Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sidique; Nilivyomwelewa Nguruvi, na mimi pia hii paper ya Dr Ziddy nilishaisoma, haielekei kwamba sheikh aliwapa fair hearing TANU kama unavyomrai Nguruvi. Jaribu kuisoma hiyo paper. Hakuna mahali sheikh amehudhuria na kutoa Faatiha kwenye mikutano ya TANU, ila alifanya hivyo kila mara kwa mikutano ya wanafunzi wake ambayo ilikuwa pinzani kwa TANU ndipo hadi akaonywa na huyo rafiki yake ambaye ni Mkomoro. Hii ilikuwa punde baada ya kurudi toka kutafuta hiyo university kule Egypt. Jaribu kupata hiyo paper, la sivyo hamtaelewana na Nguruvi anaongelea nini.
Hapo nilipo bold.
Sidhani kama kuna haja tena ya kukujibu wakati wewe mwenyewe huwezi kuthibitisha ila kwa kauli ya haielekei.
 
Zumbemkuu,
Kwani kunatatizo gani na wewe ukaandika ukasema mathalan, "Mkono wa
kulia wa Nyerere alisimama Askofu Gilbert wa Kanisa Katoliki Peramiho...
ilikuwa nyumbani kwa Mama Janeth na usiku kucha ziliimbwa pambio na hata
ilipofika alfajir misa ya pamoja ikafanyika...wengi waliamini kuwa kwa pale sasa
walipofika siku za mkoloni Tanganyika zilikuwa zinahesabika..."

Je hamna kitu mfano wa hiki katika harakati za kupigania uhuru?

Kuhusu Wapagani nijuvye mchango wao tuutie katika historia hii na tutayarishe
medali hata ikiwa "posthumous" kama ile alotunikiwa Abdul Sykes.

Mohamed Said,

Dhana ya harakati za ukombozi wa Tanganyika haikuwa uhuru wa DINI, wala nadharia ya ukombozi haikuwa DINI,

Utanganyika,Utaifa,Uzalendo na Utu ndio vilikuwa tiketi halisi,

Ndiomaana hata wasio Watanganyika/Wasio wazawa waliungana na waafrika wenzao kupigania ukombozi huo,

Dini nazo zilikuwa na mchango wao, lakini haukuwa ndio kioo cha hatarakati hizo,

Nimeeleza kwa kifupi ushiriki wa Kanisa tena nikaeleza wazi kuwa kanisa lilitafsiri biblia na kuongeza maneno ya kiukombozi ili zisomeke kwa makabila ya maeneo husika kwaajili ya kuhanikiza ukombozi wa mtanganyika,

Sielewi ndugu yangu Mohamed Said unaposema wakristu hawakushiriki katika harakati za ukombozi unamaanisha nini???

Unamaana kuwa uhuru wetu ulipiganiwa kwa tiketi ya DINI?
Kama maana yako inasimamia kwenye idadi ya watu wa dini flani basi tunaweza kuibuka na dhana nyingine nyingi sana na kuua hoja yako chochezi!

Mfano naweza kuibuka na kusema KANISA lilishiriki kupitia muumini weka Julius Nyerere, na bila kanisa (Nyerere) tusingepata uhuru!

Na zaidi naweza kusema kanisa ndilo lililoleta uhuru wa Tanganyika na sio wingi wa wale wazee unaowabebesha dini katika hili!

Ulitaka ushiri wao uweje?

Niwajuze wanajamvi ambao pengine hawajawahi kupata habari hizi juu ya USHIRIKI wa dini hizi mbili katika harakati za ukombozi hasa dini ya kikristu,

Mwalimu Nyerere baada tu ya kurejea kutoka safari yake ya KWANZA ya UNO mwaka 1955, alianza ziara ya mikoa yote ya Tanganyika kwaajili ya SALA na DUA za waamini Mungu,

Jimbo kuu la Iringa chini ya Kasisi Attilio Beltramino ndilo jimbo la kwanza kabisa katika ziara hiyo kwa misa maalumu ya usiku na mchana.

Hakufika peke yake bali alikuwa na kikosi kazi chake cha harakati za Uhuru kikiwajumuisha kama

Julius Kambarage Nyerere, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.

Baada ya kutoka Jimbo kuu la Iringa kikosi kazi hicho kikiongozwa na Julius Nyerere walifika kwa Chifu Adam Sapi nako matambiko yaliendelea kabla ya kuelekea Songea!

