Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hatukeshi hapa 24/7 kukusoma wewe...
La hasha usiote mapembe,tupo hapa kumsoma Moh Said,
Kama ulianzisha hii thread kutafuta umaarufu na credits,then kaa ukijua ya kwamba umeshushwa daraja kwnye mizani ya wale wanaofuatilia hoja na kusaka elimu...
Mkuu THE BIG SHOW, pole sana kwa kasheshe la vibaka(polisi) waliopita wakipora mali za wananchi wa Mtwara kwa kisingizio cha kutuliza ghasia! nilishuhudia kwa macho yangu wakimpiga bwana mmoja na kumnyang'anya simu yake ya mkononi. Ama kweli hatuna polisi bali vibaka!
 
Mkuu Ngongo, hebu isome hii kotoka kwa mjukuu wa mercenary soldier!
My grandfather was part of mercenaries who came to Tanganyika with Harmine von Wissman and landed in Pangani . at the turn of 19[SUP]th[/SUP] century. The Zulu were under the leadership of Chief Mohosh. The mercenaries were recruited from Kwa Likunyi. This was just after the Berlin Conference of 1884 in which Africa was partitioned between imperial powers in Europe. This caused resistance from the people of Tanganyika who rose up in arms to defend their freedom.
 
Kwani Mohamed Said anasemaje kuhusu hili? kwa nikujuavyo wewe huwezi kuamini habari yoyote kama haikuletwa na huyu mzee wako!

Katiba ya jamhuri ya muungano inasema kila mtu ana haki ya kutoa maoni hiyo ni haki yakona ni mawazo yako sikukatalii mimi ninavyo zichukulia hoja za mzee MS ni sawa na wewe unavyo zichukulia hoja za Nguruvi3,lakini hujajibu swali langu!
 


Iron,

Nafikiri hili la suala la kwanza itakuwa vizuri sana kama utafatilia mnakasha huu toka mwanzo wake. Imezungumziwa kwa kina sana gavana waliowekewa waslam wa Tanganyika kuundiwa BAKWATA. imeelezwa kwa kina sana . Pitia hilo.

Lakin la Pili kuhusu uchumi wenu Tanzania ukiondoa 26% kushikiriwa na wageni kutoka nje ya Tanzania lakin 62% umeshikiliwa na waislam.

Naomba ufanye utafiti kidogo kwa hilo. Kisha unukosoe kama nitakuwa nimekosea.



 

Spike,
Kila jambo linakwenda kama Allah alivyolipanga.

Haya ninayoandika mimi leo hii Abdu Sykes aliyaeleza katika ule mpango wa TANU
pale Mwalimu Kihere, Dossa Aziz, Abdu Sykes na Nyerere walipokubaliana iandikwe
historia ya TANU.

Nyerere akamuagiza Dk. Kleruuu afanye kazi na Abdu wakamilishe mswada.

Ofisi yao ilikuwa ile ofisi ya TANU pale Kariakoo na Lumumba.
Abdu alianza kuandika na alianza historia ya TANU kama nilivyoianza mimi.

Nyerere haikumfurahisha....
Mradi ukafa na Abdu hakunyanyua tena kalamu kuandika historia ile hadi anaingia
kaburini.

Nusu karne imepita leo tumekusanyika jamvini huu mwezi wa tano unaingia hatuna
ila tunamtaja Abdu kwa kila hali kiasi wengine wamemkejeli kwa kumwita "Rambo."

Ala kuli hali Abdu Sykes Allah kamrejesha katika historia ya chama alichokiasisi kwa
njia ya kushangaza sana.

Historia ya uhuru sasa si kama ile ya Kivukoni.
 

Ngongo,
Babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa Mwekapopo aliingia Tanganyika na
Wajerumani 1890s kama alivyoingia Sykes Mbuwane - askari mamluki.

Sijifaharishi kwa hilo wala sioni aibu.
Huu ndiyo ulikuwa ukoloni na adha zake.

Lakini najifaharisha kuwa babu yangu Salum Abdallah ameacha alama katika
historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kama alivyoacha Kleist Sykes.

Nadhani hapa panatosha kuwa ingawa hawa Wazulu, Wamanyema na Wanubi
waliingia Tanganyika kuutia nguvu ukoloni lakini watoto wao wakajakuwa wazalendo
wakubwa.

Hapa Tanganyika kulikuwa na askari "motorised" kama walivyoitwa na Waingereza na
wazee wetu waliwaita "makavirondo" nimewataja vizuri katika kitabu cha Abdu Sykes.

