Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Muheshimiwa Nguruvi3,

Nipa fursa hii kukanusha na kupinga vikali hayo maneno hapo juu nilipo-bold!!

Hata siku moja sitaweza kukwambia yayo,au labda tu kuna pahala ulikosea harufi kiduchu!?...na umekusudia vingine!?

Tafadhali nijuza ili moyo wangu nituame.

Maana sitaki nijeonekana na Wanajamvi wenzetu yakuwa nimekutusi,hasha!...kwanza nitajuaje yakuwa una maradhi hayo!?

Pole nyingi kwa yayo.

Ahsanta.

Cc;Wickama,Ritz
 

Unafurahia kujibu tusi?
 

Asalaam aleykum al akhy Gombesugu nilikuwa nakusoma kwa chat nikiwa mapumzikoni ahsanta ndugu yangu endelea kutupa mipini.
 
Asalaam aleykum al akhy Gombesugu nilikuwa nakusoma kwa chat nikiwa mapumzikoni ahsanta ndugu yangu endelea kutupa mipini.

Boko Haram,

Asalaam Alaykum Al Akhiy.

Wallahi,nalipatwa na huzuni nyingi niliposoma kwenye post yako fulani asubuhi hii, yakuwa hawa jamaa wa Jf kumbe walikufungia!?

Kama hizo ndo dasturi zao,basi watapoteza saana reputation yao...

Sisi "Team yetu" tupo kiduchu mno kwa hapa Jamvini,halafu pia wanatufanzia njama za kufungia baadhi ya ma-Strikers wetu muhimu kama wewe Al Akhiy!ahaha!!

Haina neno,la muhimu umerejea salama nami nduguyo nimefarijika mno kukusikia tena.

Tuendelee na mnakasha Insha Allah.

Ahsanta.
 

Nadhani ilikuwa ni makosa ya kiuandishi tu sio kuwa alidhamiria kutoa maana ufikiriavyo!
 



Mwanasharia Iron,

Your words sound great and read well.

However,you seems to overlook some Historical facts. Non Muslims in this country especially Christians are beneficiaries of the Colonial White Supremacy structure/s.

Muslims been allienated and marginalized for decades from Socio-economic mainstream.

The process,structure or system has never been reversed effectively todate.

I know some of you like to think,that was a long time ago,lets sweep it under the rug and move on. It's not that simple Sir!

Some of you would have us/Muslims believing we do it on our own. "Pull yourselves up by your bootstraps,sort your own problem/s and move on"!

You know what,you lot didn't make it on your own. We better not believe you!

Ahsanta.

Cc;Boko Haram
 
gombesugu,

..mimi nadhani wazee "wetu" kutoka bara wasingefika D'Salaam, basi Tanu ingebaki hukohuko kwa hao unaowaita wazee "wenu."

..kumbuka kwamba unaowaita wazee "wenu" wamenukuliwa wakidai kwamba walikuwa na draft ya madai ya uhuru wa Tanganyika, wasijue wafanye nini na draft hiyo, mpaka walipompata mtu wa bara[Kambarage mtoto wa Burito] aliyechukua draft hiyo na kwenda kuiwasilisha UN.

..zaidi, rejea taarifa alizotoa John Illife kwamba kuna wakati 2/3 ya michango ya wanachama wa Tanu ilikuwa inatokea SUKUMA LAND. Kipindi hicho nadhani Wasukuma walikuwa wanakadiriwa kuwa 1/3 ya wanachama wa Tanu.

..pamoja na kutoa mchango mkubwa zaidi ktk kuendesha Tanu, sijawahi kusikia ndugu zetu wa Sukuma Land wakigombea wapewe sifa zaidi, nafasi nyingi zaidi za uongozi, au kipande kikubwa zaidi cha rasilimali za nchi hii.

..Utata na "mzozo" ninaouona mimi ni hizi juhudi za kudunisha mchango wa Mwalimu Julius Nyerere, pamoja wa wa-Tanganyika wasio na asili ya D'Salaam, ktk harakati za uhuru wa nchi hii.

cc: Mag3, Wickama, Nguruvi3, Ritz, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,

..unadai kwamba Waislamu wamekuwa ellianated na marginalized for decades.

..wakati huohuo Barubaru haishi kutukumbusha kwamba UCHUMI wa nchi hii umeshikwa na WAISLAMU.

..mimi nashauri mkae kikao wewe na Sheikh Barubaru mtupe suluhu ya madai yenu.

cc: Jasusi, THE BIG SHOW, Mag3, Ritz, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:

Nafikiria sana,

Mohamed Said na wafuasi wake wanashindwa kutambua kuwa wapo washarika wengi sana wa harakati za Uhuru lakini hawatajwi

Hivi leo Mmalawi Mzee Nyirenda aliyeupandisha mwenge wa Uhuru mpaka kilele cha Mlima Kirimanjaro katika Nyakati za Uhuru angekuwa ni Muislamu ingekuwaje?
 
Last edited by a moderator:


Haisaidii hata ukiamua kujitoa ufaham na kupindisha hoja hiyo,masuala ya biashara waislam ni kama utamaduni wao tuh,na katika kitabu chao kina hadi miongozo ya kutosha namna gani ya kuendesha biashara hizo kwa haki na usawa..
gombesugu mnywa ghahawa amelizungumza hilo kwenye system ya serikali...

Punguza mihemko...
 
Last edited by a moderator:

Ngongo,

Awali ya yoote,nakukumbusha yakuwa japo nilishakusamehe zile kashfa na kebehi ulizonifanzia mara kadhaa hapa jamvini,tena bila hata ya kutumia hoja yoyote... lakini bado sijasahau.

Hilo neno Kamanda,binafsi nahisi limekaa kishari na kuashiria vita/mabaya!? Kwani sisi soote si tupo hapa kutafuta amani na suluhu!? Au wewe ndugu yangu umedhamiria vita hapa jamvini!?

Bakhti mbaya,ile bayana yangu nafikiri wewe binafsi na hata Wickama,hamkunifahamu labda kwa utuvu.

Kwa hakika pale nilikua nasisitiza hoja yangu kwa kunyambulisha vitu kadhaa,katika majadiliano yalokuwapo nafikiri baina yangu, JokaKuu,Iron na Wickama siku chache nyuma.

Kwa kifupi ndugu yangu Ngongo,nilikua nasisitiza yakuwa hata Nyerere kwa kuonyesha mchango unique wa Wazee wetu/Wana Mzizima,ndipo pale alipopatwa na ile guilty conscious probably...siku ya hotuba ya "muago" akataja baadhi ya Wazee wetu na kwa majina fadhila zao kwake na Taifa.

Kwa sababu wengi wenu mnamalumu Sheikh Mohammed,ati anabeza harakati za hao Wazee wa Mikoani/Vijijini...mimi sikubaliani nanyi asilan.

Ndipo nikasema,kama ni hivyo basi wa kulaumiwa ni Nyerere. Kwani katika ile Speech yake ya Muago,kwanini hakutaja hao Wazee wa Mikoani/Vijijini na hizo Family za hao Ma-Chief!? Au nae pia alibeza michango hiyo ya Vijijini!?

Unataka kuniambia ati Nyerere Mkristo mtiifu,alitamka vile kuwapa sifa za bure wale Wazee wetu...kwani hakujua michango na harakati nyingine zozote hapo Tanganyika kama vile za Makanisa,Ma-Chief na Makasisi!?

Ndipo nikasema yakuwa Nyerere ametuachia kigugumizi...maana yake amekuachieni nyinyi kigugumizi. Maana utapingana vipi na maneno au maelekezo ya "Baba wa Taifa"....kwamba Wazee wa Mzizima,ndo wao walomstiri na kumfadhili pita kiasi ndugu yao na mwenzao!?

Naona ndugu yangu Wickama,nae anadai kwamba atleast Gombesugu amethibitisha yakuwa Nyerere alifanya fadhila kwa hao Wazee!?ahaha! Kutajwa jina kwa mchango wako ni haki, na kufanyiwa fadhila ni vitu viwili tafauti.

Nafikiri hiyo sehemu pia ishawahi kunyambuliwa kiundani hapa jamvini.

Yeye Nyerere kuwataja wale Wazee ilikua ni lazima,kwasababu hii ni Historical fact,ya kwamba hata kama kuna "Plots" au harakati nyingine zozote zilizokuwapo sehemu nyingine mbalimbali hapo Tanganyika wakti huo,lakini utakuwa "Maluuni wa Kitaaluma"/Academic dishonesty,kuthubutu kufananisha na yale yalokua yakifanzwa na Wazee wetu/"Wana Kindakindaki" a.k.a Wana Mzizima.

Unataka kuniambia yakuwa Nyerere ati aliwapenda saana Wazee wachache wa KiIslamu kutoka D'Salaam,kuliko hata Wazee wa kutoka Mara au Makasisi wa Peramiho!?ahaha!!

Halafu leo anatokea Yericko,kutwambia ati Nyerere alifanyiwa matambiko makubwa saana na Makasisi!ahaha!!...Jinsi Nyerere alivyokua Mtiifu na mwadilifu wa Kanisa lake,halafu ati asahau hata kutaja hiyo "michango mikubwa" akumbuke tu michango ya Dini moja!?
Najua kabisa Nyerere asingefanza hivyo asilan!

Ndipo pia nilimpa mfano wa kistaarabu,ndugu yangu JokaKuu,kuhusu wale ndugu zetu na Wazee wa Kaskazini walivyoshughulika na ule mgogoro "wao"wa Ardhi kule Meru.

Kumbuka,wao wakti huo inawezekana kabisa walikua pia wana uwezo mzuri hata wa kifedha kuliko baadhi ya sehemu nyingi za Tanganyika...lakini waliamua kujitenga kikanda na kushughulika ki-selfish na huo mgogoro wao huko Kilimanjaro. Ndo maana hata Chadema labda wamerithi dasturi hiyo mbaya!

Lakini wakaamua kupeleka mtu/Mwakilishi wao kipekee bila hata ya klujali au kuhusisha/kushirikisha nguvu zoote na harakati kwa pamoja kwa maslahi ya Tanganyika na Watanganyika woote!?

Nyerere,soote tunajua yakuwa alikua ni "mwerevu wa kisiasa"...nina hakika ya kuwa haya yoote aliyajua kiundani mno na alizingatia saana!...nafikiri pia yaliwahi kumsumbua kichwa japo kiduchu!

Hivi unafikiri,kama wale Wazee wa kaskazini walopeleka Mwakilishi wao kipekee(japo Passport ililazim itolewe/wasaidiwe na Abdilwahid Sykes hapo D'Salaam),kama wangefanikiwa yale maombi/matakwa yao pale UN,Historia yoote ya Tanganyika ingekua vingine hivi leo...na labda Tanganyika pia isingekua nchi moja kama hivi tuijuavyo leo hii!?

Kwa kumalizia kiduchu,ile hotuba ya muago ya Nyerere,kiujumla Waislam takriban woote waliichukulia kama ni kejeli na dhihaka kwao. Zile imbalances na ahadi nyingi walizotegemea,kuahidiwa au kupanga na Nyerere nafikiri havikutimia.

Unajua Ngongo,imenilazim kunena/"kufunguka" hivi vitu ni tu sababu wewe umenidodosa mno. Lakini huwa sipendi na wala si dasturi yangu. Nafikiri ndo maaan pale nilipomjibu JokaKuu kwa ustaarabu/indirectly na kugusia kiduchu hii khabari,lakini wewe hukufahamu mantiki ya yale maelekezo yangu.

Lakini hapo namwachia Sheikh Mohammed Said,maana yeye hiyo ndio field yake kama Mtafiti na MwanaHistoria.

Nafikri ndugu yetu The Big Show nae pia huko awali,aliwahi kuyazungumzia haya masuala kwa kina.

Napenda tumwache Sheikh Mohammed aendelee kuchambua kiundani. Pia Kumradhi labda kama una suali lolote nakusihi pia muelekezee yeye.

Nashukuru kwa kunisikiza huo uchechefu wangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz,The Big Show, Sheikh Mohammed Said,Wickama,JokaKuu
 


Swadakta tuuh..
Nawewe kama unaona ya kwamba wasukuma wameachwa kupewa nafasi kwenye historia ya nchi hii muda na uhuru wa kuandika bado unao,uwanja unao mkuu,andika utufahamishe watanzania...

Kwanin Moh Said ameandika kwa ushahid na hoja za ushahid waz waz mumuone mchochez na mpuuzi??

Ondokeni basi muwaachie wale wanaothamin elimu hii waipate,ama la kama unakuja kupinga njoo upinge kwa hoja mujarabu...
 

..nadhani hujaelewa hoja yangu.

. gombesugu anadai Waislamu wametengwa.

. Barubaru anadai Waislamu wameshika hatamu za uchumi wa nchi hii.

..kuna utata hapo, na mimi naomba ufafanuzi tu kwa hao wahusika wawili.
Ritz, Nguruvi3, Wickama, Mag3
 
Last edited by a moderator:

JokaKuu,

Ndugu yangu,mimi nimeingia hapa jamvini peke yangu na nitaondoka peke yangu.

Hivyo vikao unavyonipangia...vinakhusu nini!?

Maneno yoote nisemayo au yakuumizayo,inabidi umlaumu Nyerere. Mimi nasoma na kufuatisha hiyo Khutba yake mwenyewe ambayo mwanae tena wa kumzaa mwenyewe Yericko Bin Nyerere Bin Burito,ndio kaiweka mwanzoni kabisa mwa Mada hii!?

Ahsanta.
 
gombesugu,

..nimekuelewa!!

..tuendelee tu mnakasha kwenye maeneo mengine.

..thanks!!
 
Last edited by a moderator:

Yericko,

Kama huyo Mzee Nyirenda angekua Muislamu,basi nina hakika Historia ya Kivukoni isingemtaja asilan!...na labda kama ingemtaja basi labda sentensi moja tu,kama walivyofanyiwa wale Waislamu wengine!ahaha!!
 
gombesugu,

..nimekuelewa!!

..tuendelee tu mnakasha kwenye maeneo mengine.

..thanks!!

JokaKuu,

Nakuomba usikereke ndugu yangu.

Ili tusonge mbele ni bora kuambiana ukweli utakaochoma leo,kuliko kukaa kimya kudanganyana mapenzi yaso kweli.

Sisi soote ni wamoja,nami binafsi nakuheshimu mno ndugu yangu JokaKuu.

Nashukuru kwa kunifanzia ustahamilivu na kunisikiza.

Ahsanta.
 
gombesugu,

..naunga mkono hoja asilimia 100.

..i am humbled kwa heshima uliyonipa.

..tuendelee na mnakasha.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…