Sasa ndugu kama hujui hizi habari usiwadanganye Watanzania na kuwachonganisha!

Kanisa linamengi sana juu ya Tanganyika, halitaki tu kuzungumza kwa uchochezi unaofanywa na akina Mohamed Said wakikingiwa vifua na mkuu wa nchi ambae nae huenda hajui historia ilivyo!
 
Kamanda umerejea?

Karibu sana tulikukumbuka sana kwa visu vyako vya mifupani!

Karibu karibu mkuu!

Bila shaka Zali la Mentali nae atarejea punde!
Asante sana mkuu wangu Yericko, kwa muda wote nimekuwa nasoma michango yako mwanana katika uzi huu. Tupo pamoja kamanda.
 
Joka Kuu.

Nilipo Underline.

Nimependa sana uchambuzi huo wa kuonyesha kuwa unakubali kuwa wengi ni mbumbumbu na hawapendi kujifunza lakin pia ni wavivu wa kujisomea hata kama Data zote mnazo. Hili ni tatizo kubwa sana Tz kuna tafiti nyingi sana zimefanywa na zinafanwa lakin matokeo ya tafiti hizo huwa yanawekwa kabatini na watu wengi kupenda kushabikia maneno ya vijiweni.

Sasa hebu tufafanulia uchunguzi huo kuhusu Muungano wenu mpaka kupelekea wewe kutoa fatwa niliyo BLUE umeufanyia wapi?. Kwani mimi nimekusaidia vya kutosha sana kuwa ukitaka mambo a uchumi wa nchi hizo mbili yaani Tanganyika na Znz wewe pitia RIPOTI ya wataalamu wa nchi hizo mbili ambayo wanaitoa kila Mwaka ya JOINT FINANCE COMMISSION itakupa mwanga zaidi. Nikazidi kukusaidia na kukueleza hata afisi zao zilio hapo Dar (Sukari House) .

Sasa ahali yangu nikusaidiaje tena? Mimi nakusihi ipitie ripoti hiyo ambayo io wazi kabisa kwa kila mtu kisha tuweke uzi maalum tujadili kwani mimi Uchumi ndio fani yangu tutailimishana kwa kina sana.

Na la kukuongezea zaidi pitia vile vile ripoti ya mwaka ya BOT uone kila unachodai wewe na Nguruvi3 kama mpo sahihi.

Mimi kama mchumi kila mwaka napoteza nguvu na muda wangu kupata hizo ripoti na nashauri. Lakin all in all Znz wanadhulumika kwa mengi sana.

Punguza porojo pitia hizo ripoti kisha tukae kikao kuzijadili.

Pole sana

cc: nambokola, Wickama, gombesugu, SHEIKH FARID, Nguruvi3
Barubaru,

..Shukrani.

..jambo lingine ambalo napenda kuongeza ni kwamba wenzetu mmefanya utafiti mwingi sana kuhusu muungano.

..mnajishughulisha kuhusu muungano kutuzidi sisi wa-Tanganyika.

..mimi naomba uendelee kutusaidia na kutuelekeza ni wapi tunaweza kupata data zaidi kuhusu muungano.

..naomba kama una ripoti za kamati ya Shelukindo, kamati ya Bomani, kamati ya Mtei[??], utuletee hapa JF tuweze kuzichambua.
 
Last edited by a moderator:
407979_478644612180577_803012316_n.jpg
 
Kwani anatukana tangu arudi hapa jamvini upya?

Kisu kitawapitia wote wazushi, kupitisha kisu hadi mifupani sio matusi

Yericko naomba nikuulize swali la kizushi kwasababu kunakitu nimekikuta kinazungumzwa na kamanda mmoja huku Arusha kwenye kampeni,hivi mahakama ya kadhi ni haki ya waislamu?
 
Mohamed Said,

Dhana ya harakati za ukombozi wa Tanganyika haikuwa uhuru wa DINI, wala nadharia ya ukombozi haikuwa DINI,

Utanganyika,Utaifa,Uzalendo na Utu ndio vilikuwa tiketi halisi,

Ndiomaana hata wasio Watanganyika/Wasio wazawa waliungana na waafrika wenzao kupigania ukombozi huo,

Dini nazo zilikuwa na mchango wao, lakini haukuwa ndio kioo cha hatarakati hizo,

Nimeeleza kwa kifupi ushiriki wa Kanisa tena nikaeleza wazi kuwa kanisa lilitafsiri biblia na kuongeza maneno ya kiukombozi ili zisomeke kwa makabila ya maeneo husika kwaajili ya kuhanikiza ukombozi wa mtanganyika,

Sielewi ndugu yangu Mohamed Said unaposema wakristu hawakushiriki katika harakati za ukombozi unamaanisha nini???

