Mkuu gombesugu hapa utagombana na Mzee wetu wa gerezani Mohamed Said yeye anasema Nyerere hakuwakumbuka wazee wake wala hakuwataja kabisaaaaaaaaaa.Wewe unasema aliwapa "heshma ya kipekee na kuwataja tu wazee wa Mzizima na khasa waIslam kwenye hotuba ya muago tena huku akiwataja majina na nasaba zao"
Hakika gombesugu umemuumbua mchana kweupe Mzee wetu wa Gerezani.Namsubiri kwa hamu kubwa sijui atasema nini baada ya kamanda wake kumgeuka.Mzee wetu hodari sana wa lugha najua lazima atakuja na misamiati mipya ya Gerezani ha ha ha ha.
Ngongo,
Awali ya yoote,nakukumbusha yakuwa japo nilishakusamehe zile kashfa na kebehi ulizonifanzia mara kadhaa hapa jamvini,tena bila hata ya kutumia hoja yoyote... lakini bado sijasahau.
Hilo neno
Kamanda,binafsi nahisi limekaa kishari na kuashiria vita/mabaya!? Kwani sisi soote si tupo hapa kutafuta amani na suluhu!? Au wewe ndugu yangu umedhamiria vita hapa jamvini!?
Bakhti mbaya,ile bayana yangu nafikiri wewe binafsi na hata
Wickama,hamkunifahamu labda kwa utuvu.
Kwa hakika pale nilikua nasisitiza hoja yangu kwa kunyambulisha vitu kadhaa,katika majadiliano yalokuwapo nafikiri baina yangu, JokaKuu,Iron na Wickama siku chache nyuma.
Kwa kifupi ndugu yangu Ngongo,nilikua nasisitiza yakuwa hata Nyerere kwa kuonyesha mchango
unique wa Wazee wetu/Wana Mzizima,ndipo pale alipopatwa na
ile guilty conscious probably...siku ya hotuba ya "muago" akataja baadhi ya Wazee wetu na kwa majina fadhila zao kwake na Taifa.
Kwa sababu wengi wenu mnamalumu
Sheikh Mohammed,ati anabeza harakati za hao Wazee wa Mikoani/Vijijini...mimi sikubaliani nanyi asilan.
Ndipo nikasema,kama ni hivyo basi wa kulaumiwa ni
Nyerere. Kwani katika ile Speech yake ya Muago,kwanini hakutaja hao Wazee wa Mikoani/Vijijini na hizo Family za hao Ma-Chief!? Au nae pia alibeza michango hiyo ya Vijijini!?
Unataka kuniambia ati Nyerere Mkristo mtiifu,alitamka vile kuwapa sifa za bure wale Wazee wetu...kwani hakujua michango na harakati nyingine zozote hapo Tanganyika kama vile za Makanisa,Ma-Chief na Makasisi!?
Ndipo nikasema yakuwa Nyerere ametuachia kigugumizi...maana yake amekuachieni nyinyi kigugumizi. Maana utapingana vipi na maneno au maelekezo ya "Baba wa Taifa"....kwamba Wazee wa Mzizima,ndo wao walomstiri na kumfadhili pita kiasi ndugu yao na mwenzao!?
Naona ndugu yangu
Wickama,nae anadai kwamba atleast
Gombesugu amethibitisha yakuwa Nyerere alifanya fadhila kwa hao Wazee!?ahaha! Kutajwa jina kwa mchango wako ni haki, na kufanyiwa fadhila ni vitu viwili tafauti.
Nafikiri hiyo sehemu pia ishawahi kunyambuliwa kiundani hapa jamvini.
Yeye Nyerere kuwataja wale Wazee ilikua ni lazima,kwasababu hii ni Historical fact,ya kwamba hata kama kuna "Plots" au harakati nyingine zozote zilizokuwapo sehemu nyingine mbalimbali hapo
Tanganyika wakti huo,lakini utakuwa "
Maluuni wa Kitaaluma"/Academic dishonesty,kuthubutu kufananisha na yale yalokua yakifanzwa na Wazee wetu/"Wana Kindakindaki" a.k.a Wana Mzizima.
