Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said,
Msiba wa Mzee Ally Sykes umetugusa sote tunaojua mchango wake ktk harakati za kupigania uhuru wa nchi hii! kwaniaba yangu binafsi kwanza nakupa pole wewe binafsi na kutufikishia ktk familia na ndugu wa Marehemu Allah awape subra na Imani! kwani hakika kwake tulitoka na kwake tutarejea!
Shekh MS, umetoa mchango muhimu ktk kufundisha historia ya mashujaa wetu na hasa waasisi wa vyama vilivyopigania uhuru wetu lakini cha kusikitisha kifo cha Mzee Ally Sykes pamoja na viongozi wote waandamizi na wastaafu kuhudhuria msibani, hakuna gazeti hata moja lililoripoti msiba na mazishi ya Mzee Ally Sykes?

Kadogoo,
Pole nimezipokea na Amin.

Kabla hajafa marehemu Ally Sykes aliandika historia ya maisha yake.
Kuanzia jana The Citizen wameanza serialisation kwa kuchapa vipande.

Kesho In Sha Allah ndiyo instalment ya mwisho.
 
Nambokola,

Salaam.

Mimi binafsi nakufahamu na nakuelewa kwa utuvu na nafuatilia hizi hoja za ndugu zangu JokaKuu na Nguruvi3, khasa kuhusu haya "madeni ya Muungano".

Siku chache zilizopita niliwahi kumwambia Nguruvi3 yakuwa kuna significant evidences ya kuonyesha huo Muungano wenyewe kwanza tangia awali haukuwa halali!

Na ukichungulia japo kiduchu kwenye legality of additional matters outside the Articles of Union....tayari utaona yakuwa kuna practical problems. Hapo peke yake utaona yakuwa hayo "madeni" tayari yashajifuta!

Haina neno tuendelee na mnakasha.

Shukran.


Cc; Ritz,JokaKuu,Nguruvi3
gombesugu,

..ukishaanza kucheza na legal terms au kuwa "legalistic" ujue hoja zako zina mushkeli.

..ukienda kwenye mtandao wa Joint Finance Commission kuna jedwali linaonyesha makusanyo ya ndani ya Zanzibar, na Tanzania Bara. Baada ya hapo wanajumlisha makusanyo hayo na kuyaita makusanyo ya TANZANIA.

..sasa nambokola anataka kuleta ubishi wa kisheria kwamba Tanganyika haipo hapo. mimi nasema Tanzania Bara ndiyo Tanganyika!!

..wa-Tanganyika hatuko huko kwenye mambo ya articles of the union. sisi tunazungumzia DHULUMA na UNYONYAJI unaoendelea sasa hata sasa hivi.

..Waziri wa Afya amesema wizara yake inatoa approx 36 billion kama ruzuku kwa hospitali za mashirika ya dini nchi nzima. wakati huohuo bunge la bajeti la mwaka jana lilimpatia Dr.Bilali 32 billion kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.

..billion 36 kwa wa-Tanganyika milioni 40, halafu bilion 32 kwa wa-Zanzibar milion 1.5. halafu kuna watu mna audacity ya kuzungumzia articles of Union.

..kwanini unataka kuzungumzia madeni baada ya muungano kuvunjika, which in essence ni mambo ya kufikirika?? why dont u talk about unyonyaji unaoendelea sasa hivi ambako wa-Znz wanapewa ruzuku toka Tgk??

CC: Kadogoo, Nguruvi3, Ritz, Mohamed Said, Mag3, Wickama
 
Last edited by a moderator:
Sideeq,

..je, tumeelewana kwamba Znz ndiyo inainyonya Tgk??

..zaidi, tumekubaliana kwamba kutokana na dhuluma ya muungano dhidi yetu, wa-Tgk ndio tunaopaswa kumlaani Mwalimu Nyerere na siyo nyinyi wa-Zenj??

cc: Nguruvi3, Wickama
Kweli nakubaliana nawe kuwa nyerere anapaswa kulaaniwa na Wa-Tanganyika lakini Wazanzibar nao pia wana sababu zao za kumlaani kama wanavyozitaja wenyewe.