Unamaana kuwa uhuru wetu ulipiganiwa kwa tiketi ya DINI?
Kama maana yako inasimamia kwenye idadi ya watu wa dini flani basi tunaweza kuibuka na dhana nyingine nyingi sana na kuua hoja yako chochezi!

Mfano naweza kuibuka na kusema KANISA lilishiriki kupitia muumini weka Julius Nyerere, na bila kanisa (Nyerere) tusingepata uhuru!

Na zaidi naweza kusema kanisa ndilo lililoleta uhuru wa Tanganyika na sio wingi wa wale wazee unaowabebesha dini katika hili!

Ulitaka ushiri wao uweje?

Niwajuze wanajamvi ambao pengine hawajawahi kupata habari hizi juu ya USHIRIKI wa dini hizi mbili katika harakati za ukombozi hasa dini ya kikristu,

Mwalimu Nyerere baada tu ya kurejea kutoka safari yake ya KWANZA ya UNO mwaka 1955, alianza ziara ya mikoa yote ya Tanganyika kwaajili ya SALA na DUA za waamini Mungu,

Jimbo kuu la Iringa chini ya Kasisi Attilio Beltramino ndilo jimbo la kwanza kabisa katika ziara hiyo kwa misa maalumu ya usiku na mchana.

Hakufika peke yake bali alikuwa na kikosi kazi chake cha harakati za Uhuru kikiwajumuisha kama

Julius Kambarage Nyerere, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.

Baada ya kutoka Jimbo kuu la Iringa kikosi kazi hicho kikiongozwa na Julius Nyerere walifika kwa Chifu Adam Sapi nako matambiko yaliendelea kabla ya kuelekea Songea!

Sasa ndugu kama hujui hizi habari usiwadanganye Watanzania na kuwachonganisha!

Kanisa linamengi sana juu ya Tanganyika, halitaki tu kuzungumza kwa uchochezi unaofanywa na akina Mohamed Said wakikingiwa vifua na mkuu wa nchi ambae nae huenda hajui historia ilivyo!

Yericko,
Wewe unaeleza historia kama uijuavyo na wala mimi sijakutukana wala kukubughudhi.

Wala sijakwita mchochezi.
Binadamu lazima waghitilafiane katika mengi.

Sasa hebu na wewe nisome jinsi nilivyompokea Chief Adam Sapi Mkwawa kutoka nyaraka
za Sykes:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ''Abdulwahid served in Kenya, Ceylon, India and Burma. Even before he was twenty-one years old he had risen to the rank of Regimental Sergeant-Major. This was the highest rank that could be achieved by an African. The other high rank which could be achieved by an African was that of honorary Captain which the British conferred upon Kabaka Edward Mutesa of Buganda and Chief Adam Sapi Mkwawa of the Hehe. But Kabaka Mutesa and Chief Adam Sapi Mkwawa [1] were awarded these military ranks because of theirs status as traditional rulers, while Abdulwahid earned his because of his courage, exemplary leadership qualities and smartness. Abdulwahid was also decorated with four medals-the Burma Star,1939-1945, War Medal, Defence Medal and Victory Medal. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] At the end of the war European troops forming the Allied Forces were demobilised earlier than the Africans on the claim that they were urgently needed in Europe for post-war reconstruction. African troops were released last. The KAR from Tanganyika were regrouped at Kalieni camp outside Bombay for repatriation home. While at Kalieni, Abdulwahid met his friend from home Ahmed Rashad Ali, a Zanzibari. Ahmed Rashad was a star footballer and had gone to India for studies. As the African troops from Tanganyika sailed back for home morale was very high; the only subject occupying their conversation was how would they be able to drive the British out of Tanganyika.''
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[1]Chief Adam Sapi Mkwawa's biography appears in Baragumu, April 12, 1956. He was
educated at Tabora and Makerere where he went to study medicine. He did not complete
his study as he was forced to return home to become chief of the Wahehe. He was elected
memberof the Legislative Council in 1947 at the age of 27. In 1955 Abdulwahid and Dossa
were invited by Adam Sapi to Kalenga at the ceremony of handing over the skull of Chief
Mkwawa to his great-grandson Adam Sapi.
Chief Mkwawa was secretly recruited into TANU
by Dossa Aziz thus becoming one of the very few traditional rulers to support the Party.

