gombesugu,
..sidhani kama kuna mtu anabisha kwamba D'Salaam ilikuwa ndiyo "Central Command" ya harakati za uhuru.
..nadhani "mzozo" uliopo hapa ni kama Mwalimu Nyerere, au mtu mwingine, ndiye aliyekuwa Kamanda Mkuu ktk hiyo "central command."
..je, kati ya Julius Nyerere,Sheikh Hassan Bin Amiri, Mshume Kiyate, Abdu Sykes, etc etc ni nani haswa kiongozi mkuu wa harakati za uhuru wa Tanganyika??
NB:
..simfahamu mtunzi wa maneno " sisi tunataka kuwasha mwenge.." lakini ningependa kumfahamu kwasababu anastahili kuwa-recorgnized kwa mchango wake.
Mohamed Said anasema, Prof.Njozi ameripoti ktk kitabu cha mauaji ya mwembechai kwamba Mwalimu aliyatoa maneno hayo ktk maandiko ya zamani ya Wakatoliki.
cc
😡Ritz,
Jasusi,
Mag3,
Nguruvi3,
SHEIKH FARID,
Wickama
JokaKuu,
Salaam sana ndugu yangu.
Sasa kama hakuna yeyote mwenye kupinga/kubisha yakuwa
D'Salaam ndio ilokua
"Central Command" kama ulivyoiita,kwanini tunashinda hapa jamvini kutwa kucha na baadhi yenu kuthubutu kufananisha zile harakati zilizokuwapo pale
Mzizima na huko
Mikoani/Vijijini!?
Unaposema na kukubali yakuwa
D'Salaam ndio ilokua
"Central Command" ni vizuri mno. Maana huu ni ukweli usopingika,japo nahisi yawezakuwa ukapata matata na shutuma toka kwa
wenzio hapa
jamvini!?
Ndio maana hata
Nyerere alipobaini umuhimu na ukweli huo,akakimbia toka
Mwisenge na kuhamia
Mzizima.
Sasa la muhimu hapa ni kutambua kwa yakini,yakuwa hiyo "Central Command" ilikua
sio infrastructures tu,la hasha!
Hapa sasa ndipo
Sheikh Mohammed anapoingia na kubainisha tena kwa kitaaluma,yakuwa hiyo
"Central Command"; ilikua ni watu,na watu hao walikua ni Wanamji/Wazee wetu na takriban woote walikua ni WaIslamu na pia walikuwa ni
Watanganyika/Wazanzibary. Pia walikuwa ni Waungwana wenye sifa nyingi mno zisizo mipaka.
Kwani wewe unafikiri kabla ya
Nyerere kufika D'salaam hao
Wazee wetu walikua hawana
Kiongozi/Viongozi wao!? Mimi sioni kama hili suala lina-qualify hata kuitwa
"mzozo" kama unavyodai!?
Mimi binafsi mpaka hapo sioni tatizo wala utata wowote asilan,labda kama kuna mtu ana chuki binafsi za mambo fulani au kama pia kuna mtu atayaangalia haya mambo kwa jicho la
Udini na hasada!?
Nafikiri
Sheikh Mohammed, pia ametujuza mara kadhaa na wala hana ubishi na
"umahiri wa Nyerere" na vyeo vyoote alivyowahi kuwa navyo tangu kuhamia D'Salaam,kikiwemo na kile cheo cha
"Baba wa Taifa".
Lakini yeye
Sheikh Mohammed kama ni
Scholar/Historian,kenda mbali zaidi na kutafiti/kunyambulisha kwa kina;athari,madhila,dhuluma,unafiki,vicheko,furaha na pia vingine vingi alivyofanza
Nyerere kwa wale
wenyeji wake/
Wazee wetu hapo Mzizima.
Nafikiri pamoja na mitizamo yetu tafauti lakini pia tumshukuru mno huyu
Mtafiti/MwanaHistoria Sheikh Mohammed Said.
Nimefurahi kuzungumza nawe ndugu yangu
JokaKuu,napenda mno uungwana na ustaarabu wako.
Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu.
Ahsanta.
Cc;Ritz,Sheikh Mohammed Said,Sheikh Farid,Maulaga