Kitu kimoja nadhani sote tunakubaliana ni kuwa Muungano una hasara nyingi kwa pande zote mbili kuliko faida zake, hivyo cha kufanya isiwe ni kukumbushana jinsi gani Tanganyika inavyoibeba Zanzibar ili kuwanyamazisha sauti zao za kuidai Zanzibar yao bali Muungano uvunjwe ASAP bila ya vijikauli vya tukutane EAC au sijui wapi maana huku pia nako ni kuwatisha.

Mimi ni Mtanganyika na ninadhani kuwa tutaheshimiana zaidi wakati kila mtu atakapochukua chake, mbona watu wa mipakani wanaishi kwa kuheshimiana tu angalia watu wa Tanga na Mombasa nadhani ni hivyohivyo kwa Arusha na Nairobi, Kagera na Uganda, Mbeya, Mtwara na kwengineko.
 
Jasusi,

Nakupa pole sana kwa kutaka kupotosha ukweli. Siku zote marubani wa Air force ni lazima wawe form six na sio form four nao walianzia cheo cha cadet sio private. Kwa zamani kujiunga jeshi ilikuwa hata darasa la saba alikuwa anakubaliwa lakin kwenye taaluma kama Urubani tena wa fighter lazima awe form six . Sasa yeye aliingia kwenye kozi hiyo wenzake wote wakiwa form six yeye form four je hapo napo unaona ni kawaida hiyo?
Canada wamekwenda wengi jeshini ambao wengine ni mafundi wa ndege ambao walikuwa kule Angus Ontario .

Lakin kubwa carleton kuna Kozi nyingi kuanzia certificate, diploma mpaka Ph.D. sasa be specific ni level gani kwani kwenye Degree hakuna jina lake.

Kwa uwadilifu wa Nyerere nilitegemea watoto wake wangepita katika proper channel kama wananchi wengine lakin ndio hivyo tena. Uadilifu wake upo wapi?. Jiulize aliwalipia mwenyewe au alitumia pesa za wananchi wake kusomesha watto wake kwa njia za mkato mkato?

mwisho watoto wangu wapo hapo Silver spring , mary land na insh'Allah Ijumaa mosi nitakuwa hapo likizo ya siku tatu.

Tumia facts katika kuandika kwako na sio hisia. Nimekuuliza vipi niku PM majina ya graduates wote wa Carleton kuanzia 1073 -1990 uona kama unayonena ni sahihi?

Kwa heshima ya Wickama na Yericko, sitakujibu tena. Pole mwenyewe!
 
Kweli nakubaliana nawe kuwa nyerere anapaswa kulaaniwa na Wa-Tanganyika lakini Wazanzibar nao pia wana sababu zao za kumlaani kama wanavyozitaja wenyewe.

Kitu kimoja nadhani sote tunakubaliana ni kuwa Muungano una hasara nyingi kwa pande zote mbili kuliko faida zake, hivyo cha kufanya isiwe ni kukumbushana jinsi gani Tanganyika inavyoibeba Zanzibar ili kuwanyamazisha sauti zao za kuidai Zanzibar yao bali Muungano uvunjwe ASAP bila ya vijikauli vya tukutane EAC au sijui wapi maana huku pia nako ni kuwatisha.

Mimi ni Mtanganyika na ninadhani kuwa tutaheshimiana zaidi wakati kila mtu atakapochukua chake, mbona watu wa mipakani wanaishi kwa kuheshimiana tu angalia watu wa Tanga na Mombasa nadhani ni hivyohivyo kwa Arusha na Nairobi, Kagera na Uganda, Mbeya, Mtwara na kwengineko.
Sideeq,

..kusema tukutane EAC siyo kutishana.

..EAC ndiyo chombo muafaka cha kuendeleza mashirikiano na udugu baina ya Tanganyika na Zanzibar.

..ninapoleta ushahidi kwamba Tanganyika inaibeba Zanzibar nia yangu siyo kuwanyamazisha wa-Zanzibari wasidai kuwa na mamlaka kamili.

