wasiwasi kama kweli hawa ndugu zetu wanaelewa kiundani Historia ya hao Wazungu wanaowatetea dhidi ya nchi/Bara letu. Au kwa sasa kuna
WaTanzania wameamua kuweka kando baadhi ya ukweli wa kiHistoria kwa muda ili
"kuwashughulikia" WaZanzibary!?
Wanasahau yakuwa atrocities na vita vingi mno walopiganishwa WaZanzibary na
Nyerere,si kwa kupenda au hata kushauriwa kama kanuni na vipengele kadhaa vya makubaliano au kanuni za mkataba wa Muungano inavyotaka,hasha asilan!
Na kuna vituko na vitimbi vingi mno walivyokua wanaburuzwa
WaZanzibary bila ya maridhia, na kinyume ya vipengele vya kisharia ya huo "
mkataba wa Muungano". Na haya mambo yanaendelea mpaka kesho.
Nyerere,tangia enzi zake alikua akitia ndani Viongozi au wananchi wowote wa
Zanzibar waliokua aidha wakijadili,kudai haki au kutaka kujitoa kabisa kwenye huo
"Muungano".
Sasa wao wanafikiri Nyerere alikua hajui alichokua anakifanya miaka yoote hiyo!? Au hawa jamaa zangu wanafikiri Nyerere alikua na uchungu na kuwapenda
WaZanzibary kuliko
WaTanganyika!?ahaha!!
Nyerere alikua ni master of political calculations/games...hii haina ubishi. Kwa hiyo lazim aliona manufaa makubwa saana ya Zanzibar kuliko hasara yake. Na hii ni kwa kila kitu. Ulinzi,Usalama,senti na mengineyo mengi tu.
Namkumbusha ndugu yangu
Nguruvi3 japo kiduchu,miaka hiyo ya mwanzo
Zanzibar haikutakiwa kuchangia kwenye masuala ya Ulinzi wala Usalama. Zanzibar tayari ilikua na Mkuu wa Majeshi na
Amir Jeshi Mkuu alikua ni Rais wa Zanzibar,na Idara ya Usalama Wa Taifa ilokua huru bila ya kuhusishwa kwenye Serikalim ya Muungano. Mkuu wa Majeshi alikua Yusuf Himid,Mkurugenzi wa Usalama Wa Taifa alikua Seif Bakari "Kiwavi" na Amiri Jeshi Mkuu alikua Rais Abeid Karume.
Zanzibar miaka michache baada ya Muungano,walikua tayari na Jeshi kali mno la Maji/
Navy lililokua linaheshimika kupita kiasi katika ukanda wa
Afrika ya Mashariki. Mafunzo ya kijeshi/kiunamaji,misaada na vifaa vyoote na ushirikiano wa karibu ulikua ukitolewa na enzi ile ikiitwa Shirikisho la Kijarumani/
Ujerumani ya Mashariki.
Hivi vitu vyoote havikumpendeza
Nyerere asilan,na mara kadhaa alikua akisikika na kulalama yakuwa wale
WaZanzibary hawaaminiki,siku yoyote wanaweza kuja kutuvamia.
Oscar Kambona ndie aliekua akimtuliza,kwa sababu Kambona tangia awali alikua na mahusiano mazuri mno na viongozi kadhaa wa ngazi za juu na sehemu nyeti pale
Unguja.
Ndio maana mara tu baada ya Rais Karume kuuwawa kwenye yale Mapinduzi yaloshindikina;Nyerere alitumia kila ghila na dhuluma kuhakikisha anamburuza Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi....Usalama waTaifa ukaunganishwa,Amiri Jeshi Mkuu wa zanzibar pia akawa yeye Nyerere. Kikosi mahiri cha Navy cha Serikali ya Zanzibar kikavunjwa. Wakaambiwa ati waunde KMKM maana yake ati "Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo"!?ahaha!! Yaani Nyerere UHUNI wake hauna hata haya,hivi Zanzibar kuna biashara au magendo gani tena enzi hiyo ya mpaka kusababisha jeshi zima la Maji/Navy livunjwe ili kufanya shughuli hiyo!?ahaha!!.....Ilipofika 1977,ndipo akahitimisha ule mburuzo kwa kuvunja kabisa ASP. Kwa kifupi ilobaki ni khadith tu,na ndo leo tupo hapa jamvini ndugu yangu Nguruvi3 anataka kunifungashia virago nende zangu "kwetu" Bwejuu/Bwegejuu!ahaha!!
Kwa kifupi, nahisi baadhi ya ndugu zetu wengi wa KiTanganyika hawajui yakuwa sisi pia ni wabara, na
Tanganyika ni kwetu labda hata kuliko wao wajionavyo au kufikiria. Ndo maana mie hucheka pale
Nguruvi3,anaposema
WaZanzibary ati watafunganya mabegi kurudi "kwao"...ninamuhurumia maana tusije mrejesha yeye kwenye asili yao labda huko
Guinea Bissau au
Gambia!!
Kwa sababu hivi vizazi vingi viliopo hapo
Tanzania Bara ni
Wahamiaji tu kutoka maeneo/sehemu nyingine za
Afrika karne chache zilizopita na kuja kujihifadhi hapo
Tanganyika kutokana na madhila yalowakumba huko
makwao.
Ndo maana takupa mfano,
UTangayika wa Ndugu zangu
JokaKuu na Nguruvi3 ukichanganya ndio labda, tena labda watafikia
Ubara/UTanganyika wa
Gombesugu mmoja!
Nisikuchose Al Akhiy,na
Insha Allah tuendelee na mnakasha.
Shukran.
Cc;Ritz,Nambokola,JokaKuu,Mag3,Nguruvi3,Sheikh Farid