Hawa walitumiwa na Waingereza kuzima mapambano ya wananchi dhidi ya serikali yaJe
kikoloni.

Je, tuna haki ya kuwalaumu watu hawa?
Fanya tafiti kiduchu uone ni kutoka kabila gani Waingereza waliwachukua askari hawa.
 

Joka kuu.

Kwa kukusaidia zaidi hizo kamati zote ulizozitaja ni KAMATI ZA KISIASA TU ingawa unaweza pitia ripoti zao.

Lakin mimi kama mchumi na Muungano wenu nautazama kiuchumi zaidi nimekupa wapi unaweza pata data Kamili za Wachumi waliobobea katika fani ya Uchumi wa nchi hizo mbili huru yaani Znz na Tanganyika wanapokaa pamoja kitako na kuunda JOINT FINANCE COMMISSION na kuangalia kwa kina sana kila nchi inachangia nini katika ustawi wa Tanzania ikiwemo misaada, mikopo na ruzuku zinazotolewa kwa Serikali au kupokelewa na Serikali na kuona kila upande unanufaikaje.

Kwa kweli RIPOTI zao ni za kitaalamu sana na zinabainisha fursa za kila upande na kuonyesha mengi sana ya uchumi wa nchi hizo. Na zinaweza kata ngebe za wanasiasa au wale wachache wanaosema kuwa ZNZ ni tegemezi kwa Tanganyika.

Ushauri wangu kama unataka kupata RIPOTI ya kitaalamu ya michango wa nchi hizo mbili katika Muungano wenu pitia Ripoti hizo hasa Pg 26 mpaka 34. utaona mengi sana. Ripoti za kisiasa tuwaachie wanasiasa wenyewe.

nakunasihi chukua muda wako kidogo kuzitafuta na kuzisoma zitakufungua mengi sana kiuchumi na kuachana na maneno ya wanasiasa wachache.

Siku zote ukimuona mtu mzima na akili zake timamu ANATEMA ASALI NA KUTAMANI PILIPILI ujue kuna namna hapo. Usimbeze.

Pole sana

 

Muungwana Maulaga,

Salaam sana ndugu yangu. Niwie radhi kama umekereka kwa mimi kupenyeza salaam zako kwenye ile bayana nilomwandikia Shariff Ritz.

Sijawahai asilahi kukutuhumu kwa lolote,nakusihi ondoa shaka.

Ama kwa hakika pale nalifanza udhaifu wa kimwana-Adam,nami nakubali kwalo.

Hiyo "Shit List" uizungumziayo,ama kwa hakika mimi bnafsi sina uwezo wala matarajio ya kuwa nayo. Ninachojua ni kwamba Maalim Sheikh Mohammed Said ndio anayo. Tayari ishawakumba baadhi ya Wanajamvi wenzetu kama Mag3 na pia Nguruvi3,ambae kwa sasa kama umuonavyo,amebakia kutufanzia sarakasi na kuchacharika kuso kwisha!

Natumai labda iko siku Sheikh Mohammed,ataamua kuwasemehe na kuwatoa huko kizuizini alikowatokomeza!?

Nipokelea bayana yangu hii chechefu na kunisamehe hilo kosa langu.

Nakusihi tuendelee na mnakasha wetu kwa staha ndugu yangu.
Ahsanta.

Cc;Ritz
 


Muheshimiwa Nguruvi3,

I can't imagine how you must feel. We forgive you for being bitter though!...

Ahsanta.
 

Wickama,

Nashukuru kwa maelekezo yako kiduchu.

Nimekufahamu kiasi,natumai nawe pia umenifahamu.

Ndugu yangu Wickama,sitakutusi asilan! Hayo maneno kwenye bayana yangu wala si matayarisho ya chochote kama ulivyodai. Nahisi hapa "utabiri wako" umekwenda mrama!?

Nakusihi tuendelee na mnakasha wetu kwa staha.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 

Wickama,

Haina neno,lakini naona umeamua kuhamisha goal posts!? Punguza ujanja!

The way you retreated, you remind me of this:

"I could have become a Soldier if I had waited;I knew more about retreating than the Man who invented retreating"- Private History of a Campaign that failed. By Mark Twain.

Hicho kichefuchefu chako taratibu sijetapikia hapa jamvini.

Ahsanta.
 