..nia yangu ni kuwaamsha wa-Tanganyika nao ili wadai nchi yao, yenye mamlaka kamili na inayotambulika kimataifa.
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo,
Pole nimezipokea na Amin.

Kabla hajafa marehemu Ally Sykes aliandika historia ya maisha yake.
Kuanzia jana The Citizen wameanza serialisation kwa kuchapa vipande.

Kesho In Sha Allah ndiyo instalment ya mwisho.

Mohamed,
Bahati mbaya The Citizen haliko mtandaoni. Tutazipataje wengine hizo serialization? Ahsante
 
historia ya wazee wenu mbona mnaongezeachumvi ya upotoshaji?
mara oo nyerere kafundishwa siasa na wazee wenu, mara kaenda sokoni hana hata senti akitaraji kupewa japo thumni yakununulia pilipili hoho sokoni, mara kafundishwa kuvaa na wazee wenu, mara hakujua kiswahili vizuri, ..............
mkuu Ritz umesahau hayo yote mliyasema?
Hayo mengine umeyasema wewe kwa kukazia tusiandikie mate na wino upo hebu ngoja tuangalie huu mpini.

mara oo nyerere kafundishwa siasa na wazee wenu,
Julius Nyerere"‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.


mara hakujua kiswahili vizuri
Julius Nyerere"Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.
 
Nambokola,

Salaam.

Mimi binafsi nakufahamu na nakuelewa kwa utuvu na nafuatilia hizi hoja za ndugu zangu JokaKuu na Nguruvi3, khasa kuhusu haya "madeni ya Muungano".

Siku chache zilizopita niliwahi kumwambia Nguruvi3 yakuwa kuna significant evidences ya kuonyesha huo Muungano wenyewe kwanza tangia awali haukuwa halali!

Na ukichungulia japo kiduchu kwenye legality of additional matters outside the Articles of Union....tayari utaona yakuwa kuna practical problems. Hapo peke yake utaona yakuwa hayo "madeni" tayari yashajifuta!

Haina neno tuendelee na mnakasha.

Shukran.Cc; Ritz,JokaKuu,Nguruvi3
Hebu tuambie mambo yaliongezwa katika article of union, mnagapi yalikuwa na manufaa kwa Tanganyika. FYI yalikuwa 11 yakawa 22 na sasa nadhani ni 32.
Tuwekee hayo ili tujue kuwa madeni yanajifuta vipi.
 
Sawa MS; Baada ya Salaam, At last utaona jinsi ambavyo inawakera watu kupata impression kuwa ONE family is being amplified juu ya Watanzania wengine. You are a good writer MS. No doubt. Lakini mzee MS umeruhusu sana prejudice in your sights. NINA UHAKIKA KAMA NYERERE wazazi wangeingia in this country kama Mamluki wa kwenda KUUA wahehe na wasambaa kule Lushoto, saa hizi your books zingekuwa zimejaa idadi (estimates) za hao ambao BABU au BABA yake Nyerere aliua huko kwenye ajira yake ya kuwauwa Watanganyika. But you have with caution just said wazazi wa Fulani waliingia kama MAMLUKI. Ukafanya stahiki ya heshima kwa familia husika ukaishia hapo. Lakini unapokuja kwa yule unayemchukia inabidi hata aliye mpa Matango siku Fulani iwe historia ya Kitaifa. Hutumii mizania ya HAKI. One guy whose family started its establishment with the blood of Tanganyikans on its hand (we know what mercenaries DO) is being elevated at the expense ya another person whose fault is to have a different faith other than yours.

No wonder you see reaction ya people like Zumbe, kwa vile THERE IS NO WAY ON EARTH DAR ALONE AS A CITY/TOWN WOULD HAVE WON INDEPENDENCE WITHOUT THE RESOURCES OF THE UP COUNTRY REGIONS, NO WAY. On the other hand ukiwajibu watu simply kuwa NA NYIE ANDIKENI WHILE YOU CHURN OUT MATERIALS WHICH RIDUCULE the very people who brought hope and joy in their distant lands, I find you to be too assuming. In fact you sound RUDE.

Wickama,
Nimeandika historia kadri ya uwezo wangu.