For information on chiefs who supported TANU see Sauti ya TANU, No. 22 of 28 th February,
1958.
 
LAANA ZA SHEIKH AMIR, MAPINDUZI ZNZ (MTAZAMO WENYE HEKMA)

MohaMmed Said;6448098 Mohamed Said;6437688]Ritz,
Mie si wa kujibizana na huyu.Hana moja alijualo katika hayo ayazungumzayo.
Huyu mtu anaejidai anajua sana nakuachieni nyie
Wanajamvi, hicho kinukuu hapo ni katika kukumbusha tu jinsi mzee anavyopata maumivu kiasi kwamba hoja zimekwisha sasa anaparamia kashfa na dhereu. Tunaendelea na darsa.

Mtakumbuka kuwa katika mnakasha huu na ule uliotangulia Mohamed Said alisema kuwa wote waliompinga Sheikh Amir walikufa dhalili sana. Na kuna mtu aliomba mungu amweke hadi amuone mtu wa mwisho na baada ya huyo wa mwisho kufariki wiki iliyofuata naye alifariki.

Katika kurasa mbili zilizopita kuna mchangiaji kauliza kuhusu kifo cha Mbuwane Syeks baba yao akina Sykes aliyekuwa anaelekea Iringa kuwapiga Wahehe katika jeshi la Mlamluki. Mohamed Said amekiri kuwa mzee huyo alisombwa na maji wakati wa kuvuka mto.

Kwa kuangalia waliokufa kwa dhalili kwasababu ya kumhalifu sheikh Amir hakuna tofauti na huyu Mbuwane Sykes ambaye nadhani naye atakuwa amekufa kwa laana ya kwenda kuwaua wahehe ambao tunajua walikuwa wanapinga ukoloni. Kwahiyo ni anapomkweza Amir basi asisahau kuwa laana ndiyo pia ilimsomba Mbuwane Sykes mzazi wa familia ya Sykes inayosemwa imekuja kuwakomboa Watanganyika.

Katika kitabu cha Kwaheri uhuru.... cha Ghessany ambacho Mohamed ameshiriki kuandika, pamoja na madai ya Wamakonde wa Kipumbwi na Mapinduzi harama ya ZNZ chini ya Nyerere, Mohamed Said na wenzake wanajaribu sana kuhoji kiasi cha wazanzibar waliouawa katika mapinduzi ya znz.

Kinachoshangaza Mohamed Said hajawahi kueleza ni Watanganyika wangapi waliuawawa na familia ya Sykes ambayo tunajua kuwa ilikuja kama mamluki kupigana na Watanganyika waliokuwa wanaupinga ukoloni.

Hii maana yake ni kutaka Serikali ya mapinduzi itoe idadi sijui ni kama kuiadhiri wakati huo huo yeye akiwa ameficha idadi ya Watanganyika waliouawa na familia ya Sykes. Unafiki huu !!

Kibaya zaidi hakuna mahali Mohamed Said anaunga mapinduzi ya wazanzibar mkono.
Pengine ni hasira za kuondoka kwa sultan na hilo ni tusi kubwa kwa wazanzibar.

Nadhani ni wakati wazanzibar wakamwelewa Mohamed kuwa pamoja na kuwatembelea kama mwislam lakini ana chuki illiyojificha dhidi ya wanamapinduzi, huyu ni mtu wa Sultan.
Huu nao ni aina ya unafiki, unafiki kama ule uliofanywa na Sheikh.

Wakati Mohamed Said anasema akina Bibi Titi na Tewa walimuunga mkono Sheikh Amir katika siasa zake, Titi na Tewa walikuwa ndani ya serikali ya Tanganyika(Nyerere) kama viongozi.

Pengine wakipambana humo ndani kwa ndani kama ilikuwepo dhulma(Mohamed).
Kinachoshangaza ni kitendo cha Sheikh Amir kuendesha siasa za kuiondoa serikali ile ile iliyowateua akina Titi na Tewa madarakani. Huu ni nini ndugu zangu? Kusema jambo na kutenda kinyume kwa neno moja ni nini?