Wickama,

Sasa kama ni hivi,tuchukulie vipi yale ma-scandals,unafiki,dhuluma,unyama,ugaidi na machafu mengineyo mengi mno yafanyikayo pale ndani ya Vatican na baadhi ya Makasisi wakubwa mno wa Kikatoliki wakishiriki!?

Nafikiri unaifuatilia kiundani History na lifestyle ya pale Vatican!? Maana majambo mengi mno yafanyikayo mle ndani yanalalamikiwa saana tena kwa miaka mingi mno na watu wa dunia nzima!

Je unafikiri ile Psychology ya pale Vatican na baadhi ya wale Makasisi wake "wachafu",ina uhusiano upi au inamwakilisha vipi Mkristo/Mkatoliki mtiifu mno,mvuja jasho tena maskini pita kiasi,labda wa kutoka Ngaramtoni,Montevideo/Uruguay au Mwisenge!?

Nafikiri tuyaache haya majambo ndugu yangu. Nina imani tumefahamiana japo kiduchu.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 

Gombesugu,
Ahsante ndugu yangu kwa kipande cha Mark Twain.

Nilikuwa na rafiki yangu James Brenan tunatoka Iowa
City kwa gari ndogo tunakuja Chicago.

Tulipofika mto Mississippi akawa ananionyesha.

Mimi kwa mzaha nikamwambia kuwa asijishughulishe
kwani nilipokuwa mtoto mimi na rafiki zangu Tom Sawyer
na Huckleberry Fin tukiogelea pale.

Ungeuona ule uso wa sahib wangu ulivyopigwa na mshangao!

Naamini umenielewa.
 


Sheikh Mohammed Said,

Salaam.

Kuna vijimambo vingine usitafute kujiumiza kichwa na kujilazimisha kujibu. Hawa wengi wao ni ile "pasua kichwa" tu!

Nilishampa Maulaga mifano kadhaa, maana nae pia alitaka kujua kuhusu khabari hiyo.

Hapa aidha hawa jamaa;hawajui kabisa History ya ulimwengu kiundani au wakufanzia kebehi na tashtit.

Ahsanta kwa kunisikiza.
 

Sheikh Mohammed,

Nakufahamu kwa utuvu Al Akhiy..."mioyo ya wenye kujua huwa na macho"

Wallahi,Al Akhiy huyo muungwana mie pia ndo "maradhi yangu".

Lakini kuna vijineno pia aliwahi kunena kuhusu ati Social Class ya Shakespear kwamba ilikua duni!ahaha!!

Na hivi karibuni nafikiri umesikia khabari mpya za Shakespear,kumbe nae alikua ni mlanguzi mkubwa wa bidhaa adimu wakti na zama hizo!?ahaha!! Ile hishma yake yoote ya ule "Saint" nafikiri itampungua japo kiduchu.

Wallahi,Wana-adam tuna madhaifu na viroja vingi.

Insha Allah nimefurahika kunipa fursa hii adimu kunena nawe japo kiduchu.

Ahsanta.
 

JokaKuu,

Salaam sana ndugu yangu.

Sasa kama hakuna yeyote mwenye kupinga/kubisha yakuwa D'Salaam ndio ilokua "Central Command" kama ulivyoiita,kwanini tunashinda hapa jamvini kutwa kucha na baadhi yenu kuthubutu kufananisha zile harakati zilizokuwapo pale Mzizima na huko Mikoani/Vijijini!?

Unaposema na kukubali yakuwa D'Salaam ndio ilokua "Central Command" ni vizuri mno. Maana huu ni ukweli usopingika,japo nahisi yawezakuwa ukapata matata na shutuma toka kwa wenzio hapa jamvini!?

Ndio maana hata Nyerere alipobaini umuhimu na ukweli huo,akakimbia toka Mwisenge na kuhamia Mzizima.

Sasa la muhimu hapa ni kutambua kwa yakini,yakuwa hiyo "Central Command" ilikua sio infrastructures tu,la hasha!

Hapa sasa ndipo Sheikh Mohammed anapoingia na kubainisha tena kwa kitaaluma,yakuwa hiyo "Central Command"; ilikua ni watu,na watu hao walikua ni Wanamji/Wazee wetu na takriban woote walikua ni WaIslamu na pia walikuwa ni Watanganyika/Wazanzibary. Pia walikuwa ni Waungwana wenye sifa nyingi mno zisizo mipaka.