Ikiwa haikupendezi hiyo ni bahati mbaya.
 
Sideeq,

..je, tumeelewana kwamba Znz ndiyo inainyonya Tgk??

..zaidi, tumekubaliana kwamba kutokana na dhuluma ya muungano dhidi yetu, wa-Tgk ndio tunaopaswa kumlaani Mwalimu Nyerere na siyo nyinyi wa-Zenj??

cc: Nguruvi3, Wickama

Hapana tanganyika haki yake kumhudumia mkewe z'bar ila kama mke anajifanya kujua mume haki yake kuacha ila kama anashindwa kuacha huyo ni mume ----- asie jitambua
 
Last edited by a moderator:
Hapana tanganyika haki yake kumhudumia mkewe z'bar ila kama mke anajifanya kujua mume haki yake kuacha ila kama anashindwa kuacha huyo ni mume ----- asie jitambua

Ohooooo!!!!!!!! weweeee Unamjua Sheikh Farid wewe??? Subiri
 
GombeSugu na Ritz

Nawashaurini kuwa ili muweze kuchambua jambo lolote hata kama ni lakipumbavu basi tulieni kwa dakika 5 hivi kisha mlisome kwa utulivu na hekima na kama hamjaelewa ulizeni mtaambiwa tu!


Ritz

Hujajibu maswali niliyokuuliza juu ya umri wa waasisi wa AA kipindi cha uasisi, lakini hujajibu umeingia mitini
 
Hapana tanganyika haki yake kumhudumia mkewe z'bar ila kama mke anajifanya kujua mume haki yake kuacha ila kama anashindwa kuacha huyo ni mume ----- asie jitambua
Isalia,

..mimi sidhani kama wa-Tanganyika na wa-Zanzibar watapendezwa na lugha uliyotumia hapa.

..jitahidi kuwasilisha ujumbe wako bila kutumia lugha ya kuudhi.
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya tatu...
Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa,[SUP]294[/SUP] katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo.

Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandege, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani. [SUP]295[/SUP]
Ule Mkutano wa Tabora ulikuwa umeacha kovu lake katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Huenda kama si yale masharti ya uchaguzi wa kura tatu, historia ya TANU na kwa hakika ile ya ukoloni Tanganyika isingekuwa hivi ilivyo sasa. Yamkini kusingekuwepo na mgawanyiko katika TANU wala Zuberi Mtemvu asingeunda ANC, na Mashado Plantan - AMNUT; wala suala la udini katika siasa za Tanganyika lisingewekwa katika agenda, jambo ambalo kwa miongo mitatu baada ya uhuru ngurumo zake bado zinasikika na zinatishia utengemano na uthabiti wa nchi. Waislam wanamlaumu Nyerere na Wakristo waliokabidhiwa madaraka ya kutawala nchi kwa msaada mkubwa wa Waislam. Waislam wanadai kuwa wamesalitiwa. Kwa hivi sasa Waislam wako katika mwelekeo wa kujitambua kwa mara ya pili na historia yao yenye mengi sana. Wanaamini majibu ya baadhi ya matatizo yao ya hivi sasa yamo katika historia yao ya zamani.
***
Mjini Dar es Salaam katika msikiti wa Kitumbini hawli husomwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba kumkumbuka Abdulwahid Kleist Sykes. Hii ni hafla ya kifamilia ikihudhuriwa hasa na wana-ndugu. Ukiachia mbali ule wajibu wa Waislam kurehemiana kama ilivyo kawaida katika Uislam, Abdulwahid hufanyiwa hafla hii pale msikitini kwa sababu nyingine. Katika umri wake mfupi, Abdulwahid alikuwa akiswali pale msikitini na katika msikiti ule ndipo aliposwaliwa swala yake ya mwisho kabla ya kupelekwa kuzikwa. Abdulwahid alikuwa mtu mashuhuri katika jamii ya Waislam Dar es Salaam. Alifanya shughuli nyingi chini ya Al Jamiatul Islamiyya. Halikadhalika alikuwa katibu baadae rais wa TAA. Ingawa historia ya Tanzania bado haijamtambua mchango wake ni wazi kuwa Abdulwahid ndiye aliyekuwa bongo katika kuasisi TANU chama ambacho kilikuja kuwaunganisha wananchi wa Tanganyika katika kudai uhuru wao kwa Waingereza.
Marika ya Abdulwahid bado wa hai na baadhi yao wanaswali pale msikitini. Huwa wanafurahishwa na kumbukumbu hii ya kumrehemu mwenzao. Karibu walio wengi ni maveterani wa TANU ya miaka ya 1950. Hivi sasa wao ni wazee na kwa uchungu hawana haja na siasa. Ukiacha ndugu wa marehemu Abdulwahid (sasa hivi wanajumuika na wajukuu zake), marafiki wa karibu na wanachama wa zamani wa TANU, hakuna hata mtu mmoja katika Chama cha Mapinduzi (chama kilichorithi nafasi ya TANU) anaemkumbuka. Jina la Abdulwahid halitajwi kabisa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika au katika historia ya kuasisi TANU. Juu ya haya yote Abdulwahid ndiye aliyewasha cheche za kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Jopo la wana-historia wa Chama Cha Mapinduzi waliopewa jukumu la kutafiti na kuandika historia rasmi ya TANU, hakuna hata sehemu moja waliyotaja jina la Abdulwahid katika kitabu kizima.[SUP]296[/SUP] Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa. Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule. Kitendo hiki kimeondoa hadhi na heshima ya wazalendo wengi waliopigania nchi hii na halikadhalika kimeiondolea TAA heshima ya kuitwa chama cha siasa. Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano:
Sasa inakaribia mwaka mmoja toka iundwe Tanganyika African National Union na katika kipindi hiki chama kimekua kikipata nguvu siku hadi siku, wakati mwingine chini ya upinzani mkubwa. Kama mnavyofahamu chama hiki ni badala ya Tanganyika African Union ambayo ilikuwa sawasawa na chama cha majadiliano.[SUP]297[/SUP]
Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii.[SUP]298[/SUP] Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), [SUP]299[/SUP] halikadhalika Japhet na Seaton (1966).[SUP]300[/SUP] TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), [SUP]301[/SUP] Nyerere (1953) [SUP]302[/SUP] aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri. Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema:
Tanganyika African National Union kwa mtazamo mmoja ni chama kipya, lakini kwa mtazamo mwingine ni chama kikongwe. TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu.

Itaendelea...
 
Nguruvi umenisikitisha sana kwa jinsi unavyo wazungumzia wa Znz yani wewe unaposema sasa hivi hakuna tena "cold war" kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Nyerere na Karume walituunganisha kutokana na "cold war" hayo sio maneno sahihi kwa wa znz kwahiyo wazazibar walitumika kama beleshi ujenzi ukiisha linawekwa stoo na hizo cc uliowataja nikuulize unajua maana ya neno kafir? mkubwa wacha chuki na waznz haya maneno kwamba waznz ni tegemezi angeyazungumza baba yako wa taifa sio wewe nakusikitikia sana tuendelee na mnakasha. ahsante

Sheikh Farid,

Nakuelewa kiundani hayo majonzi yakupatayo. Unajua hawa Nguruvi3 na JokaKuu,mimi binafsi ni kati ya jamaa ninaowaheshimu mno.

Ndo maana huwa napata huzuni wakija na matendo au kauli za ajabu ajabu na zenye kuonyesha chuki baina ya WaTanzania. Wapo jamaa wanaweza kuzungumza chochote na lolote hapa jamvini sisi tukadharau. Lakini hawa JokaKuu na Nguruvi3 nafikiri wanashindwa kujua yakuwa kuna wengine tunathamini michango yao hapa jamvini.

Yaani tokea ije khabari ya Zanzibar "wamefunguka" kikweli! kwa hili inanilazim nimsifu ndugu yangu Mag3,japo anachangia lakini kauli zake zimekua ni adilifu mno.