Kwahiyo tunazidi kuona kuwa
1. Waliokufa dhalili si wale wa sheikh hata walioua wahehe
2. Mohamed aje na idadi ya Watanganyika waliouawa na Mbuwane Sykes kabla ya kudai ya znz
3.Sheikh Amir alikuwa na siasa za pembeni nje ya zile za TANU za akina Titi na Tewa. Comorian kasema
4. Mohamed anapinga mapinduzi ya znz kwasababu yalimhusu sultan ambaye ni mwislam zaidi ya wanamapinduzi.

Darsa itaendelea na uchaguzi wa kura tatu kuona nani waasi......
 
Yericko,
Wewe unaeleza historia kama uijuavyo na wala mimi sijakutukana wala kukubughudhi.

Wala sijakwita mchochezi.
Binadamu lazima waghitilafiane katika mengi.

Sasa hebu na wewe nisome jinsi nilivyompokea Chief Adam Sapi Mkwawa kutoka nyaraka
za Sykes:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ''Abdulwahid served in Kenya, Ceylon, India and Burma. Even before he was twenty-one years old he had risen to the rank of Regimental Sergeant-Major. This was the highest rank that could be achieved by an African. The other high rank which could be achieved by an African was that of honorary Captain which the British conferred upon Kabaka Edward Mutesa of Buganda and Chief Adam Sapi Mkwawa of the Hehe. But Kabaka Mutesa and Chief Adam Sapi Mkwawa [1] were awarded these military ranks because of theirs status as traditional rulers, while Abdulwahid earned his because of his courage, exemplary leadership qualities and smartness. Abdulwahid was also decorated with four medals-the Burma Star,1939-1945, War Medal, Defence Medal and Victory Medal. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] At the end of the war European troops forming the Allied Forces were demobilised earlier than the Africans on the claim that they were urgently needed in Europe for post-war reconstruction. African troops were released last. The KAR from Tanganyika were regrouped at Kalieni camp outside Bombay for repatriation home. While at Kalieni, Abdulwahid met his friend from home Ahmed Rashad Ali, a Zanzibari. Ahmed Rashad was a star footballer and had gone to India for studies. As the African troops from Tanganyika sailed back for home morale was very high; the only subject occupying their conversation was how would they be able to drive the British out of Tanganyika.''
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[1]Chief Adam Sapi Mkwawa's biography appears in Baragumu, April
12, 1956. He was educated at Tabora and Makerere where he went
to study medicine. He did not complete his study as he was forced to
return home to become chief of the Wahehe. He was elected member
of the Legislative Council in 1947 at the age of 27. In 1955 Abdulwahid
and Dossa were invited by Adam Sapi to Kalenga at the ceremony of
handing over the skull of Chief Mkwawa to his great-grandson Adam
Sapi. Chief Mkwawa was secretly recruited into TANU by Dossa Aziz
thus becoming one of the very few traditional rulers to support the
Party. For information on chiefs who supported TANU see Sauti ya
TANU,
No. 22 of 28 th February, 1958.''

Ndugu,

Hoja iliyokuwepo ni wewe kusema wakristu hawakushiriki harakati za ukombozi,

Mimi nimeijibu kwakukupa mapya ambayo hukuyajua,

Maajabu nikuwa unaleta wasifu wa Adam Sapi Mkwawa!

Mzee wangu jibu hoja kama ilivyo!
 
Mimi sina haki ya kukupinga ikiwa unasema mababa askofu na wao walichangia
juhudi za uhuru kama walivyofanya masheikh wetu,

Nimekusoma na kwa kuwa umeileta Iringa nami nikaona kwa kunogesha jamvi
nikupe niyajuayo kuhusu Chief Adam Sapi Mkwawa.

Je, kuna ubaya wowote katika hilo?

Kama nilivyokuwa siujui mchango wa maaskofu na misa zao katika kupigania uhuru
wako wengi hapa JF hawakuwa wanajua Chief Adam Sapi aliingia vipi TANU kiasi cha
Nyerere kumtembelea.

Ikiwa hukupendezewa na taarifa hizi zangu basi ni bahati mbaya.
Hili halijawa suala la kujibizana hoja kwa ghadhabu na jeuri.

Ni mahali pa kuelimishana na watazamaji wakafyonza ilm kama Spike
Lee
anavyopenda kututukuza.
 
Back
Top Bottom