Kwani wewe unafikiri kabla ya Nyerere kufika D'salaam hao Wazee wetu walikua hawana Kiongozi/Viongozi wao!? Mimi sioni kama hili suala lina-qualify hata kuitwa "mzozo" kama unavyodai!?

Mimi binafsi mpaka hapo sioni tatizo wala utata wowote asilan,labda kama kuna mtu ana chuki binafsi za mambo fulani au kama pia kuna mtu atayaangalia haya mambo kwa jicho la Udini na hasada!?

Nafikiri Sheikh Mohammed, pia ametujuza mara kadhaa na wala hana ubishi na "umahiri wa Nyerere" na vyeo vyoote alivyowahi kuwa navyo tangu kuhamia D'Salaam,kikiwemo na kile cheo cha "Baba wa Taifa".

Lakini yeye Sheikh Mohammed kama ni Scholar/Historian,kenda mbali zaidi na kutafiti/kunyambulisha kwa kina;athari,madhila,dhuluma,unafiki,vicheko,furaha na pia vingine vingi alivyofanza Nyerere kwa wale wenyeji wake/ Wazee wetu hapo Mzizima.

Nafikiri pamoja na mitizamo yetu tafauti lakini pia tumshukuru mno huyu Mtafiti/MwanaHistoria Sheikh Mohammed Said.

Nimefurahi kuzungumza nawe ndugu yangu JokaKuu,napenda mno uungwana na ustaarabu wako.

Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz,Sheikh Mohammed Said,Sheikh Farid,Maulaga
 

Gombesugu,
Kuna mwanafulani sijui kutaka kunitisha au kuni impress kanijibu kwa jeuri
kwa Kizungu cha Victorian England.

Basi mie nacheka naona vituko vya karagosi kalewa tembo.
Nikamwambia mbona hiyo ina harufu ya Dickens tena "Bleak House?"

Kashika adabu yake hajanirejea tena.
Kabaki kunitukana.

Nami simpatilizi nashika hamsini zangu.
Maalim wangu Sheikh Haruna kanifunza.

Anasema tusi halina jibu.
Madrasa ina raha zake.

Ahsante ndugu yangu.
 

Sheikh Mohammed,

Nakusikia Al Akhiy. Atakuwezapi huyo,itakuwa yaleyale ya Bi sisimizi kuvinjari na Bwana Tembo!ahaha!!

Wala huyo mwafulani asikushughulishe,si unajua jamaa zetu wengine wana ile "inadi ya mbwa koko".

Insha Allah tuendelee na mnakasha wetu kwa utaratibu na staha,kama tulivyofundishwa na Wazee wetu.

Ahsanta.
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Salaam sana ndugu yangu.

Niwie radhi,nimevamia kiduchu haya majadiliano yenu na nduguyo Uthman.

Tafadhali nijuza hiyo siasa na dini, ni wakati upi huwa zinaingiliana na wakati upi huwa hazitakiwi kuingiliana. Na je vigezo hivyo hutolewa na nani na ni vipi!?

Pia kama umeamua kuyarejesha hayo mambo ya utumwa na kumwekeshea darsa Ustadh Uthman,basi nakusihi muanzie na haya hapa chini:

1494 when King John of Portugal and the Catholic Mornachs of Spain sign the Treaty of Tordesillas dividing the world between them.

Vasco Da Gama,kutokana na ile mila na dasturi zao za mirathi,hakuweza kuwa mrithi wa family yao,maana yeye hakuwa wa mwanzo kuzaliwa. Alipatwa na kizaazaa na mughala kwa muda.

His alternatives!? Well,there's always the Priesthood.
He goes as far as the Rites of Tonsure.

On july 1497,the King holding Court in Montemer,entrusts Vasco Da Gama with the command of expedition.

The following day,"The day of Our Lady",Vasco attends massive Mass in Belem and assumes command of the fleet;the flagship "Saint Gabriel".....the rest is bloody History!

Christopher Columbus;on every Island he set foot on planted a Cross,"making the declaration that are required"-The Requerimiento, to claim the ownership for his Catholic Patrons in Spain.

If the Indians refused or delayed their acceptance(or understanding) the Requerimiento continued:

I certify to you that,with the help of GOD,we shall powerfully enter in your country and shall make war against you...and shall subject you to the yoke and obedience of the Church...and shall do you all mischief that we can,as to vassals who do not obey and refuse to receive their LORD and resist and contradict him!

Nashukuru kwa kunisikiza ndugu yangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz,Uthman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…