Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Katiba ya jamhuri ya muungano inasema kila mtu ana haki ya kutoa maoni hiyo ni haki yakona ni mawazo yako sikukatalii mimi ninavyo zichukulia hoja za mzee MS ni sawa na wewe unavyo zichukulia hoja za Nguruvi3,lakini hujajibu swali langu!
Jibu zuri analo Mohamed Said!
 
Ritz

Nilishasema huna qualification za kughani na mie katika masuala nyeti ya historia

Wewe tubaki kupigiana ngano za mitaa ya kipata na nyamwezi tu
 

Gombesugu; Haya uliyoyataja ni mambo yanayoliletea aibu sana kanisa katoliki. binafsi ditadiriki kusema eti nasaidia kuliondoa na tatizo hili. Lakini angalia tayari unatumia moja ya vipingele vitatu nilivyoainisha hapo juu kujenga hoja yako dhidi ya Vatican. Which means analysis yangu haikuwa mbaya. Ahsante.
 
..nadhani hujaelewa hoja yangu.

. gombesugu anadai Waislamu wametengwa.

. Barubaru anadai Waislamu wameshika hatamu za uchumi wa nchi hii.

..kuna utata hapo, na mimi naomba ufafanuzi tu kwa hao wahusika wawili.
Ritz, Nguruvi3, Wickama, Mag3

Jokakuu,

nafikiri unahitaji kukuwa zaidi na kuona kila mtu anatazama nini katika uhuru wa Tanganyika.

Nimebainisha mimi namtathmini Nyerere kiuchumi zaidi kwa sababu ndio fani yangu na nime analyse katika fani ya uchumi na ndio nikakwambia bayana kuwa uchumi wenu upo hivyo na nikaweka bayana kama nimekosea nikosoe.

Na kama utatazama dhulma za kijamii utaona jamii ya kiislam imedhulumiwa kwa kuwekewa gavana ya kuwadhibiti yani wameundiwa BAKWATA na JMTz ili wadhibitiwe zaidi.


Je unajua kuna tofauti kati ya kuushika uchumi na kuongoza uchumi?

Sasa labda unifafanulie utata upo wapi hapo?
 


Gombesugu; I kindly request you not to cc me your posts. I have noticed you are preparing ground to insult me as you did in the past. Please respect this request
 

Swadakta yaa akhuy,

Anachotaka kubainisha ni kuchanganya mambo kimakusudi kabisa. lakin mimi nimechambua kiuchumi zaidi na nimempa room ya kukosoa kama ataona nimekwenda tenge. lakin hakufanya hivyo.

Labda cha kumuongezea kuwa Biashara katika Uislam imeelezwa sana na aina gani za biashara na namna ya kuzifanya na hata namna ya kuhifadhi kumbukumbu na namna ya kuweka benki na mifumo yote ya uchumi. na hilo ndilo lipo hewani.

Ahsantum kwa kunielewa na kusaidia kumuelimisha mwenzetu.

maa salaam
 

Gombesugu; Nikiongelea jambo ni kuwa nimeona pattern.
 
Ritz

Nilishasema huna qualification za kughani na mie katika masuala nyeti ya historia

Wewe tubaki kupigiana ngano za mitaa ya kipata na nyamwezi tu

Yericko,

Unadhani mie na muda na wewe ninachofanya ni kuwafahamisha wanajamvi upuuzi wako.

Mimi ndiyo nimekufanya ufanye editing kwenye mabandiko yako. ha haa ha.

Nakuacha na haya maneno mazito yatakusaidia.

"Uongo, kama vile nyasi juu ya maji huelea, Atafutae lulu hana budi kupiga mbizi." John Dryden


Cc.. gombesugu,
 
Last edited by a moderator:

In a way huwa nashangaa. Uliniuliza kuhusu moslem demographies ya nchi hizo mbili, nimekupa. Sasa fursa ni kusema Wickama you have LIED, then onyesha your source. Huonyeshi if I have lied, badala yake unanitangaza kuwa nahamisha magoli. Gombesugu, this is a very dishonest way to debate. You could just as well have kept quite. It is not mandatory to reply every posting.
 

You meant JOHN RAMBO?
 

Mzee MS; Ungemuuliza anashangaa nini. Mwenzio huenda hakuwa anashangalia mambo ya kuogelea misisipi utotoni pengine alidhani anaangalia zombie ambalo ni brain dead. hahahahahah
 


Twaib,Jazakallahu kheir...
 
Mzee MS; Ungemuuliza anashangaa nini. Mwenzio huenda hakuwa anashangalia mambo ya kuogelea misisipi utotoni pengine alidhani anaangalia zombie ambalo ni brain dead. hahahahahah

ha haa haa Crackpot as a Choc-ice.
 
Y. Nyerere,Chuma kinachowaka na kuchoma mamilioni ya fedha za Wa Tz huku kikieneza magonjwa ya zinaa na hatari unathubutu kuja hapa na kuusifia Mwenge? unaweza kunitajia hata angalau faida moja ya mwenge? mpaka leo najiuliza ninani aliyeleta wazo la kuwasha mwenge na kuuzungusha nchi nzima huku watu wazima wenyeakili zao wanaukimbiza na kunyanganyana!
 
MS,Asanta na shukurani kubwa kwako kutupasha khabari kubwa za Shujaa wetu marehemu Ally Sykes! Allah akulipe kila la kheri duniani na akhera! Mzee Ally Sykes Alla amsamehe madhambi yake na kumpa pepo yake inshaallah kazi aliyoifanya si ndogo!na kaswali kadogo Sheik MS, hapo juu umetaja jina la Chif Makwaia, jee. kuna uhusiano wowote kati yake na Mwandishi Makwaia wa Kuhenga wa channel 10?
 
