Zumbemkuu,
Kwani kunatatizo gani na wewe ukaandika ukasema mathalan, "Mkono wa
kulia wa Nyerere alisimama Askofu Gilbert wa Kanisa Katoliki Peramiho...
ilikuwa nyumbani kwa Mama Janeth na usiku kucha ziliimbwa pambio na hata
ilipofika alfajir misa ya pamoja ikafanyika...wengi waliamini kuwa kwa pale sasa
walipofika siku za mkoloni Tanganyika zilikuwa zinahesabika..."
Je hamna kitu mfano wa hiki katika harakati za kupigania uhuru?
Kuhusu Wapagani nijuvye mchango wao tuutie katika historia hii na tutayarishe
medali hata ikiwa "posthumous" kama ile alotunikiwa Abdul Sykes.
Mohamed Said,
Dhana ya harakati za ukombozi wa Tanganyika haikuwa uhuru wa DINI, wala nadharia ya ukombozi haikuwa DINI,
Utanganyika,Utaifa,Uzalendo na Utu ndio vilikuwa tiketi halisi,
Ndiomaana hata wasio Watanganyika/Wasio wazawa waliungana na waafrika wenzao kupigania ukombozi huo,
Dini nazo zilikuwa na mchango wao, lakini haukuwa ndio kioo cha hatarakati hizo,
Nimeeleza kwa kifupi ushiriki wa Kanisa tena nikaeleza wazi kuwa kanisa lilitafsiri biblia na kuongeza maneno ya kiukombozi ili zisomeke kwa makabila ya maeneo husika kwaajili ya kuhanikiza ukombozi wa mtanganyika,
Sielewi ndugu yangu Mohamed Said unaposema wakristu hawakushiriki katika harakati za ukombozi unamaanisha nini???
Unamaana kuwa uhuru wetu ulipiganiwa kwa tiketi ya DINI?
Kama maana yako inasimamia kwenye idadi ya watu wa dini flani basi tunaweza kuibuka na dhana nyingine nyingi sana na kuua hoja yako chochezi!
Mfano naweza kuibuka na kusema KANISA lilishiriki kupitia muumini weka Julius Nyerere, na bila kanisa (Nyerere) tusingepata uhuru!
Na zaidi naweza kusema kanisa ndilo lililoleta uhuru wa Tanganyika na sio wingi wa wale wazee unaowabebesha dini katika hili!
Ulitaka ushiri wao uweje?
Niwajuze wanajamvi ambao pengine hawajawahi kupata habari hizi juu ya USHIRIKI wa dini hizi mbili katika harakati za ukombozi hasa dini ya kikristu,
Mwalimu Nyerere baada tu ya kurejea kutoka safari yake ya KWANZA ya UNO mwaka 1955, alianza ziara ya mikoa yote ya Tanganyika kwaajili ya SALA na DUA za waamini Mungu,
Jimbo kuu la Iringa chini ya Kasisi Attilio Beltramino ndilo jimbo la kwanza kabisa katika ziara hiyo kwa misa maalumu ya usiku na mchana.
Hakufika peke yake bali alikuwa na kikosi kazi chake cha harakati za Uhuru kikiwajumuisha kama
Julius Kambarage Nyerere, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.
Baada ya kutoka Jimbo kuu la Iringa kikosi kazi hicho kikiongozwa na Julius Nyerere walifika kwa Chifu Adam Sapi nako matambiko yaliendelea kabla ya kuelekea Songea!
Sasa ndugu kama hujui hizi habari usiwadanganye Watanzania na kuwachonganisha!
Kanisa linamengi sana juu ya Tanganyika, halitaki tu kuzungumza kwa uchochezi unaofanywa na akina Mohamed Said wakikingiwa vifua na mkuu wa nchi ambae nae huenda hajui historia ilivyo!