Halafu Nguruvi3,kama dasturi yake anatoa excuse yakuwa kwenye Family tree yake pia kuna Waislamu na WaZanzibary. Ananikumbusha hawa jamaa zetu wa Kizungu huku...wakianza kushutumiwa ubaguzi wa rangi,basi ghafla wataanza kutaja nasaba na ku-count how many Cousins and Black friends they have!ahaha!!

Hayo uyazungumzayo hapo juu,ndo mpaka leo yanaleta zogo na utata mwingi kule kwenye zilizokua Eastern Block Countries. Kwa mfano mpaka kesho Poland ana hasama kubwa mno na Russia. Kwamba anahisi kumbe USSR walikuwa wala sio ndugu au marafiki wa kweli bali tu ni wanafiki na wazandik walikua wakiitumia Poland as a "buffer Zone"!

Sasa hapa ndo Nguruvi3 na JokaKuu unaona language watumiayo ina dalili zoote za hayo. Kingine labda wasichofahamu ni kuwa;lolote litakalotokea na kuvunja Muungano huo basi hakuna ati atakaekua "mshindi wa kudumu" kati ya Tanganyika au Zanzibar.

Mimi binafsi,sisemi wala sioni ubaya wa kuzungumzia haya matata ya Muungano kwa kina. Tatizo tujiepushe na hizo colourful languages. Hazijengi bali zinabomoa tu!

Embu fikiria,JokaKuu amefikia ati mpaka ya kusema sisi huku Bara Wazungu hawana ubaya na sisi lakini Waarabu tu ndio tunawaona wabaya kwa ile biashara ya Utumwa!? Hapa napata wasiwasi kama kweli hawa ndugu zetu wanaelewa kiundani Historia ya hao Wazungu wanaowatetea dhidi ya nchi/Bara letu. Au kwa sasa kuna WaTanzania wameamua kuweka kando baadhi ya ukweli wa kiHistoria kwa muda ili "kuwashughulikia" WaZanzibary!?

Wanasahau yakuwa atrocities na vita vingi mno walopiganishwa WaZanzibary na Nyerere,si kwa kupenda au hata kushauriwa kama kanuni na vipengele kadhaa vya makubaliano au kanuni za mkataba wa Muungano inavyotaka,hasha asilan!

Na kuna vituko na vitimbi vingi mno walivyokua wanaburuzwa WaZanzibary bila ya maridhia, na kinyume ya vipengele vya kisharia ya huo "mkataba wa Muungano". Na haya mambo yanaendelea mpaka kesho.

Nyerere,tangia enzi zake alikua akitia ndani Viongozi au wananchi wowote wa Zanzibar waliokua aidha wakijadili,kudai haki au kutaka kujitoa kabisa kwenye huo "Muungano".

Sasa wao wanafikiri Nyerere alikua hajui alichokua anakifanya miaka yoote hiyo!? Au hawa jamaa zangu wanafikiri Nyerere alikua na uchungu na kuwapenda WaZanzibary kuliko WaTanganyika!?ahaha!!

Nyerere alikua ni master of political calculations/games...hii haina ubishi. Kwa hiyo lazim aliona manufaa makubwa saana ya Zanzibar kuliko hasara yake. Na hii ni kwa kila kitu. Ulinzi,Usalama,senti na mengineyo mengi tu.

Namkumbusha ndugu yangu Nguruvi3 japo kiduchu,miaka hiyo ya mwanzo Zanzibar haikutakiwa kuchangia kwenye masuala ya Ulinzi wala Usalama. Zanzibar tayari ilikua na Mkuu wa Majeshi na Amir Jeshi Mkuu alikua ni Rais wa Zanzibar,na Idara ya Usalama Wa Taifa ilokua huru bila ya kuhusishwa kwenye Serikalim ya Muungano. Mkuu wa Majeshi alikua Yusuf Himid,Mkurugenzi wa Usalama Wa Taifa alikua Seif Bakari "Kiwavi" na Amiri Jeshi Mkuu alikua Rais Abeid Karume.

Zanzibar miaka michache baada ya Muungano,walikua tayari na Jeshi kali mno la Maji/Navy lililokua linaheshimika kupita kiasi katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Mafunzo ya kijeshi/kiunamaji,misaada na vifaa vyoote na ushirikiano wa karibu ulikua ukitolewa na enzi ile ikiitwa Shirikisho la Kijarumani/Ujerumani ya Mashariki.

