Iron,Waku Ritz, Mohamed Said, Wickama, nguruvi, WildCard, JokaKuu, Yericko Nyerere gombesungu na wengine wengi, heshima kwenu! Nimefuatilia mnakasha huu na hakika yapo mengi ya kujifunza ingawa yapo pia yanayohitaji ufafanuzi. Ni kama vile tunataka kuandika historia ya Taifa hili kwa misingi ya udini. Sasa mimi sio mwanahistoria. Ni mwanasheria tena nimezaliwa baada ya uhuru. Mohamed Said, kama hawa waislamu walishiriki kikamilifu, na kama walikuwa wengi, nini kimewafanya wafutike kwenye historia ya uhuru? Yaani ilikuwaje wao wenyewe wasisimame kidete kuweka historia sawa, hasa katika maandishi?
Halafu nisaidieni kujua mchango wa watu wa kaskazini (Wachaga/wameru nk) katika uhuru? Mchango wa wakina Marealle, Shangali, Mzee Mbowe upo? Mtoto wa Marealle amewahi kunijuza kuwa Mbowe ni mtoto wa Nyerere kwa sababu baba yake Mbowe alikuwa anam-accomodate Nyerere na kuchangia safari zake nje katika harakati za uhuru. Lengo sio kujua ubini wa Mbowe bali kujua ushiriki wa wazee hawa wa kaskazini katika Uhuru. Inawezekana mmeshasemea hapo nyuma, lakini kwa urefu wa hoja hii mnaweza kunisaidia tena au kunipa post rejea! Shukrani.
..alichoandika Mohamed Said ni moja kati ya plots nyingi zinazounda kitu kizima, yaani harakati za uhuru wa Tanganyika.
..anachoelezea yeye ni mchango wa wanaharakati wa D'Salaam, na wanaharakati wa Kiislamu, ktk kupigania uhuru wa Tanganyika.
..wa-Tanganyika wa maeneo mengine, wa imani mbalimbali, wa rangi mbalimbali, nao walikuwa na mchango kufanikisha juhudi hizo. Kwa mfano, kulingana na maelezo ya John Illife kuna wakati 2/3 ya michango ya kuendesha chama cha Tanu ilikuwa inatoka Sukuma Land.
..wakati mwingine ukisoma mjadala huu unaweza kufikiri kwamba maeneo mengine walikuwa wamelala usingizi, wakiwa wameridhika na utawala wa kikoloni. hilo si kweli.
..Mkoloni alikuwa amechokwa ktk maeneo mengi ya Tanganyika. tayari wananchi walikuwa wameshaanza kuji-organize kuukataa utawala wa Mwingereza. Mazingira hayo ndiyo yaliyofanya Tanu iungwe mkono Tanganyika nzima.
..Watanzania hatuna utamaduni wa kuweka kuandika na kuweka kumbukumbu ya michango yetu. nadhani tatizo hilo limejitokeza waziwazi ktk mjadala huu. wasiwasi wangu ni kwamba, inawezekana ktk waasisi wa harakati za uhuru, ni familia ya kina Sykes tu walioweka kumbukumbu ya mchango wao.
cc: Wickama, gombesugu, Mag3, Ritz, THE BIG SHOW,
Last edited by a moderator: