Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hasanalis,
Wakati wa kupambana na ukoloni Uislam ulitumika kama "ideology."

Katika mgomo wa makuli wa 1947 kilifanyika kisomo shambani kwa
Mohamed Abeid bonde la Msimbazi.

Wakati TANU bado iko changa kilifanyika kisomo cha akina Mshume
Kiyate baada ya afisa wa kikoloni kufanya njama dhidi ya Abdu Sykes
kwa kuunda TANU na kuuza kadi za TANU katika ofisi za serikali.

Abdu Sykes alifanyiwa kisomo ambacho nishakieleza hapa jamvini kwa
kirefu.

Nyerere akafanyiwa kisomo 1956 na Sheikh Mohamed Yusuf Badi
alipokwenda Lindi kwa mara ya pili kisha kikafuatia kisomo maarufu
kwa Jumbe Tambaza.

Rashid Ali Meli alipotaka kushtakiwa kwa kutoa hela za Dar Municipal
Council kumpa Idd Faiz Mafongo atunishe mfuko wa safari ya Nyerere
UNO kisomo kilifanywa.

Nyerere alipokwenda Tanga kuweka mikakati ya Kura Tatu na akina
Sheikh Rashid Sembe kisomo kilifanywa Mnyanjani.

Sasa hii saum Bagamoyo nyumbani kwa Sheikh Mohamed Ramiya
Khalifa Tariqa Qadiriyya ilikuwa mwendelezo.
 
Kuongea na Mkristu juu ya mfumo kristu Tanzania ni sawa na kuopngea na Mbuzi au ng'ombe unadhani atakusikia?Dawa kubwa ni action since action speaks more than words@all Christians in this Christian Forum!
Ni "action" zipi hizo mkuu?
 
Mkuu gombesugu hapa utagombana na Mzee wetu wa gerezani Mohamed Said yeye anasema Nyerere hakuwakumbuka wazee wake wala hakuwataja kabisaaaaaaaaaa.Wewe unasema aliwapa "heshma ya kipekee na kuwataja tu wazee wa Mzizima na khasa waIslam kwenye hotuba ya muago tena huku akiwataja majina na nasaba zao"

Hakika gombesugu umemuumbua mchana kweupe Mzee wetu wa Gerezani.Namsubiri kwa hamu kubwa sijui atasema nini baada ya kamanda wake kumgeuka.Mzee wetu hodari sana wa lugha najua lazima atakuja na misamiati mipya ya Gerezani ha ha ha ha.



 
Last edited by a moderator:
Kila binadamu ana historia yake.mHistoria hiyo yaweza kuwa mbaya au nzuri. Hata hivyo jambo moja ni kweli juu ya historia, kuwa historia imepita na hatuwezi kubadilisha kilichohistoria. Jambo la kweli ni kwamba tunaweza leo tukasimamia katika ukweli ili tuwe na historia nzuri miaka 50 au 100 ijayo. Nimshukuru Mohamed Said kwa maelekezo ya kitabu. Nitakisoma.

Pamoja na hayo, nina mambo machache ninayotaka kusema hapa.
1. Ukiangalia kwa kina mtiririko wa mada hapa, utagundua kuwa haswa haswa ni kati ya Uislamu na Ukristo. Kwamba Nyerere alifanya jitahada za makusudi, si tuu kutowatambua wiaslamu waliopigania uhuru, bali pia kuwakandamiza waislamu katika maendeleo. Wapo ambao hawataki kutamka kuwa Nyerere ni baba wa Taifa na wengine wanamtamka kwa kejeli. Vyovyote vile iwavyo, hili halimwongezei wala kumpunguzia kitu Nyerere na ukweli unabaki kuwa amekuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, na dunia imemtambua kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wetu.

2.Kuhusu malalamiko ya waislamu wa muda mrefu sidhani kwamba Nyerere anapaswa kubeba mzigo huo pekee. Pia hawezi kukwepa kabisa maana amekuwa raisi wa kwanza kwa miaka zaidi ya 20. Sababu za kwanini waislamu wanaona wapo nyuma ni nyingi na nyingine zimechangiwa na waislamu wenyewe. Hebu tazama waislamu wa Moshi/Arusha na wale wa mkoa wa Lindi! Kwanini maendeleo yao ni tofauti ingawa wote ni waislamu? Kwanini fursa zao kuendelea ni kubwa kwa baadhi ya maeneo na maeneo mengine ni ndogo?

3.Matatizo ya waislamu hayatatatuliwa kwa waislamu kusema 'ni wakati wetu sasa'. Kwamba 'wametukandamiza' vya kutosha. Hayawezi pia kutatuliwa kwa vikao vya wakristo na waislamu. Wala serikali haiwezi kutatua matatizo ya waislamu. Nionavyo mimi, suluhu ipo kwa waislamu wenyewe. Kwanza katika umoja wao watambue nini vipaumbele vyao. Waanze kuvitekeleza halafu tuone serikali gani itawazuia na kwasababu gani. Lawama hizi hazitawapelekea popote. Mimi nimetembea Kigoma, Tabora, Morogoro, Pwani, Lindi, Kilimanjaro nk. Nimeona misikiti mikubwa sana katika vijiji ambavyo maisha ya watu wake ni duni. Sasa nikajiuliza, kama upo uwezo wa kujenga haya, kwanini wasiende hatua moja zaidi kuhusu shule, zahanati, vyuo nk nk? Jukumu la serikali libakie kuwa ni kutoa fursa sawa, yaani ardhi, ruzuku, rasilimali watu nk nk

4. Upo mkakati wa kusema sasa raisi awe Mwisalmu. Kama kweli tunataka maendeleo lazima tuwaze zaidi ya hapa. Tumekuwa na maraisi wawili waislamu. Na tumeona Kikwete aliwekwa kimkakati (Hata Lipumba amekiri hilo). Na kwakweli amefanya mengi katika hayo. Bado sisi tumekuwa wakwanza kulalamikia mfumo Kristo! Kumbe kuwa na raisi mwislamu na mawaziri wote, na hata wakuu wa mikoa bado inaweza isisitatue matatizo yetu. Zipo nchi zinazoongozwa na dola ya kiislamu lakini bado malalamiko yapo kila kukicha.Tunahitaji kama taifa kuwaza beyond our religions.

5.Nimeangalia mafundisho ya baadhi ya mashekhe na hata baadhi ya michango ya watu hapa, utaona chuki ya wazi dhidi ya watu wa dini mbili hizi. Sioni kama chuki itatusaidia. Wapo ambao wamehoji kwanini baadhi ya waislamu walishirikiana na makafiri! Kwa chuki hizi,matatizo yetu hayaishi. Wengi hapa ni wasomi. Hivi kweli ukinichukia mimi kama Mkristo ndio unapataje maendeleo?

Ndio maana nasema maendeleo ya waislamu yatapatikana kama waislamu wenyewe watakaa, wakaainisha vipaumbele vyao na wakaanza kuvifanyia kazi. Serikali ifanye kazi ya promoter! Na maendeleo ya waislamu na wakristo yataonekana wazi kama Tanzania kwa ujumla wake itaendelea. Tukijiangalia kwa jicho la Uislamu na Ukristo, mwaka 2061 na hata 3011 tutakuwa bado tunazungumzia jambo hili, na pengine katika hali mbaya zaidi.

Inawezekana nimetoka nje ya mada, lakini nadhani ni vyema tushauri pia nini kifanyike ili baadae tuwe na historia sahihi ya nchi yetu. Mahali nimekosea naomba nisahihishwe, maana mimi ni kijana bado na pengine nimetawaliwa na hoja mufilisi!
 
Last edited by a moderator:

Joka Kuu.

Nilipo Underline.

Nimependa sana uchambuzi huo wa kuonyesha kuwa unakubali kuwa wengi ni mbumbumbu na hawapendi kujifunza lakin pia ni wavivu wa kujisomea hata kama Data zote mnazo. Hili ni tatizo kubwa sana Tz kuna tafiti nyingi sana zimefanywa na zinafanwa lakin matokeo ya tafiti hizo huwa yanawekwa kabatini na watu wengi kupenda kushabikia maneno ya vijiweni.

Sasa hebu tufafanulia uchunguzi huo kuhusu Muungano wenu mpaka kupelekea wewe kutoa fatwa niliyo BLUE umeufanyia wapi?. Kwani mimi nimekusaidia vya kutosha sana kuwa ukitaka mambo a uchumi wa nchi hizo mbili yaani Tanganyika na Znz wewe pitia RIPOTI ya wataalamu wa nchi hizo mbili ambayo wanaitoa kila Mwaka ya JOINT FINANCE COMMISSION itakupa mwanga zaidi. Nikazidi kukusaidia na kukueleza hata afisi zao zilio hapo Dar (Sukari House) .

Sasa ahali yangu nikusaidiaje tena? Mimi nakusihi ipitie ripoti hiyo ambayo io wazi kabisa kwa kila mtu kisha tuweke uzi maalum tujadili kwani mimi Uchumi ndio fani yangu tutailimishana kwa kina sana.

Na la kukuongezea zaidi pitia vile vile ripoti ya mwaka ya BOT uone kila unachodai wewe na Nguruvi3 kama mpo sahihi.

Mimi kama mchumi kila mwaka napoteza nguvu na muda wangu kupata hizo ripoti na nashauri. Lakin all in all Znz wanadhulumika kwa mengi sana.

Punguza porojo pitia hizo ripoti kisha tukae kikao kuzijadili.

Pole sana

cc: nambokola, Wickama, gombesugu, SHEIKH FARID, Nguruvi3
 

Nilipo RED.

Vile vile linganisha wakristo wa Moshi/ Arusha na wale wa Mtwara / Lindi je wapo sawa kimaendeleo.

Mimi ningekusihi kama unataka linganisha wewe chukulia wakristo wa Arusha. Moshi na wale waislam wa Znz wapi wapo juu kimaendeleo utaligundua hilo
.

Na jiulize je Uchumi wa Tanganyika unamilikiwa na watu wa gani pitia iimani zao?

Tuliza akili na fanya tafiti katika nyanja hii ya uchumi na sio kukurupuka.

 
Hasanalis,
Wakati wa kupambana na ukoloni Uislam ulitumika kama "ideology."
....................................
mzee wangu MS hapo ndipo historia inapopotoshwa,
labda useme kwa maeneo yaliyokuwa na waislam wengi ndo Uislam ulipotumika kama ''ideology''
Iringa,Mbeya, Bukoba, Kilimanjaro na kwingineko nako Ukristo umetumika kama ''ideology'' maana na ibada zimefanywa nyingi na hatimaye uhuru umepatikana, ndivyo siasa zinavyokuwa, ili uweze kukubalika kwa DINI zote basi unapaswa uvae kofia zote mbili, kofia ya tatu (wapagani na dini nyingine) naona hazitajwi...
Mzee MS usitugombanishe sisi ni Ndugu.
 
Ngongo, wacha uchokozi wewe! uanataka mzee wa watu jasho la uzeeni lianze kumtoka. Atakwambia na wewe uandike historia ya wazee wako, kwi, kwi, kwi!
 

Sasa hapo sijakupuruka. Nimeuliza swali ili kupata jibu. Mimi nimeona kama ni sehemu nzuri ya kuanzia. Vyema umesema tuwatazame wa Zanzibar pia. Sijafika Zanzibar ndio maana sijataja. Sasa swali linakuja, kuwa wote ni waislamu. Kwanini serikali hii ya mfumo Kristo imeruhusu maendeleo ya waislamu wa sehemu moja na kuzuia nyingine? Halafu kumbe huko walipowaislamu wengi wanaoonekana wameachwa wapo na wakristo pia?Ndio maana kama umenielewa nimesema tatizo letu kama nchi ni kubwa zaidi ya Ukristo na Uislamu! Sijui kama huko ni kukurupuka.

Kwenye suala la uchumi sijafanya tafiti nani anashika uchumi wa nchi hii. Pengine naweza pia kukosa muda wa kufanya utafiti huo. Hivyo kama unafahamu,vyema unielimishe. Nitashukuru
 

Zumbemkuu,
Kwani kunatatizo gani na wewe ukaandika ukasema mathalan, "Mkono wa
kulia wa Nyerere alisimama Askofu Gilbert wa Kanisa Katoliki Peramiho...
ilikuwa nyumbani kwa Mama Janeth na usiku kucha ziliimbwa pambio na hata
ilipofika alfajir misa ya pamoja ikafanyika...wengi waliamini kuwa kwa pale sasa
walipofika siku za mkoloni Tanganyika zilikuwa zinahesabika..."

Je hamna kitu mfano wa hiki katika harakati za kupigania uhuru?

Kuhusu Wapagani nijuvye mchango wao tuutie katika historia hii na tutayarishe
medali hata ikiwa "posthumous" kama ile alotunikiwa Abdul Sykes.
 
baasi babu umesomeka,
nia yangu ya kuja kukuona iko pale pale,
ntakuja nipate kikombe cha gahawa kwako, ila tu hasira za JF ziishie hapa hapa, teh teh teh teh
 
Ngongo, wacha uchokozi wewe! uanataka mzee wa watu jasho la uzeeni lianze kumtoka. Atakwambia na wewe uandike historia ya wazee wako, kwi, kwi, kwi!

Kamanda umerejea?

Karibu sana tulikukumbuka sana kwa visu vyako vya mifupani!

Karibu karibu mkuu!

Bila shaka Zali la Mentali nae atarejea punde!
 
baasi babu umesomeka,
nia yangu ya kuja kukuona iko pale pale,
ntakuja nipate kikombe cha gahawa kwako, ila tu hasira za JF ziishie hapa hapa, teh teh teh teh

Zumbemkuu,
Karibu ndugu yangu.

Umepata kusoma tusi kutoka kwangu?

Sina hasira ndugu yangu ndio maana unaniona
bado naendelea na mjadala juu ya yote.

Kebehi, dharau, vijembe, matusi, kuchekwa uzee nk.
 
Zumbemkuu,
Karibu ndugu yangu.

Umepata kusoma tusi kutoka kwangu?

Sina hasira ndugu yangu ndio maana unaniona
bado naendelea na mjadala juu ya yote.

Kebehi, dharau, vijembe, matusi, kuchekwa uzee nk.

sio kebehi, dharau na vijembe mkuu, watu wanajaribu kuweka historia sawa, Nguruvi3 anasema 15yrs ya historia ya uongo kwishney.
 
Last edited by a moderator:
.........etc

Pili, futa sentensi kuhusu uislam kutumika kama ideology. Isijifike mahali unashindwa kujibu hoja itakayotokana na kauli hiyo. Acha kabisa kauli hiyo! Uache Uislam kama dini na wewe endelea na yako, tafadhali acha kabisa huo ushabiki.
Kuna tatizo na kauli hiyo, nakusetiri kwanza kwa kusema usirudie tena kuisema! futa kabisa.

Tatu, kuna kitu kinaitwa Amnesia! sina hakika kama umeshawahi kukisikia
 
Kamanda umerejea?

Karibu sana tulikukumbuka sana kwa visu vyako vya mifupani!

Karibu karibu mkuu!

Bila shaka Zali la Mentali nae atarejea punde!

Unavikumbuka visu vyake poa lakini wengine tumepigwa ban bila ya kujua kosa inshaalah mnakasha uendelee.
 
Zumbemkuu,
Karibu ndugu yangu.

Umepata kusoma tusi kutoka kwangu?

Sina hasira ndugu yangu ndio maana unaniona
bado naendelea na mjadala juu ya yote.

Kebehi, dharau, vijembe, matusi, kuchekwa uzee nk.

Asalaam aleykum mzee MS kwa uwezo wa allah nimerudi pole sana kwa matusi na vijembe,kebehi kuwa mvumilivu hivyo hivyo sisi tuendelee kufyonza elimu kwako ukweli utajulikana tu.
 

Nguruvi unataka kusema mzee MS ana "AMNESIA" dah kweli umemchoka mzee nakusikitikia sana kwahilo nionyeshe mahali mzee kaandika kitu akasahau iwe ni tusi au kebehi au kwasababu amemwambia Ritz huna ujualo kuhusu Rashid Kayugwa ndio povu linakutoka hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…