Hivi vitu vyoote havikumpendeza Nyerere asilan,na mara kadhaa alikua akisikika na kulalama yakuwa wale WaZanzibary hawaaminiki,siku yoyote wanaweza kuja kutuvamia. Oscar Kambona ndie aliekua akimtuliza,kwa sababu Kambona tangia awali alikua na mahusiano mazuri mno na viongozi kadhaa wa ngazi za juu na sehemu nyeti pale Unguja.

Ndio maana mara tu baada ya Rais Karume kuuwawa kwenye yale Mapinduzi yaloshindikina;Nyerere alitumia kila ghila na dhuluma kuhakikisha anamburuza Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi....Usalama waTaifa ukaunganishwa,Amiri Jeshi Mkuu wa zanzibar pia akawa yeye Nyerere. Kikosi mahiri cha Navy cha Serikali ya Zanzibar kikavunjwa. Wakaambiwa ati waunde KMKM maana yake ati "Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo"!?ahaha!! Yaani Nyerere UHUNI wake hauna hata haya,hivi Zanzibar kuna biashara au magendo gani tena enzi hiyo ya mpaka kusababisha jeshi zima la Maji/Navy livunjwe ili kufanya shughuli hiyo!?ahaha!!.....Ilipofika 1977,ndipo akahitimisha ule mburuzo kwa kuvunja kabisa ASP. Kwa kifupi ilobaki ni khadith tu,na ndo leo tupo hapa jamvini ndugu yangu Nguruvi3 anataka kunifungashia virago nende zangu "kwetu" Bwejuu/Bwegejuu!ahaha!!

Kwa kifupi, nahisi baadhi ya ndugu zetu wengi wa KiTanganyika hawajui yakuwa sisi pia ni wabara, na Tanganyika ni kwetu labda hata kuliko wao wajionavyo au kufikiria. Ndo maana mie hucheka pale Nguruvi3,anaposema WaZanzibary ati watafunganya mabegi kurudi "kwao"...ninamuhurumia maana tusije mrejesha yeye kwenye asili yao labda huko Guinea Bissau au Gambia!!

Kwa sababu hivi vizazi vingi viliopo hapo Tanzania Bara ni Wahamiaji tu kutoka maeneo/sehemu nyingine za Afrika karne chache zilizopita na kuja kujihifadhi hapo Tanganyika kutokana na madhila yalowakumba huko makwao.

Ndo maana takupa mfano,UTangayika wa Ndugu zangu JokaKuu na Nguruvi3 ukichanganya ndio labda, tena labda watafikia Ubara/UTanganyika wa Gombesugu mmoja!

Nisikuchose Al Akhiy,na Insha Allah tuendelee na mnakasha.

Shukran.

Cc;Ritz,Nambokola,JokaKuu,Mag3,Nguruvi3,Sheikh Farid


 
Heee ! wenzangu yamekuwa hayo.

Mimi nimeuliza maswali mbona nashambuliwa kiasi hiki.
Tena imefikia mahali naitwa fataani, nimetumwa n.k. Hivi kwanini watu wanaghadhabu nami.
Yaani hata mahali nisipoingia mtu atatafuta upenyo apitishe jina langu ilimradi tu.

Gombesugu, Mohamed ndiye mwandishi na msomi pekee ninaye mfahamu anayefanya ''self quotation'' au reference.
Huko mimi sipo.

Haya tunayoongea hapa tuna ufahamu nayo. Kama tungekuwa hatujui tusingemvua Mohamed nguo, tukamfunga mikono na miguu kwa nguo hizo na hata kumchapa usoni na mtambara yake.

Wewe ulijua kuwa balozi hakuhutubia Bunge! Tulimuuliza akaingia na tarehe tukamchapa nazo usoni.
Sasa hivi amebaki na Mkoba wa Ibadan! FYI we have strong and wide background! Ninaiangalia dunia kwa mtazamo mpana siyo wa kipata au mfenesini! Gombesugu!