Unataka kuniambia yakuwa Nyerere ati aliwapenda saana Wazee wachache wa KiIslamu kutoka D'Salaam,kuliko hata Wazee wa kutoka Mara au
Makasisi wa Peramiho!?ahaha!!
Halafu leo anatokea
Yericko,kutwambia ati
Nyerere alifanyiwa matambiko makubwa saana na Makasisi!ahaha!!...Jinsi Nyerere alivyokua Mtiifu na mwadilifu wa Kanisa lake,halafu ati asahau hata kutaja hiyo "
michango mikubwa" akumbuke tu michango ya
Dini moja!?
Najua kabisa Nyerere asingefanza hivyo asilan!
Ndipo pia nilimpa mfano wa kistaarabu,ndugu yangu
JokaKuu,kuhusu wale ndugu zetu na Wazee wa Kaskazini walivyoshughulika na ule mgogoro "wao"wa Ardhi kule
Meru.
Kumbuka,wao wakti huo inawezekana kabisa walikua pia wana uwezo mzuri hata wa kifedha kuliko baadhi ya sehemu nyingi za
Tanganyika...lakini waliamua kujitenga kikanda na kushughulika
ki-selfish na huo mgogoro wao huko Kilimanjaro. Ndo maana hata
Chadema labda wamerithi dasturi hiyo mbaya!
Lakini wakaamua kupeleka mtu/Mwakilishi wao kipekee bila hata ya klujali au kuhusisha/kushirikisha nguvu zoote na harakati kwa pamoja kwa maslahi ya Tanganyika na Watanganyika woote!?
Nyerere,soote tunajua yakuwa alikua ni "mwerevu wa kisiasa"...nina hakika ya kuwa haya yoote aliyajua kiundani mno na alizingatia saana!...nafikiri pia yaliwahi kumsumbua kichwa japo kiduchu!
Hivi unafikiri,kama wale Wazee wa kaskazini walopeleka Mwakilishi wao kipekee(japo
Passport ililazim itolewe/wasaidiwe na
Abdilwahid Sykes hapo D'Salaam),kama wangefanikiwa yale maombi/matakwa yao pale
UN,Historia yoote ya Tanganyika ingekua vingine hivi leo...na labda
Tanganyika pia isingekua nchi moja kama hivi tuijuavyo leo hii!?
Kwa kumalizia kiduchu,ile hotuba ya muago ya
Nyerere,kiujumla Waislam takriban woote waliichukulia kama ni kejeli na dhihaka kwao. Zile
imbalances na ahadi nyingi walizotegemea,kuahidiwa au kupanga na Nyerere nafikiri havikutimia.
Unajua
Ngongo,imenilazim kunena/"kufunguka" hivi vitu ni tu sababu wewe umenidodosa mno. Lakini huwa sipendi na wala si dasturi yangu. Nafikiri ndo maaan pale nilipomjibu
JokaKuu kwa ustaarabu/
indirectly na kugusia kiduchu hii khabari,lakini wewe hukufahamu mantiki ya yale maelekezo yangu.
Lakini hapo namwachia
Sheikh Mohammed Said,maana yeye hiyo ndio field yake kama
Mtafiti na MwanaHistoria.
Nafikri ndugu yetu
The Big Show nae pia huko awali,aliwahi kuyazungumzia haya masuala kwa kina.
Napenda tumwache Sheikh Mohammed aendelee kuchambua kiundani. Pia Kumradhi labda kama una suali lolote nakusihi pia muelekezee yeye.
Nashukuru kwa kunisikiza huo uchechefu wangu.
Ahsanta.
Cc;Ritz,The Big Show, Sheikh Mohammed Said,Wickama,JokaKuu