RITZ,Nyundo zote hizi ulizomgonganazo Yericko kichwani! kwakuwa kachunwa uso ama hatajibu au atakuja na uongo mwingine!
 
Duh, naona mambo yanazidi kunoga, JF ni zaidi ya tuijuavyo na kweli duniani kuna mambo.. gombesugu hata wewe una uthubutu wa kutamka maneno kama hayo hapo juu! Kama ingekuwa ni swala la kuzikana kwa uongo, mbona mwalimu wako wa darsa Mohamed Said keshazikwa zamani na kusahaulika siku nyingi tu! Unakumbuka listi ya uongo wake uliodumu miaka 15 hadi ilipovinjari kwenye anga za JF! Lakini hayo tuyaache, nina maswali manne tu kwako wewe, ma Shariff na ma AL Akhiy wote katika mnakasha huu;

  1. Kuna watu humu ndani wamekataa kata kata kumeza ilmu inayodaiwa kutolewa na Mohamed Said bila kuhoji uhalali na ukweli wa madai yake, mengi yakiwa yamejikita katika uchochezi ambao hauna msingi wowote zaidi ya simulizi za chuki na fitna kutoka kwa baadhi ya wazee wake. Hapa nitataja baadhi tu ya watu wanaopinga uopotoshwaji wa Mohamed Said; sweke34, Ngongo, Wickama, zumbemkuu, Remote, Son of Alaska, Nguruvi3, JokaKuu, Mkandara, Fundi Mchundo, platozoom, chama, Gwalihenzi, Nanren, WildCard, Ogah, Wimana, Geeky, Jasusi, Mag3 na wengine wengi tu.. gombesugu, je kati ya hawa unadhani yupo Muislaam hata moja? Je unadhani yupo mwana CCM hata moja? je unadhani yupo mwana Chadema hata moja?
  2. Kuna sehemu nimetaja kwamba, pamoja na utumwa kuwepo duniani ndani ya jamii mbalimbali, ni Waarabu ndio jamii ya kwanza duniani kuutumia utumwa kibiashara. Mathalani jamii ya kiarabu ndio jamii ya kwanza kuwawinda waafrika, kuwateka na kuwasafirisha na kuwauza kama bidhaa nje ya bara hili. Hii ilifanyika miaka mingi tu kabla ya Wazungu kufika Afrika kwenye karne ya tisa (miaka ya 800) Swali, kwa nini tunapowataja Waarabu na kuwalaumu kwa udhalimu huu, nyie watetezi mnakimbilia kuutetea Uislaam kama dini inayojali utu, je Uislaam ni Uarabu?
  3. Toka tupate uhuru mwaka 1961 tumekuwa chini ya utawala wa chama kimoja TANU ambacho mwaka 1977 kiliungana na ASP na kuzaliwa CCM. Katika muda wote huo Waislaam, kulingana na mahubiri ya kichochezi ya Mohamed Said, wamebaguliwa, kupuuzwa, kunyimwa haki na kuonekana kama raia daraja la nne nchini. Kwa nini mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa mwaka 1992 chini ya uongozi wa Raisi Ali Hasan Mwinyi, kiongozi Muislaam, Waislaam hawakuutumia wingi wao (kumbuka idadi ya Waislaam nchini kulingana na ngano za Mohamed Said, ni theluthi tatu ya Watanzania!) kuhakikisha wanakiunga chama kitakachowatetea na kuwapa haki?
  4. Mathalani, baada ya awamu ya kwanza ya utawala wa Raisi Jakaya Kikwete, Muislaam, kwa nini ilipoonekana wazi mwaka 2010 kwamba mfumo Kristo unazidi kushamiri chini ya CCM, Waislaam, kulingana na kauli ya Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama cha CUF na Raisi mtarajiwa, walihakikisha CCM hiyo hiyo inarudishwa madarakani. Pamoja na kufanikiwa katika mpango huo, kwa nini bado wanatokea akina Mohamed Said, Sheikh Ilunga, Sheikh Ponda, wanahubiri chuki dhidi ya watu ambao kulingana na walivyojipanga, walihakikisha hawakamati uongozi nchini?
gombesugu, hilo la jina langu kuwekwa kwenye "shit list" ya Mohamed Said hata isikupe taabu, I feel honoured kuwa katika hiyo list kwa sababu ni hiyo listi ndiyo imemfanya ahamishie kabisa malazi hapa JF! Angesema ameniweka kwenye "ignore list" mmh, maybe...lakini alimradi yuko dirishani anapokea vidonge, hamna taabu, ingawa yawezekana ni ngumu kwake kuvimeza. Naambiwa Barubaru kaikana nchi yake kakimbilia Oman lakini familia hiyooo, Maryland Marekani huku roho yake ikiendelea kusononeka nchini si Unguja, Dar, Mwanza au Kigoma, oops, hiyo inaitwa home sickness... na wewe je ndugu yangu Al Akhiy!

Jamani ni muda tu unakosekana...humu ndani kuna ilmu na elimu zinatolewa, darsa na darasa ziko nje nje na wapo akina Spike Lee kazi kufyonza tu bila hata kuchungulia ndani ya chombo, je mrija uko salama? Naambiwa watu wananyimwa fursa katika uongozi wakati wenyewe ndio viongozi, wananyimwa fursa katika uchumi wakati ndio wafanya biashara wakubwa, wanaonewa na vyombo vya dola wakati wao ndio wameshika dola, hawapewi haki mahakamani wakati mahakama wanaisimamia wao na sasa ma Al Akhiy nao kesho watalalamika kwa kutopata fursa ya kuwa wasomi hadi wanawaweka akina Mag3 kwenye "shit list"! Chezea Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…