Kama unataka link n.k. tutoa, kwani si unataka link za jinsi gani Rukara alipata passport ya Tz.
Unataka tutaje hata ufuska na majina ya wahusika! ndivyo unataka?
Mimi nasitiri watu na kujisitiri, sipiti nikizungumzia vyumba vya watu na vitoweo hovyo barabarani, nina weledi.

Najua kinachowatia hasira ni sheikh Amir kuitwa Mnafiki na mfitini mkubwa.
Mimi nasema Amir ni mnafiki mkubwa sana nimeeleza sababu kwa kufanya quotation ya maneno ya Mohamed ili muamini zaidi. Nasema Bibi Titi alikuwa na uadilifu kuliko huyu mnafiki mkubwa anayeitwa sheikh.
Mnafiki huyu habri zake za kinafiki zinajulikana.

Nafahamu pia hasira ni kutokana na miba ya muungano, hasa kwa wznz! nawe unajua hilo kwahiyo sitegemei kusikia neno zuri kutoka kwako linalonihusu. Guess what, mimi spade naita spade sisemi ni big spoon!

Kama hakuna majibu ya maswali nitaleta link, subra yavuta heri

Mkuu

Simamia ukweli, tupo hapa yapata mwezi wa tano sasa kwaajili ya kulifua kaniki aliloharibu Mohamed Said, lazima litakate bila kuremba wala kuparamaa!

Tupo kwaajili ya kuufuta uongo na kuweka ukweli!

Tumeshabaini na kuweka ukweli kuwa wanaotetewa na kikundi hiki ambacho ni radical Muslims kinachoongozwa na Mohamed Said walikuwa ni WAASI wa TANU na serikali halali ya Tanganyika!

Na zaidi kadiri tunavyozidi kupekua tumegundua kuwa yule wanae muabudu Shehe Hassan Bin Amir alikuwa ni mchochezi, mnafiki na HAINI ambae serikali yoyote ile duniani ingemuondoa duniani, lakini kwa heshima na hekima za Mwalimu Nyerere amfukuza katika ardhi ya Tanganyika baada ya kila juhudi za kumpa kazi ya kurekebisha yale aliyokuwa akiyahubiri nje ya serikali (misikitini) kugoma!

Sasa hapo mlitaka mwalimu amfanye nini huyu fedhuri na hasidi?

Ange achwa andelee kuvuruga amani ya nchi?
 
Hayo mengine umeyasema wewe kwa kukazia tusiandikie mate na wino upo hebu ngoja tuangalie huu mpini.


Julius Nyerere"‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.



Julius Nyerere"Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Shariff Ritz,

Naona unarejea tena kwa bayana zako adimu!ahaha!!

Hapo umemwacha Nyerere mwenyewe amjibu ndugu yetu ZumbeMkuu...

Shukran.
 
GombeSugu na Ritz

Nawashaurini kuwa ili muweze kuchambua jambo lolote hata kama ni lakipumbavu basi tulieni kwa dakika 5 hivi kisha mlisome kwa utulivu na hekima na kama hamjaelewa ulizeni mtaambiwa tu!


Ritz

Hujajibu maswali niliyokuuliza juu ya umri wa waasisi wa AA kipindi cha uasisi, lakini hujajibu umeingia mitini
Yericko Nyerere,
Mimi ata siku moja siwezi kukukimbia wewe humu ukumbini najua hujui chochote mimi binafsi nimeishakuuliza maswali mengi unakimbia mimi takujibu kwa faida ya wanaumbi siyo wewe.
Hujajibu maswali niliyokuuliza juu ya umri wa waasisi wa AA kipindi cha uasisi, lakini hujajibu umeingia mitini
Waasisi wa AA ni Kleist Sykes , Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu,Raikes Kusi. Dr. James Aggrey, hawa ndiyo waasisi wa AA, Kleist Sykes wakati huo mwaka 1929 alikuwa na umri wa miaka 35. na mimi naomba kukuuliza huyo Askofu Maranta alikuwa na umri gani wakati wanakutana na huyo Sheikh Issa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom